Je, kwanini 'Urais' wa Zanzibar umemkubali na kumpendeza kwa 'haraka' sana Dkt. Hussein Ally Hassan Mwinyi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,172
2,000
Naona kama vile Urais wa Zanzibar ulikuwa unamsubiria kwa hamu Dkt. Hussein Ally Mwinyi kutokana na kwamba 'umempendeza' na 'unampendeza' halafu ameuvaa na wenyewe pia umemvaa vyema na kwa haraka sana kuliko hata 'Marais' wengine waliomtangulia. Watangulizi wake wengi 'Urais' wa Zanzibar ilionekana kama vile walikuwa 'wameubaka' tu na wenyewe ulikuwa 'hauwataki' kabisa.

Je, ni kwanini 'Urais' umemkubali kwa haraka mno Rais Dkt. Hussein Mwinyi? Je, tuanze sasa kuamini kuwa 'Urais' ni Zawadi yake Mwenyezi Mungu kwa Watu wake 'Maalum' tu?

Sijajua pia kama na Waziri Mkuu mmoja nae ikitokea akaachiwa 'Zigo' zito na gumu la Tanzania Bara hapo 2025 na 'Mkemia' wa Geita nae 'utampendeza' na 'kumkubali' kwa haraka kama wa Visiwani Zanzibar.
 

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Aug 31, 2020
1,136
2,000
Jamaaa nilijua ana akili kumbe KOPO.

Rais ni Taasisi.
Zanzibar ina Changamoto nyingi sana
Mambo ya kero za muungano.
Umasikini wa wananchi.
Mpasuko mkubwa wa kisiasa nk.
Raslimali za zanzibar.

Ni mapema sana kumpima kwa wiki moja.
 

Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,842
2,000
Kama unavyosema kuwa inaonekana wenzake waliubaka Urais wote wapo katika mtiririko uleule wa kubaka Urais, kama ilivyokawaida kitu cha kubaka hakipendezi hata huyu wa sasa Urais haujampendeza isipokuwa analazimisha.
 

chabuso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
6,128
2,000
Jamaaa nilijua ana akili kumbe KOPO.

Rais ni Taasisi.
Zanzibar ina Changamoto nyingi sana
Mambo ya kero za muungano.
Umasikini wa wananchi.
Mpasuko mkubwa wa kisiasa nk.
Raslimali za zanzibar.

Ni mapema sana kumpima kwa wiki moja.
Waafrika chini ya Jangwa la Sahara,hisia zimewazidi mpaka wanasahau uhalisia wa jambo husika..

Huyu jamaa ni mfano mzuri wa Muafrika anaeishi chini ya Jangwa la Sahara

Huyu jamaa ameweka hisia zake mbele ya kuipenda CCM mpaka anasahau uhalisia wa hali halisi ya Zanzibar
 

chabuso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
6,128
2,000
Huwa naona kama marais wengi wa Zanzibar huwa wazubavu, yaani siyo machachari . Au ni hulka ya Wazenji?
Wanachaguliwa Wazanzibari walio hivyo,wakiwa machachari wataleta tabu kwenye Muungano..

Salimini Amour aliwaendesha sana mbio mabwana zake wakati wa utawala wake hapa Zanzibar..
 

Mulokozijr12

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
1,645
2,000
Mwinyi anakarama ya uongozi unaweza kuona jinsi alivyoimudu wizara ya ulinzi kwa muda mrefu...ni mtu muadilifu Wazanzibar wampe ushirikiano nina imani tutafika mbali.
 

chabuso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
6,128
2,000
Mwinyi anakarama ya uongozi unaweza kuona jinsi alivyoimudu wizara ya ulinzi kwa muda mrefu...ni mtu muadilifu Wazanzibar wampe ushirikiano nina imani tutafika mbali.
Alieingia kwenye utawala kwa kura za wizi hawezi kuwa muadilifu..

Kumbuka wakati Uchaguzi unafanyika yeye ndie alikuwa Waziri wa Ulinzi..

Waliouliwa na Wanajeshi kule Pemba yeye ndie muhusika mkuu..

Yeye ndie alieleta Majeshi Zanzibar,CCM walikuwa wanajua vizuri nini wanafanya na nini wanategemea kutokea,

Walikuwa wamesha jitayarisha kwa lolote lile..
 

Mulokozijr12

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
1,645
2,000
Alieingia kwenye utawala kwa kura za wizi hawezi lies muadilifu..

Kumbuka wakati Uchaguzi unafanyika yeye ndie alikuwa Waziri wa Ulinzi..

Waliouliwa na Wanajeshi kule Pemba yeye ndie muhusika mkuu..

Yeye ndie alieleta Majeshi Zanzibar,CCM walikuwa wanajua vizuri nini wanafanya na nini wanategemea kutatokea,

Walikuwa wamesha jitayarisha kwa lolote lile..
Kama unaushahidi unawahi chap mahakamani Mkuu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom