Je Magufuli Unafahamu haya ya Karagwe

Mtanke

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2011
Messages
288
Points
195

Mtanke

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2011
288 195
M4C iliyofanyika Wilayani Karagwe hivi karibuni imebaini kuwa Wananchi wa Vijiji vya Kishao na Bugene Wilayani Karagwe wameonewa sana na kudhulumiwa na zoezi la uthaminishaji wa mali zao ili kupisha upanuzi wa barabara.
  1. Wapo waliolipwa fidia ndogo sana ukilinganisha na thamani ya mali zao na wapo waliolipwa fidia kubwa sana hali ya kuwa mali zao ni gharama ya chini.
  2. Watu wamelazimishwa kuhamisha makaburi ya wapendwa wao kwa gharama ya Tsh 70,000/= bila kujali idadi ya makaburi wakati gharama za kuhamisha kaburi moja ni Tsh 100,000/=
  3. Kaburi ya Mbunge wa kwanza wa Karagwe Marehemu John Erukana Byetima nalo limehamishwa bila kulipwa fidia
  4. Mjane mmoja amepooza baada ya kaona kaburi la marehemu mume wake likifukuliwa pamoja na makaburi ya wanawe.
Magufuli anapaswa kufuatilia swala hili kwani zoezi zima la uthaminishaji linadaiwa kugubikwa na rushwa kubwa.
View attachment 73187
Sehemu iliyokuwa na Kaburi la Mbunge wa kwanza wa Karagwe Marehemu John Erukana Byetima baada ya kaburi hilo kuhamishwa.
View attachment 73195


Maiti iliyofukuliwa

Zoezi la kuhamisha makaburi likiendelea na maiti ikiwa tayari imeshafukuliwa tayari kwenda kuzikwa mahali pengine katika kijiji cha kishao


Fidia ya nyumba hii ni Mil 3Fidia Mil 46
 

Attachments:

Kanundu

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
891
Points
0

Kanundu

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
891 0
Mtanke

Kwa huyu Mh. Magufuli anayemwambia Vasco da Gama aongeze kasi ya kusafiri nje!!! Usitarajie kupata ufumbuzi wa tatizo hilo. Heri hata nyie huko angalau mmepata fidia kidogo. Maeneo mengine ni maafa makubwa ndugu yangu. Watu hawakulipwa kabisa licha ya barabara kufuata makazi yao.

Kwa vile tatozo ni mfumo mbovu wa serikali ya CCM ukichanganya na ubabe wa huyo waziri, hapo no maumivu ndugu yangu. Halafu eti watu wanampigia kampeni za uraisi mtu kama huyo.
 

Forum statistics

Threads 1,389,291
Members 527,879
Posts 34,022,221
Top