JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Hii ni dhana inayotolewa na ushahidi dhidi ya Nchi zenye Rasilimali na Maliasili nyingi kushindwa kuendelea kiuchumi ukilinganisha na nchi zisizokuwa na Rasilimali nyingi.
Dhana hii ya Laana ya Rasilimali ina nadhalia kubwa tatu:-
1. Nchi zenye utajiri mkubwa katika Rasilimali na Maliasili zinakuwa taratibu kiuchumi kushinda nchi zisizokuwa tajiri katika Rasilimali na Maliasili.
2. Nchi zisizo kuwa tajiri kwenye maliasili zina uchumi mkubwa kushinda Nchi zenye utajiri wa Maliasili.
3. Nchi zenye Rasilimali nyingi zinaongoza kwa umaskini na Rushwa kushinda Nchi zisizokuwa na utajiri wa Rasilimali na Maliasili.
Hivyo dhana hii inasema kwamba Kuwa na Utajiri wa Rasilimali ni Laana ya Maendeleo katika Nchi. Katika Dhana hii kwenye ushahidi zinatajwa Nchi kama DRC, Equatorial Guinea, Sierra Leone, Liberia, Venezuela n.k.