Je lipumba anafikiria Nchi kwanza na Si Chama?

Hii article ipo kwenye Gazeti la Majira 26/11/08
Imetolewa mara ya mwisho: 26.11.2008 0003 EAT
•
Mwandosya apigiwa chapuo la urais

Habari Zinazoshabihiana
• Sigombei 'kumzibia' Mwandosya- Mwang'onda 08.06.2007 [Soma]
• Profesa Mwandosya aombwa kusaidia kuunganisha CCM 15.10.2007 [Soma]
• Karume: Sifikirii kugombea urais 2010 19.07.2006 [Soma]

Na Rashid Mkwinda, Mbeya

MWENYEKITI wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amemwelezea Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, kuwa ni mtu anayefaa kuwa Rais wa Tanzania kutokana na msimamo na uwezo aliouonesha katika kila wizara aliyoongoza.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika hitimisho la ziara yake Mbeya Vijijini mjini Mbalizi juzi, Profesa Lipumba alisema uwezo aliouonesha Profesa Mwandosya, unatosha kumfanyia tathmini kwamba ni kiongozi anayefaa kuongoza nchi.

"Katika wagombea wa CCM waliojitokeza mwaka 2005, Profesa Mwandosya walau alionesha kuwa na dalili za kuwa kiongozi mzuri ... huyu ndiye angefaa kuwa Rais wa nchi yetu ni mtu makini," alisema Profesa Lipumba.

Profesa Lipumba mwaka 2005 alikuwa mmoja wa wapinzani waliosimama kugombea urais akitumia tikiti ya CUF na kuangushwa na Jakaya Kikwete, ambaye aligombea kwa tikiti ya CCM.

Aidha, Profesa Lipumba alisisitiza kauli yake ya mara kwa mara, kwamba Watanzania hawajalaaniwa na Mwenyezi Mungu, kwani wana ardhi yenye rutuba ambayo inamea kila aina ya mazao na kwamba iwapo nchi ingekuwa na viongozi wanaojali watu wake, hakuna mwananchi ambaye angekufa na njaa.

"Watanzania hatuna laana ya umasikini kutoka kwa Mwenyezi Mungu ... tukiungana na kuimarisha umoja wa kitaifa, tutajikwamua katika lindi la umasikini lililotugubika kwa zaidi ya miaka 40," alisema.

Profesa Lipumba yuko katika ziara ya siku tano mkoani hapa, ambapo amehutubia mikutano ya hadhara katika kata za Mbeya Vijijini, akisisitiza azma yake ya kuwataka wananchi waachane na CCM akidai kuwa kimekuwa kikiwalaghai wananchi kwa ahadi hewa bila utekelezaji yakinifu.

Ujio wa Mwenyekiti huyo wa CUF umetafsiriwa kuwa ni sehemu ya kukipigia debe chama hicho katika ubunge kutokana na kiti hicho kuwa wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Bw. Richard Nyaulawa, kufariki dunia Novemba 9 mwaka huu.


Aaaah jamani, Profesa Lipumba si ndio alikuja kule kwetu jang'ombe mwaka 2005 akatuhubiria kwamba Salim Ahmed Salim ndio alikuwa bora kuliko wagombea wote wa CCM na akataka tumchague yeye kwa kuwa CCM wamemteua msanii Kikwete mtani wake? Sasa mbona leo amebadili stori na kusema Mwandosya ni bora zaidi? Siasa za pendillum! PENDULI

Nakumbuka hata vyombo vya habari vya bara wakati ule wa kampeni viliandika hiyo kauli yake kuhusu SAS

Asha
 
Lipumba ni profesa wa uchumi anayeheshimika na mwenye uwezo wa uongozi na pia urais. Kwa urais wa muungano sio siri Lipumba hapiti kwa sababu CUF bado inahusishwa na udini hivyo itakuwa ngumu kuuzika kwa Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Ziwa. Watampigia kura kiongozi muislamu toka chama kingine chochote lakini sio CUF.

Lipumba amemsifu Mwandosya ili kumtukana JK kwa kinyume nyume. Infact its very true Prof. Mwandosya is briliant with brain power. JK japo ni graduate haonyeshi briliance as far as brain power is concerned. Alichosema Lipumba ni kuwa CCM imeacha kuchagua viongozi wenye akili kama Prof. Mwandosya kimoyomoyo 'ona sasa nchi inaendeshwa na wajinga wajinga kama waliopo'

Chedema imeonyesha njia Tarime tayari sasa inaaminiwa lakina haina mtu upande wa presidential. Zitto bado ni mchanga, Dr. Slaa hauziki. Mbowe anakabiliwa na laana ya Wachaga na Wahaya kamwe kutogusa uraisi wa nchi hii. Mtu wa Chadema angekuwa Victor Kimesera lakini hakuwahi kuingia bungeni hivyo hajaweza kuonyesha uwezo wake. The time now is too short kufanya hivyo huku akiwa by passed na age.

Kama wapinzani wako serious wakaungana wakampitisha Cheyo mgombea bara makamu akawa yoyote toka Zanzibar. Cheyo atakomba kura zote Kanda ya Ziwa kura zote Kaskazini na Nyanda za Juu Kusini. Mdengereko ataambulia kura za wajinga wajinga wa Kanda ya Mashariki na Kanda ya Kati Dodoma na Singida ambako ni mabendera fata upepo. Lipumba waziri wa Fedha, Mrema mambo ya Ndani, Zito mambo ya Nje. Lissu Mwanasheria Mkuu kuwachukua baadhi ya wasomi kama Prof. Shiviji waziri wa Sheriia na engine wengi. Amini usiamini 2010 CCM Chali!.

Mkuu analysis yako nzuri kweli lakini ulipomtaja Cheyo tu ukanikosesha hamu ya kumalizia kusoma!!
 
Huyu ndugu Pasco anamatatizo ya kimsingi kabisa.Analysis yake inatokana na ukabila na ukanda ambao ameupa prominence.Mtu angekuwa anapigiwa kura kutokana na mahali anakotoka au kabila lake basi si muda mrefu Tanzania patakuwa hapakaliki au kutawalika.Msomi ambaye he/she is worth his brains angetanguliza kwanza a unifying ideology ambayo ina cut across all social barriers.Kwa siku hizi hiki ni kitu kigumu(yaani kuformulate a unifying ideology) na hata makada wa chama tawala wameingia katika mtego huo wa chaguzi za kikanda/kikabila.
JK amejaribu na karibu awateke watu wote kwa slogan ya "Kasi Mpya,Nguvu Mpya" lakini ukabaki tu kuwa msemo bila mikakati ya utekelezaji wa slogan hiyo.Sijui kama makada kama Makamba wanaelewa kiutendaji maana ya msemo huo.
Hivyo basi chama kingine chochote kitaendelea kuwa cha upinzani mpaka pale watakapotatua misimamo hiyo ambayo ni ya kimsingi.Na hii si kusema vyama vyama vya upinzani havi fanyi kazi ,la hasha,vimefanya kazi kubwa na nzuri kabisa ya kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi, kazi ambayo sasa tunaona matokeo yake.
 
LIPUMBA ni mwanasiasa aliyekomaa maana mwanasiasa aliyefilisika utamjuwa kwa kupayuka kama Mrema, Mtikila, Mbatia au Makamba! Profesa alimsifia Mwandosya huko kwao Mbeya anakokubalika! nyinyi mulitegemea Lipumba ahutubie umati wote huo halafu amponde Profesa mwana kutoka Mbeya(Mwandosya) halafu wananchi wamvurumishiye mawe ee! kama yalivyomkuta Mchungaji wa Nyumba ya Kondoo Mtikila huko Tarime! huko kunawashabiki wa CHADEMA halafu unaenda kuwapakazia mauwaji! sasa mulitaka Lipumba atwangwe mawe ili mumcheke sio! Siasa za kiafrika mtu ni lazima ujuwe kuzisheza.

Kama kuna mtu anabisha basi aende kigogo wa CCM huko Monduli halafu ktk mkutano wa hadhara aseme kuwa Lowasa ni fisadi kama hatauawa na wananchi wenye hasira!
Lipumba ni mjanja na amepata wanachama wengi sana huko Mbeya baada ya kumsifia Mwandosya!
 
Zakumi,
Mkuiu hapana kesi ya Zuma ni tofauti kabisa.. Zuma anapongezwa na wananchama wa chama kile kile cha Mbeki yaani hawa wote wanaangukia mrengo na sera moja isipokuwa ni nani kati yao ni kiongozi bora..
Alichofanya Lipumba kamsifia mtu nje kabisa ya CUF... na katoa sababu zake ambazo zinahusiana na Uongozi bora. Ina maana haoni hata kiongozi bora CUF wakuwa rais isipokuwa Mwandosya toka CCM.
Hivyo basi kama sio sera nzuri za CCM, Mwandosya asingeweza kuwa mbora na itachekesha sana kama Lipumba ataziponda sera za CCM uchaguzi ujao, wakati mwenyewe anakubali kuwa kuna sehemu zimefanya kazi kutokana na kiongozi mzuri..
Within one party ndipo unaweza kusema mtu gani ni kiongozi bora zaidi ya mwingine lakini inapofikia vyama tofauti, unatazama sera kisha ndio ahadi na uwezo wa mhusika..
Mkuu chimba kidogo hapa utaona kwamba Lipumba kasifia sera za CCM kuwa zimeweza kufanya kazi kutokana na kiongozi mzuri (Mwandosya), then why umeunda chama cha Upinzani ikiwa unaamini sera za CCM ni nzuri isipokuwa viongozi wahusika ndio problem..

Hapana Mzalendo mwenzangu , alichokifanya Lipumba ni sawa kwani amejikita kwenye uadilifu na uchapa kazi wa mtu na mhusika ni kiongozi wa serikali na wala hakuna kufuata sera katika uadilifu ,maana kama sera zinafuatwa basi CCM wote wanafuata sera zao hakuna anaepinga sera zake,ila uchapakazi ndio unaompima mtu ikiwa anafuata sera au hafuati sera.

Na Lipumba ameonyesha uzalendo maana kama angelikuwa selfish mchoyo hataki mwenziwe aonekane ni mchapa kazi angeweza kuponda tu bila ya wasiwasi wowote ,kama vile wako wanaomuona Lipumba si msomi just ni mbangaizaji tu hana uprofesa hana chochote ,lakini huko huko ndani ya CCM wapo wanaomthamini na kumsifu kwa kazi zake na kumpa anachostahiki na ndipo hapo maendeleo yanapoweza kupatikanika.

Sioni sababu ya kwa nini Raisi Kikwete hamhusishi Lipumba katika mambo ya kuinua uchumi ,Lipumba anheshimika sana katika jumuia za uchumi za kimataifa na wanaiona Tanzania au Serikali ya Tz kuwa ni dhaifu kiroho kwa kushindwa kumtumia Lipumba. Obama amewea kumuacha mkuu wa fedha ambae alikuwepo wakati wa Bush na hakuona kosa wala wenziwe hawakuona kuwa ni kosa kwa sababu anakubalika katika jamii iweje Lipumba asiwepo katika serikali ya Tz wakati ni mtu anaekubalika katika mambo ya uchumi duniani.Si ajabu ukaikuta serikali inatumia wataalamu wengine kutoka nje katika kuinua uchumi wake na huko ni kutafuta kuibiwa tu kama tuonavyo.
Serikali inanunua rada eti itakuwa na inamonita pamoja na ulinzi kwa ndege zote ziingiazo na zitokazo nchini ,pesa zimeliwa na radah ni scrape.
 
Mkuu analysis yako nzuri kweli lakini ulipomtaja Cheyo tu ukanikosesha hamu ya kumalizia kusoma!!

Ndugu yangu Mtarajiwa, pole, sio lazima awe Cheyo, nimetolea mfano na kuujengea hoja. Kwa muda uliobakia sio rahisi kupatikana kwa mgombea mmoja wa upinzani anayeuzika na kukubalika atakayesimama dhidi ya mgombea wa CCM. Hiyo inatokana na dhana ya 'If you can't get what you want, take what you get'. Upinzani Tanzania bado ni legelege kwa sababu hakuna umoja na hawa list ya viongozi shupavu ka Zitto, tatizo mchanga.(japo JK Nyerere alikuwa 49 alipochukua nchi). Kwa mtazamo wangu, John Cheyo, nilimuona ndiye mgombea anayeweza kukubalika lakini sio lazima awe yeye. Toa mapendekezo yako
 
Zakumi,
Kama kuna chama cha mkondo wa kulia nionyesheni.
CHADEMA...

Mwiba,
Nakubaliana na wazo la kumsifia mtu kwa utendaji kazi wake lakini sio kutamka kuwa huyu MTU anafaa kuwa RAIS wakati unapingana naye ktk mrengo wa chama..Sifa zinaweza kutokea tu kama mtu huyo ameshika tayari madaraka na kayafanya baadhi mazuri.. hayo baadhi ndiyo yatasifika kutokana na uwezo wake ktk jambo fulani.. yet bado hawezi kusifiwa kuwa alikuwa mbora kati ya viongozi..
Sielewi siasa za Kibongo lakini maneno kama hayo yanatakiwa kusemwa na watu kama sisi sio Kiongozi wa chama CUF ambaye mwenyewe anagombea Urais.. sasa kama Mwakyembe anafaa kuwa rais nini nafasi yake yeye na kwa nini anagombea Urais badala ya kumpigia kura Mwakyembe!

Tazama Marekani, hata huyo Clinton pamoja na mazuri yote aliyofanya huwezi kuaambia viongozi wa Republican kuwa ndiye alikuwa kiongozi bora Marekani, wao watakwambia Reagan ambaye aliikuta nchi ktk hali mbaya kiuchumi, kisiasa na kaiwezesha Marekani kuwa Super power pekee duniani..Na kwa kila hali viongozi wazuri wanaofaa kuwa rais watatoka Republican tu hiyo ndiyo imani yao..

Mfano:- Kama kawaida nawaangushia huu lakini tafadhari msinielewe vibaya..
Ni kama vile umwambie Kiongozi wa Kikristu kuwa Muislaam pia anaweza kwenda peponi kutokana na kayafanya mazuri hapa duniani. Kitendo cha kuto AMINI na KUABUDU (imani na nguzo za Kikristu), kinaondoa pepo kwa mtu huyo. Urais ni pepo ya hapa duniani kiutawala, hivyo huwezi kusifia mazuri ya mtu ukayapa daraja la Pepo ikiwa kweli wewe ni muumini..
 
Hahahahahahah, mbona unaspeculate ndugu, maana wa CCM wananiambia mie CHADEMA, wa CHADEMA wananiambia mie CUF na waCUF wananiambia mimi CCM kwa maana ya kupiga kura. Okay okay, sasa mimi kura yangu iko free na elimu niliyoipata hapa JF kwa muda mchache nilojiunga humu inaniambia nijiunge na chama. Hapa nipo katika kujua mbichi na mbivu

Kama nimekuelewa vizuri, nikiamua kujiunga na CUF basi si Lipumba wala Seif watakaokuwa wagombea wa kiti cha urais 2010 kwa Tanzania bara na visiwani respectively. Kwa maana hiyo basi, mmejiandaaje na uchaguzi 2010 ? kuna siku chache tu kuingia 2009.
Sadakta mama wewe ndio unajua siasa za nchii siyo hao wengine wasijua lolote na kujifanya kulaumu uchafu wa SISIM kumbe huko kungine kuchafu zaid labda hawaelewi kwa nini Lipumba na Seif kila mwaka hugombea licha ya kuzidiwa kete na SISIM
 
Sadakta mama wewe ndio unajua siasa za nchii siyo hao wengine wasijua lolote na kujifanya kulaumu uchafu wa SISIM kumbe huko kungine kuchafu zaid labda hawaelewi kwa nini Lipumba na Seif kila mwaka hugombea licha ya kuzidiwa kete na SISIM

Hawa watagombembea mpaka maji mtaita mma na inajulikana wazi kuwa hawa ndio tishio la CCM na wenyewe CCM wanalijua hilo kuwa hakuna Chama kinachowapa taabu kama CUF wanasikika wakisema wamegonga mwamba ,ukiangalia hakuna chama kilichobambikizwa uzushi kama CUF ,Chama Cha Wapemba ,wakaona bado ,Chama cha Magaidi wakaona bado Chama cha waarabu ,Chama Cha Kiislamu wakaona bado jamaa wa CUF wamesimama mlangoni wanawambia watoke, sasa na kila ukaribiapo uchaguzi wanaanza mbona hao hao ? Bhwahaha haha , sasa nyie si mnawashinda kila uchaguzi hamuoni kama utakuwa urahisi kwenu kutokana na kuwabwaga kila msimu? Na sasa wanasema YES WE CAN fulana zao mshaziona au bado ? Zipo mitaani.
 
Ndugu yangu Mtarajiwa, pole, sio lazima awe Cheyo, nimetolea mfano na kuujengea hoja. Kwa muda uliobakia sio rahisi kupatikana kwa mgombea mmoja wa upinzani anayeuzika na kukubalika atakayesimama dhidi ya mgombea wa CCM. Hiyo inatokana na dhana ya 'If you can't get what you want, take what you get'. Upinzani Tanzania bado ni legelege kwa sababu hakuna umoja na hawa list ya viongozi shupavu ka Zitto, tatizo mchanga.(japo JK Nyerere alikuwa 49 alipochukua nchi). Kwa mtazamo wangu, John Cheyo, nilimuona ndiye mgombea anayeweza kukubalika lakini sio lazima awe yeye. Toa mapendekezo yako

Mkuu fikiria mwingine siyo huyu Cheyo ndumilakuwili,pandikizi la CCM.Huyu hauziki popote ukiacha jimboni kwake anakoringia ukabila ambako pia akipatikana mgombea mzuri atamburuta vilevile.
Mgombea wa kushinda 2010 siyo lazima awe tayari ni mwanachama wa chama fulani.Mbona wapo wanaharakati wengi tu ambao kama watapewa nafasi na kukiwa na mikakati mizuri ya kampeni wangeweza kumsumbua JK.
 
Kadogoo,
Mkuu Lipumba hakuwa na haja kabisa ya kumtaja Mwandosya kwa sifa ya Urais unless nikitazama upande wapili wa shilingi hiyo hiyo inaweszekana kuwa ni tactic ya kisiasa kwa malengo ya kuanzisha mgogoro wa kisiasa ndani ya CCM Mbeya!..

Mimi namheshimu sana Lipumba na nafahamu uwezo wake ktk uchumi na pengine kuwa mbora zaidi ya wagombea wengi wa Urais lakini kisiasa hakuwa na sababu kabisa ya kumpandisha chat Mwandosya kuwa ndiye anafaa kuwa rais..Hapa nikitazama nafasi ya CUF ktk kugombea urais mkoani Mbeya inaonyesha wazi tayari kisha wachagulia rais na toka chama gani...
 
Lipumba, Seif wawania kutetea nafasi zao CUF

Habari Zinazoshabihiana
• Lipumba: CUF iko imara hata bila Maalim Seif 16.08.2007 [Soma]
• CUF waandamana, wawafungia mlango Lipumba, Seif 16.06.2007 [Soma]
• CUF: Kikwete nchi imevimba, inapasuka 10.10.2008 [Soma]

Na Mwandisi Maalumu

MWENYEKITI wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo kwa mara nyingine.

Taarifa iliyotolewa jana na chama hicho, ilisema hiyo ni hatua ya kujenga chama chenye misingi ya demokrasia ya kweli ambapo pia wanachama wanaendelea kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama kwa ngazi ya Taifa.

Ilisema Profesa Lipumba mwenye kadi ya uanachama namba 00431 ZB ya Aprili 20, 1995 iliyotolewa katika tawi la Ilolangulu, Uyui, mkoani Tabora, alichukua fomu hiyo katika tawi hilo Novemba 11 na kuirejesha Novemba 28 mwaka huu.

Wanachama wengine waliojitokeza hadi sasa kuchukua fomu ni Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye pia anatetea nafasi hiyo.

Taarifa ilisema mkutano mkuu wa CUF Taifa unatarajiwa kufanyika kuanzia Febnruari 23 hadi 27 2mwakani katika ukumbi wa VIP Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo utafanya uchaguzi wa viongozi wa kitaifa ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu mkuu, na wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi.

Kalenda ya uchaguzi ilibanisha kuwa Novemba 30 mwaka huu, ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kwa wanachama kuchukua fomu za maombi katika matawi yao na Desemba itakuwa siku ya mwisho kurejesha fomu kwa Katibu Mkuu.
 
Back
Top Bottom