Je, Kwa njia ya maombi na imani Tanzania itaishinda Corona?

Amalrik TZ

JF-Expert Member
Aug 9, 2020
341
301
Jemedali yoyote yule wa vita huchagua mbinu za vita kabla ya kuingia vitani. Aina za mbinu na silaha atakazo tumia inategemeana sana na uwezo wa jeshi lake, silaha zilizopo hamala huku pia akipima ubora na mapungufu ya jeshi lake dhidi ya mshindani wake.

Dunia ipo katika vita vikali dhidi ya Corona. Ikiwa imepita mwaka mmoja tuu toka Corona ilipo ibuka huko China, mpaka leo hii tarehe 20/02/2021 dunia imekwisha kupoteza watu zaidi ya milioni 2.45 huku zaidi ya watu milioni 111 wakipata maambukizi ya virusi vya Corona.

Mwongozo wa Shirika la afya duniani(WHO) wa namna ya kupigana vita hii ni pamoja na kunawa mikono kwa maji yanayotiririka kwa sabuni au vitakasa mikono, kuvaa barakoa kwenye mikusanyiko na kama iwapo una kikohozi/ mafua/homa /husikii harufu yakupasa kujitenga na mikusanyiko.

Tofauti na wenzetu wote duniani sisi tumeamua kupigana vita hii kwa kutumia silaha ya maombi na imani. Kuwa na imani ni jambo jema na lampendeza Mwenyenzi Mungu.

Jana Rais John Mgufuli alipokuwa kwenye msiba wa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John.W.H Kijazi alitangaza siku tatu za maombi “ kwa siku tatu kwa kuomba na kufunga, nina hakika tutashinda. Tutahangaika sana Mungu ni kila kitu.”

Lakini imani maana yake ni nini?

“Basi imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” (Waebrania 11:1). Lakini pia maandiko yanazidi kutuambia kwamba ili maombi yetu yajibiwe ni lazima tusiwe na mashaka moyoni tukiwa na shaka tuu kamwe hatutapokea kile tumuombacho Mungu.
“Amini nawaambia, Ye yote ataye uambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni kwake ila aamini kwamba hayo ayasemayo yametukia, yatakuwa yake.”( Marko 11:23).

Hivyo basi Rais wetu John Magufuli yupo sawa anaposema tusivae barakoa na maisha yaendelee kama kawaida kwani hiyo ndiyo misingi ya imani na mwenye imani hutembea kwa imani na sio kwa kuona.
Vita na Corona vinatoa changamoto kubwa sana kwa wale wanaoishi kwa imani kwa kuyafuta maandiko maishani mwao.

Mtu mwenye imani akisha ombea nchi dhidi ya Corona hubadilisha mtindo wake wa maisha kwani huanza kuamani kama Corona imekwisha toweka. Kama maandiko yasemavyo “Kwa sababu hiyo nawaambia Yo yote myaombayo mkisali, aminini kwamba mmekwisha yapokea nayo yatakuwa yenu.”(Marko: 11-24)

Hivi ndivyo maandiko yanavyotuelekeza katika mambo ya imani na maombi yetu kwa Mwenyezi Mungu.

Lakini swali la kujiuliza hapa ni kwamba Watanzania tunayo imani au tunaigiza kuwa na imani?

Kuwa na imani kwa maana yangu mimi ni kwamba tunaishi maisha yanayompendeza Mwenyezi Mungu kwa kuzifuata sheria zake alizoziandika kwenye vitabu vyake vitakatifu.

Nikimaanisha kwangu mimi Mkristo nimemkubali Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yangu na kila siku naishi maisha yanayompendeza Mungu.

Kama maandiko yasemavyo kutoka (Yohana1:12-13) “Wote waliompkoea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.”

Kutokana na msingi huo niliojijengea maishani na kuwa na kibali mbele zake hivyo basi hata nikimuomba husikia maombi yangu kwa maana mimi ni mwana wake na nafanya mapenzi yake hapa duniani.

Kama asemavyo katika 1Petro3:12 “Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya”.

Hivyo basi kutokana na kibali hicho na kuwa na uhakika wa mambo ni nayomuomba Mungu kama isemavyo (Matahayo7:7-8). Uhakika ninaoupata hata katika janga hili la Corona naishi kana kwamba Corona imekwisha ondoka kwangu baada tuu ya kuomba.

Huo ni upande wa mtu mwenye imani na maishani kwake anaishi kwa imani sio kwa kuona.

Mtu wa namna hiyo kwenye jamii ya sasa lazima aonekane akili hazimo kwani kwa imani yake ataishi kana kwamba hakuna Coroa bila ya kuvaa barakoa, kutembea na vitakasa mikono na kutokufwata masharti yote na kanuni za kujikinga na Corona.

Tatizo ambalo naliona kwa Watanzania walio wengi mioyo mwao imani kwa Mwenyezi Mungu haipo lakini midomo yao imejawa na maneno ya upako na utukufu wakiwa hawamaaanishi kutoka moyoni kile wanachokiongea.

Na nawatambua kwa matendo yao kama maandiko yasemavyo katika (Mathayo 7:16-20)“Mtawatambua kwa matendo yao ,…………..mti mzuri huzaa matunda mazuri na mti mbaya huzaa matunda mabaya……..”

Nakumbuka kuna WhatsappStatus iliyokuwa inasema siku zote Mtanzania akikuambia “Nitakuombea jua hapo ndipo kashakuombea tayari kwani baada ya hapo hata kaa kamwe akuombee tena”.

Katika nyakati hizi za Corona tulizonazo tuchague tutakaye mtukia. Maandiko yanasema ni bora kuwa moto au baridi na sio vuguvugu.
Hivyo basi yatupasa kuomba hekima na kuchagua kimoja kama tunasimama na sayansi tusimame kweli huku tukimuomba Mungu awasaidie wanasayansi wagundue dawa ya Corona mapema.

Lakini Kama tumeamua kusimama upande wa Mungu yatupasa tumtafute kwa bidiii na tuwe tayari kuyaacha yote kwani yeye mwenyewe anasema “Nanyi mtanitafuta na kuniona mtakapo nitafuta kwa moyo wenu wote.” Yeremia 29:13
 
Imeandikwa kwenye Luke 4:12 "do not put the Lord your God to the test."

Kama ni maombi kwa nini kwenye Corona tu? Kwanini si kwenye magonjwa mengine yote?

Kwanini maombi kwenye magonjwa tu? Kwanini si kwenye Nyanja zote? Usalama, ulinzi, usalama, uchumi, ujenzi, kilimo, usafiri, uvuvi, nk?

Kutegemea maombi hakuna tofauti na kutegemea ramli tu.

Maombi asili yake kwa beberu. Ramli hiyo ndiyo yetu kweri kweri. Sawa na kiingereza na kiswahili tu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Lakini sasa ndo njia Kiongozi wa nchi aliyoichagua
 
Mungu wenu hajaridhika na kafara za kina Ben Saanane, Azory Gwanda Kanguye, Akwilini Akwilini mlizotoa labda anahitaji kafara zaidi ili awasikie
 
Mungu wangu ninaye muamini hataki kafara za watu kwani alikwisha mtoa mwanamae wa pekee kabisa ambaye kila atakaye mwamini awe na uzima tele kupitia yeye.
 
“Mwamini Mungu, lakini mfunge vizuri Ngamia wako”-Mtume Muhammad S.A.W

Mungu huwa halipi maombi bali hulipa jitihada!Kupiga maombi ya nguvu wakati hakuna mipango wala hatua(Actions) sahihi,stahiki na madhubuti za kupambana na Corona ni kumkejeli Mungu.Ukimkejeli Mungu tarajia mapigo saba ya ghadhabu ya Mungu.
 
Shukrani sana ndugu imesema vyema sana. "Mungu hujibu jitihada zako." I take this in my daily life. Be blessed
 
Unafukuzwa na Simba mzee ambaye hana uwezo wa kukamata wanyama wengine na ana njaa. Wanasema usipige magoti kumwomba mungu akusaidie bali timka kweli kweli na huku ukimwomba mungu (mungu nisaidie huku ukitimua mbio). Katika hali hiyo ukipiga magoti kuomba mungu akusaidie Simba akifika atakuralua kweli, sijui nadharia ni kweli!
 
Jemedali yoyote yule wa vita huchagua mbinu za vita kabla ya kuingia vitani. Aina za mbinu na silaha atakazo tumia inategemeana sana na uwezo wa jeshi lake, silaha zilizopo hamala huku pia akipima ubora na mapungufu ya jeshi lake dhidi ya mshindani wake.

Dunia ipo katika vita vikali dhidi ya Corona. Ikiwa imepita mwaka mmoja tuu toka Corona ilipo ibuka huko China, mpaka leo hii tarehe 20/02/2021 dunia imekwisha kupoteza watu zaidi ya milioni 2.45 huku zaidi ya watu milioni 111 wakipata maambukizi ya virusi vya Corona.

Mwongozo wa Shirika la afya duniani(WHO) wa namna ya kupigana vita hii ni pamoja na kunawa mikono kwa maji yanayotiririka kwa sabuni au vitakasa mikono, kuvaa barakoa kwenye mikusanyiko na kama iwapo una kikohozi/ mafua/homa /husikii harufu yakupasa kujitenga na mikusanyiko.

Tofauti na wenzetu wote duniani sisi tumeamua kupigana vita hii kwa kutumia silaha ya maombi na imani. Kuwa na imani ni jambo jema na lampendeza Mwenyenzi Mungu.

Jana Rais John Mgufuli alipokuwa kwenye msiba wa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John.W.H Kijazi alitangaza siku tatu za maombi “ kwa siku tatu kwa kuomba na kufunga, nina hakika tutashinda. Tutahangaika sana Mungu ni kila kitu.”

Lakini imani maana yake ni nini?

“Basi imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” (Waebrania 11:1). Lakini pia maandiko yanazidi kutuambia kwamba ili maombi yetu yajibiwe ni lazima tusiwe na mashaka moyoni tukiwa na shaka tuu kamwe hatutapokea kile tumuombacho Mungu.
“Amini nawaambia, Ye yote ataye uambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni kwake ila aamini kwamba hayo ayasemayo yametukia, yatakuwa yake.”( Marko 11:23).

Hivyo basi Rais wetu John Magufuli yupo sawa anaposema tusivae barakoa na maisha yaendelee kama kawaida kwani hiyo ndiyo misingi ya imani na mwenye imani hutembea kwa imani na sio kwa kuona.
Vita na Corona vinatoa changamoto kubwa sana kwa wale wanaoishi kwa imani kwa kuyafuta maandiko maishani mwao.

Mtu mwenye imani akisha ombea nchi dhidi ya Corona hubadilisha mtindo wake wa maisha kwani huanza kuamani kama Corona imekwisha toweka. Kama maandiko yasemavyo “Kwa sababu hiyo nawaambia Yo yote myaombayo mkisali, aminini kwamba mmekwisha yapokea nayo yatakuwa yenu.”(Marko: 11-24)

Hivi ndivyo maandiko yanavyotuelekeza katika mambo ya imani na maombi yetu kwa Mwenyezi Mungu.

Lakini swali la kujiuliza hapa ni kwamba Watanzania tunayo imani au tunaigiza kuwa na imani?

Kuwa na imani kwa maana yangu mimi ni kwamba tunaishi maisha yanayompendeza Mwenyezi Mungu kwa kuzifuata sheria zake alizoziandika kwenye vitabu vyake vitakatifu.

Nikimaanisha kwangu mimi Mkristo nimemkubali Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yangu na kila siku naishi maisha yanayompendeza Mungu.

Kama maandiko yasemavyo kutoka (Yohana1:12-13) “Wote waliompkoea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.”

Kutokana na msingi huo niliojijengea maishani na kuwa na kibali mbele zake hivyo basi hata nikimuomba husikia maombi yangu kwa maana mimi ni mwana wake na nafanya mapenzi yake hapa duniani.

Kama asemavyo katika 1Petro3:12 “Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya”.

Hivyo basi kutokana na kibali hicho na kuwa na uhakika wa mambo ni nayomuomba Mungu kama isemavyo (Matahayo7:7-8). Uhakika ninaoupata hata katika janga hili la Corona naishi kana kwamba Corona imekwisha ondoka kwangu baada tuu ya kuomba.

Huo ni upande wa mtu mwenye imani na maishani kwake anaishi kwa imani sio kwa kuona.

Mtu wa namna hiyo kwenye jamii ya sasa lazima aonekane akili hazimo kwani kwa imani yake ataishi kana kwamba hakuna Coroa bila ya kuvaa barakoa, kutembea na vitakasa mikono na kutokufwata masharti yote na kanuni za kujikinga na Corona.

Tatizo ambalo naliona kwa Watanzania walio wengi mioyo mwao imani kwa Mwenyezi Mungu haipo lakini midomo yao imejawa na maneno ya upako na utukufu wakiwa hawamaaanishi kutoka moyoni kile wanachokiongea.

Na nawatambua kwa matendo yao kama maandiko yasemavyo katika (Mathayo 7:16-20)“Mtawatambua kwa matendo yao ,…………..mti mzuri huzaa matunda mazuri na mti mbaya huzaa matunda mabaya……..”

Nakumbuka kuna WhatsappStatus iliyokuwa inasema siku zote Mtanzania akikuambia “Nitakuombea jua hapo ndipo kashakuombea tayari kwani baada ya hapo hata kaa kamwe akuombee tena”.

Katika nyakati hizi za Corona tulizonazo tuchague tutakaye mtukia. Maandiko yanasema ni bora kuwa moto au baridi na sio vuguvugu.
Hivyo basi yatupasa kuomba hekima na kuchagua kimoja kama tunasimama na sayansi tusimame kweli huku tukimuomba Mungu awasaidie wanasayansi wagundue dawa ya Corona mapema.

Lakini Kama tumeamua kusimama upande wa Mungu yatupasa tumtafute kwa bidiii na tuwe tayari kuyaacha yote kwani yeye mwenyewe anasema “Nanyi mtanitafuta na kuniona mtakapo nitafuta kwa moyo wenu wote.” Yeremia 29:13
Haleluya ❗ Ni mwendelezo wa kushinda na zaidi ya kushinda, kwa kila jaribu katika nchi yetu Tanzania; kupitia Rais wetu mpendwa, Dkt.John Magufuli.
 
Back
Top Bottom