Je, kwanini kusiwe na chombo maalumu cha kusajili magari na leseni zote za uendeshaji vyombo vya moto tofauti na TRA?

h120

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
2,530
3,315
Habari wakuu,

Nimewaza na kutafakari kwa kina kwanini kusiwepo na chombo maalumu kitakachosimamia usajili wa magari pamoja na leseni zake zote zikiwemo za udereva n.k

Hichi chombo kiwe ndani au chini ya SUMATRA. Kiitwe TANZANIA DEPARTMENT OF MOTOR VEHICLES.

TRA ijikite kwenye masuala yanayohusu kodi tu, maana suala la ukusanyaji wa kodi linachangamoto nyingi ukizingatia ukubwa wa nchi na kuwafikia wafanyabiashara wote inabidi kazi kubwa ifanyike.

Tuwapunguzie mzigo TRA wabaki na jukumu moja tu la kuhakikisha wanatengeneza mipango mizuri ya kukusanya kodi kwa watu wengi zaidi ili kupunguza mzigo unaowaelemea walipa kodi wachache hapa nchini.

Nini maoni yako msomaji?
 
Hili wazo zuri sana, ingekuwa poa kama LATRA wangepewa jukumu hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwenye magari hakuna KODI?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kodi zipo? usimamizi wa usajili na ufuatiliaji ukiamishwa haina maana kodi hazitalipwa.

Chukulia mfano leseni za biashara zinazotolewa na kusimamiwa na Halmashauri za majiji au manispaa, unadhani leo ukiamua hiyo kazi ya kutoa leseni uwakabidhi TRA watashindwa? jibu ni kwamba wataweza kufanya hilo zoezi ila utakua umewaongezea mzigo hivyo ufanisi lazima upungue.

Nakupa mfano mdogo.
Hapo zamani minara ya simu hiyo unayoiona ilikuwa inamilikiwa na mitandao ya simu kama tigo, voda, airtel, kwa hivyo walilazimika kuhudumia minara, kupambana kupata wateja wapya, na kukimbizana na ushindani wa soko, baadae wakaona ili waweze kufanya vizuri kwenye masoko yako ilibidi wapunguze mzigo na wahamishe nguvu nyingi kwenye masoko na wateja wao, minara mingi kama sio yote ikachukuliwa na makampuni ambayo kazi yao ilikua ni kuhakikisha inafanya kazi kama ilivyokusudiwa hivyo mitandao ya simu wanakua kama wamekodisha huduma, wao wanachotaka ni uhakika tu wa huduma, nadhani imewasaidia sana.

Leo angalia Tanesco inavyohangaika kwa ufanisi hafifu, jibu ni kwamba wanaelemewa na kamwe hawawezi kujiendesha kwa faida, Tanesco ilitakiwa ipambane na masoko kuhakikisha bili zote zinalipwa hamna upotevu wala wizi wa umeme ihakikishe inawafikia wateja wengi yani kitengo cha masoko kilitakiwa kiwe bize sana, ila sasa kupambana na nguzo mara usambazaji mara maintenance vyote hivyo kwa pamoja vinawashinda.

Nikirudi kwenye hoja kuu TRA wakijikita kwenye kodi pekee ufanisi utaongezeka watakua na jambo moja tu KODI akili zao zitakua zinawaza na kuchakata mbinu za kuboresha makusanyo na kuhakikisha kila mmoja anaridhika katika ulipaji.

Kwa takwimu tupo watanzania karibu milioni 50 - 60 ila wanaolipa kodi ni milioni 2 kwa makadirio je ni kweli kuna wafanya biashara milioni 2 tu kwa Tanzania hii?
 
Huna point TRA wanapaswa kusimamia mambo mengi yahusuyo pesa ili kuleta ufanisi. Hata kaodi ya ardhi wangepewa TRA kusimamia. Malipo yote ya serikali yangepitia kule. Yaan faini za polisi, Bandari nk zingepitia direct TRA. Shida yetu tuna taasisi nyingi za kukusanya pesa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huna point TRA wanapaswa kusimamia mambo mengi yahusuyo pesa ile kuleta ufanisi. Hata kadi ya ardhi wangepewa TRA kusimamia. Malipo yote ya serikali yangepitia kule. Yaana faini za polisi, Bandari nk zingepitia direct TRA. Shida yetu tuna taasisi nyingi za kukusanya pesa

Sent using Jamii Forums mobile app

Ufanisi hauletwi kwa kujitwisha majukumu mengi, kama leo nikienda posta kutuma parcel yangu kwa EMS iende mbeya nalipia 15000 kwenye risiti kuna vat tayari tra wana makusanyo yao bila shida.

Hoja yangu hapo ni kwamba ufanisi hauletwi kwa kushika kila jambo kisa unadhani linakuhusu, ufanisi huletwa kwa mifumo mizuri inayofanya shughuli zake smoothly.
 
Alafu wakichukue kitengo Cha trafiki kiwe chini yao kiutendaji ila kiwajibike kwa wizara ya mambo ya ndani.... Nawaza ujinga
 
Ufanisi hauletwi kwa kujitwisha majukumu mengi, kama leo nikienda posta kutuma parcel yangu kwa EMS iende mbeya nalipia 15000 kwenye risiti kuna vat tayari tra wana makusanyo yao bila shida.

Hoja yangu hapo ni kwamba ufanisi hauletwi kwa kushika kila jambo kisa unadhani linakuhusu, ufanisi huletwa kwa mifumo mizuri inayofanya shughuli zake smoothly.
VAT ni ishu nyingine bro.. tutakuja kukuelekeza mbeleni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
VAT ni ishu nyingine bro.. tutakuja kukuelekeza mbeleni

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo ni mfano mdogo sana kwamba kodi zote stahiki zitafika TRA endapo kuna mifumo madhubuti.

Sioni tija kuona leseni ya udereva unaenda kuchukua kwenye mamlaka ya mapato, na wamefanya hivyo kwasababu mfumo mzima wa usajili wa magari upo chini yao.

Angalia EFD mashine zipo lakini imeshindikana kutumika kama ilivyokusudiwa ndio maana nasema wabaki na ku deal na ishu za TAX tu, mtu ana mashine ya EFD lakini anakadiriwa kodi, na anakadiriwa kwasababu hawaiamini mashine yao wenyewe, na hawaimani kwasababu wanajua wafanyabiashara hawatoi risiti na wafanyabiashara hawataoi risiti kwasababu hamna usimamizi mzuri na mipango ya kuhakikisha kila mfanyabiashara mwenye mashine anatoa risiti hilo ni jukumu la TRA kusimamia.

Hiyo mifano yote najaribu kuchukua sehemu ambazo nina uhakika wanaweza kusimamia effectively.

Yapo mengi TRA wanaweza fanya kuongeza ufanisi kwenye makusanyo, ila sio kujilimbikizia majukumu mengi yasiyo na direct impact kwenye utendaji wao.
 
Habari wakuu,

Nimewaza na kutafakari kwa kina kwanini kusiwepo na chombo maalumu kitakachosimamia usajili wa magari pamoja na leseni zake zote zikiwemo za udereva n.k

Hichi chombo kiwe ndani au chini ya SUMATRA. Kiitwe TANZANIA DEPARTMENT OF MOTOR VEHICLES.

TRA ijikite kwenye masuala yanayohusu kodi tu, maana suala la ukusanyaji wa kodi linachangamoto nyingi ukizingatia ukubwa wa nchi na kuwafikia wafanyabiashara wote inabidi kazi kubwa ifanyike.

Tuwapunguzie mzigo TRA wabaki na jukumu moja tu la kuhakikisha wanatengeneza mipango mizuri ya kukusanya kodi kwa watu wengi zaidi ili kupunguza mzigo unaowaelemea walipa kodi wachache hapa nchini.

Nini maoni yako msomaji?

Wazo zuri, kwani kuundwa kwa hicho kitengo au idara maalum yaani executive pia kutaondoa majukumu yote ambayo yamelimbikizwa kwa TRA na idara ya usalama barabarani.

Pia ikiundwa idara hii chini ya wizara ya usafirishaji itawezesha kutoa mwanya wa kutengenza ajira kwa watanzania wengi tu ambao bado wanazurura mitaani.

Halafu, kutatoa nafasi ya kupanua wigo wa njia mbalimbali za kiteknolojia ambazo zitasaidia kutengenza kanzidata ya madereva na magari ya nchi nzima.

Hivyo ni idara yenye mkurugenzi mkuu au afisa mtendaji mkuu na watu wake wanapiga kazi na maisha yanaenda.
 
Habari wakuu,

Nimewaza na kutafakari kwa kina kwanini kusiwepo na chombo maalumu kitakachosimamia usajili wa magari pamoja na leseni zake zote zikiwemo za udereva n.k

Hichi chombo kiwe ndani au chini ya SUMATRA. Kiitwe TANZANIA DEPARTMENT OF MOTOR VEHICLES.

TRA ijikite kwenye masuala yanayohusu kodi tu, maana suala la ukusanyaji wa kodi linachangamoto nyingi ukizingatia ukubwa wa nchi na kuwafikia wafanyabiashara wote inabidi kazi kubwa ifanyike.

Tuwapunguzie mzigo TRA wabaki na jukumu moja tu la kuhakikisha wanatengeneza mipango mizuri ya kukusanya kodi kwa watu wengi zaidi ili kupunguza mzigo unaowaelemea walipa kodi wachache hapa nchini.

Nini maoni yako msomaji?
Umewaza mbali sana mdau.hebu chukua nyag ndogo hapo (ntalipa mm)ili ku-replace akili ulotumia hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom