Je, Maalim Seif ndiye aliyemchongea Mzee Jumbe kwa Mwalimu??

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,269
54,664
..sijui kama wengi wenu mlikuwepo au mnakumbuka mtafaruku wa kisiasa uliosababisha kujiuzulu kwa Makamu wa Raisi wa Muungano na Raisi wa Zanzibar Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi.

..nakumbuka mtafaruku huo ulipelekea mpaka Raisi wa Msumbiji wakati ule, Field Marshal. Samora Moises Machel, kuja Tanzania na kuhutubia Halmashauri Kuu ya CCM.

..Mzee Ali Hassan Mwinyi alichukua nafasi ya Aboud Jumbe -- inasemekana alipendekezwa na Sheikh Thabit Kombo Jecha. Maalim Seif Shariff Hamad aliteuliwa Waziri Kiongozi kuchukua nafasi ya Brigadier.Ramadhani Haji Faki.

..nimeipata makala hii toka gazeti la Raia Mwema, na kuna madai na tetesi kwamba Maalim Seif Sharriff alihusika na kuchomoa toka ofisini kwa Raisi wa Zanzibar makala kesi ya kikatiba dhidi ya serikali ya Muungano.

Joseph Mihangwa | Raia Mwema said:
Chaguo la Nyerere la mrithi wa Kawawa lilishutua wengi. Edward Moringe Sokoine, ambaye kabla ya kuteuliwa, alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, hakuwa mmoja wa wanafunzi au wafuasi wa Mwalimu; wala hakuwa na jina kwenye duru za siasa kabla ya uhuru. Uteuzi wa Sokoine kwa nafasi ya Waziri Mkuu nusura uvunje Muungano wa Tanzania. Kwa nini?

Rais Aboud Jumbe Mwinyi, Rais wa Awamu ya Pili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais, aliyechukua wadhifa huo kufuatia kifo cha Mzee Abeid Amani Karume, mwaka 1972; tofauti na Karume, alipania kuimarisha kwa vitendo Muungano kwa kuwa karibu kiutendaji na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Nyerere.

Tena tofauti na Karume, Jumbe aliweza kumwakilisha Nyerere nje ya nchi mara nyingi; alitembea nchi nzima akitoa hotuba ndefu kutetea Muungano na hatimaye kuridhia kuunganishwa kwa vyama vya ASP na TANU kuunda CCM, jambo ambalo lisingewezekana enzi za Karume.

Kwa sababu hii, Jumbe alianza kujihesabu kama mrithi halali wa Nyerere asiyeepukika kwa kiti cha Rais wa Tanzania. Jumbe akatumia muda mwingi kwa shughuli za Muungano na kumwakilisha Rais nje; akaitelekeza Zanzibar kwa matarajio ya kuukwaa urais wa Jamhuri ya Muungano.

Nao utendaji kazi wa Sokoine ulianza kujionyesha muda mfupi tu baada ya kuteuliwa. Alijipambanua kama mtekelezaji na mfuatiliaji mzuri wa maamuzi ya Serikali, mkweli na mwenye kujali watu; hasa Wanyonge. Hakupenda kuonea wala kuonewa.

Kwa sababu hii, alipendwa na wengi, hasa watu wa tabaka la chini; kiasi kwamba katika kipindi kifupi Taifa liliimba na kushangilia jina na sifa zake. Nyerere akafurahi na kumweka moyoni.

Habari zikavuja kwamba tayari Mwalimu Nyerere alikuwa amemweka Sokoine moyoni na katika kitabu chake kuwa mrithi wake mtarajiwa baada ya kung'atuka. Naye Jumbe akanusa upepo; uhasama ukaanza kati ya viongozi hao wawili.

Hatua ya kwanza ya Jumbe ilikuwa ni kuhoji mfumo wa uhalali wa Muungano na Sheria iliyouanzisha. Nayo Redio Zanzibar ikadaka haraka wimbo wa Jumbe, kwa kutangaza maneno ya kashfa dhidi ya Muungano kupitia kipindi kilichojulikana kama "Kiroboto Tapes", au Kanda za Kiroboto.

Na katika Sherehe za Mapinduzi mjini Unguja, Januari 12, 1984 ambazo Mwalimu alihudhuria, Jumbe aliendeleza uchokozi wake wa kuhoji Muungano na kuwataka Wazanzibari watulie wakati akishughulikia suala hilo. Akasema ikibidi angelifikisha kwenye Mahakama Maalum ya Kikatiba ili kupata ufumbuzi.

Hatua nyingine aliyochukua ni ya kumrejesha kwao Bara, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mheshimiwa Damian Lubuva; na badala yake akamteua Al-Haji Bashir Kwaw Swanzy, raia wa Ghana, na rafiki wa Jumbe tangu 1958.

Kisha Jumbe alimwagiza Swanzy kuandaa Hati kupeleka Mahakama ya Kikatiba kuhoji mfumo na uhalali wa Muungano.

Na baada ya hati hiyo kuwa tayari na kuwekwa mezani kwa Jumbe ili aitie sahihi, ilipotea katika mazingira ya kutatanisha, na kuibukia mikononi mwa Mwalimu Nyerere. Duru zinadai kuwa ni Seif Sharif Hamad aliyepora hati hiyo na kuipeleka kwa Mwalimu.

Mwalimu akachemka, akaitisha kikao cha dharura cha NEC mjini Dodoma ambako Jumbe aliitwa kujibu tuhuma za kutaka kuvunja Muungano. Na baada ya kukiri kuandaa hati hiyo, alivuliwa nyadhifa zote za Chama na Serikali na ikatangazwa "Hali ya kuchafuka kwa hali ya hewa ya Kisiasa Visiwani".
 
Ndio ni kweli seif sharif hamad alimchoma jumbe kwa nyerere ,na lengo lake ni kwamba alitegemea kwamba atapewa urais wa zanzibar lakini hakupewa .cha ajabu ni kwamba sasa hivi seif anapiga kelele za kuvunja muungano .but why he didn't support jumbe at that time?well the answer is the guy is a fraud anapenda madaraka .siku zote katika kugombea urais wa zanzibar kwa tiketi ya cuf hamruhusu mtu yoyote kuchukua form .
 
..sijui kama wengi wenu mlikuwepo au mnakumbuka mtafaruku wa kisiasa uliosababisha kujiuzulu kwa Makamu wa Raisi wa Muungano na Raisi wa Zanzibar Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi.

..nakumbuka mtafaruku huo ulipelekea mpaka Raisi wa Msumbiji wakati ule, Field Marshal. Samora Moises Machel, kuja Tanzania na kuhutubia Halmashauri Kuu ya CCM.

..Mzee Ali Hassan Mwinyi alichukua nafasi ya Aboud Jumbe -- inasemekana alipendekezwa na Sheikh Thabit Kombo Jecha. Maalim Seif Shariff Hamad aliteuliwa Waziri Kiongozi kuchukua nafasi ya Brigadier.Ramadhani Haji Faki.

..nimeipata makala hii toka gazeti la Raia Mwema, na kuna madai na tetesi kwamba Maalim Seif Sharriff alihusika na kuchomoa toka ofisini kwa Raisi wa Zanzibar makala kesi ya kikatiba dhidi ya serikali ya Muungano.

This is very interesting sikuwa naijua hii hehehehe kazi kweli kweli
 
Kilichomponza Jumbe ni udhaifu wake mwenyewe pale aliporuhusu Faki na genge lake kumzidi nguvu. Nakumbuka Jumbe hali ilimuwia ngumu huko akaamua kuja bara na kukaa Musoma Desemba 1983 yote pale Musoma Hotel. Alirejea kwao siku ya sherehe za mapinduzi 1984. Ilikuwa kero hata kwa mzee Mwingira (RC wa Mara wakati huo) kwani pengine kwa hasira za mwalimu, hata gari la ikulu kwa siku zote hizo hakupewa, akawa anatumia la RC.

Hotuba aliyoitoa mwalimu siku ya sherehe za mapinduzi 1984 inaeleza kwa ufasaha kuchukizwa kwake na udhaifu huo wa Jumbe!
 
Thanks Mkuu, Hizi nyeti sikuwahi kuzisikia...
 
kwa maana hiyo muelewe kuwa hadithi inakuwa na pande mbili sasa tukichukuwa huo upande mmoja wa kuwa seif alimchomea Mzee Aboud jumbe inamana leo hii watanganyika msingeweza kutuchezea au kuingilia mambo ya Zanzibar kama ilivyokuwa kabla ya kunganisha ASP na TANU
na mgekuwa mnaendelea kuingia na pass na kama sio vissa kabisa ,kwa hiyo mshukuruni seif Hamadi kama kweli alifanya hayo na ndio leo mnajivunia kuwa na Nchi yenye proper name for the first na kulikana Tanganyika.
 
Mbona mnasikiliza upande mmoja tu, Aboud Jumbe naye ameandika kitabu kuhusu sakata hili, kinaitwa:

The partner-ship -Tanganyika-Zanzibar union : 30 turbulent years
by Aboud Jumbe
Published in 1994, Amana Publishers (Dar es Salaam, Tanzania)
 
Kinapatikana katika maduka gani hichi kitabu Mkuu
 
Mimi nina nakala ya zamani ila naona online kipo, kigugo; pia tafuta kitabu hiki ambacho kina taarifa mpya kuhusu sakata hilo la kuchafuka kwa hali ya hewa:

  • £24.95
Pan-Africanism or Pragmatism

Lessons of the Tanganyika-Zanzibar Union
Issa G. Shivji

The Pan-Africanist debate is back on the historical agenda. The stresses and strains in the union of Tanganyika and Zanzibar since its formation some forty years ago are not showing any sign of abating. Meanwhile, imperialism under new forms and labels continues to bedevil the continent in ever-aggressive, if subtle, ways. The political federation of East Africa, which was one of the main spin-offs of the Pan-Africanism of the nationalist period, is reappearing on the political stage, albeit in a distorted form of regional integration. It is in this context that the present study is situated. Backgrounding the major dramas of the union of Tanganyika and Zanzibar this book studies the personalities involved and their politics, and includes an account of the Dodoma CCM conference that toppled President Jumbe. It is also a detailed legal analysis of the union incorporating powerful new material.

ISBN 9789987449996 | 336 pages | 229 x 152 mm | 2008 | Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania | Paperback
 
Mi kama namuona Seifu amesimama mbele eti ndio ananiongoza, ntarudi kwetu kulima. Kuna watu wanaota madaraka tu hawana lolote la kuchangia.
 
Mimi nina nakala ya zamani ila naona online kipo, kigugo; pia tafuta kitabu hiki ambacho kina taarifa mpya kuhusu sakata hilo la kuchafuka kwa hali ya hewa:

  • £24.95
Pan-Africanism or Pragmatism

Lessons of the Tanganyika-Zanzibar Union
Issa G. Shivji

The Pan-Africanist debate is back on the historical agenda. The stresses and strains in the union of Tanganyika and Zanzibar since its formation some forty years ago are not showing any sign of abating. Meanwhile, imperialism under new forms and labels continues to bedevil the continent in ever-aggressive, if subtle, ways. The political federation of East Africa, which was one of the main spin-offs of the Pan-Africanism of the nationalist period, is reappearing on the political stage, albeit in a distorted form of regional integration. It is in this context that the present study is situated. Backgrounding the major dramas of the union of Tanganyika and Zanzibar this book studies the personalities involved and their politics, and includes an account of the Dodoma CCM conference that toppled President Jumbe. It is also a detailed legal analysis of the union incorporating powerful new material.

ISBN 9789987449996 | 336 pages | 229 x 152 mm | 2008 | Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania | Paperback

Akhsante sana kwa msada wako.
 
kwa maana hiyo muelewe kuwa hadithi inakuwa na pande mbili sasa tukichukuwa huo upande mmoja wa kuwa seif alimchomea Mzee Aboud jumbe inamana leo hii watanganyika msingeweza kutuchezea au kuingilia mambo ya Zanzibar kama ilivyokuwa kabla ya kunganisha ASP na TANU
na mgekuwa mnaendelea kuingia na pass na kama sio vissa kabisa ,kwa hiyo mshukuruni seif Hamadi kama kweli alifanya hayo na ndio leo mnajivunia kuwa na Nchi yenye proper name for the first na kulikana Tanganyika.

Ni nani wanaoingia kwa mwenzake sana???mie nafikiri wazanzibar ndio wanaingia bara sana na kujenga huko!!au???na wazanzibar wangeingia bongo kwa visa na pasi na kutulipa fees kibao za ukazi.wamshukuru Seif kwa kuwakoa hao wapemba waliojazana kariakoo na iilala wangetulipa kodi kibao.
 
Kama kawaida watu wanapiga soga bila ya kujadili maada kimtazamo.Mie nimesoma sababu za Seif na gurupu lake kumtema Jumbe...kwa character za Jumbe, anavyosema Seif ni kuwa huyo kiumbe alikuwa ni kama Sadam.

Nao waliona kama Jumbe angelifanikiwa, basi Zanzibar kungelipatikana dictator mwengine.Hiyo ndio sababu yake ya msingi kutoka katika kitabu chake...

Sasa alie na kitabu cha Jumbe ameeleza nini kuhusiana na scandal hiyo...mimi sipati kitabu hicho kwenye google na wala sina kopi.Mwenye nacho tafadhali tupatie sababu za Jumbe tuzisikie kwanini wazanzibari wakamchezea mchezo wa kumtema.
 
Ndio ni kweli seif sharif hamad alimchoma jumbe kwa nyerere ,na lengo lake ni kwamba alitegemea kwamba atapewa urais wa zanzibar lakini hakupewa .cha ajabu ni kwamba sasa hivi seif anapiga kelele za kuvunja muungano .but why he didn't support jumbe at that time?well the answer is the guy is a fraud anapenda madaraka .siku zote katika kugombea urais wa zanzibar kwa tiketi ya cuf hamruhusu mtu yoyote kuchukua form .
Duh! ndugi yangu Muunguja, baada ya chuki zako na majungu juu ya Maalim Seif kutokufanya kwenye mzalendo, umeonelea uje hapa na majungu yako. Ni wapi wewe umewahi kusikia Maalim Seif ametamka kuwa ana adh-ma ya kuvunja Muungano? Wewe ni Mu-Islamu na huu ni mwezi wa ramadhani, heshimu funga yako na heshimu mwezi huu mtukufu.

Watu kama hawa ni wabaya kuachiwa kwenye forum kama hizi. Hawa ndio wanao palilia fujo, pengine hata hayupo Tanzania. Mara ya mwisho kumsikia Maalim seif juu ya Muungano huo. Ni kuwa Zanzibar haiko tayari kuwa na adui jirani. Kwa maana kam unavunja Muungano, basi kutakuwa na Tanganyika akiwa ni adui yako. Leo tuna ona India na Pakistan. Wamekuwa na ugomvi wa siku nyingi. India ikasambaratika, kukawa na pakistani, Bangaladesh, Sril lanka... Pakistan wamekuwana vita na India kitambo.

Juzi tu, India ametowa msaada wa dola milioni tano. Pakistan amezipokea bila kutaka. Lakini utafanyeje wakati huyo ndo jirani yako, sisi waislamu tunafunzwa kitu cha mwanzo ni jirani yako, ikisha ndio ndugo yako... Muunguja, Tahadhari na mdomo wako, usiwashe moto usiweza kuuzima....
 
Nawasalimu ..nDUGU WANA jf naomba mwenye ufahamu au any document ya kilichomsibu mzee A.J Mwinyi enzi zile akiwa madarakani, na uhusika wa Maalim Seif Sharif Hamad, na CCM yao kwa ujumla na Mwl. JKN enzi zile..Nauliza hivi kwani nakumbuka niliwahi soma article fulani ambayo ilikuwa ni kijikaratasi tu, ikavuta hisia zangu..Taf. kama ilikwisha anikwa hapa jamvini miaka au siku zilizopita naomba nielekezwe,,Ahsante..
 
Duh! ndugi yangu Muunguja, baada ya chuki zako na majungu juu ya Maalim Seif kutokufanya kwenye mzalendo, umeonelea uje hapa na majungu yako. Ni wapi wewe umewahi kusikia Maalim Seif ametamka kuwa ana adh-ma ya kuvunja Muungano? Wewe ni Mu-Islamu na huu ni mwezi wa ramadhani, heshimu funga yako na heshimu mwezi huu mtukufu.

Watu kama hawa ni wabaya kuachiwa kwenye forum kama hizi. Hawa ndio wanao palilia fujo, pengine hata hayupo Tanzania. Mara ya mwisho kumsikia Maalim seif juu ya Muungano huo. Ni kuwa Zanzibar haiko tayari kuwa na adui jirani. Kwa maana kam unavunja Muungano, basi kutakuwa na Tanganyika akiwa ni adui yako. Leo tuna ona India na Pakistan. Wamekuwa na ugomvi wa siku nyingi. India ikasambaratika, kukawa na pakistani, Bangaladesh, Sril lanka... Pakistan wamekuwana vita na India kitambo.

Juzi tu, India ametowa msaada wa dola milioni tano. Pakistan amezipokea bila kutaka. Lakini utafanyeje wakati huyo ndo jirani yako, sisi waislamu tunafunzwa kitu cha mwanzo ni jirani yako, ikisha ndio ndugo yako... Muunguja, Tahadhari na mdomo wako, usiwashe moto usiweza kuuzima....
ndugu yangu angalia huyo jirani yako yukoje!

Je huo uislam unaoutaja umeridhika na jirani huyo alieuwa watu zaidi ya 10,000 huku Zenj?
 
Ni kweli kabisa. Kwa mara ya kwanza nilisoma makala ya Salva Rweyemamu kwenye gazeti la Mwananchi tarehe 30 Septemba 2005. Rweyemamu mwandishi mahiri wa kipindi kile (siku hizi anatakata kwa whisky za ikulu) alieleza kwa kirefu mkasa huo. Pia nimesoma machapisho mbalimbali.

Seif ni mnafiki sana kama alivyo Vasco da Gama. Mwalimu pamoja na misimamo yake juu ya uadilifu katika serikali hakumpenda kabisa mtu mnafiki. Mwalimu alifahamu fika Seif kayafanya yale si kwa kuupenda muungano bali kwa kutaka madaraka. Alimfahamu fika kama mtu mwenye tamaa ya madaraka.

Kunyimwa kwa urais wa Zenj kulimfanya Seif aanze chokochoko zake zilizompelekea kuandika barua kali ya kumtukana Mwalimu panapo Mei 1988. Pamoja na yote hayo Mwalimu aliendelea kumvumilia Seif hadi Agosti 1988 pale CCM ilipoona Seif havumiliki.

Hiyo ni historia tu. Lakini jasiri haachi asili.

Tabia ya Seif ni kupenda madaraka kwa gharama yoyote ile hata kama watu wengine wataumia. Sote tukirejea yaliyotokea Zenj baada ya chaguzi tatu za 1995, 2000 na 2005 tunaelewa maana yake. Kuna wakati Seif aliwagharimu wabunge wa CUF kwa vile yeye hakupata urais.

Tunaona kilichotokea baada ya uchaguzi wa mwaka jana. Seif kapewa wadhifa katulizana tuli kana kwamba si yeye yule ngangari. Nape hakosei kumtukana.

Ukiisoma ile makala ya Seif na mustakabali wa muungano ambayo imo humu JF, unaweza ukadhani umekosea kuielewa. Ni Seif yupi huyo? Mbona wa sasa na mwandishi wa makala yale ni viumbe wawili tofauti kabisa? Huyo ndiyo Seif.

Nimeandika mengi nje ya hoja ya msingi. Nimefanya hivi makusudi ili kuonesha ninavyomwelewa na kumtafsiri Seif.

Najibu swali sasa la hoja. Sitaki kuwa kama Ndugai.

Ni kweli Seif ndiye aliyeichomoa ile hati ya mashitaka ya Jumbe, akamchomea utambi kwa Mwalimu. Kuanzia hapo ameendelea kufanya yale tunayoyasoma, kuyasikia na kuyaona.

Ahsanteni.
 
Duh! ndugi yangu Muunguja, baada ya chuki zako na majungu juu ya Maalim Seif kutokufanya kwenye mzalendo, umeonelea uje hapa na majungu yako. Ni wapi wewe umewahi kusikia Maalim Seif ametamka kuwa ana adh-ma ya kuvunja Muungano? Wewe ni Mu-Islamu na huu ni mwezi wa ramadhani, heshimu funga yako na heshimu mwezi huu mtukufu.

Watu kama hawa ni wabaya kuachiwa kwenye forum kama hizi. Hawa ndio wanao palilia fujo, pengine hata hayupo Tanzania. Mara ya mwisho kumsikia Maalim seif juu ya Muungano huo. Ni kuwa Zanzibar haiko tayari kuwa na adui jirani. Kwa maana kam unavunja Muungano, basi kutakuwa na Tanganyika akiwa ni adui yako. Leo tuna ona India na Pakistan. Wamekuwa na ugomvi wa siku nyingi. India ikasambaratika, kukawa na pakistani, Bangaladesh, Sril lanka... Pakistan wamekuwana vita na India kitambo.

Juzi tu, India ametowa msaada wa dola milioni tano. Pakistan amezipokea bila kutaka. Lakini utafanyeje wakati huyo ndo jirani yako, sisi waislamu tunafunzwa kitu cha mwanzo ni jirani yako, ikisha ndio ndugo yako... Muunguja, Tahadhari na mdomo wako, usiwashe moto usiweza kuuzima....
Maalimu mwenyewe aliandika kwa mkono wake miaka michache iliyopita akionesha namna asivyoutaka muungano. Si lazima utamke wazi unataka kuuvunja muungano. Kuandika huutaki maana yake unaweza fanya lolote kuuvunja.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom