Je, magazeti yetu ndivyo yalivyo au...?

Mwakilishi

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
484
29
Katika kusoma kwangu habari nyingi katika magazeti yetu napata wasiwasi kuwa si ajabu habari nyingi kama sio zote zimeandikwa au niseme zinaandikwa kishabikishabiki zaidi na wakati mwingine waandishi badala ya kuripoti tukio zima ataelemea kwenye kipengele kimoja anachoona kitauza gazeti lake na hivyo kupelekea kutoa taarifa nusunusu au hata kupotosha ukweli wa tukio zima.

Mifano iko mingi ila nakumbuka hii ya hivi karibuni, huu unaomhusu waziri Masha? Je ni kweli aliitisha mkutano akiwa na ajenda kuu ya kumtetea Ridhiwani Kikwete au ajenda kuu ilikuwa nyingine na hili la Ridhiwani lilikuwa katika "mengineyo" aka "by the way" na siyo mada kuu kama ambavyo mwanahalisi walivyoiweka?

Vilevile katika mkutano wa chadema je kilichoongelewa ni ufisadi tu kama inavyoripotiwa au kuna mengine yanayohusu sera za chama hicho ambayo yaliongelewa ila waandishi wameona hayalipi na hivyo kutoyaripoti?

Hivi magazeti yetu ndivyo yalivyo? Najiuliza tu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom