Je maduka ya kenya yamefurika bidhaa za tanzania kama alivyodai jk? Idumu eac!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je maduka ya kenya yamefurika bidhaa za tanzania kama alivyodai jk? Idumu eac!!!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by JokaKuu, Nov 25, 2010.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Nov 25, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,732
  Likes Received: 4,950
  Trophy Points: 280
  ..kwenye hotuba yake bungeni Kikwete alidai kwamba sasa hivi Tanzania inauza zaidi Kenya kuliko wao wanavyouza Tanzania!!

  ..yaani kwa maana nyingine ni kwamba ktk suala la trade imbalance imekula kwa Wakenya.!!

  ..je, ukitembelea Kenya basi utakuta maduka yao yamesheheni bidhaa toka Tanzania?

  ..kama si hivyo tunauza kitu gani huko Kenya na kwa faida gani na ya nani?
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Labda atudanganye kuhusu ulaya anapokwendaga mara kwa mara pengine walala hoi hawawezi kufika huko lakini kwa Kenya, asitudanganye hata kidogo.
   
 3. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mkuu tunauza raw materials tu huko kenya kama machungwa ya tanga, mananasi,mahindi, maziwa fresh ambayo wanaya-pack na kuturudishia kwenye ma-box na kujaza maduka yetu hatuna finished good tunazouza kenya mkuu!
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Nov 25, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,732
  Likes Received: 4,950
  Trophy Points: 280
  ..hii statement ilitakiwa itengenezewe political ad.

  ..upinzani wakati mwingine naona kama wako magoi-goi.
   
 5. G

  Gaza Senior Member

  #5
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 103
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  inawezekana raisi kadanganywa tena kwa sasa niko Kenya sioni bidhaa yoyoteya Tz kwenye maduka ya hapa kidogo naona maji ya uhai Mombasa kwa Nrb sijaona labda mazao kama mandi ,mashudu, ngwasha
   
 6. G

  Gaza Senior Member

  #6
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 103
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  inawezekana raisi kadanganywa tena kwa sasa niko Kenya sioni bidhaa yoyote ya Tz kwenye maduka ya hapa kidogo naona maji ya uhai Mombasa kwa Nrb sijaona labda mazao kama mandi ,mashudu, ngwasha
   
 7. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2010
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280

  Mbayuwayu akikwambia kitu changanya na za kwako :redfaces:
   
 8. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2010
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,960
  Likes Received: 20,299
  Trophy Points: 280
  Nadhani rais anajua tofauti ya bidhaa malighafi, na pia anajua kabisa hawezi kuulizwa na mtu atoe ufafanuzi wake kwa sababu anajua wengi wa watz si wenye kupenda kuelewa na kuutafuta ukweli (inquistive). Ninachoweza kueleza kuwa mheshimiwa rais alikuwa anaeleza kinyume chake kwamba Kenya wanaongoza kwa kuingiza bidhaa zao na sisi tumezizoea na kuzipenda na kuziona ni kama zetu vile na ndiyo maana unapoiona OMO unadhani ni ya Tz na kwa kuwa sasa hapa dsm imepotea m2 unafikiri uchaguzi umesababisha bidhaa hii ipotee

  Tuutafute ukweli na kwa hapa bwana JMK alitudanganya makusudi na wala sio kusema kwamba alishauriwa vibaya.
  :hungry:
  INAWEZEKANA KABISA MTU ASIJUE KUSOMA LAKINI HATOELEWEKA AKIIGEUZA PICHA CHINI JUU
   
 9. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Wakuu acha Kenya ni Mbali Bidhaa zetu zenyewe sizioni kwenye maduka yetu Tanzania.... Thinking about it Kuna mtu anaweza kunitajia bidhaa tofauti 20 ambazo zinatengenezwa Tanzania, I fail to name even 5 hapa tu nilipo sasa nikione mezani kwangu from kalamu, karatasi, nguo, viatu, etc none of them has made in Tanzania
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  Nov 25, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Asikudanganye mtu mkuu, niko hapa na tunauza bidhaa moja tu, nayo ni pombe, Castle lager tu, anayebishi aje na data.

  Na hayo matunda yakifika hawasemi kuwa yanatoka bongo bali wanasema yanatoka ukambani. jamani tuache siasa za uongo majukwani twende kwenye utendaji majimboni!
   
 11. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #11
  Nov 25, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Ndiyo maana nasema JK na watu wake wasidhani sisi watanzania ni wajinga sana..

  Sijawahi kuona bidhaa ya TZ kenya hata siku moja.. ni kwa nini bei ya bidhaa zetu ziko juu sana.

  Mf. X-Pel dawa ya mbu hapa tanzania kwanza haipatikani, pili ukiipata ni Tshs. 7,500/= sasa ukinunua kwa bei hiyo hapa kenya itauzwa shilingi ngapi wakati DOOM inauzwa kenya kwa Tshs. 3500 za kibongo.?

  sisi tunapeleka kule malighafi tu tena tunauza bei ya kutupa... wanazitengezeza na kuzipack wanarudisha hapa bei juu..
   
 12. N

  Newvision JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maskini tanzania yangu kama ni kudanganywa na presdooo tunadanganywa kweli!!
   
 13. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Kakae chalinze uone malori ya mwekezaji mufindi papers yanavyopita kuelekea nairobi huku yakiwa yamebeba rolls za miti ghafi utalia na huku tz tuna import karatasi toka brazil,sa hiyo ni kutudangaya watz na sasa wachina wameamua kenya kuwa business point ya africa
   
 14. Tundapori

  Tundapori JF-Expert Member

  #14
  Nov 25, 2010
  Joined: Aug 12, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Sio kweli. Sisi watanzania tutabaki wadanganyika mpaka kufa.
   
 15. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #15
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Na ninyi msiwe mnabisha tu! Ni kweli bidhaa za Tanzania zimejaa Kenya. Nyumba nyingi Nairobi zina ma house-maid kutoka Tanzania, na hasa singida na kondoa na kuna akina mama ambao biashara zao kubwa ni kuwauza hawa mabinti kwa wakenya ili wakatumike kwa kazi za ndani. Halafu pia CD za hii miziki ya kitoto (Bongo flava) iliyochakachuliwa pia iko kibao Nairobi. JK is right, we are exporting more to Kenya (snigger!)
   
 16. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,791
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  ushuzi mtupu.
  hakuna bidhaa za TZ zilizofurika KE.

  wakenya wanakuja Shinyanga na Mwanza na kisha wananunua Ng'ombe then wanakwenda nao huko kwao na kuwachinja na kuwahifadhi vizuri kisha kuja kuuza nyama ktk makampuni ya Migodi ya huko huko Tanzania, nyie mpo tu mnasubiri kujilia ugali na kumbikumbi siku ipite...
  Amkeni
   
 17. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Sijui Nchi yetu inapokwenda... viwanda vimetushinda, kilimo kimetushinda, kodi zetu zinaashia kwenye matumbo ya wachache, mwatex, general tyre e.t.c they are all gone. Still viongozi wetu wanacheza na statistics kwamba uchumi umepanda, wawekezaji wameongeza, maisha bora.... ALL I KNOW NI KWAMBA LIFE SUCKS UNLESS YOU ARE FISADI
   
 18. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #18
  Nov 26, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,278
  Likes Received: 19,430
  Trophy Points: 280
  mbwabwajaji tu huyu nayo .. anatudanganay kama watoto
  mim natajka tu niione kigoma ikiwa kama dubai
   
 19. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #19
  Nov 26, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Naungana na wewe mkuu, hii ni kutupumbaza tu. Hakuna bidhaa inayozalishwa Tanzania inayoweza ku-compete kwenye soko la Kenya. Tunachouza Kenya ni malighafi tu, na katika dunia ya leo ukiona mtu anajitapa kwa kuuza malighafi basi ujue kuwa huyo hazimo kichwani. Sasa hivi hata magengeni utakuta bidhaa nyingi zimetengenezwa Kenya, ukiingia supamaketi kama utaona bidhaa ya Tanzania sanasana ni kahawa ya Africafe. Otherwise sioni kitu cha maana chenye ongezeko ya thamani kinachozalishwa TAnzania. kama kipo basi ni sigara, bia, maji ya chupa...ambavyo kenya pia vipo tena vizuri na bei rahisi zaidi.
   
 20. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #20
  Nov 26, 2010
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 430
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hizo zilikuwa "Fix" za Kikwete ili kupamba hotuba yake. Tutauza bidhaa gani Kenya wakati CCM walishahujumu viwanda vyote alivyoacha Nyerere kwa kuwakabidhi "maswahiba" zao wahindi na manyang'au wengine waliogeuzaviwanda vyetu kuwa ma"godowns" ya mitumba toka kwao? Hujuma za chama hiki zimeirudisha tanzania miaka 30 hadi 40 nyuma kwani sasa Tanzania ni Teja la nchi hata zilizokuwa chovu zaidi yetu wakati tunajitawala. CCM imetufikisha mahala ambapo hata vichokoo meno (tooth picks) chupi, sidiria na soksi tunaagiza toka China, Taiwan na hata Vietnam! Sasa anayesema tunauza bidhaa nyingi Kenya atuambie ni bidhaa zipi hizo kama sisi wenyewe tunaagiza hadi chupi toka nje tena za mitumba!
  Watanzania wenzangu wakati wa kuungana kudai mabadiliko ya Katiba yatakayoibana serikali "kuhaini" maamuzi yetu ni sasa. CCM haina jipya labda hizi blaablaa za Kikwete za udini na ukabila anaouhubiri awamu hii kwa nia ya kuandaa mazingira ya kusukuma agenda zake za kuvunja Katiba siku za mbele.
  Nasema utawala wa CCM miaka mitano ijayo ni maafa ya taifa yanayoweza ponyeka kwa miaka mingi ijayo. Binafsi siwalaumu wapiga kura kwani wote tunaelewa walichofanya hawa manyang'au ili kuupiundua uamuzi halali na sahihi wa wananchi, uhaini utakaohukumiwa na vizazi vyote vijavyo.
   
Loading...