Je madaktari waliogoma wanaweza kufungiwa leseni za kufanya kazi popote pale?

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,442
3,198
Naomba kujua kama madaktari waliogoma wanaweza kufutiwa/ kufungiwa vyeti au vibali vyao vya kutoa huduma sio tu hapa nchini bali katika nchi yoyote kwa kiuka kiapo chao. Sheria zinasemaje?
Naomba kuwakilisha.
 
Hapana, kila nchi inautaratibu wake. Hivyo ukitaka kwenda kufanya kazi nchi nyingine itakubidi ufuate taratibu za usajiri wa nchi husika. Hapa tanzania unasajiriwa na Tanganyika Medical Council.
 
Je nchi haiwezi kuwanyanganya vyeti au kuwazuia wasiende nje ya nchi kwa kuwa wana kesi ya kujibu i.e ikiwa watafunguliwa kesi mahakamani?
 
Unapotaka kwenda kufanya kazi nchi nyingine unahitaji nyaraka mbili. 1. registration toka nchi yako kuonyesha kuwa umesajiliwa kama daktrari nchini kwako na 2. certificate of good conduct, kuthibitisha kuwa huna kesa wala misconduct katika nchi uliyopractice.
Iwapo daktari atathibitika kukiuka maadili na akaadhibiwa kwa kufuata kanuni za maadili anaweza kukosa nyaraka hizi na kushindwa kufanya kazi nje ya nchi. Hata hivyo kuna nchi ambazo hazizingatii sana nyaraka hizi kutegemeana na aina ya majukumu atakayopewa daktari husika katika nchi hiyo.
 
Nilisikia Raisi akisema, hatua za kinidhamu zitachululiwa na mwajiri dhidi ya madaktari waliogoma
 
Ndiyo Serikali inaweza kukufuta kazi(unapoteza nafasi) na utumishi(vyeti vyako vinapigwa ban).
 
Back
Top Bottom