Je, kwa nafasi yako wewe hili ungelifanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, kwa nafasi yako wewe hili ungelifanyaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kipenzi Chao, Mar 31, 2011.

 1. K

  Kipenzi Chao Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukiwa mwanaume, umeoa na umekuwa na mzunguko wa hapa na pale katika kutafuta mkate wa familia. Umebahtika kumpata mtoto wako mmoja....! Umekuwa ni wa dunia ya leo na hivyo ukawa mmepanga na mkeo kuweka interval fulani katika maamuzi ya kumtafutia mwana wenu mdogoye...! Lakini ukiwa safarini ukawa na tabia ya kuwasiliana na mkeo mara kwa mara, na katika mawasiliano hayo mkeo akakudokeza jambo lilikupelekea kuumia ilhali imekuwa vigumu kuamini; ya kuwa mama yako mzazi eti anamshauri mkeo abebe mimba without your concern....!!!

  Uliporudi ulimuuliza mkeo vizuri kwa kuwa fikra za kwamba huenda mkeo anamsingizia mama yako jambo kama hilo, na akafafanua kwa undani. Nawe ukaamua kufanya uchunguzi wa kina, na hatimaye ukabaini ya kuwa ni kweli mama yako alipata kumshauri mkeo jambo kama hilo...!

  SWALI:


  1. Ukiwa mwanaume utalishughulikiaje hilo swala?
  2. Ukiwa mke wa mtu, je, wewe ungechukua hatua ipi juu ya ushari wa mama mkwe?
  3. Ukiwa mzee, mwenye kulea ndoa ya wanao, ni nini hasa kinachowafanya wazee kuwa na tabia kama hii?
   
 2. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Ndoa ni ya watu wawili ukishaanza kuingiza mtu wa tatu tu kwisha habari yake
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Mbona hilo dogo sana
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Ubaya ungekuwa abebe mimba ya mtu mwingine...

  Wamama hupenda kupata wajukuu wengi wawaone kabla hawajafa...
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280

  baadhi ya ndoa kutegemea na tamaduni
  familly member wanahusika kwenye watoto,
  waitwe majina gani,walelewe vipi,
   
 6. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mjomba wangu mkewe alijifungua mm akili zikiwa zishaanza kujua baya na zuri. Babu akataka kumpa jina yule binamu yangu..... Uncle akamuuliza Babu, kwani yeye (Uncle) alipewa jina alilo nalo na nani? Babu akasema yeye mwenyewe (Babu) ndio alimpa hilo jina. Basi Uncle akasema niache na mimi nimpe jina maana ni wangu kama ulivyotumia nafasi yako kutupa majina.

  Ingekuwa ni mm ningetumia maamuzi haya ya Uncle...........
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Baada ya watoto kuzaliwa sawa wanaweza kuchangia mawazo na kutoa mapendekezo.Ila sio kuwapangia wazae lini..wangapi kwasababu wenye ndoa ndo wanaojua kwanini wamepanga wanavyokua wamepanga.After all..wao ndo watakaokua responsible kwa hao watoto na sio ndugu wengine!
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  kweli but wazazi huwa hawaelewi
  ukiwaambia huzai eti huna pesa...
  Wao wanataka wajukuu wengi iwezekanavyo
   
 9. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,710
  Trophy Points: 280
  Maamuzi ni ya watu wawili, wazazi wanapenda iwe hivyo lakini nyie ndio wahusika wakuu kwenye maisha yenu cha msingi ni kupanga kuendana na matakwa yenu
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Matokeo yake ikitokea wazazi wakafariki kundi la watoto linanyanyasika kwasababu hamna atakae wapokea...au wanchukuliwa kufanywa vijakazi!
   
 11. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Panga maisha yako kulingana na kipato chako na asitokee mtu wa kukusukuma kufanya maamuzi ambayo unakuwa huwa radhi nayo,mama atabaki katika nafasi yake ya umama na mpaka wake kwa familia yako unaishia hapo na si zaidi ya hapo.
   
Loading...