Je makampuni ya simu huwaibia watumiaji wa mikoani

Masulupwete

JF-Expert Member
Feb 15, 2012
2,180
2,000
Mara nyingi niendapo mikoani nakuta spidi ya internet ni ndogo sana kiasi cha kutumia muda mrefu kuaccess web. Sasa najiuliza hili lina maana gani? Kama watumiaji wa miji mikubwa hasa dsm internet inafunguka kwa spidi ya upepo, iweje kuwe na utofauti kwa mikoani.

Ni nini kinachokuwa kimebadilika hasa ukizingatia watu hawa wote hufanya malipo kwa viwango vile vile? Kwanini mtumiaji wa mkoani hapati huduma inavyostahili?
 

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
7,684
2,000
Sam kwenyewe hy network bado ni majanga!
TCRA nadhani wanajua jukumu Lao pekee ni kutoa leseni za mawasiliano pekee!
Nashindwa kuelewa mfano wa hizo us codes kwa ajili ya ku access huduma mbalimbali Kila mtandao unajiwekea tu unakuja mfano airtel wana mi codes kibao huduma zinafanana lkn mi code kibao.... Mara *149*99# Mara 154*99 Mara 148*22 zote hizi ni kwa ajili ya ku access Internet kiasi ambacho wangeweka huduma zote kwenye menu moja isipokuwa kuongeza items tu hizo. Kuna taasisi ni mizigo TCRA ni moja wapo.
 

luck

JF-Expert Member
Oct 3, 2009
970
1,000
Ni kweli. Kuna kitu kinafanywa ndivyo sivyo na makampuni ya simu. Spidi ya neti ni ndogo sana mkoa.Kitu unachoweza kukipata kwa dakika 2 utahitaji dak.30 au zaidi kukipata na pengine usikipate kabisaa ukiwa mkoa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom