Je, majasusi kutoka ughaibuni wanatumia NGOs za Afya kuja kupeleleza nchi za kiafrika?

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Haya ni mambo fikirishi kutokana na experience yangu ya kuona mambo mbalimbali.

Je kama watanzania tumejiandaa vipi kukabiliana na uwezekano wa hali hii?

Ieleweke kuwa Afya ni eneo nyeti katika mustakabali wa nchi na wananchi.

Aidha ni muhimu kujua kuwa vita baridi vinaweza kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo mipango mikakati na ya muda mrefu katika kudhoofisha afya au kuhadaa umma hivyo afya ni tool muhimu ya vita.

Nisiwachoshe sana bali ni muhimu kama jamii tufikiri kwa kina aina za vita au hujuma zinazoweza kutumika kupitia sekta ya afya.

Umakini mkubwa unahitajika katika usimamizi wa Sekta hii.

NGOs nyingi nchini zinaingia kwa gear hii je zinafuatiliwa kwa jicho la afya na jicho la usalama?

TUTAFAKARI!MWENYE KUELEWA ANANIELEWA !

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
 
Kwasababu Nchi hii imewekeza zaidi katika kuvidhibiti kuvidhoofisha na hatimae kuviua vyama vya upinzani
Sidhani kama hizo NGO zitapewa vipaumbele kwasababu ccm inaangalia maslahi yake tu wananchi huwa ni baadae.
 
Umaskini ni kitu kibaya sana.
Sasa hivi hata wale tuliowapa dhamani ya kusimamia afya zetu wala si waamini tena maana kuna chanjo za kipuuzi nyingi zinahamashwa hadi unashindwa kuelewa kimetokea kitu gani siku hizi yaani ni kutishwa tishwa na vitafiti vya kipuuzi.
Shida naiona kwa hawa tuliowapa dhamana ya kutulinda wanatetea maslahi yao sababu ya umaskini wao
 
Umenikumbusha "Peace Corps" miaka ile...
Mkuu heb tupe vitu ..hawa jamaa ilikuaje maana 2010 nimefanya nao kaz ludewa mm nikiwa s.p.w
Kuna dada mmoja mzungu wa peace corps nilimkuta kule ana muda sana mpaka anaongea kipangwa aisee..Bt i was naive to think this fr
 
Hapa majasusi yameingia kwa mfumo wa 'Vyoo'.,hahah.
tapatalk_1574965554979.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu heb tupe vitu ..hawa jamaa ilikuaje maana 2010 nimefanya nao kaz ludewa mm nikiwa s.p.w
Kuna dada mmoja mzungu wa peace corps nilimkuta kule ana muda sana mpaka anaongea kipangwa aisee..Bt i was naive to think this fr
Unawezaje kumuachia "jirani atunze familia yako" wakati wewe "umeenda kutafuta maisha"? Yawezekana utakaporudi watoto wako wanaweza kukuita "baba mdogo"...
 
Jingalao

ARV unapewa bure.
Condom unapewa bure.
Zaidi ya 50% ya budget wanakupa wao.
Zaidi ya 50% ya viongozi wako wamesoma kwao.
Gari unalotembelea wametengeneza wao.
100% ya zana za kijeshi wametengeneza wao na nyingine wamekupa msaada.
Madini unayochimba wao ndio wanunuzi.
Dini mnazoabudu wao ndio walileta.
Internet mnayotumia ni wao wagunduzi.
Laptop zenu zote mnazotumia ni wao.
Simu za mkononi hizo iphone ni zao..
OS kwenye mifumo yenu ni zao..
Wao wana drones huna uwezo wa kuziona.
Kule angani wameweka satelite na wanaona kila kitu..

Mimi nafikiri tuendelee tu kula ugali tuache kelele..
 
Back
Top Bottom