Je, majini ni kitu gani na yanataka nini?

Status
Not open for further replies.

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Ndugu wana JF, mara nyingi nimekuwa nikijiuliza majini ni kitu gani. Na najiuliza hivi kwa vile sijawahi kusikia mtoto au mke wa waziri, mbunge au rais fulani ana majini. Bali wote wanaokuwa na majini mara nyingi ni watu wa kawaida na maskini.

Mtoto (binti) wa mdogo wangu kaenda huko Kimanzichana (Mukuranga) kwa mwezi hivi na aliporudi nikaambiwa amepata majini. Sikuamini. Leo (10/02/2010) alianza kupiga kelele kwa sauti ya juu sana na wakati huo akiwa anaongea kama Kiarabu hivi (sijui kama ni correct Kiarabu au la). Kwa kweli nilishindwa cha kufanya.

Mke wangu akawa ananishauri nimwite sheikh ili ayatulize lakini kwa imani yangu sikufikiria kama kufanya hivyo ni sahihi.

Basi mama akaleta maji ya baraka kutoka kanisani na alipomumwagia akacharuka na kutaka kumpiga mama. Akawa anasema anataka kubadili dini. Basi nilichukua yale maji nikamumwagia zaidi na kisha "hilo jini" likasema linaondoka ila litarudi kumtembelea tena.

Kisha akaonekana kama mtu anayetoka usingizini na amechoka. Nikamwuliza: unataka kubadili dini? Akajibu hapana. Nikamwuliza tena, unafahamu Kiarabu? Akajibu hapana.

Hii ni phenomenon ambayo nataka niifanyie research. Ila kwa imani yangu nadhani inatokana na mtu kuwa na mlundikano wa mawazo (unfinished business) ya kusononesha na hivyo ni mojawapo ya 'effects' zake. Yaani, it's more psychological than real. Je, wan JF mnasemaje?
 
(Na Prof. Dkt. Shaykh 'Umar Suleiman al-Ashqar)
imefasiriwa na Shaibu H.Kifea
Al-Amash Asimulia Jinsi Alivyokutana na Jini
Kumekuwa na utata juu ya maumbile na maisha ya viumbe wenzetu wanaoitwa majini. Watu wengi katika jamii mbalimbali wamekuwa wakisikia habari za viumbe hawa lakini bado uhalisia wao haufahamiki kwa wengi.
Pengine hii ni mada tete kwa mtafiti kuiendea lakini kwa hakika ni mada inayoweza kuvuta hisia za wengi ambao wanataka kujuwa hasa hawa majini ni viumbe gani, wakoje kimaumbile, wanakula chakula gani, je wanazaa watoto, je na wao wanakufa kama binadamu?.... na maswali mengine mengi.
Kama kuna mtafiti ambaye amefanya utafiti wa aina yake basi ni Dk Umar Suleiman al-Ashqar, Profesa wa Shariah katika Chuo Kikuu cha Jordan. Profesa huyu ameandika kitabu chenye kurasa 243 kuhusiyana na Majini.
Lakini jambo la muhimu ni watu kusoma na kuelewa yale aliyoyaandika mtafiti ambayo, kwa kiasi kikubwa, yametokana na ushahidi wa Qur'an na Hadith za Mtume (saw).
Makala haya yanaanza kwa kuwatambulisha wasomaji majina ya Majini:
Majina ya Majini kwa Kiarabu
Kwa mujibu wa wanazuoni wa Masuala ya Lugha ya Kiarabu, kuna aina mbalimbali za Majini:
1. Iwapo mtu anazungumzia majini tu peke yao basi
wanaitwa hivyo hivyo "Majini".
2. Iwapo mtu anazungumzia Majini wanaoishi na wanadamu, basi hao wanaitwa "aamar" au kwa jina la wingi "amaar".
3. Ikiwa mtu anazungumzia Majini wanaowafanyia uwaduwi vijana, basi hao wanaitwa "arwaah"
4. Ikiwa mtu anazungumzia Majini wanaowafanyia uwadui wanadamu wote, basi hao wanaitwa Mashetani
5. Kama wanaleta madhara makubwa na kuwa na nguvu zaidi wanaitwa "afriit"

Aina za Majini
Mtume (saw) kasema, "kuna aina tatu za Majini, aina ya kwanza ni yule anayeruka angani, aina ya pili ni mbwa na nyoka, na aina ya tatu ni yule anayekaa kwenye makazi na anayesafiri huku na kule".
Hakuna hoja ya kukanusha kuwepo kwa majini
Wapo watu wachache wanaokanusha kuwepo kwa kiumbe anayeitwa Jini. Baadhi ya washirikina walidai kuwa maana ya jini ni roho za sayari. Baadhi ya wanafalsafa nao wanadai kuwa majini ni nguvu za uwovu katika roho za wanadamu kama ambavyo Malaika ni nguvu za wema katika roho za wanadamu.
Baadhi ya watu wa hivi leo wanadai kuwa majini ni bakteria na vijidudu ambavyo sayansi ya leo imevigunduwa hivi karibuni.
Katika sherehe yake ya Surati al-Jinn ya Qur'an, Muhammad al-Bahi anasema kuwa majini ni Malaika. Kwa mtazamo wake, majini na malaika kiumbe mmoja, hakuna tofauti kati yao. Ushahidi anaoutoa ni kwamba malaika nao pia hawawezi kuonekana kwa macho ya wanadamu.
Kutokuwa na elimu ya kuwajuwa majini si ushahidi wa kutokuwepo kwao
Zaidi wanachoweza kukisema wakanushaji hawa ni kuwa wao hawana elimu inayohusu maisha ya majini. Lakini kutokuwa na elimu hiyo si ushahidi kuwa majini hawapo
Ukweli wa mambo
Hoja sahihi ni kuwa majini ni aina ya tatu ya viumbe mbali ya malaika na wanadamu. Ni viumbe wenye akili na ufahamu. Si vijidudu wala si nguvu za uovu zinazodhaniwa na wanafalsafa.
Majini ni viumbe wanaowajibika kwa vitendo vyao na wameamrishwa na MwenyeziMungu kufanya baadhi ya mambo na kuzuiwa kufanya mengine. Ushahidi wa hoja hii ya kuwepo kwa majini umetolewa na makundi mbalimbali ya watu.
Katika kitabu chake, Majmul al-Fatawa, Imam Ibn Taymiya anasema: Makundi ya Waislamu hayajahitilafiana juu ya kuwepo kwa majini, na wala hayajatofautina juu ya ukweli kuwa Muhammad (saw) aliletwa kuwa Mtume wa Majini piya.
Na hata watu wa kitabu miongoni mwa Wayahudi na Wakristo pia wanakubali kuwepo kwa majini vile vile kama wanavyoamini Waislamu, ingawaje mtu anaweza kukuta watu miongoni wakikanusha kuwepo kwao, kama ambavyo mtu anaweza kukuta watu miongoni mwa Waislamu wakikanusha kuwepo kwao kama vile Jahamiyya na Mutazila.
Lakini madhehebu mengi na wanazuoni wao wanakubali majini wapo. Hii ni kwa sababu simulizi juu ya maisha ya majini zimekuja kwa njia ya mutawaatir kutoka kwa Mitume jambo ambalo lina elimu yenye ushahidi wa hakika na moja kwa moja.
Ni jambo la hakika kuwa wanaishi, wanafikiri na wanatenda mambo kwa hiyari. Wameamrishwa kufanya mambo fulani na kukatazwa kufanya mambo mengine. Majini si sifa wala khulka za wanadamu au viumbe wengine kama wanavyodai baadhi ya washirikina.
Kwa kuwa suala hili la majini limesimuliwa kwa njia ya mutawaatir kutoka kwa Mitume, wanazuoni na umma unawajuwa na hakuna kundi linalojinasibisha na Mtume linaliweza kuwakana.
Aidha katika ukurasa wa 13, Ibn Taimiya kaandika: makundi yote ya waislamu yanakubali kuwepo kwa majini kama wanavyokubali watu wa kitabu, washirikina miongoni mwa Waarabu na wengine waliotokana na kizazi cha Ham (mtoto wa Nuhu).
Ushahidi wa Qur'an na Hadith
Kuna aya nyingi za Qur'an na kuna Hadith nyingi zinazothibitisha kuwepo kwa majini. Mathalani MwenyeziMungu anasema katika Qur'an:
Sema, "imefunuliwa kwangu kuwa kundi moja la majini lilisikiliza Qur'an ........ (72:1)".
"Na kwa hakika kulikuwa na wanaume miongoni mwa wanadamu wakijikinga kwa wanaume miongoni mwa majini, kwa wakawazidishia takhlifu... (72:6)."
Kwa kweli kuna aya nyingi za Qur'an zinazowahusu majini ambazo tutazinukuu huko mbele InshaAllah.
Simulizi za kuwaona majini kwa macho
Kuna watu wengi wa zama hizi, hizi zetu na wengine wa zama zilizopita ambao wameona jambo la majini, japokuwa watu wengi kati yao waliowaona au kuwasikia majini hawakutambuwa kuwa hao waliowaona au kuwasikia walikuwa ni majini.
Huwenda baadhi yao walidhani ilikuwa ni mizuka, mapepo, vivuli, viumbe wa angani na kadhalika. Watu wengi wa kuamika katika zama hizi na zama zilizopita wamusimulia mikasa inayohusu majini
Mwanazuoni mashuhuri wa Hadith, al-Amash kasimulia mkasa huu, "jini lilijitokeza miongoni mwetu. Mimi mwenyewe nikamuuliza, ‘ni chakula gani unachokipenda?' Akajibu, ‘Wali'. Sisi tukamletea kiasi cha chakula hicho na (kwa macho yangu) nikaona kijiko kikienda juu na chini lakini mwenyewe sikumuona. Nikamuuliza, ‘hivi na nyie mnao watu wa matamanio (na bidaa) kama tulionao sisi?' Akajibu ‘ndiyo'.
Baada ya kunukuu kisa hicho, Ibn Kathir kaandika hivi: "niliwasilisha isnadi ya kisa hiki kwa mwalimu wetu Imam Abu al-Hajjaj al-Mizi, akasema: ‘hiyo ni isnadi ya hakika kutoka kwa al-Amash.' Kisha akasema, ‘hata Ibn Asaakiir alinukuu maelezo ya al-Abbas ibn Ahmad al-Dimishqi kwamba kasema, "niliwasikia baadhi ya majini wakighani hivi: "nyoyo hudhikika mpaka zikurubiane na yule zinaempenda na ziko pamoja naye mahali popote pale, Magharibi au Mashariki, zimejawa na mapenzi juu ya allah, na Allah ndiye Mola wao, nazo zinajikurubisha kwa Allah tu na si kwa kiumbe chake.
Dk Ashqar, mwandishi wa makala haya, anaongeza hapa kusema: "watu wengi wa kuaminika wamenisimulia jinsi walivyosemeshana na majini na wengine kuwaona kabisa. InshaAllah mikasa hii tutaisimulia pale tutakapozungumzi uwezo wa majini wa kujitokeza kwa sura tofauti.'

Itaendelea...
 
Mfululizo Wa Mada Ya Majini (2)

(Na Prof. Dkt. Sheikh 'Umar Suleiman al-Ashqar)
imefasiriwa na Shaibu H.Kifea




Binadamu Hatuwaoni Majini Lakini Punda, Mbwa Wanawaona.
Wanadamu hatuwaoni majini kwa macho yetu japo tuko nao, tunapishana nao lakini wao wenzetu wanatuona. Wakati sisi wanadamu hatuwaoni majini, baadhi ya wanyama kama Punda kihongwe na Mbwa wanaofugwa majumbani huwaona Majini.
Katika vitabu vya Hadith vya Musnad Ahmad na Sunan Abu Dawud imenakiliwa Hadith yenye isinadi sahihi kutoka kwa Jabir kwamba Mtume (saw) kasema:
"Mkisikia mlio wa kubweka wa mbwa au mlio wa punda vihongwe wakati wa usiku, basi ombeni ulinzi kwa MwenyeziMungu kujikinga na Shetani kwani wanyama hao huona kile msichokiona nyinyi."
Kisayansi, jambo hili si geni kwani wanasayansi wengi wamethibitisha kuwa wanyama wanaweza kufanya mambo mengi ambayo wanadamu hawayawezi. Kwa mfano, nyuki huweza kuona mionzi isiyoonekana kwa macho ya binadamu na pia huweza kuliona jua katika mchana uliogubikwa na wingu zito. Na bundi naye huweza kumuona panya usiku wa manane kwenye rundo la makorokoro au magunia ya nafaka yaliyoshonana.
Ibilisi na Jini
Ibilisi ambaye MwenyeziMungu kamtaja mara nyingi ndani ya Qur'an, anatokea katika ulimwengu wa Majini. Mwanzoni alipoumbwa, Ibilisi alikuwa akimuabudu MwenyeziMungu. Katika maisha yake ya awali aliishi pamoja na Malaika mbinguni. Akaingia mpaka Peponi.
Lakini baada ya hapo akamuasi Mungu pale alipokataa kumsujudia Adam kutokana na majivuno, kiburi na husuda. Kwa sababu hiyo, MwenyeziMungu akamfukuzilia mbali kabisa na Rehema Zake.
Kwa lugha ya Kiarabu, Ibilisi ni jina la jumla kwa muasi yeyote aliyetakabari. Jina hili hutumika zaidi kwa yule ibililisi mwenyewe kwa sababu yeye ndiye aliyetakari na kumuasi Mungu. Katika Surati Nisaa ya Qur'an, aya ya 76, Ibilisi katajwa kwa jina la Twaghuuti. Kwa mujibu wa kitabu kiitwacho "Ibilisi" kilichoandikwa na Bw. Aqad, Twaqhuut ndilo jina mashuhuri kwa watu wengi duniani.
Kiumbe huyu aliyeasi kaitwa jina hili kwa sababu amechupa mipaka kwa kumuasi Mungu na kudiriki kujikweza kama mungu wa kuabudiwa. Kiumbe huyu amekata tamaa ya kupata Rehema za MwenyeziMungu ndio maana Mungu kamwita Ibilisi (ibliis).
Neno Alabalas la Kiarabu maana yake ni yule asiye na kheri kwa nafsi yake. Na neno ublis maana ni aliyekata tamaa na aliyepotea. Wanazuoni wengi wa awali wamesema kuwa kabla ya kumuasi Mungu, kiumbe huyu alikuwa anaitwa azaaziil. Mungu ndiye ajuaye kama hilo ndilo jina sahihi.
Ibilisi ni kiumbe
Mtu anayesoma Qur'an na Hadith za Mtume (saw), anajua kuwa Ibilisi ni mmoja wa viumbe vya MwenyeziMungu ambaye ana akili, ana uwezo wa kuelewa mambo na kadhalika. Hayuko kama wasemavyo baadhi ya watu wasiomjuwa kuwa ni "nguvu ya uovu inayochukua sura ya silika mbaya katika sehemu ya unyama ya mwanadamu, nguvu ambayo humuongoza mtu pale inapokaa mahali pa silika njema ya roho moyoni mwa mtu huyo." (Taz. Dairat al-Maarif al-Haditha, uk. 357).
Asili ya Ibilisi
Tayari tumekwishasema kuwa Ibilisi ni jini. Baadhi ya waandishi wa zamani na wa hivi leo wamepinga jambo hili. Wao wanatoa ushahidi wa tamko la Mungu kwa jamii ya Malaika kuwa wamsujudie Adam:
"Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote isipo kuwa Iblis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri" [2:34]
Wanadai kuwa waliotakiwa kusujudu hapa ni malaika kwa sababu jina lililotumika kwa ujumla wao ni "malaikati", kama kulikuwa na kiumbe mwingine asiyekuwa malaika basi tamko hilo halikumuhusu, kwa hiyo amri ya kusujudu isingemuhusu isipokuwa labda na yeye angetajwa kwa jina lake. Na kama amri ilimuhusu, basi na yeye alikuwa Malaika na huu ndio utaratibu wa kusemeshana.
Katika vitabu vingi vya tafsiri ya Qur'an na vitabu vya historia tunakuta maelezo haya haya kuwa ibilisi alikuwa ni wa jamii ya malaika na kwamba yeye ndiye aliyekuwa mtunzaji wa Pepo au wa mbingu ya chini kabisa. Alikuwa Malaika bora na wa kuheshimika na kadhalika. Katika sherehe yake ya Qur'an, Ibn Kathir kasema hivi:
Visa hivi vimepokewa kwa simulizi kutoka kwa wanazuoni wengi wa zamani. Visa vingi kati ya hivyo vimetokana na Hadith za Kiisraliati (ngano za Wayahudi na Wakristo) ambavyo lazima vichunguzwe kwa undani.
MwenyeziMungu tu ndiye Ajuaye usahihi wa simulizi za aina hii. Vingi ni vya uongo uliodhahiri kwani vinapingana na ukweli tulionao mikononi (Qur'an na Hadith za Mtume). Chochote kilichomo ndani ya Qur'an kinajitosheleza na hatuhitaji kutegemea visa hivyo vya watu wa kale.
Simulizi zao hazikusalimika na mabadiliko, nyongeza na upungufu. Watu hawa wametiya maneno mengi ya uongo katika simulizi zao. Hakukuwa na watu waadilifu miongoni mwao kama wale ilionao jamii ya Waislamu ambao wangeweza kulinda maandiko yao na simulizi zao zisiharibiwe na wakorofi.
Jamii ya Waislamu imekuwa na wanazuoni, wataalamu, Maimamu, Mahafidhi, na watu wachaMungu wa kuweza kuthibisha vipi kati ya hivyo ni zipi simulizi sahihi, ni zipi za kukubaliwa, ni zipi dhaifu, ni zipi za kutupiliwa mbali, ni zipi za kutunga na za uongo.
Waislamu walifahamu ni akina nani wazushi na ni nani waliosimulia visa hivyo bila wao wenyewe kujulikana ambao hawapaswi kuaminiwa kabisa. Hii ni kutokana na nafasi ya Mtume Muhammad na kwamba yeye ndiye muhuri wa Mitume na kiongozi wa walimwengu.
Kwa sababu hiyo, mambo ya kughushi na ya kupotosha hayakuweza kubambikizwa kwake na kukubaliwa na Wanazuoni.

Inaendelea ......
 
Mfululizo Wa Mada Ya Majini (3)

(Na Prof. Dkt. Sheikh 'Umar Suleiman al-Ashqar)
imefasiriwa na Shaibu H.Kifea
Je, Majini Huoa Na Kuzaa? Je, Wanaweza Kuoana na Binadamu?
Kuhusiana na ushahidi wao kuwa MwenyeziMungu alimtowa Ibilisi katika jamii ya Malaika, huu si ushahidi wa hakika. Maelezo hayo yanaweza kuwa ya mkumbo au jumla-jumla tu yaani kwa vile fulani na fulani wameyakubali.
Katika Qur'an, MwenyeziMungu ameeleza bayana kuwa Ibili alikuwa ni mmoja wa majini.: "Na (kumbukeni) tulipowaambia Malaika, msujudieni Adamu. Basi wakasujudu isipokuwa Ibilisi, yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake..." (18:50)
Aidha imethibitika katika Hadith sahihi kwamba majini hawafanani na malaika wala binadamu. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)kasema: "Malaika wameumbwa kwa Nuru, majini wameumbwa kwa moto na Adam aliumbwa kwa udongo." (Taz.sahih Muslim)
Al-Hassan al-Basri kasema: Ibilisi hakutokana na malaika hata kwa (nukta ya) kubwenza jicho (hata kidogo). (Taz. Ibn Kathiir, al-bidaaya wa al-Nihaaya Juz. 1, uk.79)
Naye Ibn Taimiya kasema, "Kwa kweli, Ibilisi alikuwa na haiba ya Malaika alipotoka kwa malaika lakini hakuwa na asili ya malaika na wala hakuwa na umbile sawa na malaika. (Taz. Majmu al-Fatawa, Juz. 4, uk. 235 na 346).

Je Ibilisi ndiye chimbuko la majini wote?
Hatuna matini yenye maelezo ya wazi kuwa Ibilisi ndiye mzazi wa majini wote. Rai ya Ibn Taimiya ni kwamba Ibilisi ndiye mzazi wa majini wote kama ambavyo Adamu ni mzazi wa wanadamu wote. (Taz.Majmu al-Fatawa, Juz.4, uk. 235 na 346).

Chakula na Kinywaji cha Majini
Majini ambao miongoni mwao wamo mashetani hula na kunywa. Katika Sahihi Bukhari, imenakiliwa Hadith kutoka kwa Abu Huraira kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)alimwambia (yeye Abu huraira) amletee mawe kadhaa ili asitanjie baada ya haja kubwa.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)akamwambia Abu Huraira "usiniletee mifupa au mavumba". Abu Huraira akamuuliza Mtume kwanini kasema asiletewe vitu hivyo huku akivitaja kwa majina.
Mtume akamwambia: "hivyo ni vyakula vya majini. Ulinijia ujumbe (wa majini) kutoka Nasiib. Hawa walikuwa ni majini wazuri kabisa ambao waliniuliza kuhusu vyakula vyao. Nikawaombea kwa Allaah kuwa wasiyapite mavumba au wasiipite mifupa ila wakute kitoweo katika vitu hivyo."
Na imenakiliwa Hadith yenye isinadi sahihi katika Kitabu cha Sunan at-Tirmithi kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)kasema: "msisitanjie mavumba au mifupa kwani hivyo ni vyakula vya ndugu zenu majini". (Taz. Sahih al-Jaami, Juz. 2, uk. 154).
Pia katika kitabu cha Hadith cha Sahihi Muslim imenakiliwa Hadith kutoka kwa Ibn Masud kuwa mjumbe mmoja kutoka jamii ya majini alikwenda kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wakaondoka wote. Huko Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)akawasomea (majini) baadhi ya Aya za Qur'an. Mtume (aliporejea), akawaonesha watu mabaki ya vijinga vya moto vya majini hao. Watu wakamuuliza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)kuhusu chakula chao, naye akawaambia; "Kila mfupa ambao umesomewa jina la Allaah ukiwa na nyama juu yake ni kwa ajili yenu. Na mavumba ni chakula cha wanyama wenu. Kisha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)akasema, "msisitanjie vitu hivyo kwani ni vyakula vya ndugu zenu" (majini).
Aidha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)ametuambia kuwa mashetani wa jamii ya majini hulia mkono wa shoto, na akatutaka sisi tulie mkono tofauti na huo. Katika kitabu chake i cha Hadith mashuhuru kwa jina la Sahih, Bw.Muslim amenakili amenakili Hadith kutoka kwa Ibn Umar kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)kasema:
"Ikiwa mmoja wenu anakula, basi alie mkono wa kulia. Na anapokunywa anywe kwa mkono wa kulia. Kwa hakika, Shetani hula kwa mkono wa kushoto na hunywa kwa mkono huo wa kushoto."
Katika kitabu cha Musnad Ahmad, imenakiliwa Hadith ifuatayo:
"Yeyote anayekula kwa mkono wa kushoto, Shetani hula pamoja naye. Na yeyote anayekunywa kwa mkono wa kushoto, shetani hunywa naye."
Hadith ifuatayo pia imenakiliwa katika kitabu hicho Musnad Ahmad:
"Mtu akilitaja jina la Allaah (Bismillah) pale aingiapo nyumbani mwake na akala chakula humo ndani, Shetani husema, "Hamna pa kulala wala chakula kwangu humu (ndani)'.
Lakini mtu akiingia nyumbani mwake na kupuuzia kulitaja jina la Allaah pale aingiapo, Shetani husema, "nimepata pa kulala kwako." Na asipolitaja jina la Allaah (asiposema Bismillah) anapokula chakula, Shetani husema: "nimepata pa kulala na na chakula." Hadith hii pia imenakiliwa na Muslim. Hadith hizi zipo katika matini sahihi zikithibitisha kuwa mashetani hula na kunywa.
Halikadhalika ni haramu kwa binadamu kula nyama yoyote ambayo haikusopmewa jina la Allaah. Mtume wa Allaah kawaruhusu majini walioamini kula mfupa wowote uliosomewa jina la Allaah. Hawaruhusiwi kula nyama isiyosomewa jina la Allaah. Vitu vyote vinavyoliwa bila kutaja jina la Allaah huwapatia chakula majini yasiyoamini ambao ndio mashetani.
Kwa maneno mengine mashetani hujihalalishia vyakula vyote ambavyo havikusomewa jina la Allaah. Ndiyo maana wanazuoni wengi wakatoa rai kuwa mizoga ya wanyama waliojifia ni chakula cha cha mashetani.
Akisherehesha Aya hii, "Enyi mlioamini! Bila shaka ulevi ulevi na kamari na kuabudiwa asiyekuwa MwenyeziMungu na kutazamia kwa mishare ya kupiga ramli ni uchafu na ni kazi ya shetani. Basi jiepusheni ili mpate kufaulu."(5;90), Ibn Qayyim kasemahivi:
"vinywaji vya kulevya ni vinywaji vya mashetani. Ulevi ndicho kinywani ambacho shatani huwataka washirika wake wanywe, naye hushiriki nao katika kunywa kinywaji hicho, kuchuma dhambi ya kitendo hicho na hatimaye kuadhibiwa.
Ni dhahiri kuwa majini wana maingiliano ya kijinsia. Kuthibitisha hili, baadhi ya wanazuoni hurejea maelezo ya Qur'an kuhusu wanawake wa peponi. MwenyeziMungu anawazungumzia wanawake hao hivi:
"watakuwamo humo wanawake watulizao macho yao, hajawagusa, hapo kabla, binadamu wala jini yeyote." (55:56)
Mwandishi wa Kitabu kiitwacho Lawaami al-Anwaar al-Bahiya kataja Hadith ambayo isinadi yake inahitaji kutazamwa kwa makini kama ni sahihi au la. Hadith hiyo inasema:
"Majini wana watoto kama binadamu walivyo na watoto lakini watoto wa majini ni wengi zaidi. Riwaya hii ilisimuliwa na Abu Haatim pamoja na Abu al-Shaikh ikiwa imepokewa kutoka kwa Qataada."
*Kwa jinsi riwaya hii inavyorejewa, yaonekana kuwa inatoka katika riwaya za Mursal za Qataada. Riwaya hizi husadikiwa kuwa ni dhaifu ila tu labda zihakikishwe kupitia vyanzo vingine. Yasikitisha kuwa toleo jipya la Tafsiri ya Ibn Haatim halikuiendea kwa mapana na marefu Surati Rahman (sura ya 55) ili kuihakiki isinadi nzima.
Baadhi ya watu hudai kuwa majini hawali, hawanywi wala hawajamiiani lakini dai hili halina ukweli kwani tumekwishaonesha ushahidi wa wazi kutoka ndani ya Qur'an na Hadith.
Baadhi ya wanazuoni wana rai yao kuwa wapo majini wa aina mbalimbali ambao baadhi yao hula au kunywa ilihali wengine hawali wala kunywa. Bw. Wahb ibn Munabih kasema, "wapo majini wa aina mbalimbali. Aina ya kwanza ni jini twaharifu ambalo liko kama upepo, jini huyu hali, hanywi, hafi wala hazai watoto.
Na ipo jamii nyingine ya majini ambao hula, hunywa, hujamiiana, huzaana na hufa. Na hawa ndio wale mashetani wa kike, mashetani wa jangwani na kadhalika." Hii ilinakiliwa na Ibn Jarir at Tabari. (Taz. Lawaami al-Anwaar, Juz. 2, uk. 222)
Lakini hayo aliyoyasema Bw. Wahb nayo pia yanahitaji dalili hivyo hayawezi kuwa ushahidi unaojitehemea.
Wanazuoni wengi wamedadisi namna majini wanavyokula; je ni sawa na walavyo binadamu, je nao humeza chakula au wao hupitishia chakula puani na kadhalika? Ni makosa na haiswihi kudadisi mambo haya wala hatuhitajiki kuyajua mambo haya. Hakutujuza mambo haya MwenyeziMungu wala Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
 
Mfululizo Wa Mada Ya Majini (4)


(Na Prof. Dkt. Sheikh Umar Suleiman al-Ashqar)
imefasiriwa na Shaibu H.Kifea
Ndoa Ya Jini Na Binaadamu


WATU wamepata kusikia kuwa mwanaume fulani kaowa Jini au mwanamke fulani kaolewa na Jini au mwanamke fulani kachumbiwa na Jini. Al-Suyuut kataja mikasa mingi ya aina hiyo iliyosimuliwa na watu wa jamii za awali.
Aidha wanazuoni nao wamebainisha kuwa zipo ndowa baina ya binadamu na majini. Mwanazuoni mashuhuri Ibn Taimiyya kasema, "Binadamu na Majini wamepata kufunga ndowa na kupata watoto. Jambo hili limetokea mara nyingi na linafahamika kabisa." (Taz. Majmuu Fatawa, Juz. 19, uk. 39)
Izingatiwe kuwa hakuna rejea ya moja kwa moja ya jambo hili. Mtume (saw) hakuwahi kabisa kuzungumzia jambo hili. Simulizi zinazohusu mikasa hiyo kutoka kwa Maulamaa waliokuja katika zama za baadae, haziwezi kusadikika kama dalili za jambo hili.
Isitoshe hailekei kama kuna ushahidi wa kuwepo kwa watoto wenye ubadhi wa sifa za kibinadamu na ubadhi wa sifa za kijini (chotara wa jini na binadamu). Hivi leo katika falme za Kiarabu kuna ukoo unaodai kuwa umetokana na mwanamke wa kijini. Hata hivyo, maumbile ya watu hao hayatofautiani na binadamu wengine. Hivyo, ni vigumu kuthibitisha dai hili.
Hata ikijaaliwa kuwa zipo ndowa hizo lakini wanazuoni wengi wameonesha kutozipendelea. Wanazuoni kama vile al-Hassan, Qataada, al-Hukum na Ishaaq wao wamefahamika kuwa hawakulipendelea jambo hilo.
Imam Malik pamoja na kwamba hakuweza kupata aya ya kuharamisha ndowa hiyo lakini yeye binafsi hakupendelea itokee na alitoa hoja hii: "sipendelei kwani litakuwa tatizo tukimuona mwanamke mjamzito na kumuuliza, "mume wako nani?" Naye atajibu ‘jini moja hivi.' Uovu mwingi utatokea kwa jambo hili. (Kwamba wanawake watazini na wakipata mimba, wasingizie majini).
Kundi fulani la watu linatowa rai kuwa hairuhusiwi kuoana na majini. Kwa Rehema Zake, MwenyeziMungu Katuumbia wake wa jinsi yetu ya kibinadamu. Anasema katika Qur'an:
"Na katika Ishara Zake ni kuwa Amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mpate utulivu kwao, naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu." (32:21).
Iwapo kungetokea ndoa hiyo, ingekuwa vigumu kupata utulivu na mapenzi hayo baina ya wanandowa kutokana na tofauti ya jinsi zao. Lengo na hekima ya ndowa haingeweza kufikiwa kwani utulivu na mapenzi yaliyotajwa na MwenyeziMungu hayangewezekana.
Vyovyote iwavyo, ijapokuwa watu wanadai kuwa ndowa hizo zinatokea hata hivi sasa na zimetokea zamani lakini kutokea kwake ni jambo la nadra na ni kioja. Isitoshe mtu anayefunga ndoa hiyo lazima atafute hukumu ya Uislamu kuhusiana na ndoa hiyo. Labda lingekuwa shauri jingine kama yule anayefunga ndowa hiyo, kwa kujitambua, katenzwa nguvu na hana namna ya kuliepuka jambo hilo.
Kinachoipa uwezekano ndoa ya Jini na Binadamu ni kule kutajwa kwa wanawake wa peponi katika Qur'an. MwenyeziMngu Anawaelezea wanawake hao hivi
"watakuwamo humo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa binadamu wala jini yeyote kabla (ya hao waume wao). (55:56).
Aya hiyo inabainisha kuwa viumbe wote wawili Binadamu na Majini wanastahili kuozwa wanawake hao.
Je mashetani nao hufa?
Hapana shaka kuwa majini na mashetani nao hufa. Aya ifuwatayo ya Qur'an inawahusu wote:
"Kila kilichoko juu (ya ardhi na mbingu) kitatoweka. Inabaki Dhati ya Mola wako Mwenye utukufu na hishima. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu mnayoikanusha?" (55:26-2.
Katika Sahihi Bukhari imenakiliwa Hadith kutoka kwa Ibn Abbas kuwa Mtume[Salallahu alaihi wasalam] alikuwa akisema: "najikinga kwa Utukufu Wako ewe Mpweke ambaye hakuna mungu mwingine ila Wewe Mmoja usiyekufa ambapo majini na wanadamu hufa."
Kuhusiana na kitambo cha maisha yao, sisi hatujuwi mengi isipokuwa yale aliyotuambia MwenyeziMungu kuhusiana na Ibilisi aliyelaaniwa ambaye amepewa muda na uhai hadi Siku ya Hesabu. MwenyeziMungu Anasema:
Na hakika Tulikuumbeni kisha Tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika" ‘Msujudieni Adamu." Basi wakasujudu isipokuwa Ibilisi hakuwa miongoni mwa waliosujudu. MwenyeziMungu Akasema: "Nini kilichokuzuiya kumsujudia nilipokuamrisha?' Akasema, "Mimi ni bora kuliko yeye. (Mimi) umeniumba kwa moto naye umemuumba kwa udongo". Akasema (MwenyeziMungu), "Basi shuka huko, haikufalii kufanya kiburi humo. (Haya) toka; hakika wewe ni miongoni mwa wadhalilifu." Akasema: "Nipe muda (nisife) mpaka siku watakapofufuliwa viumbe" (MwenyeziMungu) Akasema: "Utakuwa miongoni mwa waliopewa muda." (7:11-15)
Kuhusiana na majini au mashetani wengine, hatujuwi muda wao wa kuishi. Ila tunajuwa kuwa muda wao wa kuishi ni mrefu zaidi kuliko ule wa wanadamu
Ushahidi zaidi kuwa viumbe hawa hufa ni kwamba Khaalid ibn Waliid alimuua shetani wa al-uza (mti ambao Waarabu walikuwa wakiuabudiya) na hapo Sahaba huyo akamuua Jini aliyejitokeza kwa sura ya nyoka kama itakavyokuja kuelezwa huko mbele.

Makazi ya majini, mahali na muda wanaoweza kukutikana
Majini wanaishi hapahapa duniani wanapoishi binadamu. Wengi miongoni mwao huweza kukutikana kwenye magofu na maeneo makongwe, na pia hukutikana mahali palipo na najisi nyingi kama vile Toilet . Pia wanakutikana kwenye maficho ya bangi, kwenye mazizi ya ngamia na Makaburini.
Ndiyo sababu Mwanazuoni Ibn Taimiyya kasema kuwa wale waliokaribu na Ibilisi mara nyingi hukaa kwenye maeneo hayo. Kuna Hadith zisemazo kuwa mtu asisalie Toilet kwa sababu ya najisi iliyomo humo na kwa sababu hayo ni makazi ya shetani na asisalie makaburini kwani jambo hili hupelekea kwenye ushirikina na pia makaburini ni makazi ya Mashetani.
Aidha Mashetani wengi wa kijini wapo kwenye maeneo yenye maasi kama vile sokoni. Mtume (Salallahu alaihi wasalam) alimpa Sahaba mmoja nasaha hizi:
"Ukiweza, basi usiwe mtu wa kwanza kuingia sokoni. Na usiwe mtu wa mwisho kuondoka sokoni. Kwani hayo ni makazi ya Ibilisi na humo ndimo anamosimamisha bendera yake." Hadith hii imenakiliwa katika Sahih Muslim.
Mashetani pia huishi ndani ya majumba wanayoishi watu. Mtu anaweza kuwazuwia wasiingie ndani ya nyumba au anaweza kuwafukuza ndani kwa kulitaja Jina la MwenyeziMungu (Bismillah), kumdhukuru au kumtaja Allah, kusoma Qur'an hasa hasa "Ayatu Qursiyu ya Surati Baqara (ambayo ni aya ya 255 ya sura hiyo).
Mtume (swalallahu alaihi wasalam] kasema kuwa mashetani huzagaa na kurandaranda kwa wingi pale giza linapoanza kuingia. Kwa sababu hii, amewanasihi Waislamu kuwarudisha ndani watoto wao katika muda huo. Haya yamesemwa katika Hadith iliyonakiliwa na Bukhari na Muslim.
Mashetani huikimbia Adhana na hushindwa kustahamili kuisikiliza. Katika Mwezi wa Ramadhani Mashetani hufungwa minyororo (pingu).
Mahali wanapopenda kukaa au kukusanyika Mashetani
Mashetani hupendelea kukaa baina ya kivulini na juani (katikati ya kivuli na mwanga wa jua. Kwa sababu hiyo Mtume(swalallahu alaihi wasalam] kawakataza Waislamu kukaa sehemu hizo. Hadith hii sahihi imenakiliwa katika vitabu vya Sunan na vitabu vingine.
Wanyama wa Majini
Katika Hadith ya Ibn Masud iliyonakiliwa katika Sahih Muslim, Majini walimuuliza Mtume (swalallahu alaihi wasalam] kuhusu chakula chao. Akawaambia, "kila mfupa uliosomewa Jina la Allah ni chakula chenu. Muda uleule mfupa utakapofika mikononi mwenu utavikwa nyama. Na kinyesi cha (ngamia) ni chakula cha wanyama wenu." Hivyo, Mtume (swalallahu alaihi wasalam) katujuza kuwa majini wanao wanyama wao ambao chakula chao ni kinyesi cha wanyama wa binadamu.
Wanyama maalum ambao mashetani huandamana nao
Mashetani huandamana na wanyama kadha wa kadha kama vile ngamia. Mtume (Salallahu alaihi wasalam) kasema:

"Kwa hakika ngamia kaumbwa kutokana na mashetani. Na nyuma ya kila ngamia yupo shetani." (Hadith hii ilinakiliwa na Said ibn Mansuur katika kitabu chake Sunan ikiwa na isinadi ya Mursal hasan. Taz. Sahih al-Jaami, Juz. 2, uk. 25.)
Kwa sababu hiyo, Mtume (swalallahu alaihi wasalam) katukataza kusalia kwenye mazizi ya ngamiya. Imenakiliwa Hadith katika Vitabu vya Musnad Ahmad na Sunan Abu Dawud kuwa Mtume (Salallahu alaihi wasalam) kasema:
"Msisalie katika mazizi ya ngamia, kwani wanatokana na mashetani. Ila salieni kwenye machungio ya kondoo kwani wana bar-ka". (Mfasiri hakukuta kauli hizi mbili kwa pamoja katika matini. Bali Mtume (Salallahu alaihi wasalam)kama alivyonukuliwa katika vitabu vilivyorejewa, aliulizwa swali juu ya kusalia kwenye mazizi ya ngamia na katika machungio ya kondoo na akajibu kila swali kwa nyakati tofauti. Allah ndiye Mjuzi wa yote.)
katika Kitabu chake, Sunan, Ibn Majah kanakili Hadith yenye isinadi sahihi kuwa Mtume kasema:
"Msisalie mahali wanapopumzikia ngamia (yaani pale waendapo baada ya kunyweshwa maji, kwani wao wameumbwa kutokana na mashetani." Hadith hii inakanusha madai ya wale wanaosema kuwa sababu ya kukatazwa kusalia kwenye mazizi ya ngamia ni kuwa mkojo na kinyesi chao ni najisi. Ukweli ni kuwa mkojo na kinyesi cha mnyama yeyote yule anayesadikika kuwa ni halali kuliwa hakihesabiwi kuwa ni najisi.

Inaendelea ..../5
 
Mfululizo Wa Mada Ya Majini (5),


(Na Prof. Dkt. Sheikh Umar Suleiman al-Ashqar)
imefasiriwa na Shaibu H.Kifea
Wajihi Wa Shetani unatisha! Ana Pembe!
Shetani ana wajihi wa kuchukiza sana. Hili ni jambo linalokubalika kabisa akilini. MwenyeziMungu Anavifananisha vichwa vya Mashetani na matawi ya Mzaqqum (mti wa Motoni). Anasema:
"Je, karibisho la namna hii silo bora au kupata mti wa zakkum? (Mti mchungu kabisa watakaolishwa watu wa Motoni). Kwa yakini sisi tumeufanya ni adhabu ya madhalimu. Hakika huo ni mti (unaoota) katikati ya Jahanamu. (Panda za) Matunda yake (zinatisha) kama kwamba ni vichwa vya mashetani". (37:62-65).
Wakristo wa zama za kati walikuwa wakimchora shetani kwa picha ya mtu mweusi mwenye ndevu moja ya mshale, nyusi za wima, mdomo unaotoa miale ya moto, mapembe, kwato na mkiya. (Taz. Dairat al-Maarif al-Haditha, uk. 357).
Shetani ana mapembe mawili

Katika Sahihi Muslim, imenakiliwa Hadith kutoka kwa Ibn Umar kuwa Mtume (Salallahu alaihi wasalam) kasema: "Msipendelee kusali wakati jua linapochomoza au wakati linapozama. Kwa hakika linachomozea (na kuzamia) katikati ya mapembe mawili ya shetani". Pia imenakiliwa Hadith katika Bukhari na Muslim kwamba Mtume [Salallahu alaihi wasalam) kasema:
"Iwapo juwa linazama basi acha kusali hadi litoweke kabisa. Na msikawize sala zenu hadi jua linapochomoza au linapozama. Kwani kwa hakika linazamia na kuchomozea katikati ya mapembe mawili ya shetani".
Hadith hizi zinawarudi washirikina miongoni mwa Waarabu ambao walikuwa na kawaida ya kuliabudia jua na wakawa wanalisujudia pale lilipokuwa linachomoza au kuzama. Kwa sababu hiyo, shetani hujiimarisha katika njia hiyo ili ibada yao ielekee kwake.
Mtume (Salallahu alaihi wasalam) ametukataza kusali nyakati hizo. Kwa kweli, rai sahihi ni kwamba sala, katika nyakati hizo, inaruhusiwa iwapo kuna sababu fulani ya kufanya hivyo, kama vile sala ya kuingilia msikitini. Lakini hairuhusiwi ikiwa hakuna sababu hiyo ya kusali Sala hiyo ya Sunna.
Maana ya maneno haya ya Mtume (Salallahu alaihi wasalam) ni kuwa mtu asikusudie kusali katika nyakati hizo.
Na miongoni mwa riwaya nyingine ambazo zinataja pembe la shetani ni hii ambayo imenakiliwa katika Sahih ya Bukhari: Ibn Umar kasimulia kuwa alimuona Mtume (Salallahu alaihi wasalam) akinyoosha kidole mashariki na kusema:
"Kwa hakika fitna itakuja kutoka huku, maangamizi yatatokea huku ambako pembe la shetani huchomozea".

Uwezo na Nguvu za Jini
MwenyeziMungu Amewajaalia majini uwezo na kipawa ambacho Hakuwapa wanadamu. Allah ametufahamisha baadhi ya vipawa vyao ikiwa ni pamoja na kasi ya mwendo.
Mmoja wa majini alimuahidi nabii Suleiman kuwa angeweza kukileta Jerusalem kiti cha Malkia wa Sheba kwa muda mfupi mno hata kabla mtu hajaweza kuinuka mahala alipokaa. Lakini yule aliyepewa ilimu ya Kitabu akasema, "Mimi nitakileta hata kabla hujabwenza jicho".
MwenyeziMungu amelielezea tukio hili katika aya zifuwatazo:
"Mjasiri mmoja wa majini akasema, Mimi nitakuletea kabla hujainuka mahali pako hapo na mimi bila shaka ninazo nguvu za hayo (na) ni mwaminifu." Akasema yule aliyekuwa na ilimu (kwelikweli) ya Kitabu (cha MwenyeziMungu): "Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako (kufumba na kufumbua)." Basi alipokiona kimewekwa mbele yake, alinena: "hayo ni kwa fadhila za Mola wangu, ili anijaribu nitashukuru au nitakuwa mwizi wa fadhila; Na anayeshukuru, anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake, na anayekufuru, kwa hakika Mola wangu ni Mkwasi (si muhitaji) na Karimu." (27:39-40).
Majini waliwatangulia wanadamu kwenda angani
Majini walikuwa na kawaida ya kupaa hadi mbingu ya chini kusikilizia kwa wakaazi wa huko (Malaika) kama kuna fununu juu ya mambo yatakayotokea wakati ujao. Pale alipotumwa Mtume (Salallahu alaihi wasalam) na ujumbe wake, ulinzi ukaimarishwa mbinguni. Idadi ya walinzi ikaongezeka.
Katika Qur'an, MwenyeziMungu Anawanukuu majini wakisema:
"Nasi tulizigusa mbingu (tulikwenda mbinguni) tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na nyota (zing'arazo). Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini sasa anayetaka kusikiliza atakuta kimondo (kijinga cha moto) kinamvizia." (72:8-9).
Halikadhalika Mtume (Salallahu alaihi wasalam) naye kaelezea jinsi majini walivyojaribu kuiba aya mbinguni. Abu Huraira kasimulia kuwa Mtume (Salallahu alaihi wasalam) alimwambia hivi: "MwenyeziMungu Anapoamuru jambo mbinguni, malaika hutikingishika mbawa kutii kauli yake.
Wanapoondolewa woga nyoyoni husemezana, "Mola wenu kasemaje?" na hupata jibu kuwa alichokisema ni haki, Naye ndiye Aliye juu na Mkuu'. Hapo ndipo wale wanaosikiliza kwa wizi (Majini) nao husikia kauli hii.
Wao wanakuwa hivi: baadhi yao huwa juu ya wengine. Kisha yule anayesikia neno hulipeleka kwa wa chini yake, naye hulipeleka kwa wa chini yake na inakuwa hivyo hivyo hadi pale mmoja wao atakapolipitisha mdomoni mwa mtabiri au mwaguzi.
Mara nyingi kimondo huwa kinampata huyu kabla ya kulifikisha neno hilo (kwa mtabiri) ambaye naye hulichanganya na maneno mia ya uwongo. Hapo watu huuliza, "jamani, fulani si aliwahi kusema neno fulani tarehe fulani (si aliwahi kutabiri)? Mtabiri huyu huaminika kwa sababu ya neno hilo lililosikiwa (na majini) mbinguni". (Imenakiliwa na Bukhari katika Sahih).
Imani za ushirikina katika zama za ujahili
Kwa kuijuwa sababu kwa majini walipopolewa na vimwondo, ikakomeshwa ile imani ya kishirikina waliyokuwa wakiieneza watu wa zama za ujahili. Ibn Abbas kasimulia Hadith iliyotoka kwa sahaba wa Mtume (saw) miongoni mwa Ansar ambaye kasema kuwa usiku mmoja walikuwa pamoja na Mtume (Salallahu alaihi wasalam) na wakaona nyota ya kimondo.
Mtume akawauliza, "mlikuwa mkisemaje kuhusiana na nyota ya kimwondo kama ile katika zama za ujahili?" Wakasema, "MwenyeziMungu na Mtume wake ndio wajuao zaidi. Tulikuwa tukisema kuwa usiku huo (wa nyota ya kimwondo) huzaliwa mtu muhimu au hufa mtu muhimu.
Mtume (Salallahu alaihi wasalam) akasema "(nyota hiyo ya kimondo) haitokei kwa sababu ya kufa na kuzaliwa kwa mtu yeyote yule. Bali MwenyeziMungu Anapoamua jambo, Malaika wanaobeba Kiti cha Enzi huimba kumtukuza kwa Sifa Zake na wale wa mbingu inayofuata nao hufanya hivyo hivyo na wengine halikadhalika hufanya hivyo hivyo hadi mbingu ya chini kabisa.
Kisha wale walio karibu na malaika wanaobeba Kiti cha Enzi huwauliza hao wanaobeba Kiti hicho, "kasema nini Mola wenu?" Hapo huambiwa kile ambacho ameamrisha MwenyeziMungu.
Kisha na wao hupeleka habari hiyo mbingu inayofuata na mlolongo huwa hivyo hivyo hadi habari hiyo ifike mbingu ya chini kabisa. Hapo sasa majini nao huisikiliza na kuipeleka kwa watumwa wao. Malaika wanapowafuma, huwashambulia kwa vimondo.
Laiti Majini wangelikuwa wanasimulia vile vile habari nzima waliyoisikia, basi wangelikuwa wakweli. Lakini, kinyume chake, wao huichanganya na kuitia chumvi. (Hadith imenakiliwa katika Sahih Muslim)
Majini wana ujuzi wa kujenga majengo na wanajua ufundi mwingine
MwenyeziMungu Ametufahamisha kuwa majini waliokuwa wametiishwa katika ufalme wa Suleiman walifanya mambo mengi ya ajabu ambayo ni uthibitisho wa uwezo wao wa kimwili, akili na maarifa yao. Katika Qur'an, MwenyeziMungu Anasema:
"Na katika majini (kulikuwa na wale) waliofanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake. Na kila anayejitenga na amri Yetu miongoni mwao Tunamuonjesha adhabu ya Moto uwakao. Walikuwa wakimfanyia alipendalo, kama ngome na masanamu na mabunguu (madaste) makubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa sana yasiyoondolewa mahala pake (34:12-13)
Huenda majini pia walikuwa na mawasiliano ya masafa na masafa mithili ya Radio na Televisheni. Ibn Taymia kaeleza kuwa, mmoja wa Masheikh waliopata kuwasiliana na majini alimfahamisha kuwa majini waliwaonesha wao kitu kilichokuwa kinameta-meta kama maji au kioo. Na ndani ya chombo hicho waliwaonesha kila walichokitaka kuhusiana na habari.
Mtu aliyemsimulia jambo hili Ibn Taimiya kasema kuwa majini hao wakaweza kuyaleta maelezo ya yule aliyekuwa anaomba msaada wangu, nami nikamjibu ambapo maelezo yangu wakayanasa kuyarejesha kwake." (Taz. Majmu Fatawa, Juz. 11, uk. 309)
Pengine-labda majini waliweza kuvumbua teknolojia ya Radio na Televisheni muda mrefu huko nyuma.

Uwezo wao wa kujitokeza kwa maumbile mbalimbali

Majini wana uwezo wa kujitokeza kwa maumbile ya wanadamu au wanyama. Katika Vita ya Badri, shetani wa kijini aliwatokea washirikina kwa umbile la Suraaqa ibn Malik na kuwaahidi msaada na ushindi katika vita hiyo.
MwenyeziMungu aliteremsha wahayi kuhusiana na tukio hili:
"Na (kumbukeni) Shetani alipowapambia vitendo vyao na kusema: "Leo hakuna watu wa kukushindeni na mimi ni mlinzi wenu," (8:48).
Lakini pale majeshi yalipokutana na yeye shetani kuona malaika wakiteremka kutoka mbinguni, akatimua mbio. Aya hiyo inaendelea: "Lakini yalipoonana (yalipokutana) majeshi mawili, (Shetani) alirudi nyuma na kusema: "Mimi si pamoja nanyi, mimi naona msioyaona nyinyi, mimi ninamuogopa MwenyezziMungu; na MwenyeziMungu ni Mkali wa kuadhibu."

Inaendelea …./6
 
Mfululizo Wa Mada Ya Majini (6)


(Na Prof. Dkt. Sheikh Umar Suleiman al-Ashqar)
imefasiriwa na Shaibu H.Kifea

Jini huweza kujitokea kwa maumbile mbali mbali

Abu Huraira kasimulia mkasa ufuatao ambao umenakiliwa katika Sahihi Bukhar na vitabu vingine. Swahaba huyu kasema kuwa Mtume (swalallahu alaihi wasalam) aliwahi kumpa kazi ya kusimamia usalama wa mali ya zaka iliyotolewa katika mwezi wa Ramadhani.
Kwa maneno yake Abu Huraira anasimulia, "akanijia mtu mmoja na kuanza kuchukua mafungu ya chakula. Mimi nikamkamata na kumwambia kuwa nitampeleka kwa Mtume wa Allah. Mtu huyo akalalama, "Nina dhiki kubwa na nina watoto wanaonitegemea."
Kwa kutoa sababu hii, basi mimi nikamwachia aende zake. Asubuhi ya kesho yake Mtume (swalallahu alaihi wasalam) akaniuliza, "vipi yule mtu uliyemkamata usiku Abu Huraira?" Mimi nikajibu, ‘Ewe Mtume wa Allah mtu yule alinililia kwa dhiki kubwa aliyonayo na kwa watoto wanaomtegemea, kwa hiyo nikamuonea huruma na kumwacha aende zake.'
Mtume (swalallahu alaihi wasalam) akasema, "kakudanganya huyo na atarudi tena.' Kwa hiyo nikajuwa tu mtu huyo atarudi maadam Mtume (Salallahu alaihi wasalam) kasema hivyo. Nikakaa kumsubiri. Alipokuja, akaanza tena kusombelea mizigo ya chakula.
Nikamkamata tena na kumwambia kuwa nakupeleka kwa Mtume. Lakini aliponisihi, "niachie niende, nina dhiki na watoto wanaonitegemea mie', nikamuonea tena huruma. Asubuhi Mtume (saw) akaniuliza tena, ‘Abu Huraira vipi yule mtu wako uliyemkamata usiku?'
Nikajibu, ‘ewe Mtume wa Allah, kanilalamikia juu ya dhiki kubwa aliyonayo na watoto wanaomtegemea, nami nikamuachia tena aende zake.' Mtume (swalallahu alaihi wasalam) akasema, "kakudanganya huyo na atarudi tena'. Kwa mara nyingine tena nikamsubiria na akaja na kuanza kusomba mizigo ya chakula.
Sasa nikamwambia ‘bwana wee, safari hii nakupeleka kabisa kwa Mtume wa Allah. Hii ni mara ya tatu sasa unatenda kitendo hiki.' Akaniambia, ‘ukiniachia niende, nitakufunza maneno ambayo Mungu atakunufaisha sana kwayo! "Upandapo kitandani mwako kulala, soma Ayatu Qursiyu kuanzia pale, ‘MwenyeiMungu, hakuna mola ila Yeye Mwenye uhai wa Milele' hadi mwisho wa aya.
Ukifanya hivi, atakujia mlinzi kutoka kwa Allah kukukinga na mashetani mpaka asubuhi.' Basi mimi tena nikaamua nimuache tu mtu huyo aende zake. Asubuhi Mtume akaniuliza kwa mara nyingine tena, ''vipi yule mtu wako uliyemkamata usiku?'
Mimi nikajibu, 'alijidai kunifunza maneno ambayo yangeninufaisha mno". Mtume (swalallahu alaihi wasalam) akasema, ‘kasema kweli ingawaje ni muongo. Je wewe unamjua mtu yule ambaye umekuwa ukiongea naye nyakati za usiku mara tatu?'
Mimi nikajibu, hapana. Mtume (swalallahu alaihi wasalam] akasema, "alikuwa shetani yule". Kwa hadith hii, ni dhahiri kuwa shetani huyu wa kijini alijitokeza kwa umbile la kibinadamu.
Majini pia huweza kujitokeza kwa umbile la wanyama kadha wa kadha, mathalani ngamia, punda kihongwe, ng'ombe, mbwa au paka. Lakini hasa hasa, majini hujitokeza kwa umbile la mbwa mweusi.
Mtume (swalallahu alaihi wasalam] kasema kuwa mbwa mweusi alipata kuingilia kati sala yake na akaeleza kuwa mbwa huyo alikuwa ni shetani. Mwanazuoni wa kuaminika Ibn Taimiya naye kasema, "mbwa mweusi ndiye shetani wa mbwa.
Na mara nyingi majini hujitokeza kwa umbile lake. Vile vile majini hujitokeza kwa umbile la paka mweusi (hata hivyo hakuna ushahidi wa Qur'an au Hadith kuwa ni sahihi kusema kuwa majini hujitokeza kwa umbile la paka mweusi. Kauli kama hizi huhitaji kuthibitishwa kwa dailili zilizosahihi).
Rangi nyeusi ndiyo yenye nguvu mno kwa mashetani kushinda rangi nyinginezo, ndani yake kuna nishati ya joto-joto"

Majini ndani ya majumba ya wanadamu
Majini hujitokeza kwa maumbile ya nyoka machoni mwa wanadamu. Ndiyo sababu Mtume (swalallahu alaihi wasalam) amekataza uuwaji holela wa nyoka wanaoonekana ndani ya majumba kwa sababu ya kuchelea kwamba wanaweza kuwa majini waliosilimu.
Katika Sahih bukhari imenakiliwa Hadith kutoka kwa Abu Sa'id al-Khudhri kuwa Mtume (swalallahu alaihi wasalam) kasema, "jamii moja ya majini imesilimu mjini Madina. Kwa hiyo yeyote amuonaye mmoja wa majini hao, ampe tahadhari mara tatu. Kama atajitokeza tena baada ya hapo, basi auwawe kwani huyo lazima atakuwa ni shetani."
Swahaba mmoja wa Mtume (swalallahu alaihi wasalam] aliua nyoka mmoja nyumbani mwake ambapo kitendo hiki kikamletea maafa. Katika kitabu chake, Sahih, Muslim amenakili Hadith kuwa Abu al-Saib alikwenda nyumbani kwa Abu Saiid ambako alimkuta anaswali. Akaa kumsubiri amalize kuswali.
Mara akasikia chakara-chakara kwenye rundo la kuni ambazo zilikuwa pembezoni mwa nyumba. Alipotazama, akaona nyoka. Ilikuwa bado kidogo tu amuue nyoka huyo pale Abu Said alipomuashiria akae chini.
Baada ya kumaliza kuswali, Abu Said akakinyooshea kidole chumba kimoja na kusema, ‘unakiona chumba hiki?' al-Saib akajibu, ‘ndiyo'. Abu Saiid akasema, "basi aliwahi kuwepo mtu mmoja ambaye alikuwa kwenye fungate la harusi, mtu huyu tukaenda kushiriki naye katika vita vya Handaki tukiwa pamoja na Mtume (swalallahu alaihi wasalam]
Bwana huyu alikuwa na kawaida ya kumuomba ruhusa Mtume[swalallahu alaihi wasalam] kwenda kumuona mkewe. akamuhadharisha kuwa aende huko na silaha zake kwani alikuwa akichelea (mashambuzi) ya BanuQuraidha (kutokea upande wa nyuma)
Basi bwana huyo akabeba silaha zake na aliporejea kwa mkewe, akamkuta amesimama baina ya milango miwili ya nyumba. Bwana huyo akapandwa na ghadhabu za wivu na akamjeruhi mkewe kwa mkuki wake.
Mkewe akamwambia aweke kando mishale na kisha aingie ndani aone mwenyewe kile kilichomfanya yeye atoke nje ya nyumba. Bwana huyo akaingia ndani na kukuta bonge la joka kitandani.
Akalichoma mkuki na kulitoboa. Alikikilisana nalo kulitoa nje lakini joka hilo lilikuwa na nguvu kubwa na kumuuma bwana huyo. Hakuna mtu aliyejua ni nani aliyeanza kufa kutokana na purukushani hiyo ya mtu na nyoka.
Watu wakamsimulia Mtume (swalallahu alaihi wasalam] mkasa huu na kumuomba amuombe MwenyeziMungu amuhuishe mtu huyo. Lakini akasema, "Muombeeni maghfira mwenzetu. Hapa Madina kuna majini ambao wamesilimu. Yeyote kati yenu akimuona mmoja wao (ambaye ni nyoka) basi ampe tahadhari ya siku tatu. Ikiwa atatokea tena baada ya hapo basi auwawe kwa sababu ni shetani huyo."
Mambo ya kuzingatia hapa

1. Kanuni hii inayokataza uuaji wa wanyama inahusu nyoka tu na si wanyama wengine.
2. Kanuni hii haijuzu kwa kila nyoka isipokuwa wale tu wanaokutwa ndani ya nyumba. Wale wanaokuwa nje wanaweza kuuliwa.
3. Iwapo mtu atamuona nyoka ndani ya nyumba amsihi kwa maneno sawa na haya, "Nakupia kwa jina la Allah uondoke nyumba hii na uipeleke shari yako mbali nasisi, usipofanya hivyo, tutakuua." Iwapo utamuona tena nyoka huyo baada ya siku tatu, muuwe.
4. Sababu ya nyoka kuuliwa baada ya siku tatu ni hatua ya tahadhari ili kuhakikisha kuwa mtu hamuuwi jini ambaye amesilimu. Kama ni jini huyo basi ataondoka katika nyumba hiyo. Na asipoondoka basi auliwe, kwani, kwa hali hiyo, huyo ni jini-asi ambaye anastahili kuuliwa kutokana na madhara anayoweza kuyaleta kwa wakaazi wa nyumba hiyo.
5. Kuna aina moja ya nyoka waonekanao majumbani ambao, ruhusa maalum imetolewa kuwauwa bila kuwasihi waondoke. Katika Sahihi Bukhari, imenakiliwa Hadith kutoka kwa abu Lubaba kuwa Mtume (swalallahu alaihi wasalam) kasema:
"Msiue jini isipokuwa yule mmoja mwenye mistari miwili mgongoni kwani hawa husababisha uzazi wa mtoto njiti na hufifiliza uoni wa macho. Hivyo, wauweni".

Je hukumu hii kuwa nyoka ni majini, ina maana kuwa kila nyoka ni jini au baadhi yao tu?

Mtume (swalallahu alaihi wasalam) kasema, "Nyoka ni aina ya mabadiliko ya umbile la jini kama vile walivyogeuzwa nyani na nguruwe bani-Israili (wana wa Israili)." (Hadith hii ilinakiliwa na at-Tabaraani na Abu ash-Shaikh katika Udhma ikiwa na isinadi sahihi. Taz. Muhammad Nasir al-Din albani, Silsilaat al-Ahadith al-Sahiha, Juz. 3 uk. 103. (Hiyo ndiyo rejea iliyotolewa katika matini ya Kiarabu. Kwa usahihi ni Juz. 4, uk. 439. Aidha al-Albani anaelezea nukta hii muhimu ifuatayo katika uk. 440:
"Juweni kuwa Hadith hii haina maana kuwa nyoka waliopo hivi leo wametokana na umbile la jini, bali, hii ina maana kuwa baadhi ya majini waligeuzwa kuwa nyoka, ni sawa na ilivyotokea kwa wale mayahudi walivyogeuzwa kuwa nyani na nguruwe. Hata hivyo hawakuzaliana kama inavyoelezwa katika Hadith sahihi, ‘kwa hakika Allah hakuwafanyia kizazi viumbe waliogeuzwa maumbile. Kwa hakika nyani na nguruwe walishakuwepo kabla ya hilo."

 
Mfululizo Wa Mada Ya Majini (7)


(Na Prof. Dkt. Sheikh Umar Suleiman al-Ashqar)
imefasiriwa na Shaibu H.Kifea
Shetani humtembea Mwanadamu mithili ya damu itembeavyo kwenye mishipa
Katika Sahih Bukhari na Sahih Muslim imenakiliwa Hadith kuwa Mtume (Salallahu alaihi wasalam) kasema:
"Kwa hakika, Shetani humtembea mwanadamu kama inavyotembea damu." Pia imenakiliwa Hadith katika Sahih hizo mbili kuwa Safiyya bint Hayy, mke wa Mtume (Salallahu alaihi wasalam) kasema, "Mtume wa Allah alikuwa akifanya Itiqaf msikitini na nikamletea kikoi usiku. Nikaongea naye kisha nikainuka kuondoka. Mtume naye akainuka kuongozana nami. Nilikuwa naishi katika nyumba ya Usama ibn Zaid. Wanaume wawili wa Ansar wakatupita. Mtume (Salallahu alaihi wasalam) alipowaona, akawaendea haraka na kusema,'Yule ni Safiyya bint Hayy.' Wakasema, "Subhana-Allah, ewe Mtume wa Allah (sisi hatukuwa na hisia mbaya juu yako).' Mtume (Salallahu alaihi wasalam) akawaambia, "Ibilisi humtembea mtu kama inavyotembea damu. Nilichelea kwamba angepenyeza tuhuma mbaya katika nafsi zenu."'
Udhaifu na upungufu wa majini

Katika baadhi ya mambo, majini na mashetani wana uwezo lakini katika mambo mengine nao wana udhaifu. MwenyeziMungu anasema;
"Hakika hila za Shetani ni dhaifu." (4:76).
Hapa tutataja baadhi ya mambo ambayo MwenyeziMungu na Mtume (Salallahu alaihi wasalam) wametufahamisha.
Meshetani wa kijini hawana uwezo mbele ya Wachamungu
MwenyeziMungu hakumpa Ibilisi uwezo wa kuwashurutisha wanadamu kuuendea upotofu na ukafiri. Katika Qur'an MwenyeziMungu anasema:
"Hakika waja wangu huna mamlaka juu yao. Na Mola wako anatosha kuwa Mlinzi (wao)." (17:65).
Aidha MwenyeziMungu anasema:
"Na bila shaka Ibilisi alisadikisha dhana yake juu yao, nao wakamfuata isipokuwa kundi la walioamini (kwelikweli). Na yeye hakuwa na mamlaka yoyote juu yao, ila kwa sababu Tudhihirishe nani mwenye kuamini Akhera na nani anayetilia shaka.." (34:20-21).
Maanake ni kwamba Shetani hana namna ya kuwahadaa ima kwa njia ya ishara au kwa nguvu yoyote ile. Hata Ibilisi mwenyewe analitambua hili kama inavyosema aya hii ya Qur'an:
"(Ibilisi) akasema, ‘Mola wangu! Kwa sababu umenihukumu kupotea basi nitawapambia (upotofu) katika ardhi na nitawapoteza wote isipokuwa wale waja wako waliosafika kweli kweli." (15:39-40).
Nguvu yake ya ushawishi huwahadaa wale watu na majini wanaoridhia mambo yake na wale wanaohiari wenyewe kumtii na kumfuata. MwenyeziMungu anasema:
"hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao isipokuwa wale wenye kukufuata (kwa hiyari yao) katika hao wapotevu." (15:42).
Siku ya kufufuliwa viumbe, Ibilisi atawaambia wale waliomfuata katika upotevu na ufisadi;
"Na Shetani atasema itakapokatwa hukumu (ya wema kwenda Peponi na wabaya kwenda Motoni; atawaambia wale waasi watakaomng'ang'ania): ‘MwenyeziMungu alikuahidini ahadi ya kweli (na leo ameitimiza) nami nilikuahidini; lakini sikukutimizieni. Wala sikuwa na mamlaka juu yenu (ya kukulazimisheni kunifuata) isipokuwa nilikuiteni tu, nanyi mkaniitika. Basi msinilaumu bali jilaumuni wenyewe; siwezi kukusaidieni, wala nyinyi hamuwezi kunisaidia...." (14:22).
Aya nyingine ya Qur'an inasema
Nguvu zake (shetani) ni juu ya wale wanaomfanya rafiki (na kumfuata), na juu ya wale wanaomshirikisha MwenyeziMungu" (16:100).
Nguvu za shetani ni uchochezi na upotoshaji. Huwachochea na kuwazuzua hadi kuwapeleka kwenye ukafiri na ushirikina. Anawaandama mpaka waingie huko. Na katu hawaachii. MwenyeziMungu anasema:
"Je! Huoni ya kwamba Tumewatuma mashetani juu ya makafiri wanawachochea (kufanya mabaya)? (19:83).
Uwezo alionao shetani juu ya watu na majini wanaomfuata si wa ishara wala hoja bali kwa sababu tu mambo anayowaitia yanaendana na matashi na matamanio yao. Watu hawa wamehujumu wenyewe nafsi zao kwa kumruhusu adui yao mkubwa, Shetani awe rafiki yao na bwana mkubwa wao.
Yote haya ni kwa sababu wanakubaliana na yale anayoyataka kwao. Wanapomnyooshea mikono, huwa wafungwa wake, hii ikiwa ni aina ya adhabu kwa matendo yao wenyewe.
MwenyeziMungu hakumpa Ibilisi mamlaka juu ya mja wake yeyote yule hadi pale mja mwenyewe alipomfungulia njia shetani kwa kumtii na kumshirikisha na MwenyeziMungu. Hapo ndipo MwenyeiMungu anapoacha Shetani amtawale mja na kuwa na mamlaka juu ya yake.
Shetani huwa na nguvu kwa waumini wanaotenda dhambi
Hadith moja inasema, "MwenyeziMungu huwa pamoja na hakimu maadam tu hafanyi dhuluma. Akifanya dhuluma, MwenyeziMungu hujitenga naye na kumuweka shetani pamoja naye." (Hadith hii imenakiliwa na al-Hakim na al-Baihaqi kwa isinadi ya hasan. Taz al-Albani, sahih al-Jaami, juz. 2 uk. 130)
Abu al-Faraj ibn al-Jauzi amesimulia kisa cha aina yake kutoka kwa Al-Hassan al-Basri. Kisa hiki, kutegemeana na usahihi wake, kinaonesha uwezo alionao binadamu kumshinda shetani pale anapokuwa mkweli kwa MwenyeziMungu na anapokuwa na Ikhilasi katika dini yake. Pia Hadith hii inaonesha kuwa shetani hupata nafasi pale mtu anapopotoka.
Al-Hasan al-Basri kasimulia kuwa, kulikuwa na mti mmoja uliokuwa ukiabudiwa badala ya MwenyeziMungu. Bwana mmoja akaamua aukate mti huo. Pale alipokuwa njiani kwenda kuukata mti huo kwa ghadhabu za kutafuta radhi za Allah, akakutana na Ibilisi akiwa katika umbile la binadamu.
Ibilisi akamuuliza mtu huyo, ""Kitu gani unachopanga kufanya?" Bwana huyo akajibu, "nakwenda kuukata ule mti unaoabudiwa badala ya MwenyeziMungu." Ibilisi akasema, " Kama wewe huuabudii, unakudhuru nini wengine wanapomuabudia?"
Mtu huyo akajibu, "mimi nitaukata tu". Ibilisi akamwambia, "Je unataka kitu kizuri zaidi ya hicho? Usiukate mti huo, utapata dinari mbili kila asubuhi chini ya mto wako wa kulalia." Mtu huyo akauliza, " zitatoka wapi (hizo dinari)?"
Ibilisi akasema, "mimi nitakupatia". Bwana huyo akarejea kwake na asubuhi iliyofuata, akakuta dinari mbili chini ya mto wake." Asubuhi iliyofuata akakuta tena dinari mbili chini ya mto wake.
Lakini asubuhi ya kesho yake hakukuta kitu. Akafazaika na kutoka kwenda kuukata mti huo. Kwa mara nyingine Ibilisi akamtokea katika umbile lilelile la binadamu. Ibilisi akauliza, "unataka kufanya nini?"
Bwana huyo akajibu, "nataka kuukata ule mti unaoabudiwa badala ya MwenyeziMungu." Ibilisi akasema, "unasema uongo". Hakuna njia kwako ya kuweza kuukata mti huo."
Mtu huyo akatoka hapo kwenda kuukata mti huo. Ardhi ikammeza na kumkaba hadi akakaribia kuuawa. Ibilisi akauliza, "hivi, wewe unajua mimi ni nani? Mimi ndiye Ibilisi. Nilikutana nawe kwa mara ya kwanza ulipokuwa na hasira za kutafuta radhi za Allah ambapo mimi sikuwa na uwezo juu yako.
Nikakudanganya kwa dinari mbili nawe ukaacha kile ulichokuwa umenuia kukifanya (kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah). Lakini safari hii umekuja kwa sababu ya hasira tu za kukosa dinari mbili, nami ndiyo hivyo nimepata mamlaka juu yako". (Taz. Ibn al-Jauzi, Talbiis Ibliis, uk.43).
(Mwandishi wa Kitabu hiki, al-Ashqar kadokeza kuwa usahihi wa kisa hiki unahitaji kuthibitishwa. Yaelekea zaidi kuwa hiki ni kisa cha Kiisrailiyati au visa vya Wayahudi na Wakristo. Al-Ashqar kasema kuwa kisa hiki kinabainisha namna mchaMungu anavyoweza kumshinda Ibilisi. Haina maana kwamba kinaonesha kuwa mtu huyo aliyedhamiria kuukata mti kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah alishindwa kuishinda hila ya shetani dhidi yake. Allah Ndiye Mjuzi wa Yote).
Vilevile MwenyeziMungu ametufahamisha katika Kitabu chake kuwa mtu mmoja alipewa Aya za MwenyeziMungu na akazifahamu lakini baada ya hapo akazitelekeza zote na MwenyeziMungu akamuacha shetani amtawale. Shetani akamwandama na kumpoteza na matokeo yake akawa fundisho kwa wengine na akawa hadithi ya kusimuliwa. MwenyeziMungu anasema;
"Na wasomee habari za wale tuliowapa Aya zetu, kisha wakajivuna nazo (wasizifuate). Na shetani akawaandama, wakawa miongoni mwa waliopotea. Na kama tungelitaka, tungewanyanyua kwazo lakini wao waligandamana na dunia na wakafuata matamanio yao. Basi hali yao ni kama hali ya mbwa, ukimpigia kelele anahema, na ukimuacha pia huhema. Hiyo ndiyo hali ya watu waliozikadhibisha aya zetu. Basi simulia hadithi huenda wakatafakari (7:75-76).
Ni dhahiri kuwa kisa hiki cha mfano kinamuhusu mtu anayeujua ukweli na kuukataa kama Mayahudi ambao walimjua Mtume Muhammad (Salallahu alaihi wasalam) kuwa alikuwa Mtume wa kweli wa Mwenyezi lakini wakamkataa.
Baadhi ya watu wanasema kuwa aya hiyo inamzungumzia Balaam ibn Bauura ambaye alikuwa mchaMungu na baadae akawa kafiri. Wengine wanasema kuwa Aya hiyo inamzungumzia Umayya ibn Abu as-Salit ambaye alimuabudu Allah katika zama za ujahili na akakutana na Mtume lakini akakataa kumuamini kutokana na husuda. Yeye alikuwa na matarajio kuwa ndiye angetumwa kuwa Mtume. Hatuna matini sahihi inayofahamisha kwa uwazi ni nani hasa aliyezungumziwa na aya hii.
‘Kupokea Aya za MwenyeziMungu na kisha usiziamini' ni maelezo juu ya mtu anayefanana kabisa na Ibilisi. Hii ni kwa sababu Ibilisi aligeuka kuwa kafiri baada ya kuujuwa na kutambuwa ukweli wazi wazi. Hili ndilo jambo miongoni mwa mambo ambayo Mtume (Salallahu alaihi wasalam) aliyachelea zaidi kwa umma wake.
Al-Hafidh Abu Yala kanakili Hadith kutoka kwa Hudhaifa bin al-Yaman kuwa Mtume wa MwenyeziMungu kasema: "katika mambo ninayoyahofia kwenu ni mtu kusoma Qur'an hadi ukaona utukufu wake kwake. Vazi lake likawa Uislamu na akalivaa mpaka Allah akapenda na baada ya hapo akalitupa nyuma ya mgongo wake na kumshambulia jirani yake kwa upanga na kumshutumu kwa ushirikina. (Hudhaifa) akauliza, "ewe Mtume wa Allah yupi hapo auliwe, yule anayeshambulia au anayeshambuliwa? Mtume (saw) akasema, "Yule anayeshambulia." (Ibn Kathiir kasema, "isnadi yake ni safi". Taz. Tafsiir ibn Kathiir, juz. 3, uk. 252).
Shetani huwaogopa na kuwakimbia baadhi ya waja wa Allah
Iwapo mja anashikamana barabara na Uislamu, ana Imani ya dhati kabisa moyoni mwake na anachunga mipaka iliyowekwa na MwenyeziMungu basi shetani humgwaya na kumkimbia. Mtume (Salallahu alaihi wasalam) alimwambia hivi Umar,
"Kweli kabisa, kabisa Shetani anakukimbia Umar". (Hii imenakiliwa na Ahmad, at-Tirmidh na ibn Hiban kwa Isinad Sahih. Taz. Al-Albani, Sahih al-Jaami, juz. 2. uk. 74).
Pia Mtume (Salallahu alaihi wasalam) alisema hivi juu ya Umar;
""Kwa hakika nawaona mashetani wa kijini na kibinadamu wakikukimbia Umar". (Imenakiliwa na al-Tirmidh kwa isnadi sahihi. Taz. Sahih al-Jaami, juz. 2, uk. 329).
Lakini jambo hilo si kwa Umar pekee. Yeyote yule mwenye imani thabiti huweza kumshinda shetani,'humbwaga' na ‘kumtweza'
Inaelezwa katika Hadith;
"Muumini humnyongesha (hummiliki au humuendesha) shetani wake kama vile vile mmoja wenu anavyomnyongesha (anavyomuendesha) ngamia wake wakati akisafiri naye." (Hii imenakiliwa na Ahmad. (shuaib al-Arnauut na Adil murshid wanasema kuwa Hadith hii ni dhaifu kwa sababu inamjumuisha Abdullah ibn Lahiya ambaye alikuwa na upungufu wa kumbukumbu. Taz. Shuaib al-Arnauut na adil Murshid, Musnad al-Imaam Ahmad (Beirut: Muasassah al-Risaalah, 1997), juz. 14, uk. 504.
Isinadi pia ina upungufu mwingine ambao hawakuutaja. Upungufu huu ni kwamba yeye huyo huyo Lahiyya alikuwa akikariri tadliis (ambapo akawa anatumia neno la kutatanisha ambalo halikubainisha jinsi alivyopokea Hadith) na katika riwaya hii akatumia neno tata katika Isinadi yake. Ndiyo kusema basi mtu hawezi kupata uhakika ni kwa nani hasa Lahiya aliisikia Hadith hii.
Baada ya kuinakili Hadith hiyo, ibn Kathiir kasema: " (mtu) kumkamata shetani wake maana yake ni kumnyaka utosini na kumtenzanguvu kama anavyofanywa ngamia pale anapotoroka na kukamatwa tena. (Taz. Ibn Kathiir, Al Bidaayatu wa al-Nihaayah, juz. 1,.uk. 73) Sherehe hii ya ibn Kathiir inaegamia kauli isiyo sahihi ya Hadith. Allah ndiye Ajuaye.
Inaweza hata kutokea kuwa Muislamu huweza kuwa na athari kubwa kwa "mshirika" au Swahibu wake kutoka jamii ya majini ambaye huweza kusilimu. Muslim na Ahmad wamenakili Hadith hii kutoka kwa Mtume (Salallahu alaihi wasalam);
"Hakuna hata mmoja kati yenu asiye na "jamaa" (partner) yake kutoka jamii ya majini" Watu wakauliza, "hata wewe Mtume wa Allah?" Mtume (saw) akajibu, "hata mimi isipokuwa tu MwenyeziMungu amenisaidia dhidi yake na hivyo, (jini huyo) huniamrisha kufanya mema tu."
Imam Ahmad naye pia kainakili Hadith hii kutoka kwa Ibn Abbas ikiwa na kauli hii, "lakini MwenyeziMungu amenisaidia dhidi yake na amesilimu". Muslim naye kanakili kutoka kwa Aisha, "lakini Mola wangu kanisaidia dhidi yake mpaka kajisalimisha."


Inaendelea ..../8
 
Mfululizo Wa Mada Ya Majini (8)


(Na Prof. Dkt. Sheikh Umar Suleiman al-Ashqar)
imefasiriwa na Shaibu H.Kifea
Majini walivyotiishwa kumtumikia Suleiman

MwenyeziMungu aliwatiisha Majini na mashetani wote kumtumikia Nabii Suleiman (as) na wakamfamfanyia vile alivyotaka. Alikuwa akiwaadhibu na kuwatia kifungoni wale waliokataa kutii. Katika Qur'an, MwenyeziMungu anasema,
"Na wengine wafungwao minyororo (wanapokhalifu amri zake) (38:38)
Pia Anasema,
"Na kwa Suleiman (Tukatiisha) upepo (uliokwenda) safari yake ya asubuhi (mwendo wa) mwezi mmoja, na safari yake ya jioni (mwendo wa) mwezi mmoja. Na Tukamyeyushia chemchem ya shaba. Na katika Majini (kulikuwa na) waliofanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake. Na kila anayejitenga na Amri yetu miongoni mwao Tunamuonjesha adhabu ya Moto uwakao. (34:12).
Utiifu huu kwa Suleima ni majibu ya dua ambayo Suleiman aliiomba kwa MwenyeziMungu,
"Akasema: "Mola wangu! Nisamehe na Unipe ufalme, asiupate yeyote baada yangu. Bila shaka wewe ndiwe Mpaji (38:35)
Ilikuwa ni dua hii ambayo ilimzuia Mtume Muhammad (saw) kumdhibiti na kumdhihirisha yule jini aliyewahi kumkamata ambaye alimuwekea Mtume kijinga cha moto usoni na kutaka kumtupia. Katika Sahihi Bukhar imenakiliwa Hadith hii kutoka kwa Abu al-Dardai:
"Mtume wa Allah alikuwa amesimama wima (kusali) na akasikiwa akisema, "Najikinga kwa Allah kuepukana nawe", baada ya kusema hivyo, akasema, "Nakulaani kwa laana za Allah."
Mtume alisema maneno haya mara tatu kisha akanyoosha mkono wake akionesha kama anakamata kitu fulani. Alipomaliza kuswali, akaulizwa, "Ewe Mtume wa Alllah, wakati ukiswali, tulikusikia ukisema jambo fulani ambalo hatujawahi kukusikia ukilisema katika Sala, na tukakuona ukikunjua mkono wako".
Mtume (Salallahu alaihi wasalam) akawaambia, "Adui wa Allah, Ibilisi alinijia na kijinga cha moto kuniwekea usoni, ndiyo sababu nikatamka mara tatu, ‘nakulaani kwa laana za MwenyeziMungu'. Halafu nikasema mara tatu, "najikinga kwa Allah kuepukana nawe". Lakini bado hakuondoka. Ndipo nikajaribu kumkamata. Wallah kama si dua ya ndugu yangu Suleiman, angedhibitiwa na kugeuzwa dubwasha la kuchezewa na watoto wa Madina".
Mkasa kama huo ulitokea zaidi ya mara moja. Imam Muslim kanakili Hadith ifuatayo kutoka kwa Abu Huraira; Mtume wa Allah kasema, Afriit (aina ya shetani) wa kijini alichapuka kunivurugia sala usiku wa jana, lakini MwenyeziMungu akanijaalia nguvu za kumshinda, hivyo nikamkamata na kutaka kumfunga kwenye nguzo moja ya msikiti, lakini papo hapo nikakumbuka dua ya ndugu yangu Suleiman, ‘Basi MwenyeziMungu akamgeuza kuwa duni na dhalili"
Wayahudi walimsingizia uwongo Suleiman
Wayahudi na wale wanaowaiga katika kuwatumia majini kwa njia ya sanaa ya uchawi, hudai kuwa Suleiman alitumia uchawi ili kuwatawala majini. Wengi miongoni mwa wanazuoni wa awali wanaeleza kuwa, pale Suleiman alipotawafu, mashetani wakaandika vitabu vya uchawi na kufuru na kuviweka kwenye kiti chake cha ufalme, halafu wakasema, "Suleiman alikuwa akitumia vitabu hivi kuwatawala Majini"
Jambo hili likawafanya watu wengine waseme kuwa kama sanaa hii ya uchawi ni haramu mbona Suleiman aliifanya! MwenyeziMungu akashusha wahai huu,
"Na walipojiwa na Mitume kutoka kwa MwenyeziMungu, mwenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nao, kundi moja miongoni mwa wale waliopewa Kitabu lilitupa kitabu cha MwenyeziMungu nyuma ya migongo yao kama kwamba hawajui (2:101).
Kisha MwenyeziMungu akabainisha kuwa walifuata yale waliyosomewa na mashetani wakati wa uhai wa Suleiman, kisha Allah akamfutia Suleiman tuhuma hizo za uchawi na kufuru
"...na Suleiman hakukufuru bali mashetani ndio waliokufuru, wakiwafundisha watu uchawi ulioteremshwa kwa Malaika wawili, Haruta na Maruta (kakika mji wa) Babil. Wala Malaika hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie, "hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru (2:102)
Majini hawana uwezo wa kufanya miujiza
Majini hawawezi kufanya miujiza kama ile ya Mitume ambayo ni uthibitisho wa ukweli wa mafundisho yao. Baadhi ya Makafiri walidai kuwa Qur'an ilitokana na maandiko ya Shetani, ndipo Allah akashusha wahai huu,
"Wala mashetani hawakuteremka nayo (hii Qur'an kama walivyodai hao makafiri). Wala haiwi kwao (kuiteremsha Qur'an) na hawawezi. Bila shaka wao wamezuliliwa kusikiliza (yanayosemwa na malaika mbinguni) (26:210-212)
MwenyeziMungu anatoa changamoto kwa binadamu na majini wote katika aya ifuatayo:
"Sema: "Hata wakijikusanya watu (wote) na majini ili kuleta mfano wa hii Qur'an basi hawangaliweza kuleta mfano wake hata kama watasaidiana vipi wao kwa wao (17: 88)

Majini hawawezi kutokea kama Nabii katika uoni wa macho au ndoto
Majini hawawezi kujitokeza kwa sura ya Mtume katika upeo wa macho. Tirmidh kanakili Hadith kwa Isinadi sahihi kuwa Mtume (Salallahu alaihi wasalam) kasema,
"Yeyote anayeniona mimi, basi ni mimi, kwani mashetani hawawezi kijitokeza kama mimi." Na katika Sahih zote mbili, kauli ni hii, "yeyote anionaye mimi, basi uoni wake ni sahihi kwani mashetani wa kijini hawawezi kujitokeza kwa umbile langu".
Maana inayodhihiri katika Hadith hii ni kuwa mashetani hawana uwezo wa kujipa umbile la Mtume wa Allah. Lakini hii haina maana kuwa hawawezi kujitokeza kwa maumbile ya watu wengine na kudai utume.
Hivyo, haijuzu kujenga hoja kwa kutumia Hadith hii kuwa kila amuonae yule anayemdhania kuwa ni Mtume katika ndoto basi amemuona kweli Mtume isipokuwa labda mtu huyo anayeonwa atimimize wasifu wa Mtume(Salallahu alaihi wasalam) unaokutikana katika vitabu vya Hadith. Watu wengi hudai kumuona Mtume ndotoni lakini wasifu wanaoutoa unatofautiana na ule ambao umenakiliwa katika vitabu sahihi.
Majini hawewezi kuvuka mipaka waliyowekewa mbinguni
MwenyeziMungu anasema katika Qur'an,
"Enyi jamii ya majini na watu! Kama mtaweza kupenya katika mbingu na ardhi basi penyeni! Hamtapenya ila kwa nguvu zangu. Basi ipi katika neema za Mola wenu mnayoikanusha? Mtaletewa mwako wa moto wa shaba wala nyinyi hamtaweza kujilinda navyo. (55: 33-35)
Licha ya nguvu na kasi yao ya mwendo, hawana uwezo wa kuvuka mipaka hiyo, na wakithubutu, wataangamia.

Majini hawawezi kufungua milango iliyofungwa
kwa jina la Allah
Mtume (Salallahu alaihi wasalam) kasema,
"Fungeni milango na isomeeni jina la Allah, kwani Shetani hushindwa kufungua mlango uliofungwa (kwa kusomewa jina la Allah) (Hadith hii imenakiliwa na Abu Dawd, Ahmad,ibn Hibban na al-Haakim kwa isnadi sahihi. Taz. al-Albani, Sahihi al-Jaami, Juz. 1, uk. 229).
Aidha kuna Hadith hii katika Sahih zote mbili;
"Kwa hakika, Shetani hafungui mlango uliofungwa. Funikeni ndoo zenu na zisomeeni jina la Allah, hata kama ni kuweka kitu kidogo tu humo. Na zimeni taa zenu. (Sahihi al-Jaami, juz. I, uk.270)
"Fungeni milango yenu na funikeni vyombo vyenu na fungeni viriba vyenu vya maji na zimeni taa zenu, kwani Shetani hafungui mlango uliofungwa wala hafunui mfuniko wala hafungui viriba vya maji."

Majini kuwajibika kwa matendo yao
Lengo kuu la kuumbwa kwao:
Majini waliumbwa kwa lengo lilelile waliloumbiwa wanadamu. (al-Dhaariyat 56).
Kwa hiyo, majini wanawajibika kwa matendo yao na wameamrishwa kufanya baadhi ya mambo na kukatazwa kufanya mengine. Yule anayetii, MwenyeziMungu atakuwa radhi naye na ataingia Peponi. Yule asiyetii au anayeasi, hupata adhabu ya Moto wa Jahanamu. Aya na Hadith nyingi zinabainisha jambo hili.
Siku ya hukumu, MwenyeziMungu atawaambia viumbe wote wawili, majini na wanadamu maneno haya: Enyi makundi ya majini na wanadamu ! je hawakuwafikieni mitume miongoni mwenu kukubainishieni aya zangu na kukuonyeni mkusanyiko wa siku yenu hii leo? Watasema tumeshuhudia juu ya nafsi zetu[kuwa sisi wabaya]yaliwadanganya maisha duniya. Nao watajishuhudia wenyewe ya kwamba walikuwa makafiri (al-Anam 130)
Aya hii inathibitisha kuwa maamrisho ya Mungu yamewafikia majini na kwamba wamefikiwa na Mitume waliowaonya na kuwafikishia ujumbe. Aya za kuthibitisha kuwa majini wataadhibiwa katika Moto wa Jahanamu ni nyingi:
"Wako wapi mliokuwa mkiwaabudu badala ya MwenyeiMungu?'' watasema "wametupotea'' na watajishuhudia wenyewe kwamba walikuwa makafiri... Atasema [Mwenyezi Mungu siku ya kiyama kuwaambiya]:"Ingieni motoni pamoja na nyumati zilizopita kabla yenu za majini na watu
(al-Araaf 37-38)
'' Na bila shaka tumewaumbiya moto wa jahanam wengi katika majini na wanadamu[kwa sababu hii] nyoyo wanazo, lakini hawafahamu kwazo na macho wanayo, lakini hawaoni kwayo, na masikiyo wanayo lakini hawasikii kwayo na hao ni kama wanyama;bali wao wamepotea zaidi. Hao ndio alioghafilika[al-Araaf 179)
"Kwa yakini nitaijaza jahanamu kwa wote hawa ;majini na watu
(al-Sajdah 13)
Na ushahidi kuwa majini walioamini wataingia Peponi ni huu:
''Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya mola wake atapata mabustan[pepo]mawili (alRahman 46-47)
Aya hii na na hizo nyingine zilizonukuliwa na kwa ujumla Sura nzima inawahusu viumbe wote wawili, Majini na Wanadamu. Sura hiyo inazungumzia neema za Allah kwa majini na kuingia kwao Peponi.
Laiti kama majini hawangekuwa viumbe wa kupata neema hii ya Pepo, iweje basi ielezwe kuwa ni neema kwao. Katika kitabu chake, al-Furu, Ibn Mufleh kasema:
Majini huwajibika kwa vitendo vyao, hii ni kulingana na rai ya pamoja (ya Maulamaa). Wale ambao sio waumini wataingia motoni, jambo hili linaafikiwa na (Maulamaa) wote. Waumini miongoni mwao wataingia Peponi, hii ni kwa mujibu wa Malik na Shafii.
Kwa rai yao hii, majini hawatageuzwa udongo kama wanyama na kwamba malipo ya waumini miongoni mwao ni kunusurika tu kukaa katika moto wa Jahanamu ambapo rai hii inatofautaina na ile ya Abu Hanifa, al-Laith ibn Saad na wengineo.
Ni wazi kuwa rai ya kwanza ndiyo sahihi. Majini watakuwa Peponi pamoja na Wanadamu kulingana na mizani ya amali zao. Hii pia inatofautiana na ile rai kuwa majini hawatakula wala kunywa Peponi; jambo hili lilisemwa na na Mujaahid.
Na vilevile hii inatofautiana na rai iliyoshikiliwa na Umar ibn Abdul Aziz ambayo inasema kuwa majini watakuwa pembezoni mwa Pepo. Ibn Hamad yeye kasema katika kitabu chake kimoja, "majini wako sawa na wanadamu katika kuwajibishwa kwa vitendo na kwa Ibada." (hii imenukuliwa kutoka Lawaami al-Anwaar, juz. 2, uk. 222-223).
Majini huwajibishwa kwa kadri ya uwezo walionao
Ibn Taimiya kasema hivi,
Majini wameamrishwa kufanya matendo ya msingi na matendo ya ziada kulingana na uwezo (wasaa) walionao. Hawafanani na binadamu kwa haiba na maumbile. Yale mbayo wao wameamrishwa kuyafanya au wamekatazwa kuyafanya, hayafanani kabisa na yake ambayo wameamrishwa au kukatazwa wanadamu. Ila wanalingana katika kuhukumiwa kwa yale ambayo wameamrishwa kuyafanya, na yale ambayo wamekatazwa kuyafanya. Ninavyojua hakuna khitilafu juu ya jambo hili miongoni mwa Waislamu. (Taz. Ibn Taimiya, Majmuu Fatawa, juz. 4, uk. 233).
Hakuna ushirika kati ya majini na Allah (SW)
Majini, kama ilivyoelezwa, ni miongoni mwa viumbe vya Allah ambao, kama walivyo viumbe wengine, wanatii Kwake. Majini waliumbwa kwa ajili ya kumuabudia na kumtii Allah tu na wanawajibika kutekeleza maamrisho Yake.
Maelezo hayo yanafutilia mbali zile imani za kishirikina zilizokuwa zimeshamiri kutokana na dhana potofu juu ya msingi sahihi wa mambo au kutokana na ukosefu wa elimu.
Wayahudi na washirikina wa Kiarabu walikuwa wakiamini kuwa MwenyeziMungu alioa wake kutoka jamii ya majini na matokeo ya uhusiano huo ndio wakapatikana malaika (Subhana-Allah). Katika Qur'an, MwenyeziMungu analitaja jambo hili na kusema kuwa ni la uzushi. MwenyeziMungu anasema:
"Na wameweka makhusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini wamekwisha jua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa".
"Subhana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo msingizia."
(al-Saffaat 158-159).
Katika sherehe yake ya aya hii, Ibn Kathiir kaandika hivi:
Mujahid kasema, "washirikina walisema, ‘malaika ni watoto wa kike wa Mungu, SubhanaAllah'. Abubakar akawauliza, "mama zao ni kina nani?" Wakajibu, (mama zao) ni mabinti wa majini bora."
Ibn Zaid na Qatada wote wawili walitoa maelezo kama hayo ya Mujahid...Al-Aufi naye kasimulia Hadith kutoka kwa ibn Abbas, ‘maadui wa Allah walidai kuwa MwenyeziMungu na Ibilisi ni ndugu. Na Allah ametakasika na uzushi huo mzito,"


Inaendelea ……9
 
Mfululizo Wa Mada Ya Majini (9)


(Na Prof. Dkt. Sheikh Umar Suleiman al-Ashqar)
imefasiriwa na Shaibu H.Kifea
Majini wameumbwa kwa moto, wataunguaje motoni?
‘Baadhi ya watu wamezusha ubishi au shaka wakisema kuwa, "nyie si mnakubaliana na ukweli kuwa majini wameumbwa kwa moto. Sasa mbona tena mnasema kuwa makafiri miongoni mwao wataadhibiwa motoni, na yule anayethubutu kuiba habari a mbinguni hutupiwa kimwondo. Huu moto utawadhuru vipi ikiwa wao wenyewe wameumbwa kwa huo huo moto?'
Jawabu ni kwamba kwa asili wameumbwa kwa moto lakini baada ya kuumbwa kwao hawakuwa moto tena. Wakawa viumbe tofauti na moto. Jambo hili linaweza kutolewa mfano wa binadamu ambao wameumbwa kwa udongo. Baada ya kuumbwa kwao wakawa tofauti kabisa na udongo.
Iwapo mtu atampiga mwenziwe na dongo, atamuumiza sana au hata kumuua kabisa. Mwanadamu akifukiwa udongoni, atakosa hewa na kufa. Ndiyo kusema basi, ingawaje yeye mwenyewe katokana na udongo, bado udongo huo huo humdhuru. Basi hali ni hiyo hiyo kwa Majini na moto.
Je wahy (ufunuo) huwafikiaje Majini?
Kwa kuwa majini watahukumiwa kwa matendo yao, basi hapana shaka kuwa wahai wa MwenyeziMungu lazima uwafikie na kuwa "ushahidi" dhidi yao. Lakini jambo hili huwatokeaje? Je na wao wana Mitume miongoni mwao kama walionao binadamu au Mitume wao ndio hao hao wa jamii ya wanadamu?
MwenyeziMungu anasema katika Qur'an,

"Enyi makundi ya majini na wanadamu! Je hawakukujieni Mitume miongoni mwenu kukubainishieni Aya zangu na kukuonyeni juu ya mkusanyo wa siku yenu hii ya leo?" (6:130).
Aya hii inabainisha kuwa MwenyeziMungu aliwatumwa Mitume kwa majini lakini aya hii haijasema wazi hao Mitume wenyewe walikuwa ni majini wenzao au binadamu? Neno ‘miongoni' au "minkum" kwa Kiarabu ambalo Mfasiri wa Kiingereza Picktball amelifasiri kwa maneno, "Of your own" laweza kuwa na maana kuwa ama Mitume hao walikuwa wa jamii yao wenyewe au laweza kuwa maana kuwa Mtume mmoja wa kibinadamu katumwa kwa viumbe wa jamii zote mbili.
Kwa hali hiyo, kuna tofauti ya rai kuhusiana ipi hasa maana ya aya hii. Kimsingi, kuna rai mbili juu ya jambo hili. Rai ya kwanza ni kwamba majini walipelekewa Mitume wa jamii yao wenyewe. Hii ni rai ya al-Dhuhhaak. Ibn al-Jauz kasema hii ndiyo maana ya wazi zaidi ya aya hii
Ibn Hazm kasema kuwa hakuna Mtume yeyote wa jamii ya binadamu aliyetumwa kwa majini kabla ya Mtume Muhammad (Salallahu alaihi wasalam).
Rai ya pili ni kuwa Mitume wote waliotumwa kwa Majini walikuwa wanadamu. AlSuyuuti kaeleza katika kitabu chake, Luqat al-Marjaan kwamba wengi miongoni mwa wanazuoni wa awali na wa baadae wamesema kuwa majini hawakuwahi hata mara moja kuwa na Mtume au nabii wa jinsi yao. Rai hii ilisimuliwa kutoka kwa ibn Abbas, Mujahid, al-Kalbi na Abu Ubaid. (
Taz.Lawaami al-Anwaar, juz. 2, uk. 223-4).
Kinachoifanya rai hii ya pili ionekane kuwa na nguvu zaidi ni ile kauli ya majini baada ya kuisikia Qur'an;
(Majini) wakasema, "Enyi watu wetu! Hakika Kitabu kilichoteremshwa baada ya Musa......" (46:30) Hata hivyo aya hii si uthibitisho wa wazi wa jambo husika. Swala linalobishaniwa hapa halihitaji ijitihadi yeyote kwa upande wa Waislamu na wala hakuna aya iliyowazi kuhusiana nalo. Kwa hiyo basi, hakuna haja ya kulijadili kwa kina zaidi.
Ujumbe wa Muhammad (Salallahu alaihi wasalam) kwa majini na wanadamu

Mtume Muhammad (Salallahu alaihi wasalam) alitumwa kwa wote majini na watu. Ibn Taimiyya kasema, "Kuna makubaliyano ya rai juu ya jambo hili miongoni mwa Maswahaba na wale waliofuta baada yao na maimamu wa Waislamu na makundi mbalimbali ya Waislamu, ahl al-sunna wa al-jamaa na wengineo. MwenyeziMungu awawie radhi." (Taz. Ibn Taimia, Majmuu al-Fatawa, juz. 19, uk. 9.
Kinachoitia nguvu rai hii ni changamoto ya Qur'an kwa majini na binadamu ikiwataka watunge kitabu sawa na Qur'an. MwenyeziMungu anasema katika Qur'an.

" Sema, ‘hata wakijikusanya watu (wote) na majini ili kuleta mfano wa hii Qur'an basi hawangaliweza kuleta mfano wake hata kama watasaidiana (vipi) wao kwa wao." (17:88)
Baadhi ya majini haraka wakabadilika na kuwa waumini walipoisikia Qur'an ikisomwa. Qur'an inasema: "Sema, ‘imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikia (Qur'an) likasema, ‘hakika tumeisikia Qur'an ya ajabu, inaongoza katika uongofu, kwa hivyo tumeiamini wala hatutamshirikisha yeyote tena na Mola wetu.'" (72:1-2).
Wale walioisikiliza na kuiamini Qur'an ni wale wanaotajwa katika aya ifuatayo kutoka surat al-Ahqaaf, "Na (wakumbushe) tulipokuletea kundi la majini (kuja kwako) kusikiliza Qur'an. Basi walipoihudhuria wakasema (wakaambiana) ‘nyamazeni (msikilize maneno ya MwenyeziMungu)'. Na ilikwisha (somwa) wakarudi kwa wenzao wakiwaonya, ‘enyi wenzetu! Hakika tumesikia Kitabu kilichoteremshwa baada ya Musa, kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake na kinachoongoa katika haki na katika njia iliyonyooka. Enyi wenzetu! Muitikieni mlinganiji (muitaji) wa MwenyeziMungu na mumuamini, atakusameheni (MwenyeziMungu) madhambi yenu na atakukingeni na adhabu iumizayo. Na wasiomuitikia Muitaji wa MwenyeziMungu, basi wao hawatamshinda hapa katika ardhi wala hawatakuwa na walinzi mbele yake. Hao wamo katika upotofu (upotevu) uliodhahiri."(46:29-32).

Walipoisikia Qur'an, wakaiamini na kurejea kwa wenzao kuwalingania wailekee tawhiid na imani na wakawapa habari njema pamoja na kuwaonya.
Kisa cha majini hawa kumsikiliza Mtume (Salallahu alaihi wasalam) kimenakiliwa katika Bukhari na Muslim kwa mapokezi ya ibn Abbas. Ibn Abbas kasimulia kuwa Mtume wa Allah alikuwa akisafiri na baadhi ya Maswahaba, wakiwa na madhumuni ya kwenda sokoni eneo la Ukaz.
Katika kipindi hicho, kulikwishakuwa na kizuizi kwa majini kupata habari za mbinguni ambapo vijinga vya moto vilikuwa vikirushwa dhidi yao. Kwa hiyo majini (waliokwenda mbinguni) wakarudi kwa wenzao ambako waliulizwa kulikoni.
Wakajibu, "vizuizi fulani vimewekwa baina yetu na habari za mbinguni'. Wakaambiana, "yawezekana labda kuna jambo limetokea. Kwa hiyo nendeni sehemu za mashariki na magharibi ya dunia mkaone nini kimetokea na kusababisha vikwazo hivi baina yetu na habari za mbinguni. Wakafanya hivyo.

Kundi moja likaenda hadi kufika Tihama ambao ni msitu wa michikichi ulio jirani na soko la Ukaz. Muda huo Mtume (Salallahu alaihi wasalam) alikuwa akiwaswalisha Maswahaba swala ya Alfajir. Majini hao waliposikia kisomo cha Qur'an, wakaambiana, ‘tusikilize jamani'. Kisha wakasemezana, ‘hii ndiyo imesababisha vizuwizi baina yetu na habari za mbinguni." Majini hawa wakarejea kwa wenzao na kuwaambia, "Enyi wenzetu, sisi wenzenu tumesikia kisomo cha ajabu (Qur'an ya ajabu) ambayo inaongoza katika njia iliyonyooka nasi tunaiamini". Kisha MwenyeziMungu akamshushia aya hii,
"Sema, ‘Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikia..."(Qur'an) (72:1). Hii ni kwamba MwenyeziMungu alimfahamisha Mtume kile walichosema majini.
Ujumbe wa majini

Tukio lililosimuliwa hapo juu lilikuwa ni tukio la kwanza kwa majini kuusikia ujumbe wa Mtume (Salallahu alaihi wasalam). Waliisikiliza Qur'an bila Mtume (Salallahu alaihi wasalam) kujua kama walikuwepo (hakuwaona). Kundi moja kati yao likaamini na kurudi kwa wenzao kuwasambazia ujumbe huu.

Baada ya tukio hilo, ujumbe wa majini ukamfikia Mtume (Salallahu alaihi wasalam) kupata elimu fulani kwake. Mtume (Salallahu alaihi wasalam) akawapa ahadi na baadae akakutana nao na kuwafundisha yale ambayo MwenyeziMungu kayaaamrisha kwao. Na akawasomea Qur'an na kuwapa habari za mbinguni
Tukio hili la pili lilitokea Maka kabla ya Mtume kuhamia Madina. Muslim katika Kitabu chake, Sahih, na Ahmad katika kitabu chake Musnad wamenakili Hadith kutoka kwa Alqama kuwa alipata kumuuliza Abdullah ibn Masud kama kulikuwa na mtu yeyote aliyemsindikiza Mtume (Salallahu alaihi wasalam) usiku huo aliokutana na majini, Ibn Masud akasema "hapana, hakuna yeyote kati yetu aliyekwenda.
Lakini tulikuwa pamoja na Mtume (Salallahu alaihi wasalam) usiku huo na tukapotezana nae. Tukamtafuta hadi kwenye mabonde na vilima na tukaambizana, "huenda labda amechukuliwa (na majini) au ameuawa kwa siri.
Akasema, " Tuliishi katika usiku m-baya ambao watu hawakuwahi kuishi'. Alfajiri ndio tukamuona anakuja akitokea upande wa Hiraa. Tukamwambia, ‘Mtume wa Allah tulipotezana nawe na kukutafuta lakini hatukukuona na tukaishi katika usiku mbaya ambao watu hawajapata kuishi'
.
Mtume (Salallahu alaihi wasalam) akasema, "alikuja kwangu jamaa fulani kuniita kwa niaba ya majini, na nikaondoka naye (hadi kwa wenziwe) ambako niliwasomea Qur'an'. (Ibn Msud) akasema, 'Halafu (Mtume) akaenda nasi kutuonesha mabaki ya vijinga vyao vya moto'. Majini hao walimuuliza Mtume kuhusu chakula chao, naye akawaambia, ‘Kila mfupa uliosomewa jina la Allah ni chakula chenu. Muda ule ule mfupa unapotua mikononi mwenu, utavikwa nyama. Na kinyesi cha ngamia ni chakula cha wanyama wenu.'"
Na pia ipo riwaya hii kutoka kwa ibn Masud katika kitabu cha al-Tabari, "Nilipitisha usiku mmoja nikiwasomea majini Qur'an mahali paitwapo al-Hujuun (ndani ya Maka).
Miongoni mwa aya alizowasomea ni ni Surati al-Rahmaan. Katika Hadith nyingine Mtume (Salallahu alaihi wasalam) kasema, "Nilisoma (surati Rahman) kwa majini katika usiku wa majini nao wakiitikia kwa mwitiko bora kuliko mlivyofanya nyinyi. Nilipofikia sehemu inayosema, "ni ipi kati ya neema za Mola wenu mnayoikanusha?" Wakaitikia, ;hakuna neema yoyote kati ya neema zako tunayoikanusha. Na sifa ni zako" (hii ilinakiliwa na al-Bazaar , al-Hakiim na ibn Jarir ikiwa na isinadi sahihi. Taz. Al-Albani, Sahih al-jaamii, juz. 1, uk. 30)
Haikuwa mara hiyo moja tu Mtume kuwasomea majini bali mikutano yake na majini ilifanyika mara nyingi baadae. Katika sherehe yake ya surati al-Ahqaaf, ibn Kathiir kanakili Hadith mbalimbali ambapo Mtume (Salallahu alaihi wasalam) kakutana na majini.
Katika baadhi ya Hadith hizo, inaelezwa kuwa ibn Masud alikuwa karibu sana na Mtume (Salallahu alaihi wasalam) usiku huo.
Katika Hadith iliyonakiliwa katika Sahih al-Bukhari, kuna maelezo ya baadhi ya majini waliotoka sehemu iitwayo Nasiib nchini Yemen kwenda kumtembelea Mtume (Salallahu alaihi wasalam). Bukhari kanakili Hadith kutoka kwa Abu Huraira kuwa Mtume (Salallahu alaihi wasalam) kasema,
"Ujumbe wa majini wa Nasiib (sehemu ya Yeman) ulinijia-nao walikuwa ni majini wema walioje-na wakaniuliza vyakula vyao, Nikawaombea dua kwa MwenyeziMungu kuwa wasiupite mfupa wowote au kinyesi cha mnyama isipokuwa wakuta chakula chao juu yake."
Majini kuwahubiria binadamu

Katika baadhi ya Hadith sahihi kuna riwaya kuwa baadhi ya majini walichangia kuwaongoa wanadamu kadha wa kadha. Katika Sahih Bukhari, imenakiliwa kuwa Umar ibn al-Khatab alimuuliza mtu mmoja aliyekuwa mtabiri zama za ujahili kuhusu jambo moja la ajabu ambalo jini wa kike wa mtabiri kapata kumfahamisha
Mtabiri huyo akamwambia Umar hivi, "siku moja mwanamke huyo jini alinijia katika hali ya hofu. Akasema, ‘Hivi wewe hujaiona hali ya kukata tamaa na kushindwa waliyonayo majini (yaani hali ya kushindwa kupata habari za mbinguni), na kwa sababu hiyo, sasa wanawafuata waendesha ngamia tu'".
Umar akasema, ‘huo ndio ukweli' (Mtabiri huyo) akasema, nilikuwa nikilala jirani na masanamu ambapo alikuja mtu mmoja aliyekuwa na ndama wa ng'ombe ambaye alimtowa muhanga kwa ajili ya sanamu. Ndama huyo akapiga yowe ambalo sijawahi kusikia mfano wake.
Ndama huyo alisema, '"ewe Julaih, ewe muovu jeuri, una jambo la mafanikio mbele yako. Mtu mwenye kauli njema, anasema, ‘Hakuna wa kuabudiwa isipokuwa MwenyeziMungu'.

(watu kusikia hivyo, wakapatwa na woga), wakatimua mbio kutoka mahali hapo. Yowe hilo likaja kusikika tena. Mimi nikaondoka halafu siku chache baadae, watu wakawa wanasema, ‘Nabii katokea.."'
Baada ya kunakili Hadith katika sherehe yake ya Surat al-Ahqaaf. Ibn Kathiir kaandika hivi: "Hii ni matini ya Bukhari. Al-Baihaqi naye kanakili kitu kama hiki kutoka kwa ibn Wahb." Kisha akasema, ‘ni wazi kuwa riwaya hii inafuata dhana ile ile potofu kuwa alikuwa ni Umar aliyepiga yowe hilo wakati mnyama huyo akitolewa muhanga. Jambo hili linabainishwa kwa Hadith dhaifu kutoka kwa Umar. Riwaya nyingine zote zinamtaja mtabiri kuwa ndiye aliyesimulia kile alichokiona na kukisikia. MwenyeziMungu ndiye ajuaye." Kisha akaongeza kuwa, "mtu huyo aliyekuwa mtabiri alikuwa ni Sawaad ibn Qaarib".
Kuamrisha mema na kuwa mashahidi kwa Waislamu
Ile Hadith ya Mtume (Salallahu alaihi wasalam) inasema kuwa jini wa Mtume alisilimu na akawa anamuhimiza Mtume kufanya mambo mema tu kama itakavyoelezwa huko mbele.
Abu Sa'id al-Khudhri alimwambia Abu sasa al-Ansari, "Mimi nakuona wewe kama kondoo na pori. Hivyo, unapokuwa na kondoo wako au uwapo porini, piga adhana ya Sala, basi ima binadamu au jini au kiumbe yeyote yule atakuwa shahidi wa adhana hiyo Siku ya Kufufuliwa". Abu Sai'id akaongeza kusema, "mimi nilisikia hivyo kwa Mtume wa Allah" (imenakiliwa na Bukhari). Akasema kuwa majini waliosikia adhana ya Sala watakuwa mashahidi wake Siku ya Kufufuliwa.
Majini wana daraja tofauti za wema na uovu
Majini wana matabaka mbalimbali. Baadhi yao ni watiifu watendao mema na kuishi maisha ya uchaMungu. Wengine wako katika kiwango chini cha wema na uchaMungu, na wengine ni wakaidi, na wengine ni makafiri kabisa, na hawa ndio wengi mno.
MwenyeziMungu anawaezea hivi wale majini walioisikiliza Qur'an;
"Na hakika katika sisi wako wema na wengine katika sisi ni kinyume cha hayo, tumekuwa njia mabalimbali."
(72:11). Kwa maneno mengine baadhi yao ni wachaMungu kwelikweli, baadhi ni wachaMungu wa wastani na wengine ni wapotevu. Na wao wana njia na fikra tofauti kama walivyo wanadamu."
MwenyeziMungu anawanukuu majini wakisema;
"Nasi wamo miongoni mwetu waliosilimu na wamo miongoni mwetu wanaosilimu hao ndio waliofuata uwongofu. Na wanaokengeuka hao watakuwa kuni za jahanamu" (72:14-15).
Kwa maneno mengine baadhi yao ni Waislamu na wengine wamedhulumu nafsi zao kwa ukafiri. Yeyote yule ambaye amesilimu amejielekeza katika njia ya uwongofu kwa matendo yake na ambaye amedhulumu nafsi yake atakuwa kuni Jahanamu.
Asili ya Ibilisi
MwenyeziMungu amewapa majini hiyari ya kuwa waumini au makafiri ambapo huyu Ibilisi mwanzoni alikuwa akimuabudu Allah pamoja na Malaika. Kabla hajawa muasi.

Alipoasi akauridhia uovu na kuuhangaikia ijapokuwa uovu utakuwa sababu ya kuadhibiwa kwake. Aliridhia kufanya maasi na kuwachochea wengine kufanya maovu
"(Shetani) akasema, ‘Na-apa kwa haki ya utukufu wako, bila shaka nitawapoteza wote (hao watoto wa adui yangu-Adam). Isipokuwa wale waja wako waliosafishwa". (38:82-83)
Hali ni hiyo hiyo kwa binadamu. Nafsi ya mtu ikiwa ovu, hutamani kile kinachoidhuru na huridhika na matendo maovu. Kwa hakika nafsi hiyo, kwa mapenzi huyafurahia maovu hata kufikia kiwango cha kumuharibu mtu, kuharibu dini, kuharibu maadili, afya ya mwili na mali.
Itoshe tu kutoa mfano wa wale wanaokunywa pombe, au wanaovuta sigara. Vitu hivi humdhuru hata kumuua yule anayevitumia. Ingawaje vinaweza kumsababishia mtu kifo lakini bado mtu hushindwa kuviacha isipokuwa kwa ugumu.
 
Mfululizo Wa Mada Ya Majini (10)


(Na Prof. Dkt. Sheikh Umar Suleiman al-Ashqar)
imefasiriwa na Shaibu H.Kifea
Majini Kuwahubiria Binaadamu
Je Jini, Shaytwaan Anaweza Kusilimu?


Katika baadhi ya Hadith sahihi kuna riwaya kuwa baadhi ya majini walichangia kuwaongoa wanadamu kadha wa kadha. Katika Sahih Bukhari, imenakiliwa kuwa Umar ibn al-Khatab alimuuliza mtu mmoja aliyekuwa mtabiri zama za ujahili kuhusu jambo moja la ajabu ambalo jini wa kike wa mtabiri huyo kapata kumfahamisha.
Mtabiri huyo akamwambia Umar hivi, “siku moja mwanamke huyo jini alinijia katika hali ya hofu. Akasema, ‘Hivi wewe hujaiona hali ya kukata tamaa na kushindwa waliyonayo majini (yaani hali ya kushindwa kupata habari za mbinguni), na kwa sababu hiyo, sasa wanawafuata waendesha ngamia tu’”.
Umar akasema, ‘huo ndio ukweli’ (Mtabiri huyo) akasema, nilikuwa nikilala jirani na masanamu ambapo alikuja mtu mmoja aliyekuwa na ndama wa ng’ombe ambaye alimtowa muhanga kwa ajili ya sanamu. Ndama huyo akapiga yowe ambalo sijawahi kusikia mfano wake.
Ndama huyo alisema, ‘”ewe Julaih, ewe muovu jeuri, una jambo la mafanikio mbele yako. Mtu mwenye kauli njema, anasema, ‘Hakuna wa kuabudiwa isipokuwa MwenyeziMungu’.
(watu kusikia hivyo, wakapatwa na woga), wakatimua mbio kutoka mahali hapo. Yowe hilo likaja kusikika tena. Mimi nikaondoka halafu siku chache baadae, watu wakawa wanasema, ‘Nabii katokea..”’
Baada ya kunakili Hadith hii katika sherehe yake ya Surat al-Ahqaaf. Ibn Kathiir kaandika hivi: “Hii ni matini ya Bukhari. Al-Baihaqi naye kanakili kitu kama hiki kutoka kwa ibn Wahb.” Kisha akasema, ‘ni wazi kuwa riwaya hii inafuata dhana ile ile potofu kuwa alikuwa ni Umar aliyepiga yowe hilo wakati mnyama huyo akitolewa muhanga. Jambo hili linabainishwa kwa Hadith dhaifu kutoka kwa Umar. Riwaya nyingine zote zinamtaja mtabiri kuwa ndiye aliyesimulia kile alichokiona na kukisikia. MwenyeziMungu ndiye ajuaye.” Kisha akaongeza kuwa, “mtu huyo aliyekuwa mtabiri alikuwa ni Sawaad ibn Qaarib”
Kuamrisha mema na kuwa mashahidi kwa Waislamu
Ile Hadith ya Mtume (salallahu alaihi wasalam) inasema kuwa jini wa Mtume alisilimu na akawa anamuhimiza Mtume kufanya mambo mema tu kama itakavyoelezwa huko mbele.
Abu Sa’id al-Khudhri alimwambia Abu sasa al-Ansari, “Mimi nakuona wewe kama kondoo na pori. Hivyo, unapokuwa na kondoo wako au uwapo porini, piga adhana ya Sala, basi ima binadamu au jini au kiumbe yeyote yule atakuwa shahidi wa adhana hiyo Siku ya Kufufuliwa”.
Abu Sai’id akaongeza kusema, “mimi nilisikia hivyo kwa Mtume wa Allah” (imenakiliwa na Bukhari). Akasema kuwa majini waliosikia adhana ya Sala watakuwa mashahidi wake Siku ya Kufufuliwa.
Majini wana daraja tofauti za wema na uovu
Majini wana matabaka mbalimbali. Baadhi yao ni watiifu watendao mema na huishi maisha ya uchaMungu. Wengine wako katika kiwango chini cha wema na uchaMungu, na wengine ni wakaidi, na wengine ni makafiri kabisa, na hawa ndio wengi mno.
MwenyeziMungu anawaezea hivi wale majini walioisikiliza Qur’an;
“Na hakika katika sisi wako wema na wengine katika sisi ni kinyume cha hayo, tumekuwa njia mabalimbali.” (72:11).
Kwa maneno mengine baadhi yao ni wachaMungu kwelikweli, baadhi ni wachaMungu wa wastani na wengine ni wapotevu. Na wao wana njia na fikra tofauti kama walivyo wanadamu.”
MwenyeziMungu anawanukuu majini wakisema;
“Nasi wamo miongoni mwetu waliosilimu na wamo miongoni mwetu wanaokengeuka, na waliosilimu, hao ndio waliofuata uwongofu. Na wanaokengeuka hao watakuwa kuni za jahanamu” (72:14-15).
Kwa maneno mengine baadhi yao ni Waislamu na wengine wamedhulumu nafsi zao kwa ukafiri. Yeyote yule ambaye amesilimu amejielekeza katika njia ya uwongofu kwa matendo yake na ambaye amedhulumu nafsi yake atakuwa kuni Jahanamu.
Asili ya Ibilisi

MwenyeziMungu amewapa majini hiyari ya kuwa waumini au makafiri ambapo huyu Ibilisi mwanzoni alikuwa akimuabudu Allah pamoja na Malaika. Kabla hajawa muasi.
Alipoasi akauridhia uovu na kuuhangaikia ijapokuwa uovu utakuwa sababu ya kuadhibiwa kwake. Aliridhia kufanya maasi na kuwachochea wengine kufanya maovu.
“(Shetani) akasema, ‘Na-apa kwa haki ya utukufu wako, bila shaka nitawapoteza wote (hao watoto wa adui yangu-Adam). Isipokuwa wale waja wako waliosafishwa”. (38:82-83)
Hali ni hiyo hiyo kwa binadamu. Nafsi ya mtu ikiwa ovu, hutamani kile kinachoidhuru na huridhika na matendo maovu. Kwa hakika nafsi hiyo, kwa mapenzi huyafurahia maovu hata kufikia kiwango cha kumuharibu mtu, kuharibu dini, kuharibu maadili, afya ya mwili na mali.
Itoshe tu kutoa mfano wa wale wanaokunywa pombe, au wanaovuta sigara. Vitu hivi humdhuru hata kumuua yule anayevitumia. Ingawaje vinaweza kumsababishia mtu kifo lakini bado mtu hushindwa kuviacha isipokuwa kwa ugumu.

Je shetani wa kijini anaweza kusilimu?

Ni dhahiri kuwa kwa mujibu wa Hadith, inawezekana kwa shetani wa kijini kusilimu kama alivyosilimu shetani wa kijini wa Mtume (salallahu alaihi wasalam). Hata hivyo, baadhi ya wanazuoni wanaikataa kauli hii na kusema kuwa shetani wa kijini hawezi kuwa muumini. Mufasiri wa al-Aqiida al-Tahaawiya yeye rai yake ni hiyo ya pili.
Watu wa kundi hili wanatoa hoja kuwa neno aslam (lililotajwa katika Hadith kuhusiana na kusilimu kwa shetani wa kijini wa Mtume lina maana kuwa jini-shetani huyo alitii sheria za Kiislamu (bila yakini wala imani).
Baadhi ya wanazuoni wanasema kuwa kauli sahihi ni ile ya Mtume (saw) kusema, “mimi nimesalimika naye”. Mfasiri wa al-Tahaawiya yeye ana rai kuwa kuliweka neno aslam katika kiima ni makosa.
Lakini al-Nawawi, katika tafsiri yake ya Sahihi Muslim kasema, “Hizo ni kauli mbili zilizothibitishwa.” Yeye anasema kuwa al-Khaatabi anaona kuwa kauli yenye nguvu zaidi ni ile yenye dhamma (yaani ile yenye neno katika kiima).
Miongoni mwa wale wasemao kuwa shetani wa kijini anaweza kusilimu ni ibn Hiban. Akisherehesha Hadith iliyotajwa hapo, kasema, “ katika riwaya hii, kuna ashahidi kuwa shetani wa kijini wa Mtume ((salallahu alaihi wasalam) alisilimu na hakumchochea Mtume ((salallahu alaihi wasalam)) kufanya kingine chochote ila mambo mema. Pamoja na hivyo Mtume wa Allah alikuwa amesalimika hata kama shetani alikuwa kafiri.”
Kuna hatihati kuhusiana na rai ya Mfasiri wa al-Aqiida al-Tahaawiya kwamba shetani wa kijini anabakia kuwa kafiri tu. Kama ana maana kuwa neno shetani hutumika tu kwa majini waliokufuru, basi rai hiyo ni sahihi.
Lakini kama ana maana kuwa shetani wa kijini hawezi kubadilika na kusilimu , basi rai yake iko mbali na usahihi ambapo Hadith hiyo ni ushahidi dhidi yake.
Kwa mtazamo wa kisheria, haionekani kuwa sahihi kwamba majini waliokufuru wawajibike kwa matendo yao halafu tena, wakati huo huo, wasiweze kusilimu.
Majini wataadhibiwa ikiwa ujumbe umewafikia na kuukanusha. Hii tu inaonesha kuwa na wao wana uhuru wa kuwa waumini au makafiri. Ndiyo kusema, na wao pia wanaweza kuwa Waislamu kama wanataka kuwa hivyo.
Uadui kati ya Ibilisi na Mwanadamu
Sababu ya uadui, historia yake na ukubwa wake
Uadui kati ya wanadamu na Ibilisi mzizi wake ni kadhia iliyotokea muda mrefu huko nyuma. Msomaji rejea nyuma kabisa hadi siku ambayo MwenyeziMungu Alimuumba Adam, kabla hajampulizia roho iliyotokana na Yeye.
Shetani akamzunguukia na kusema, “(we Adam) ukipewa mamlaka juu yangu, kwa kweli, mimi nitakuasi. Na nikipewa mamlaka juu yako, nitakuangamiza.”
Katika Sahihi Muslim, imenakiliwa Hadith kutoka kwa Anas kuwa Mtume ((salallahu alaihi wasalam)) kasema, “MwenyeziMungu alipomuumba Adam Peponi, alimuacha kwa kitambo alichotaka ambakishe huko. Ndipo Ibilisi alipomzunguukia kutaka kuona kuwa yeye ni kitu gani hasa, na alipoona kuwa yu mtupu kwa ndani, akatambua kuwa kiumbe mpya kaumbwa akiwa na umbile ambalo lisingejimiliki lenyewe”.
MwenyeziMungu alipompulizia Adam roho iliyotokana naYeye, akawaamuru Malaika wamsujudie. Ibilisi alikuwa akimuabudu Allah pamoja na Malaika, hivyo, naye amri hii ilimuhusu.
Lakini yeye akajiona bora na kwa majivuno, akakataa kumsujudia Adam. Alijigamba, “mimi ni bora kuliko Yeye. Mimi umeniumba kwa moto na Yeye umemuumba kwa udongo.”
Na pale Adam alipofumbua macho yake akaona ishara ya utukufu na fadhila, Malaika wakimsujudia. Lakini pia aliona uadui mkubwa ukimsubiri, ni uadui wa kumpotosha na kumpeleka yeye na kizazi chake katika maangamizi.
Ibilisi alitolewa nje ya Pepo kutokana na majivuno yake lakini akaomba muda kwa MwenyeziMungu aachwe hai hadi Siku ya Hukumu
“Akasema, ‘nipe muda (nisife) mpaka Siku watakapofufuliwa (viumbe).” (7:14). Kiumbe huyu aliyelaaniwa alitoa ahadi na kula kiapo kuwa atakipoteza kizazi cha Adam na atawafanyia hila.
“(MwenyeziMungu) Akasema: “Utakuwa miongoni mwa waliopewa muda.’ Akasema, ‘Kwa kuwa umenuhukumia upotevu basi nitawakalia (waja) wako) katika njia Yako iliyonyooka. Kisha nitawafikia kwa mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao; wengi katika wao hutawakuta (hutawaona) wenye kushukuru”. (7:15-17).
Kauli hii ya mwisho inaonesha ukubwa wa vita vyake vya kuwapotosha wanadamu. Atatega kila njia aiwezayo dhidi yao, kuliani kwao, kushoto, mbele na nyuma yao.
Atawapiga vita kila upande. Katika sherehe yake ya aya hii, Alzamakhshari kaandika hivi: “atawajia pande zote nne kama ilivyo kawaida ya adui, yeye ndio atakuwa mchochezi wao. Pia atawarubuni kwa njia yoyote aiwezayo. Qur’an inasema;
“Na wavute uwawezao miongoni mwao kwa sauti yako, na uwakusanyie (jeshi lako la) wapanda farasi na waendao kwa miguu. Na shirikiana nao katika mali (yao) na watoto (wao), na waahidi (ahadi za uwongo). Lakini shetani hawapi waadi ila kwa udanganyifu.” (17:64).
 
Majini au mapepo ni viumbe ambavyo havionekani kwa macho, ni viumbe kama malaika isipokuwa majini na mapepo yalifukuzwa mbinguni pamoja na shetani baada ya kuasi, na yalitupwa duniani yakisubiri siku ya mwisho ya hukumu.

Shetani na majini, wanajua kabisa kuwa jehanum ya moto ipo kwa ajili yao, ndiyo maana wanafanya kila mbinu wasiingie peke yao huko jehanum, shetani ni mwongo, laghai anawatumia sana wachawi, waganga wa kienyeji, wasoma nyota kupandikiza majini, kuiba nyota yako ya mafanikio, kuchukua watu misukule nk.

Kuna aina nyingi za majini baadhi yake ni kama:-

1) Murafari - hili ni jini linalozuia mafanikio ya kupata fedha, mafanikio ya elimu nk.
2) Latifu - hili jini linaloleta ufukara, mateso, hata ukipata pesa matumizi yake yanakuwa ni hovyo
3) Jahari - Jini anayetumiwa kuiba mali na kuzuia biashara kustawi
4) Hasinani - jini hili ni la fujo, ulevi wa pombe, bangi na dawa za kulevya
5) Jube - jini hili linasababisha utasa
6) Subiani - jini la ajali, linasababisha wanawake kutokupata siku zao, na kunyonya damu za akina mama siku zao za hedhi ambapo wanapata maumivu makali sana.
7) Sumil - jini hili huangamiza mimba changa
8) Waidadat - jini hili husababisha wanaume kuvaa hereni kusuka nywele na kutoga masikio.
9) Alibadiri - jini la kifo, likikupata kifo hutokea wakati wowote.
10) Anzura - Linawazuia vijana wa kike na kiume kuolewa/kuoa
11) Maimuna - linawakamata wanaume wenye ndoa zao hadi ndoa inavunjika
12) Makata - linasababisha vifo vya mfululizo kwenye familia
13) Faziur - jini la maandishi. Unaletewa barua ukiisoma tayari umelikwaa
14)Subha - jini hili linasababisha mtu kuwa na kiburi sana na kujiinua.
15) Maulan - jini linalofanya watu kuwa kichaa, au mtu ananuka wakati wowote
16) Al-maul - jini hili linamfanya mtu kuwa ombaomba
17) Zuhura au Zohari - Jini la fujo
18) Araba - Jini hili linafanya mtu apende sana ubani
19) Farkh - jini hili linatumwa hasa kwa wakristo kuangalia kama ana kinga (Wokovu)
20) Baradi - jini hili likikupata basi ndoa yako ni lazima itavunjika.
21) Shamsu - jini hili huvaa umbile la binadamu kwa sura yoyote.(sasa hivi mitaani majini haya yapo mengi sana)
22) Abuni - jini wa hasira
23) Kaimu - jini la kutambua nyota za watu
24) Tajuruni - jini la utajiri wa kichawi - ni lazima utoe kafara ya mwanao, mkeo au kufanya tendo la ndoa na mama yako mzazi
25) Al-taliki - jini hili linapoteza watu katika mazingira ya kutatanisha
26) Naluju - linasimamia lugha
27) Janatusi - linatumwa alfajiri kabla ya adhana kuleta usingizi kwa Wakristo wasifanye sala
28) Riyaron - jini hili linamfanya mtu afanye kila kazi peke yake
29) Zaitun - Jini hili linasababisha wasichana kuwa na maringo
30) Ruyati - jini linalosimamia ndoto mbaya
31) Al-rahabu - jini linalosababisha hitilafu ya umeme
32) Hadharaji - jini hili linafanya kazi ya kukata kichwa cha mtu ili wapate damu
33) Anazihaji - jini hili ndilo linachukua roho yako ukifa kwenye dhambi
34) Nghruk - linasababisha maafa
35)Munkara - jini la makaburini
36) Takadhuru - jini linaloleta mali za masharti.
37) Rabindi - jini la Waislamu pekee yao ili wafanye fujo.
38) Balishebe - jini la magonjwa yasiyopona
39) Sajiduri - jini linalokusaidia kupata pesa, kisha zinapotea kwa haraka
40) Rumiran - linasimamia uwongo
41) Lairlihabi - linasimamia hofu, kutojiamini na kukata tamaa
42) Rohani - jini la mateso na fujo
43) Betrah - jini hili linasimamia mapambo, kwa mwanamke huwa anajipamba isivyo kawaida, halikadhalika mwanaume
44)Hanshari - linatumiwa sana na waarabu kulinda maduka yao
45) Walihuni - linazunguka nyumba likilinda biashara
46) Kurasih - jini la kupoteza fahamu
47) Tarik - huondoa amani nyumbani, kazini. Linafanya watu wasielewane
48) Atha - mungu wa kiarabu wa kuabudu sanamu
49) Munakir - linapoteza watu kimiujiza
50) Malik - jini la kumiliki biashara
51) Ghatabu - jini la kulainisha macho wa wanawake. Wanakuwa wanarembua
52) Khatuh - jini la uchawi wa kuchukua kucha, nywele na nguo za ndani
53) Fanken - jini hili linasimamia mtu kuzunguza kiswahili cha pwani
54) Zamzam - jini la marashi na kusimamia mikataba ya imani. Mkristo anaposilimishwa basi hutupiwa jini hili kupofushwa akili yake.
55) Mukitala - linatumwa kuangalia kinga za watu
56) Laufili - jini la uvivu
57) Al-khah - linakula damu iliyoganda
58 Abasaa - jini la hasira wivu na jeuri
59) Aherumi - jini la homa za mara kwa mara
60) Muba - jini la maradhi ya kuambikiza
61) Kamariram - jini hili linatoa kinga kwa majambazi
62) Zubiran - jini la uongo na uzushi
63) Abadi - Jini la wizi, umalaya na ujambazi
64) Muzamili- jini la matambiko ya kiarabu
65) Ruhadi - jini la wizi, umalaya na umasikini
66 Usuran - jini la wizi, umalaya, ujambazi na umaskini
67)Tubuyali - jini hili linamfanya mtu kuiba vitu vya ndani ya nyumba. Haibi nje ya nyumba
68) Zirach - jini la wizi, umalaya, ujambazi na umaskini
69) Ashuran - jini la utasa na maradhi ya akina mama

Kinga ya majini haya ni nyepesi ni KUOKOKA na kusimama katika neno la Mungu. Kama unayo dalili yoyote iliyosababishwa na majini hayo hapo juu na umeokoka, taja jina la hilo jini, ni lazima litaitika, kisha liwashie moto.

Kama hujaokoka usiyarushie mawe au moto yatakuumiza. Mwuone kiongozi yeyote wa kanisa akuongoze sala ya toba, kisha anza kuwasha moto, hakika yatakimbia na kuacha biashara, kazi, ndoa, na watoto wako huru.
 
However, Abu `Uthman Sa`id ibn Al-`Abass Ar-Razi said in his book Al-Ilham wa Al-Waswasah that it was reported that some Yemeni people wrote to Imam Malik: "A male jinni has come to us and proposed to marry a young (human) woman saying, ‘I seek to stick to the right path by this proposal.'" Imam Malik answered, "I see that there is nothing wrong in doing so, but I dislike to expose this woman to a situation where she might be asked about her husband and she would answer, ‘It is a male jinni.'
 
wakuu kuhusu kuwa na majini hii inaweza ikawa proved scientifically kama multiple personality disorder

multiple personality,
a very rare psychological disorder in which a person has two or more distinct personalities, each with its own thoughts, feelings, and patterns of behavior. The personalities often are direct opposites and dominate at different times, with abrupt transitions triggered by distressful events or memories. Each may be entirely unaware of the other but aware of unexplained gaps in remembered time. In psychiatry the condition is known as dissociative identity disorder.

Read more: multiple personality: Definition from Answers.com
 
However, Abu `Uthman Sa`id ibn Al-`Abass Ar-Razi said in his book Al-Ilham wa Al-Waswasah that it was reported that some Yemeni people wrote to Imam Malik: "A male jinni has come to us and proposed to marry a young (human) woman saying, ‘I seek to stick to the right path by this proposal.'" Imam Malik answered, "I see that there is nothing wrong in doing so, but I dislike to expose this woman to a situation where she might be asked about her husband and she would answer, ‘It is a male jinni.'

So, Jinns can marry them and vice versa
 
Majini, mapepo, mizimu nk ni majina yanayowakilisha kundi la malaika walioasi mbinguni chini ya uongozi wa shetani ama Lusifa. Hawa wamegawanyika katika makundi makuu matatu. 1.) Falme na malaka, 2.) wakuu wa giza hili, 3.)majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Source ni Bible...kitabu cha waefeso 6:10-12.
 
Ubarikiwe mtumishi kwa elimu hii ya kumtambua shetani na jeshi lake la Majini(pepo wachafu) nami kwa mamlaka makamilifu ya nguvu za jina la Yesu Kristo mfufuka, nimeyataja kwa majina na kuyapiga ban from nao on. Hakuna cha kumpa nyoka wa ndani siku tatu wala nini, sekunde ile tu atakapoonekana ni Rungu kwa jina Yesu.
 
Hivi jamani watu wanaoweza kuwaza kiroho, kwa habari ya kisa cha mtu aliyetoka vitani na kumkuta mkewe mlangoni, na alipomkasirikia mke akamtaka aje aone kile kilichomfanya atoke ndani. Kuingia ndani anakuta nyoka kitandani na katika pilika za kumuuwa, walikufa nyoka na mwanamume pia. Mtume anatoa ushauri wa kwamba ukimkuta nyoka usifanye haraka kumuuwa maana anaweza kuwa ni jini aliesilimu, hapa mtume anaashiria nini? Yaani Rushdie ana haki kabisa kumhusisha huyu jamaa na aya za shetani. HAKIKA BAADA YA KUSOMA VISA HIVI VYA MUHAMADI NA MAJINI HAKUNA YEYOTE JUU MBINGUNI WALA DUNIANI ATAKAEWEZA KUNISHAWISHI NISIMUONE MHAMADI NI MJUMBE ALIYEPOKEA UJUMBE KUTOKA KWA YULE JOKA(JINI) KUU, YAANI IBILISI NA SHETANI. MJUMBE YULE YESU ALIEYENENA HABARI ZAKE, 'MKUU WA ULIMWENGU HUU, YUAJA, HANA KITU KWANGU'!!.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom