Je, Lengo la kupata 99% ya wawakilishi linanufaisha taifa?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,603
8,741
Kila siku kuna watu wamekuwa wanajisifu kwamba CCM itapata 99% ya wabunge. Kama watapata kwa njia halali kitu ambacho hakiwezekani kutokana na tofauti za Watanzania.Tatizo litakuja pale tu serikali itakapo lazimisha na haya ndiyo tutayapata

1. Vikwazo vya kiuchumi au viongozi kuwekewa mapingamizi. Vikwanzo mfano ni pamoja na kuweka zuio la raia kutembelea kama nchi ya Cuba ambayo US wameweka kikwazo kwa raia wao kwenda huko.

2. Usalama: Hata kama tukiweka polisi hatuwezi kuendesha uchumi na polisi wa mtutu mitaani huo sio usalama. Kuna dalili zote Zanzibar kutatokea haya tusikokuwa makini

Je kuna lipya lipi? Tofauti na zamani serikali kwa sasa imeshtukiwa na tayari Tanzania tumewekwa kwenye list na US Kitu ambacho hakijawahi kutokea nyuma. Pili, nguvu ya mitandao; yaani Mtanzania wa kawaidia ana uwezo wa kutuma ujumbe kwa viongozi wowote Dunia kitu ambacho zamani hakikuwepo

Lakini inawezekana wanaopanga wana sababu kubwa za uchumi na kukomboa nchi yetu kiasi kwamba kuongeza viongozi kutoka 70% mpaka 100% itasaidia lakini watupe hizo sababu ili tuzijue.

Hawa viongozi wasipotoa sababu ina maana manufaa sio kwa nchi yatakuwa manufaa binafsi. Hivyo wanaosema wenyewe ni wazalendo na wana support mbinu za kubana demokrasia watueleze kuna kitu gani kipya ambacho kwa sasa hawawezi kukifanya lakini wakiwa na 100% ya kila kitu wataweza.

Tupeni data na sio kutumia tu maneneo ya ubeberu bila kuwa na hoja. Kama kweli ni kwa manufaa ya taifa tuta support lakini tuelimisheni.
 
Watu walio radhi kununua wapinzani huku watoto wakikaa chini, unategemea wana utimamu!
 
Nyumba tunayoijenga ni moja kwanini tugombanie fito. Uchama uchama unasaidia nini? nyinyi mboga mboga hampendi kukosolewa maendeleo gani uwa yanakuja pasipo kuwa na mtu wakukupa mtazamo hasi katika lile ulilolipanga na kuona kweli hapa nisipokuwa makini nitakuwa nimeingia choo cha kike tatizo fisiemu uwachukulia wapinzani ni kama maadui wa maendeleo wakati wapinzani ni wasahishaji wa mambo ulioyaona kwako ni sahihi wakati kwa wananchi wao waliowachaguwa sio sahihi
 
Kila siku kuna watu wamekuwa wanajisifu kwamba CCM itapata 99% ya wabunge. Kama watapata kwa njia halali kitu ambacho hakiwezekani kutokana na tofauti za Watanzania.Tatizo litakuja pale tu serikali itakapo lazimisha na haya ndiyo tutayapata

1. Vikwazo vya kiuchumi au viongozi kuwekewa mapingamizi. Vikwanzo mfano ni pamoja na kuweka zuio la raia kutembelea kama nchi ya Cuba ambayo US wameweka kikwazo kwa raia wao kwenda huko.

2. Usalama: Hata kama tukiweka polisi hatuwezi kuendesha uchumi na polisi wa mtutu mitaani huo sio usalama. Kuna dalili zote Zanzibar kutatokea haya tusikokuwa makini

Je kuna lipya lipi? Tofauti na zamani serikali kwa sasa imeshtukiwa na tayari Tanzania tumewekwa kwenye list na US Kitu ambacho hakijawahi kutokea nyuma. Pili, nguvu ya mitandao; yaani Mtanzania wa kawaidia ana uwezo wa kutuma ujumbe kwa viongozi wowote Dunia kitu ambacho zamani hakikuwepo

Lakini inawezekana wanaopanga wana sababu kubwa za uchumi na kukomboa nchi yetu kiasi kwamba kuongeza viongozi kutoka 70% mpaka 100% itasaidia lakini watupe hizo sababu ili tuzijue.

Hawa viongozi wasipotoa sababu ina maana manufaa sio kwa nchi yatakuwa manufaa binafsi. Hivyo wanaosema wenyewe ni wazalendo na wana support mbinu za kubana demokrasia watueleze kuna kitu gani kipya ambacho kwa sasa hawawezi kukifanya lakini wakiwa na 100% ya kila kitu wataweza.

Tupeni data na sio kutumia tu maneneo ya ubeberu bila kuwa na hoja. Kama kweli ni kwa manufaa ya taifa tuta support lakini tuelimisheni.

Pascal P uko wapi kuchangia hii?
 
Back
Top Bottom