Benito Mussolini
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 381
- 322
Wanabodi,
Mpaka sasa, nafikiri kwamba wengi tutakuwa tumeisha uzoea mwaka 2025. Mwaka ambao kama watanzania, tutatekeleza haki yetu ya kikatiba ya kuchagua viongozi wetu.
Wafuasi wa vyama vya upinzani watakuwa wakwanza kurusha jiwe na kuiponda serikali ya Rais Samia kwa mapungufu ambayo kwa kweli ni madogo sana. Miradi ya maendeleo ya kila aina itakayo endelea kutekelezwa kwa miaka mingi ijayo, uongozi bora katika kipindi kigumu cha kubadili madaraka,hamasa kwa wananchi wanao mpenda na kumuunga mkono rais wao, ni sukari nyingi sana kwenye chumvi kidogo sana.
Chumvi hiyo kidogo ndio imechochea kauli mbiu ya “No reforms, no election” kutoka kwa wana CHADEMA. Ingawa mapendekezo ya Tundu Lissu ya kuahirisha uchaguzi ili kupisha mchakato wa katiba mpya na tume huru yanakosa uhalisia, ni vyema kulitazama upya suala hili la uchaguzi ili kufahamu kama kuna vichocheo vingine vinavyoweza kubatilisha uchaguzi wa mwaka huu.
Chama chochote kilichosajiliwa nchini kinatakiwa kiweze kufanya shughuli zake za uenezi na kwasababu hiyo kuongeza wanachama. Kuelekea uchaguzi kama wa mwaka huu, wanachama waaminifu ni rasilimali kubwa kwa vyama vya siasa. Rasilimali hii inaweza isiwe mbaya, lakini pia huweza kuleta ushindani usiohalali ambao husababishwa na ukongwe na mabavu.
Kwenye uchaguzi wa 2020, watu 14,662,764 hawakupiga kura. Waliopiga kura ni watu 15,091,950 ambayo ni sawa na asilimia 50.72 ya watu wote walio sajiliwa. Kwa takwimu hizi, kuwa na wanachama 12,000,000 (ambao tayari watakuwa wamefanya maamuzi ya viongozi wanao wataka kabla ya kipindi cha kampeni) kama ilivyo elezwa na mwenezi wa CCM Amos Makala, ni advantage ambayo ni unfair na ambayo haiendani na misingi ya demokrasia.
Kuna ambao watasema kwamba wengi wape hata kama kuna upendeleo lakini Ile chumvi kidogo inadhirisha kwamba kuna hitilafu zaidi ya hii niliyoeleza kwenye sheria za uchaguzi na hata labda ugandamizi wa uhuru wa vyama vya siasa nchini katika kufanya shughuli zao.
Jambo hili linaweza kutatuliwa kikatiba kwa kuwa na utaratibu wa kuwezesha ushindi wa mgombea yoyote wa urais kuwa sawa kwenye majimbo yote. Yaani kama mshindi wa jimbo anapewa pointi kwa kushinda jimbo moja, basi pointi hizi ziwe sawa kwa majimbo yote. Kama utaratibu huu utafuatwa basi mshindi wa uchaguzi wa urais atakuwa yule aliyepata pointi kadhaa na sio yule mwenye idadi ya kura nyingi.
Lakini bado ni chumvi kidogo kwenye sukari nyingi na kwasababu hiyo ni ngumu sana kwa vuguvugu hili kuleta manufaa yoyote. Sitegemei hili kuwa sababu ya Rais Samia kushindwa uchaguzi au sababu ya CCM kupotea kwenye ramani ya siasa,hiyo sio nia yangu. Nia yangu ni kwa chama tawala kutumia nguvu na uzoefu ulionao kutenda mema na sio kuwaonea wanyonge.