Je kwa nini kusiwepo na Ukomo wa ubunge?

Tundapori

JF-Expert Member
Aug 12, 2007
645
260
Jamani naomba kueleweshwa hivi kwa nini kusiwepo na kipindi cha ukomo cha ubunge kama ilivyo kwa raisi.
Raisi TZ ana vipindi viwili vya miaka mitano mitano cha kuwa raisi.

Unakuta mbunge huyohuyo anakuwa mbunge zaidi ya miaka 35 yaani sawa na vipindi 7 vya miaka mitano mitano, mpaka huyo mbunge anachoka ile mbaya na inafikia hatua hawezi tena kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jimbo lake.

Au kukiwepo na ukomo kwa ubunge tatizo tunaweza kujikuta tunapata uhaba wa mawaziri? Maana huwezi kuwa waziri bila kuwa mbunge kwanza.
Labda inawezekana bongo tuna uhaba wa watanzania ambao wanaweza kuwa wabunge.
 
The real question is, kwa nini bunge lisifutwe kabisa?

Mi sioni kazi yake.
 
unasema kweli hakuna sababu ya kuwa na vunge, ondosha kabisa hii kitu watu wanaenda kula hela yetu hakuna bunge wala nini hebu nisaidieni bunge limenisaidia nini katika maisha yangu? tukiwa na bunge tuwe na bunge la kujitolea tuone nani atakuwa mbunge vipindi viwili
 
hivi kweli tukiwa na wabunge wa kujitolea itakuwaje? yaani wawe na kazi zao zingine zaidi wasilipwe na bunge watu watakuwa kweli wanagombania majimbo? ni mawazo tu.
 
Unategemea kuwe na ukomo wakati walioshikilia mpini ni akina mungai,makweta,shellukindo,galinoma,sarungi,nk?
 
Jamani naomba kueleweshwa hivi kwa nini kusiwepo na kipindi cha ukomo cha ubunge kama ilivyo kwa raisi.
Raisi TZ ana vipindi viwili vya miaka mitano mitano cha kuwa raisi.

Unakuta mbunge huyohuyo anakuwa mbunge zaidi ya miaka 35 yaani sawa na vipindi 7 vya miaka mitano mitano, mpaka huyo mbunge anachoka ile mbaya na inafikia hatua hawezi tena kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jimbo lake.

Au kukiwepo na ukomo kwa ubunge tatizo tunaweza kujikuta tunapata uhaba wa mawaziri? Maana huwezi kuwa waziri bila kuwa mbunge kwanza.
Labda inawezekana bongo tuna uhaba wa watanzania ambao wanaweza kuwa wabunge.

Hilini jambo zuri sana ambalo nilishawahi kulisema huko nyuma. Nitajiunga nawe siku nyingine tulijadili. Lina tija sana kwa nchi iwapo viongozi wote wa kucahguliwa na wananchi watakuwa na term limits: madiwani, wabunge na Rais; limits hizo zisivuke miaka minane.
 
Jamani naomba kueleweshwa hivi kwa nini kusiwepo na kipindi cha ukomo cha ubunge kama ilivyo kwa raisi.
Raisi TZ ana vipindi viwili vya miaka mitano mitano cha kuwa raisi.

Unakuta mbunge huyohuyo anakuwa mbunge zaidi ya miaka 35 yaani sawa na vipindi 7 vya miaka mitano mitano, mpaka huyo mbunge anachoka ile mbaya na inafikia hatua hawezi tena kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jimbo lake.

Au kukiwepo na ukomo kwa ubunge tatizo tunaweza kujikuta tunapata uhaba wa mawaziri? Maana huwezi kuwa waziri bila kuwa mbunge kwanza.
Labda inawezekana bongo tuna uhaba wa watanzania ambao wanaweza kuwa wabunge.

Ubunge ajira za watu kaka, majimbo washayafanya mali zao.
 
The real question is, kwa nini bunge lisifutwe kabisa?

Mi sioni kazi yake.
Kulifuta? Ya akina Richmond yangeibukia wapi? Tulipunguze Bunge letu. Ni kubwa mno kwa uchumi wetu wa sasa. Kila Halmashauri/ Manispaa iwe na Mbunge mmoja tu makini. Serikali yetu isiundwe na Wabunge. Baraza la Mawaziri liwe dogo na wizara ziwepo KIKATIBA sio Rais aachiwe kuunda wizara kulingana na idadi ya washikaji/wapambe/wafadhili alionao.
 
Mawazo mazuri ila iwe kazi ya kujitolea.
 
waziri mkuu pinda alitoa hoja juu ya kuwepo na ukomo kwa wabunge kuwa na ukomo maalum wa vipindi vitatu tu.. ila cha ajabu wadau wengi walimpinga,hasa wengi wao wakiwa ni wabunge wanaotetea matumbo yao hasa waliofanya majimbo kuwa mali zao binafsi. binafsi hoja ya kuwepo na ukomo ktk ubunge na pia ktk nyadhifa za kisiasa nakubaliana nalo kwa kzaidi ya 100%..kwa sasa nikiangalia utendaji kazi na ufanisi wa bunge naona ni kama mchezo wa kuigiza na pia mnaona ni kama sehemu ya kuchuma utajiri kwani hamna wanachokifanya, naamini kwa kuruhusu damu changa itasaidia kuleta hamasa na changamoto nyingi bungeni..nyie wadau wengine mnalionaje hili?
 
hujui maana ya uchaguzi? Let democracy do the talking! Kama wananchi wanapenda kuliwa...waache waliwe tu! Kama wanaogopa kuuliza maswali mazito...waache waliwe tu! Huwezi kuweka kikomo katika ubunge. Let us dissect the problem from a different angle. Wewe unaona shida ni nini hasa? Wabunge kuwa unproductive au kujaza matumbo?
 
Wabunge wetu wamekuwa un productive na hiyo ni labda kutokana na kukaa muda mrefu natumai kuna ambao wako pale zaidi ya miaka 25 na hakuna mabadilliko yoyote majimboni kwao nafikiri kwa utaratibu wa ukomo tunaweza kuona tofauti ya utendaji.
 
Niambie nchi gani duniani ina ukomo wa ubunge.Kama hakuna kwanini Tanzania iwe ya kwanza.Nchi iliyoanza demokrasia duniani (USA) haina ukomo wa wabunge,nao wamekosea?
 
Back
Top Bottom