Je, maafisa Kilimo huwa wana ofisi zao vijijini ambapo kuna Wakulima wengi?

Lipijema

JF-Expert Member
Mar 8, 2015
574
1,000
Binafsi nimeamua kujiajili kwenye sekta ya Kilimo, nimejikita kwenye zao la Mahindi na Karanga.

Changamoto mbalimbali zinanikuta kutokana na wadudu waharibifu wa mazao, kuna dawa ambazo wanatuuzia hawa wahudumu wa haya maduka lakini ukifuata maelekezo yao ya mdomo unakuta sivyo kabisa

Mara kadhaa nimejikuta napata hasara kwa kuweka vipimo ambavyo sivyo!

Swali, Je, hawa maafisa huwa wanazo Ofisi sehemu za Kata, Wilaya na Mikoani tu, huku vijijini hawapo? Wakulima wengi tupo vijijini.
 

Ricecooker

JF-Expert Member
Aug 9, 2017
493
1,000
Ukisubili maafisa kilimo wa serikali itakula kwako,tengeneza network na wakulima wenzako kila kitu kitakua poa.Wataalam Tanzania ni wachache,wengi wapo kuvizia semina na maonyesho ili wapate posho sio kujifunza na kusoma vitabu ili wawe nondo kudeliver kwa wakulima.
 

chilundu

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
300
250
Aisee kumbe ni shida sana na ishu kama kilimo ni sayansi inabidi mtu ajiupdate wakati wote kuhusu teknolojia mpya na pembejeo sa akiwa mtendaji miaka kadhaa tu mweupe kichwani
Wapo ndiyo,sema wengi wao Wana ACT WAEO (Afisa Mtendaji Kata/Kijiji) hata mambo ya Kilimo wameshasahau

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom