Je, Magufuli atafikisha hata asilimia 45% kwenye uchaguzi wa 2020?

Mimi mwenyewe ccm na kuna kundi kubwa la watu wa ccm washagoma kumpa kura kama hatomwondosha batishe asafishe la batishe nadhani anaweza kupata ila kwa bashite kutuburuza asahau
 
Acha kujichosha kijana.
2020 Kura za Urais za Magufuli zitaongezeka Sana. Wengi tunaelewa dhamira yake ya dhati ya kusaidia wananchi, hasa wa chini.
Nyinyi Endeleeni kulalama na kujifarji.
Subirini mpaka 2025, over.

Hata Nyere alikuwa na dhamira ya dhati lakini aliua uchumi. Alikuwa na "tunnel vision". Maoni ya wengine yalikuw mabovi kwake hatima yake akaachia ngazi mwenyewe akikubali kushindwa. Consensus ni muhimu. Hamna anaejua kila kitu. Tunanunua ndege hata hatujui hela itarudi vipi. Ana nia nzuri ila apunguze maamuzi ya jazba ana hasira
 
Kimahesabu, kufika mwaka 2020, CCM itakuwa na wanachama zaidi ya milioni 17 wanaolipa ada ya uanachama kwa hiari kila mwaka. Na kwa mwaka huo wapiga kura wanaweza kufika milion 24 ama 25.
 
sijamwona mpinzani atayemsumbua magufuli tena uchaguz ujao atashinda kwa kishindo watanzania wengi wapiga kura wapo vijijn na waandishi wengi na wapiga kelele mitandaoni sio wapiga kura na kadi zao za wapiga kura wanatumia kwa kusajilia line za simu na kujisajil na huduma za kibenk na sio za kupigia kura km zilivyokusudiwa
 
eti kayakuta mauza uza sasa sera ya elimu bure na madudu yake ililetwa na kikwete?? kusema tununue madawati huku walimu hamna wala vitabu wala maabara ililetwa na kikwete pia??? mkuu kma huna hoja ni heri mkae kimya tu mnajidhalilisha sana kila mnapotaka kutetea kila kitu tena pasi hoja!!! nmewadharau sana wanaccm humu JF ur such empty tins eti "utaisoma namba" bullsh**t !!! mie nmesoma nje tokea o level ssa nasomaje namba kwenye elimu???
Mjirekebishe watetezi mnakera sana kila anayekosoa eti mpiga dili sijui atasoma namba sijui muuza unga!! aaaaarggghh


Enzi ya Kikwete elimu ilikuwa ziro kabisa. Jamaa alikuwa haishi nchini, yeye kila kukicha alikuwa angani, hiyo nchi angeiendeshaje?
 
Wakuu nimeamua kuwauliza swali kama mkuu wetu wa nchi kama atafikisha hata asilimia 45% katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Kwasababu nikianza kuangalia pande zote za nchi kuna vilio tupu. Wafanyakazi wanalia, Bukoba wanalia kwa kudhulimiwa hela za maafa, wabuge wanalia bila shaka mlijionea wenyewe juzi JK alipotua bugeni, wananchi wanakufa kwa njaa serikali haina shamba, wafanyabiashara wanalia, bashite kulelewa.

Hayo ni baadhi ya mambo machache ambayo mimi binafsi nitaendelea kutoichagua CCM maishani mwangu. CCM lazima tuipige chini 2020


Kwa spidi hii, Mh. rais atapata Zaidi ya hiyo 45%.....huyu ni wa kupata kura 90 - 100% kutokana kazi yake anayoifanya. Mungu amlinde Mh. rais wetu.
 
haya nijibj mmi hizi hoja maana unasema hakuna hoja
1.mikopo
2 thamani ya shilingi
3.mzunguko wa pesa
4. Kushuka kwa biashara na uwekezaji
5.Elimu kuporomoka (rejea matokeo ya form 4)
6. Viwanda??
7. Bajeti hewa??
8. Mahakama ya mafisadi imemfunga nani
9. Madawa ya kulevya nani kati ya wale mapapa waliotajwa kadhibitiwa??
10. Huduma za afya hasa vijijini average ya kituo cha afya kimoja ni baada ya kilometre 60 hapa tanzania je hapo vp
11. Umaskini (IMF inasena dollar 2 kwa siku tatu)

Niendeleee....... hizo ni zangu tu bado za wanasiasa,walimu,wafanyakazi na kero ya 15% heslb,bado waendesha malori, mkuuu kazi ipo 2020 ??
Embu tuanzie hapo kwanza

Ni maswali ya kitoto yatajibiwa na watoto wenzio."Baba mbona hujaleta mkate umeleta mhogo" ndiyo mfano wake.Tembelea vijijini upime kushindwa kwa huduma za kijamii.Mvua isiponyesha pia unategemea wenye akili timamu wahoji mbona bei ya vyakula imepanda?
IMF taarifa za uchambuzi wao wa miaka 5 iliyopita unatarajia mabadiliko yake yatokee ndai ya mwaka mmoja.Pole.2020 mtaishiwa maswali.
 
6tag_080417-160605.jpg
 
Sijalipwa hela yangu ya likizo ya mwaka jana na likizo ya mwaka huu imeshafika, ukiulizia unaambiwa no fund!!! alafu uje uchague vitu vya ajabu..!!! Yaani mtu utafikilia moyo wake hausukumi damu!!! miaka mitano inamtosha sana..
 
Ni maswali ya kitoto yatajibiwa na watoto wenzio."Baba mbona hujaleta mkate umeleta mhogo" ndiyo mfano wake.Tembelea vijijini upime kushindwa kwa huduma za kijamii.Mvua isiponyesha pia unategemea wenye akili timamu wahoji mbona bei ya vyakula imepanda?
IMF taarifa za uchambuzi wao wa miaka 5 iliyopita unatarajia mabadiliko yake yatokee ndai ya mwaka mmoja.Pole.2020 mtaishiwa maswali.
Mkuu jibu basi hizo hoja!! eti za kitoto haya niambie hizo za kiutu uzima basi hapa maana unakalia IMF huku hutoi specifc data tuzichambue hapa nikuonyeshe mlivyo waongo!!!
Haya bas at least nijibu hya maraisi

1.je ni sawa kujenga airport chato mji ambao hauna kivutio chochote cha utalii au movement ya biashara huku kilometer 10 tu kutokan airport hakuna maji wala choo??

2. Viwanda vitaanza kunjengwa lini kma mlivyoahidi kwenye kampeni??

embu tuanzie hapo kabla sijakuuliza kuhusu kwanno mnaweka bajeti kubwa mwisho wa siku utekelezaji wake ni chini ya 40%
 
Hivi zile million 50 zimeshatoka kwa kila kijiji?? Najaribu kuwaza kwa sauti
 
Wakuu nimeamua kuwauliza swali kama mkuu wetu wa nchi kama atafikisha hata asilimia 45% katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Kwasababu nikianza kuangalia pande zote za nchi kuna vilio tupu. Wafanyakazi wanalia, Bukoba wanalia kwa kudhulimiwa hela za maafa, wabuge wanalia bila shaka mlijionea wenyewe juzi JK alipotua bugeni, wananchi wanakufa kwa njaa serikali haina shamba, wafanyabiashara wanalia, bashite kulelewa.

Hayo ni baadhi ya mambo machache ambayo mimi binafsi nitaendelea kutoichagua CCM maishani mwangu. CCM lazima tuipige chini 2020
Rais Magufuli anaauwezekano mkubwa katika uchaguzi mkuu wa 2020 akapata kati ya asilimia 70 na 80. Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015 kiu kikubwa cha watanzania ilikuwa ni mabadiliko na Rais Magufuli bila kujali kupoteza umaarufu wa chama chake ameamua kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya serikali na ndani ya chama tawala. Kiongozi yeyote ambaye analeta mabadiliko huwa umaarufu wake hushuka sana lakini baada ya muda fulani umaarufu wake hupanda kwa kasi. Tuangalie jinsi ya utendaji wa Rais Magufuli :
1. Vita dhidi ya ufisadi ameonyesha dhamira ya kweli ufisadi umepungua kwa asilimia kubwa.
2. Vita dhidi ya ujangili imefanikiwa kwa kiasi kikubwa na hii itafanya sekta utalii kukua sana.
3. Vita dhidi ya madawa ya kulevya imefanikiwa sana na Tanzania imesifiwa sana kwa vita hivi.
4. Vita dhidi ya uvuvi haramu imefanikiwa sana tutegemee samaki kuongezeka kwa kiasi kikubwa.
5. Matumizi mabovu ya serikali yamedhibitiwa.
6. Ukwepaji wa kodi na misamaha ya kodi yamepungua sana.
Pamoja na deni la taifa kukua nina uhakika baada ya serikali ya awamu ya tano ikiweka mambo yake sawa wataweza kulipa deni hilo kwa haraka kwani ilikuwa ni lazima kwa serikali kuchukua mikopo baada ya serikali ya awamu ya nne kuiacha nchi katika hali mbaya ya kiuchumi. Kwa muda wa miaka miwili serikali imeonyesha inaweza kufanya maendeleo makubwa mfano:
1. Kufufuliwa kwa shirika la ndege la Tanzania
2. Ujenzi wa reli wa Dar - Morogoro
3. Kufufua sekta ya afya kwa kugawa vifaa kwenye hospital zote nchini
4. Ujenzi wa hospital ya rufaa Mara
5. Ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa chuo kikuu Dar uliochukua gharama ndogo na muda mfupi.
Hapo ni nimeorodhesha baadhi ya jitihada ya serikali ya awamu ya tano, je miaka mitatu mingine tutatarajia mengi zaidi. Pamoja na makusanyo ya kodi kushuka uwiano huo utaenda na matumizi mazuri wa serikali.
Ndugu zangu Watanzania bila kujali Itikadi ya chama lazima tuangalie nia madhubuti ya serikali ya awamu ya tano. Wafadhili wameona nia dhabiti ya serikali hii ndio maana kwasasa wameamua kutoa mikopo na misaada kwa Tanzania.
In conclusion President Magufuli ia a great asset to Tanzania.
 
Kura zake ziko katika kinywa cha mwenyekiti wa tume ya uchaguzi! Haziko kwenye sanduku la kura! NA tangazo la Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi haliwezi kupingwa mahakamani! Sheria hairuhusu kupinga mahakamani! Goli la mkono linalodaiwa na Nape lipo hapo!!!!
 
Watanzania wana akili sn km ulikuwa hujui na pia ni wanafiki wazuri...subir uone upinzaninunavyofeli tena
 
Back
Top Bottom