Je kwanini mahali haimaliziwi kulipwa?

Askari Muoga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
6,113
4,645
kuna utamaduni nimesikia sana eti ukiandikiwa mahali kiasi Fulani basi ni bora utoe pungufu na usimalizie ebu tupeni uzoefu kidogo hapo
mfano mahali 2Mil basi unaweza peleka 800000
 
Unaweza kumaliza na hakuna tatizo lolote na tena ni vyema ukiweza umalize kabisa maana huko mbele likitokea tatizo na ikabidi kuachana wengi hawakumbuki au hawataki tena kumalizia mahari kitu ambacho kitakuletea matatizo.
asante
 
Sijui wapi huko unapozungumzia ila kwa kawaida mahari haimaliziwi kwenye jamii nyingi.
 
kuna utamaduni nimesikia sana eti ukiandikiwa mahali kiasi Fulani basi ni bora utoe pungufu na usimalizie ebu tupeni uzoefu kidogo hapo
mfano mahali 2Mil basi unaweza peleka 800000
Laki8 toka 2mil ni pafupi mno huwa haimaliziwi pesa Kidogo tu kama laki2 au 3.
 
Nadhani Mahari haimaliziwi kwasababu ya kuimarisha mahusiano tu hasa kufanya watu muendelee kuwasiliana, kwa mfano ndugu wa upande wa wife kama wajomba na shangazi waendelee kukupigia na kukutania kwamba wanakumbushia mahari yao, kwa upande wangu mimi sikumalizia Tshs150,000 ambayo wakati mwingine wajomba zangu kwa upande wa wife mara nyingi wamekua wananitania kwamba mimi ni mdaiwa sugu, hivyo natakiwa kuwapunguza hasira kwa kuwanunulia bia, kuna siku tulipanga Safari familia yangu yote tukisindikizwa na Mjomba tulienda kijijini kwa ghalama ya zaidi ya Milioni moja ili tukapunguze deni Tshs50,000 na hili deni limedumu zaidi ya miaka kumi sijamaliza mpaka sasa
 
Huwa ipo hivyo mkuu.
 
Swala la mahari kutokumalizika kijamii walituambia Wazee wakati wetu kwamba itakufanya uendelee kuwa karibu na familia ya mke
Kurudi kuwasalimu kuwapelekea vijizawadi bado unaendelea kumalizia mahari sio lazima iwe pesa

Vijana mkimaliza mahari mnaweza msionekana mpaka msiba au mtiweke kabisa

Kitamaduni ni namna ya kuishi na kuunganisha familia mbili
 
Back
Top Bottom