Papa D
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 753
- 182
Jamani wana JF, mataifa ya ulaya wanaamini Afrika ni bara la giza. Kuna baadhi ya nchi za Asia wanaamini Afrika ni Bara la watu waliochaganyikwa, wasiojua kipi kizuri na kipi kibaya, Wao wanajiendea tu bila kujua wanapokanyaga. Hawa Waasia wameenda mbali zaidi kwa kusema kwamba Waafrika wana hali hiyo kwa sababu wanachomwa na mionzi ya jua katika masaa mengi ya siku. JE, HOJA HII INA UKWELI WOWOTE? Kama si kweli kwanini mambo yetu kuanzia kwa wasomi wenye elimu zao hadi wale wa chini wanatenda mambo yasio na upeo? NA kama ni kweli Je, tufanye nini ili kuondokana na adha hii inayotudhalilisha mbele ya mabara mengine?