Je! MALI ASILI TULIZONAZO NCHINI,RAIS KIKWETE ALISTAHILI KUITWA MSAFIRI KILA SIKU??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je! MALI ASILI TULIZONAZO NCHINI,RAIS KIKWETE ALISTAHILI KUITWA MSAFIRI KILA SIKU???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by commonmwananchi, Feb 11, 2012.

 1. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,183
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  ndugu zangu watanzania na wana JF,kwanza nawasaimia popote pale mlipo!,
  baada ya kuona na kuzisoma thread mbalimbali humu ndani,zikihusiana na safari za mheshimiwa rais wetu JK.Nimetafakari na kujiuliza bila majibu swali hilo hapo kwenye heading.
  Ninavyoelewa mimi ni kwamba urais ndio cheo cha juu kuliko vyote katika maamuzi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania yetu.
  Kulingana na hilo sina tatizo na rais atakapo safiri nje ya nchi ili kutimiza majukumu yake ya ki-rais pale itakapomlazimu kufanya hivyo kulingana na umuhimu utakaokuwa umejitokeza kwa safari husika kwa maslahi ya taifa letu la Tanzania.
  Safari ya rais wa nchi inayoitwa maskini kama yetu inapaswa kuwa safari ya kimaskini pia,kwa kuzingatia hali halisi ya pato na uchumi wa nchi yetu,rais anaposafiri nje ya nchi anapaswa kupanga bajeti ndogo kwa kadri inavyowezekana ili kubana matumizi,ili fedha hizo zisaidie katika sekta nyingine ndani ya nchi yetu ikiwemo ile ya elimu ambako mpaka sasa kuna watoto wetu wanasoma wakiwa wamekaa chini ardhini ndani ya madarasa yao na huku idadi yao ikimshihda hata mwalimu kuwadhibiti ndani ya darasa na wakati huohuo mwalimu huyo huyo akiwa na kero zake kichwani zinazotokana na wizara husika mojawapo ikiwa madai ya malimbkizo ya malipo mbalimbali halali aliyostahili kulipwa na bado akiidai serikali(mungu awape walimu moyo wa uvumilivu).

  Pia bajeti ndogo ya safari za rais ingeokoa fedha ambazo zaweza elekezwa mahospitalini ambako hakuna madawa na wagonjwa ni wengi hadi wengine tumewaona wakifikia hatua ya kulala chini ndani ya wodi, na hizo ni kwa uchache tu. mahitaji ya fedha ni makubwa kiasi kwamba kama serikali ingekuwa makini basi ingepunguza kadri iwezavyo hizo safari ambazo kwa ujumla mtanzania wa kawaida haoni manufaa yake ya moja kwa moja zaidi ya rais mwenyewe kutuambia kuwa huenda kutembeza BAKULI.
  Kwa mujibu wa takwimu mbalimbali,mpaka sasa rais amekwisha safiri mara 322,kwa wastani wa kila safari kumchukua rais siku zipatazo nne akiwa ughaibuni, na ukizidisha siku nne mara safari 322 basi utapata siku 1288.ukizigawa siku 1288 kwa 365{ambazo ni mwaka mmoja}basi utapata jumla ya miaka ipatayo mitatu na ushei....(hii ni kwa mujibu wa takwimu zinazotolewa sehemu mbalimbali ikiwemo JF)huu ni mwaka wa takriban sita na ushei tangu JK ameingia madarakani.

  Tunaona kuwa ametumia nusu ya kipindi chake akiwa safarini,tukiachilia mbali gharama za safari husika ambazo ni milioni mia tatu kwa safari moja unaweza kuona ni fedha kiasi gani nchi inagharimika kwa safari hizi na pia ingeweza kuokoa kiasi gani kwa kuzipunguza safari hizo.
  Nchi kama rwanda zimepiga hatua kubwa ndai ya miaka michache tu tangu ilipotoka kwenye mauaji ya kimbari,wako juu kitakwimu wako juu yetu kiuchumi ingawa ni aghalabu kuona rais kagame akiwa anasafiri kwenda nje kama hapa kwetu.majirani zetu kenya na uganda pia hivyo hivyo wanafanya vizuri kuliko sisi na pia ni mara chche utawasikia marais wa nchi hizo wakiwa wanakuja kubadili nguo na kurudi ulaya ziarani tena.

  TANZANIA tumejaaliwa maliasili nyingi kwa uchache Dhahabu,Almasi,Tanzanite,Gesi,Mkaa wa mawe,Uranium,samaki katika maziwa na bahari zetu,Hifadi za taifa kwa utalii wa picha na uwindaji,achilia mbali misitu kwa mbao na pia raslimali watu.
  Zote hizo ni utajiri tosha na tunu pekee tuliyojaaliwa duniani ambazo kwa yeyote yule mwenye uelewa wa kawaida hawezi kumueleewa rais wetu anapokwenda kutembeza bakuli huko nje
  Jambo ambalo ni sawa na kutudhalilisha watanzania,nakifananisha na kitendo cha mtu mwenye duka kubwa la bidhaa ambaye analiacha duka lake na kwenda kuomba chumvi mtaa wa saba.

  MY TAKE...kwa maliasili tulizo nazo ,na kwa mahitaji ya kiwango cha juu waliyonayo wazungu(nchi zilizoendelea)kwa maliasili hizo, ni dhahiri hata kama rais wetu angekaa nchini zaidi akitimiza majukumu yake muhimu.basi hao hao wakubwa wa dunia wangelazimika kuja nchini kumuona yeye.nikifananisha na mzee mwenye mabinti warembo ambaye hana haja ya kuwatafuta wakwe bali kusubiri washenga nyumbani kwake akiwa kajituliza tuli akinywa kahawa yake.
  Jambo hili litaepusha gharama kubwa taifa linazoingia kwa safari nyingi za rais zenye kutugharimu fedha nyingi na pale inapobidi rais kusafiri ni vema pia suala la idadi ya maofisa wanaoandama na msafara wa rais ikapunguzwa ili kuepuka gharama zisizo za lazima.

  Naomba mchango wenu katika hili........

  .
  .
   
Loading...