Je, kweli shetani yupo? Kuzimu kupo?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,791
Shetani ni nani? Ni mtu au ni mnyama? Ni wa kike ama ni wa kiume?
Je shetani ana ukoo wake na je ana familia yake?
Je shetani anazaa? Anakua? Anazeeka? Anakufa!!?
Je mazishi yake yakoje!? Na uzazi wake wa uzao vikoje?
Je shetani naye ana dini yake? Ana imani yake? Ana wafuasi wake? Ana msahafu wake!? Ana midundo yake? Ana verses zake?
Je shetani ana hisia?
Za upweke!?
Za kutamani?
Za mapenzi?
Za ngono?
Je shetani naye anakasirika!? Anafurahi? Ana wivu?

Je shetani ana kiasi!? Anatosheka? Anaumwa njaa!!! ? Anaugua!? Anatibika? Anapona?
Je shetani anaroga? Anarogeka? Ana kilinge?
Je shetani anafanya kazi? Anakosa kazi? Anapokea ujira? Anapiga mishe?

Je shetani ni mchichamwiba!? au ni msagaji? Au ni ngangaripoa!? Je shetani anadanga? Ni mwizi?
Je shetani ni mwanamichezo!!? Ana washindi na washindwa? Ni mlabata?

Je shetani ana utajiri? Ufukara je? Je anafilisika? Je shetani ni maskini?
Shetani ni nani?
Ni Lucifer?
Ni mzimu?
Ni pepo?

Je kuzimu kupo? Ni kweli kuna ziwa liwakalo moto? Kwanini wanasema kuzimu kuko chini? Huko chini ni wapi? Kuna umbali gani kutoka hapa tulipo? Je ni kukubwa kiasi gani?
Je kuzimu ni dhana halisi au ni dhana dhanifu!?

Jibu utakayoweza ama la ongeza mengine!!!

20221114_213111.jpg
 
Jibu moja linalojibu maswali yote

"Shetani hayupo"

Kwahiyo maswali yote jibu ni No
Kisichopo hakipo hakijulikani hivyo hakiwezi kutajwa popote kwa majina wala kwa michoro wala kwa picha
giphy.gif
 
Spiderman, harrypotter, Batman, unicon, na pazi aliyebebwa na jogoo kichwa chini miguu juu

Hao niliowataja hapo, wapo kihalisia?

Tangu nyakati za kale, wanadamu wamekuwa wakijenga, kuchonga na kuweka sanamu za aina nyingi kwa sababu mbalimbali. Baadhi hutumiwa kuwaheshimu watu maarufu na kuwakumbuka, na wengine wanaabudiwa kama miungu. Kwa muda mrefu hata hivyo, imekuwa nadra kuona sanamu ambayo inahusishwa moja kwa moja na shetani au shetani.

Screenshots_2022-11-14-22-30-48.jpg
 
Shetani hakai kuzimu Kama watu wengi wanavyodhani Ila huwa anakaa kwenye mbingu ya level ya chini,na majeshi ya pepo wachafu ,pamoja na mizimu pia nayo wanakaa angani
 
Kila kitu kinaanzia kwenye imani. Imani hii ndiyo inayoumba shetani, kuzimu na vinginevyo vya namna hiyo. Pia imani ndio chanzo pekee cha kuvitia nguvu vitu hivyo ili kutenda jambo. Bila imani hakuna Mungu, shetani, mbingu wala jehanamu
Imani ni uhai na inaishi inazaliwa inakuwa na kufa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom