Je kwa muda huu ni waziri gani ni jipu?

msemakweli95

Member
Mar 30, 2017
5
6
Habari za usiku ndugu zangu leo ningependa tujiulize kwa muda wa zaidi ya mwaka mzima ni waziri yupi unamuona kama jipu kwa upande wangu naona waziri wa elimu ni jipu yaani mipango yake mingi ni kupunguza wasomi sio kuboresha elimu kwan elimu ingebidi swala la kupandisha gredi liwe la mwisho kwanza wangeanza kuboresha mazingira ya kusomea kuongeza walimu na kuboresha maisha ya walimu yan mipango ya waziri ni kumkomoa mtoto wa maskini anayesoma shule ya kata.
 
Habari za usiku ndugu zangu leo ningependa tujiulize kwa muda wa zaidi ya mwaka mzima ni waziri yupi unamuona kama jipu kwa upande wangu naona waziri wa elimu ni jipu yan mipango yake mingi ni kupunguza wasomi sio kuboresha elimu kwan elimu ingebd swala la kupandisha gredi liwe la mwisho kwanza wangeanza kuboresha mazingira ya kusomea kuongeza walimu na kuboresha maisha ya walimu yan mipango ya waziri ni kumkomoa mtoto wa maskini anayesoma shule ya kata
Tukuulize na wewe, sahivi ni nani kwenye familia yenu ni jipu? Siyo wewe kweli?
 
Naona kama Mhe Rais amekuwa mtendaji zaidi. Kwa namna hiyo, inakuwa vigumu kidogo kwa wasaidizi wake ambao ni mawaziri kufanya kazi zao za kumsaidia sawasawa. Nadhani Mhe Rais angeshauriwa akawa msimamizi na kutoa maelekezo ya kuboresha kwa wasaidizi wake.Naona kama Raisi angekuwa mwangalizi wa kazi za Waziri Mkuu, na hata mawaziri wote kwa kusaidiana.

Sehemu kubwa wa wasaidizi wa Mhe Rais ni kama wamekuwa waoga kutenda kwa kuogopa huenda wasifanye kama anavyotaka Mhe Rais. Ingekuwa vizuri sana kama kila Wizara ingekuwa na mwongozo wa ni kitu gani Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara wanatakiwa kufanya katika kila Wizara. Kwa kufanya hivyo tusingekuwa na shida ya kuweza kupima utendaji wa Mawaziri wetu, maana tungewapima kwa kiwango walichoweza kufanya.

Kitendo cha kuachia kila Waziri afanye kwa kadri atakavyoona inafaa ni tatizo, na hakuna anayeweza kusema kwa hakika waziri huyu ameweza au ameshindwa. Kwa sasa tunaweza kusema huyu ameshindwa au ameweza labda kwa yale ya kawaida kabisa ambayo si ya kitaalamu ambayo hata mwananchi wa kawaida anaweza kubaini, kupitia hotuba zao. Unaweza kubaini kupitia hotuba ya waziri ikiwa anachosema Waziri ni ubabaishaji, siasa au ni kitu halisi na cha kweli. Hiyo s njia sahihi ya kuweza kupima utendaji wa Waziri au Katibu Mkuu wa Wizara.
 
Huwezi kusema waziri fulani ni jipu ilihali inajulikana kuwa wanafanya kazi kwa tension kubwa.

Jipu ni Magufuli mwenyewe pamoja na DAB.
 
Mawaziri woooote ni wazuri...hakuna jipu.Labda hawana instrument au hawajapata semina elekezi au wanafanya mgomo baridi.Ukweli wooote ni wazuri.
 
Naweza kusema wote ni majipu kwa kukaa kimya pale utaratibu toka mamlaka ya juu unapokiukwa mf. kutumbuliwa kwa Nape kwa kuwa tu alifuata utaratibu wa kazi yake Maoni yangu walipaswa kujiuzulu kwa mwenzao kuonewa, kwakuwa leo kwa Nape kesho kwao. Kukaa kwao kimya kunaleta ukakasi juu ya uwezo wao na uzalendo wao kwa nchi
 
Back
Top Bottom