Je, kwa sasa ni kitu gani kipya cha maana wanasoma pale UDSM?

Engineer gani? Tangu chuo kianzishwe kuna kitu gani kipya mme innovate hapa Tanzania

Kila kitu tunaagiza
Tofautisha engineering na entrepreneurship.

Tanzania kutokuwa na viwanda vya ndani siyo kwa sababu hakuna mainjia bali hakuna enterprenuers za kuanzisha viwanda hivyo. Ninafahamu kuwa kuna watanzaia wengi engineers wanaofanaya kazi Botswana, Namibia, South Africa na sehemu nyingine za dunia.
 
Declaration of interest, Sijasoma undergraduate Udsm, Nimeishi pale kwa miaka kadhaa miaka ya mwishoni mwa 1987 mpaka Mwanzoni mwa miaka ya 1997 sio permanent bali kwa kuingia na kutoka tu, Mara nyingi tuliingia kuhitaji Data na study za wazungu fulani pale walikuwa walimu toka nje

Off Topic kidogo:

Enzi hizo kulikuwa na faculties tu yaani vitivo, Watu wote waliokuwa wanajihusisha na masomo ya sanaa iwe Profesa au Wanafunzi waliitwa Penguin au Mangwini na walidharaulika sana

Nilijisemea moyoni wakati ule mwanangu hata soma mambo ya sanaa na hata soma Udsm

Yaliyokuwa mazuri wakati huo na chuo kiliitwa chuo kweli, Hakukuwa na mambo ya sasa ya semister uchwara

1.Midaharo ilikuwa inawaka moto pale Nkurumah Hall kuanzia ya Multi party system inavyoingia, Hoja kwa hoja, Ilikuwa ni mnyukano na mapambano makali sana ya hoja kwa wakati huo, Kwa sasa midahalo yao naona wanasifia tu kupitia Tv

Yasiofaa na ambayo yanaendelezwa
1.Watoto wanasoma nadharia tu, Hakuna tofauti ya Mwanafunzi wa sociolojia au Political science akimaliza chuo na Form four au Darasa la saba

2.Engineering ni kama pambo tu pale udsm kama mapambio mengine, Sikuwahi ona Practical yeyote ya maana zaidi ya zile project wakati wa kumaliza chuo nazo ni copy and Paste

3.Madarasa mengi walijaa wachaga na wahaya na wanyakyusa pia, Cha kushangaza na kujiuliza walimu wengi enzi hizo walikuwa wahaya, Makabila mengine watu walihesabika

Je kwa sasa ni kitu gani kipya cha maana wanasoma pale udsm?
Ni kazi ya chuo kikuu kufundisha nadharia. Nadharia ndiyo inayotumika katika ugunduzi na kutatua matatizo katika jamii. Ukitaka kujifunza kutengeneza vitu/ vifaa - hii inafanyika kwenye vyuo vya ufundi ambako wanafundishwa nadharia kidogo sana ili muda mwingi watumie kwenye kutengeneza vitu/ vifaa. Elimu ya chuo kikuu ilikuwa ni kutengeneza wataalamu- ambao wanatumia nadharia kutatua matatizo kwa kuvumbua vitu vipya, michoro mipya nakadhalika. Je nchi yetu inahitaji watu wa aina gani? Kila kukicha mambo mapya yanagundulika - je tunaachwa nyuma na dunia?
 
🤔ulikuwa unapita tu hujasoma? Midahalo ilikuwa mikali sanaa? Project wakati wa kumaliza chuo hay we umeyajuaje mkuuuu kama hujasoma hapooo? Unajadiliii nini sasa na ulikuwagah tu mpita njia
 
Je kwa sasa ni kitu gani kipya cha maana wanasoma pale udsm?
Mkuu upo Dar es Salaam? Kama ndiyo, badala ya kutaka stori za watu ni vyema ukashuhudia mwenyewe. Kuanzia tarehe 24/05/2022 hadi 26/05/2022 kutakuwa na Wiki ya Maonyesho ya Tafiti na Ubunifu (UDSM Research and Innovation Week). Hapo kutakuwapo pavilions nyingi nyingi zikionyesha activities mbalimbali za kila college/school au taasisi iliyopo UDSM, na pengine walau unaweza ukapata jibu la swali lako kama kuna kipya au hakuna. Ila sijajua reference yako itakuwa ni nini maana umesema haujawahi kusoma UDSM (na sijajua pia level yako ya elimu).

Kuhusu lecturers kuwa wengi kutoka makabila fulani, nadhani kwa nyakati hizi si suala jema kujadili mambo ya makabila katika karne hii, wengine walibebwa na historia za waliotuletea elimu kupita na kuwekeza maeneo yao, kwa hiyo sikushauri sana kuipa hoja hiyo kipaumbele. Nenda kaangalie na kaulize maswali ya kitaaluma, huwezi kutoka kapa
 
Ni kazi ya chuo kikuu kufundisha nadharia. Nadharia ndiyo inayotumika katika ugunduzi na kutatua matatizo katika jamii. Ukitaka kujifunza kutengeneza vitu/ vifaa - hii inafanyika kwenye vyuo vya ufundi ambako wanafundishwa nadharia kidogo sana ili muda mwingi watumie kwenye kutengeneza vitu/ vifaa. Elimu ya chuo kikuu ilikuwa ni kutengeneza wataalamu- ambao wanatumia nadharia kutatua matatizo kwa kuvumbua vitu vipya, michoro mipya nakadhalika. Je nchi yetu inahitaji watu wa aina gani? Kila kukicha mambo mapya yanagundulika - je tunaachwa nyuma na dunia?
Ni kweli kabisa na upo sahihi. Mtu anayejivunia kusoma practical tu huwa namchora tu, maana tafsiri yake ni kwamba anatumia applications za wengine waliosoma theory, na wala yeye hana mpango wa kuwa mgunduzi wa applications mpya
 
Wanasomea yale yote ambayo yako advanced katika namna ambayo ubongo wako wewe hauwez/ akili yako haiwezi ku-discern
 
Mkuu upo Dar es Salaam? Kama ndiyo, badala ya kutaka stori za watu ni vyema ukashuhudia mwenyewe. Kuanzia tarehe 24/05/2022 hadi 26/05/2022 kutakuwa na Wiki ya Maonyesho ya Tafiti na Ubunifu (UDSM Research and Innovation Week). Hapo kutakuwapo pavilions nyingi nyingi zikionyesha activities mbalimbali za kila college/school au taasisi iliyopo UDSM, na pengine walau unaweza ukapata jibu la swali lako kama kuna kipya au hakuna. Ila sijajua reference yako itakuwa ni nini maana umesema haujawahi kusoma UDSM (na sijajua pia level yako ya elimu).

Kuhusu lecturers kuwa wengi kutoka makabila fulani, nadhani kwa nyakati hizi si suala jema kujadili mambo ya makabila katika karne hii, wengine walibebwa na historia za waliotuletea elimu kupita na kuwekeza maeneo yao, kwa hiyo sikushauri sana kuipa hoja hiyo kipaumbele. Nenda kaangalie na kaulize maswali ya kitaaluma, huwezi kutoka kapa
Taaluma gani inapatikana pale Udsm ya maana zaidi ya kukariri tu

Hakuna tofauti ya Mwanafunzi wa chuo kikuu na wa Form four kwa sasa

Unamaliza chuo unakuja kuanza maisha kama ya mtu uliyemuacha form four

Wewe Itakuwa labda mwalimu umeajiriwa na unalipwa pesa bure za kodi ya wananchi ndio maana umevimbiwa

Hapa tunaongelea uhalisia kwenye uwanja wa mapambano mtaani, Wanafunzi wa Udsm wanaondoka na kitu gani kipya?
 
ulikuwa unapita tu hujasoma? Midahalo ilikuwa mikali sanaa? Project wakati wa kumaliza chuo hay we umeyajuaje mkuuuu kama hujasoma hapooo? Unajadiliii nini sasa na ulikuwagah tu mpita njia
Sisi ni wafanyabiashara, Tunahitaji data

Tunafanya biashara kwa data mkuu, Walimu tunaowafuata ni wale ambao wanatumia muda mwingi kwenye Tafiti sio wale Maprofesa njaa
 
Duh!
We dogo, unaelewa tofauti ya Technician na Engineer ?!!!
Usilinganishe vitu tofauti!
You know nothing about the reality
Kama tungekuwa imara tangu chuo kianzishwe kimetoa Ma engineer wengi sana, Hao engineer wana msaada gani kwenye miradi yetu au kila kitu ni Chinese engineering Companies

Engineer makaratasi, Ukimpoka cheti hana anachojua kichwani
 
Hapa tunaongelea uhalisia kwenye uwanja wa mapambano mtaani, Wanafunzi wa Udsm wanaondoka na kitu gani kipya?
Kama hukusoma degree hiyo ni shauri yako na uwezo wako mdogo darasani, na kama hukusoma UDSM ndo hivyo tena, siongei sana nisije nikawatibua na wasiohusika. Mtu anafeli Form Four, akifungua biasahara yake ya duka basi anaona amewazidi saana waliosoma, kumbe wanamchora tu. Mama ongeza posho za safari tuwakereee!
 
You know nothing about the reality
Kama tungekuwa imara tangu chuo kianzishwe kimetoa Ma engineer wengi sana, Hao engineer wana msaada gani kwenye miradi yetu au kila kitu ni Chinese engineering Companies

Engineer makaratasi, Ukimpoka cheti hana anachojua kichwani
Yapo mengi tu yanayofanyika, ila watu wa stori za vijiweni kama wewe ni vigumu kujua..
Moja ya karibuni hii hapa:
 
Back
Top Bottom