Je, Makonda naye yupo mtegoni, suala la watumishi hewa?

Chief wa kibena

JF-Expert Member
Mar 13, 2016
686
394
Wanajamvi,

Kutokana na Anne Kilango kutumbuliwa kwa kudanganya kuwa mkoa wa Shinyanga hauna watumishi hewa, turudi Dar ambapo mkuu wa mkoa aliitangazia Tanzania kuwa mkoa wake unawatumish hewa 11.

Kiukweli Dar ni moja ya mikoa yenye watumishi wengi sana katika halmashauri zake na ni mkoa unao vutia watu wengi kufanya kazi. Lakini lazima tuangalie kwa mapana zaidi, hii inawezekana mkoa kuwa na watumishi hewa 11 tu.

Mimi naamini kwamba sehemu yeyote inayokimbiliwa, kuwa uwezakono mkubwa vile vile kwa watu wengi kuondoka pia. Kufuata maslahi zaidi.

Naamini mkuu wa mkoa kadanganywa na wasaidizi wake, siamini kabisa kama mkoa mzima una idadi hiyo ya watumishi hewa. Hasa kutokana na hofu ya hawa watendaji kutumbuliwa kama wangeitaja idadi halisi.
 
wanajamvi, kutokana na Anne kilango kutumbuliwa kwa kudanganya kuwa mkoa wa shinyanga hauna watumishi hewa. turud dar ambapo mkuu wa mkoa aliitangazia Tanzania kuwa mkoa wake unawatumish hewa 11. kiukweli dar ni moja ya mikoa yenye watumish weng ssna ktk halmashauri zake, na ni mkoa unao vutia watu wengi kufanya kazi. lakin lazma tuangalie kwa mapana zaid, hii inawezekana mkoa kuwa na watumish hewa 11 tu. me naamin kwamba sehemu yeyote inayokimbiliwa, kuwa uwezakono mkubwa vile vile kwa watu weng kuondka piah. kufuata maslahi zaid. naamin mkuu wa mkoa kadanganywa na wasaidiz wake. siamin kabsa kama mkoa mzima una idadi hyo ya watumishi hewa. Hasa kutokana na hofu ya hawa watendaji kutumbuliwa kama wangeitaja idadi halisi.
In short kadanganya, anastahili kutumbuliwa na kwasasa baba Riz yupo majuu
 
wanajamvi, kutokana na Anne kilango kutumbuliwa kwa kudanganya kuwa mkoa wa shinyanga hauna watumishi hewa. turud dar ambapo mkuu wa mkoa aliitangazia Tanzania kuwa mkoa wake unawatumish hewa 11. kiukweli dar ni moja ya mikoa yenye watumish weng ssna ktk halmashauri zake, na ni mkoa unao vutia watu wengi kufanya kazi. lakin lazma tuangalie kwa mapana zaid, hii inawezekana mkoa kuwa na watumish hewa 11 tu. me naamin kwamba sehemu yeyote inayokimbiliwa, kuwa uwezakono mkubwa vile vile kwa watu weng kuondka piah. kufuata maslahi zaid. naamin mkuu wa mkoa kadanganywa na wasaidiz wake. siamin kabsa kama mkoa mzima una idadi hyo ya watumishi hewa. Hasa kutokana na hofu ya hawa watendaji kutumbuliwa kama wangeitaja idadi halisi.
Magufuli anagwaya Makonda hata angesema hawapo asingefanya kitu .
 
kuna watu Makufuli hawezi kuwagusa kabisa kama yule aliyepeleka zuio feki la Mahakama kwenye uchaguzi wa meya dar
 
Anachokifanya Magufuli ni kutumbua wale ambao hawakuwa chaguo lake hivyo anawatafutia kosa hata liwe dogo namna gani ili awaondoe aweke wale chaguo lake, hivyo kwa Makonda, Nape, Mwigulu, Kitwanga na January Makamba hata wafanye madudu kiasi gani kamwe hawezi kuwafanya chochote kwani anajua wazi wamempigania ili yeye aonekane ameshinda nafasi ya Urais.
 
Kwa Dar kila taasisi inawafanyakazi hewa... kuna taasisi zingine na mawizara zina watu waliopitia field tu na kuondoka lakini wamewekwa kwenye payroll...

Kuna watu wanahesabika waajiriwa lakini wanambiwa wao ni vibarua mpaka kazi zitokee.. mishahara yao wanachukua wajanja...
 
hizi nafas za kupeana watu hawafanyi kazi,.......kazi umbea tu ndugu......
mawazo nafas zao na wakuu wengine wawe wanashindanishwa kwa interview........na anaepatikana apewe madaraka
 
Anachokifanya Magufuli ni kutumbua wale ambao hawakuwa chaguo lake hivyo anawatafutia kosa hata liwe dogo namna gani ili awaondoe aweke wale chaguo lake, hivyo kwa Makonda, Nape, Mwigulu, Kitwanga na January Makamba hata wafanye madudu kiasi gani kamwe hawezi kuwafanya chochote kwani anajua wazi wamempigania ili yeye aonekane ameshinda nafasi ya Urais.
akonda jembe sana
 
Magufuli anagwaya Makonda hata angesema hawapo asingefanya kitu .
Mkoa wa Dar hauwezi kuwa na watumishi hewa 11tu labda angetuambia mia tatu mia nne tungemwelewa.Dar ndio makao makuu ya wizara zote.Wapiga madili wakubwa wako huko na wachonga mihuri fake wote.Afadhali hata yeye alijitokeza na idadi ndogo na kasema wazi sio kwamba zoezi limekamilika bali ni endelevu.Kosa la mama Kilango alikataa kata kata kuwa mkoa wake hauna mtumishi hewa ikatia shaka toka mwanzo.Laiti angekumbuka pamoja na kuwaagiza watendaji wake wa chini kufanya zoezi hilo kwa umakini na kwa muda uliotolewa angeweza pia kutuma kikosi kidogo toka ofisi ya usalama wa taifa nao kwa siri kuendeleza zoezi hilo hivyo kupata majibu sahihi.Vyombo hivi kwenye mkoa viko chini yake.Kosa la pili la hawa wakuu wa mikoa na wilaya walisahau wanufaika wa mishahara hewa ni hao hao anaowaagiza kuchunguza.Nasema baadhi sio wote wa wakurugenzi,makatibu tawala wa wilaya,w/viti halmashauri na wakuu wa maidara wengi wao ndio wanufaika wa hiyo mishahara hewa.Sasa wategemee wawapelekee orodha ya watumishi hewa ili watumbuliwe wao na kulipishwa hasara zote zilizolipata taifa?Tatu ni kosa la serikali kutoa muda mfupi kwa zoezi hatari kama hilo huku wakielewa hao wakuu wa mikoa na maras wote walikuwa wageni wote.Vyovyote vile nao wangewaagiza wa chini yao kwa ukali ule ule wa kutumbuliwa kwanza wao na kuwasilisha taarifa zao kwa mkuu wa mkoa mapema hivyo wao walipewa muda mfupi zaidi ili mkoa ujumuishe wilaya zote na kutoa ripoti.Raisi wa nchi angeweza kutoa onyo kwa mkuu wa mkoa ila kilichomuumiza zaidi kufikia uamuzi wa kutengua uteuzi ni kuwa tayari taifa lilishapata hasara ya mil.339.9 ambazo zingeweza kuokolewa.Hata hivyo hawa wateule wa raisi hakuwatupa amesema atawapangia kazi nyingine.Niwakumbushe tu wote wanaoteuliwa katika nafasi mbali mbali za uongozi na bahati nzuri ni wale wale hapo nyuma kidogo walikuwa wakisema mtaisoma namba wawe makini na uongozi wa Magufuli sio ule wakati wa kusubiri kuletewa taarifa za uongo maofisini,kujibu maswali magumu kwa majibu rahisi na kuandaa ngonjera na halaiki kwa raisi mtaisha wote kwa utendaji huu wa mazoea.Mwisho napendekeza ipitishwe verification kali kwa kila mkoa kuhakikisha hawa watumishi hewa mikoa mingi hesabu zake haziko sawasawa.Naamini kuna sehemu baadhi ya watumishi walioko likizo ndefu za uzazi na masomoni waliorodheshwa kama hewa kwa makusudi kukomoana au kwa uharaka wa zoezi.Uelewe kumfuta mtumishi kimakosa kwenye payroll na register kumrudisha upya ni kazi kubwa sana.
 
acheni roho mbaya zenu kwa kijana Makonda, huyu alisema kuna 47 na zoezi linaendelea maana watumishi wengi wa dar mara nyingi huwa safarini
 
Kwa Dar kila taasisi inawafanyakazi hewa... kuna taasisi zingine na mawizara zina watu waliopitia field tu na kuondoka lakini wamewekwa kwenye payroll...

Kuna watu wanahesabika waajiriwa lakini wanambiwa wao ni vibarua mpaka kazi zitokee.. mishahara yao wanachukua wajanja...
Nakutunuku Phd ya uongo. Ameen
 
hapa ikulu penyewe wapo zaidi ya hiyo idadi na M
Wanajamvi,

Kutokana na Anne Kilango kutumbuliwa kwa kudanganya kuwa mkoa wa Shinyanga hauna watumishi hewa, turudi Dar ambapo mkuu wa mkoa aliitangazia Tanzania kuwa mkoa wake unawatumish hewa 11.

Kiukweli Dar ni moja ya mikoa yenye watumishi wengi sana katika halmashauri zake na ni mkoa unao vutia watu wengi kufanya kazi. Lakini lazima tuangalie kwa mapana zaidi, hii inawezekana mkoa kuwa na watumishi hewa 11 tu.

Mimi naamini kwamba sehemu yeyote inayokimbiliwa, kuwa uwezakono mkubwa vile vile kwa watu wengi kuondoka pia. Kufuata maslahi zaidi.

Naamini mkuu wa mkoa kadanganywa na wasaidizi wake, siamini kabisa kama mkoa mzima una idadi hiyo ya watumishi hewa. Hasa kutokana na hofu ya hawa watendaji kutumbuliwa kama wangeitaja idadi halisi.

hapo ikulu penyewe wapo zaidi ya hao na Magu anawajua, mi namshauri asichukue mkopo kwenye taasisi yoyote apeleke SITE, manake wakati wowote nyongo yaweza tumbuka
 
Back
Top Bottom