Je kwanini JK huwa mwepesi kwenye mambo madogo na mgumu katika mambo makubwa na muhimu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je kwanini JK huwa mwepesi kwenye mambo madogo na mgumu katika mambo makubwa na muhimu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Father of All, Mar 7, 2012.

 1. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]JK: Polisi aliyetinga disko na SMG afutwe [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 06 March 2012 20:54 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] Chanzo: Mwananchi
  Rehema Matowo, Moshi
  Rais Jakaya Kikwete amesema matendo ya utovu wa nidhamu likiwamo la askari kuingia disko na bunduki,yasivumiliwe kwa sababu ni ya hatari na yanaweza kuondoa uhai wa watu wasiokuwa na hatia.Akizungumza katika mkutano wa kuboresha jeshi la polisi, uliofanyika jana katika chuo cha Polisi Moshi na kuhudhuriwa na maofisa waandamizi, Rais Kikwete aliwataka viongozi hao kusimamia nidhamu ya askari wake.

  Alisema askari asiyekuwa na nidhamu ndani ya jeshi hilo hafai kuwapo bali ni mamluki aliyeingia ndani ya jeshi.
  Alisema sifa ya kwanza ya polisi ni kuwa na nidhamu na kwamba anapokosa hafai kuwa polisi.Kikwete alisema taarifa ya askari kuingia disko na bunduki aliisoma kwenye gazeti hili na kwamba kitendo hicho kimeonyesha dhahiri kuwa wapo askari ambao hawana nidhamu.

  “Nimesoma kwenye gazeti, askari hapa Moshi ameacha lindo na kuingia disko na bunduki huyu mtasema ni askari wenu kweli, amelitia aibu jeshi la polisi na hafai kuwa polisi, wachunguzeni askari wenu mtabaini ni walevi, wala rushwa na muwaonye mara moja akirudia watoeni maana hawawafai,”alisema.

  Rais Kikwete aliutaka uongozi wa polisi kuangalia upya utaratibu wa vijana wanaoomba nafasi za kujiunga na jeshi hilo kwani itafika mahali jeshi hilo litaonekana ni la wahuni na sio la ulinzi wa raia na mali zao.

  Aliwataka kuwa na utaratibu wa ndani wa kuangalia tabia za askari wao ili wajue tabia zao na kuzirekebisha kabla hazijaleta madhara kwa wananchi .

  “Mimi nimepata malalamiko mengi tu kwa wananchi wapo wanaolala baa ,walevi,wahuni,wala rushwa,wapo wanaoshirikiana na majambazi, wachunguzeni mkiwabaini waonyeni kwa mara ya kwanza wakirudia watoeni wapo vijana waaadilifu wanatafuta nafasi hizo hawajazipata, wanaochezea watoeni,”alisisitiza.

  Alisema kwa kufanya hivyo itawasaidia kujenga imani kwa wananchi na kuondokana na lawama zinazotolewa kwa jeshi hilo mara kwa mara. Alitaka jeshi hilo kuweka utaratibu utakaowasaidia wananchi kutoa malalamiko yao kwa uhuru na bila hofu.

  Alitaka jeshi hilo kutoa mafunzo ya ueledi kwa askari wake kwani mafunzo ya ueledi ni msingi wa jeshi hilo. "Kuvaa magwanda sio kuthibitisha kuwa huyu ni askari anayefaa,"alisema.

  Alisema magwanda na vifaa vya kisasa havitamjenga askari kama hana mafunzo ya ueledi ambayo yatampa mbinu za kukabiliana na uhalifu katika kipindi hiki wahalifu wamekuwa wakitumia mbinu za sayansi na teknolojia kufanya maovu.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Anaogopa kuchemka ndio maana anawatuma kina pinda kuja kujiahibisha.
   
 3. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Makubwa yanamzidi umri!
   
 4. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Bingwa wa kupasia mpira watu wengine kwenye masuala magumu
   
 5. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Ni kwa sababu ana uwezo kushughulikia mambo madogo lakini hawezi mambo magumu na muhimu. Jibu liko ndani ya swali lako rafiki.
   
Loading...