Je, kwa mshahara wa Shilingi 310,000 unaweza kuishi Dar es Salaam?

Kwa mujibu wa Shirika la Takwimu Nchini,
Wastani wa pato la Mtanzania kwa mwaka ni Tsh.2,386,826.1..Ambapo kwa mwezi ni sawa na Tsh.198,902.17
...
Nikirudi kwenye mada, Yawezekana kabisa kwa kiasi ulichobainisha wapo wenye uwezo wa kuishi nacho,na wapo wasioweza kuishi kwa kiasi hicho.

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Habari wadau!

Ebu nisaidieni hivi kweli 310,000/= inatosha mtu kufanya kazi na kuishi DAR au unatakiwa kuwa na miundombinu mingine?
wakati mwingine tusiogope.
miaka 12 nyuma nilikuwa nawawezesha wanakijiji na watu wenye kipato cha chini jinsi gani waweze kufanikiwa na kwa mara ya kwanza nilienda katika eneo ambalo watu wengi walikuwa hawajawahi kunywa hata soda kiasi tulipofanya sherehe za mafanikio walizitaja soda kwa rangi zake.
huo ndio ukweli anayekataa na akatae kwa kuzoea.
sasa katika success story zilizonivutia ni mwanakijiji mmoja baada ya kukopa mkopo wa shilingi 80,000/- alisema ni mkubwa na atatumia fedha hiyo kujenga nyumba ya matofari! hiyo ni elfu 80 na sio laki nane upo hapo. binafsi niliingiwa na hofu pamoja nilikuwa nawaaminisha katika kutumia kiasi kidogo kwa mafanikio lakini kwa tukio hili pose liniliisha kwa kweli.
lakini jamaa alifanikiwa na sasa ananyumba zaidi ya tatu anakula kodi na analipa kodi ya majengo mwezeshaji bado napanga!
nilivyomuhoji alisema alianza kununua mchanga kwa wakati ule lorry moja lilikuwa 30,000/- akanunua mchanga malorry matatu kwa kuongezea hela.
wauza mchanga wakamkopesha malorry mengine mawili akawa na mchanga lorry tano akaongeza bidii na kuongeza kazi zaidi akalipa mkopo pamoja na mchanga ndipo alipoanza kukopa kwa kufyatua tofari na baada ya muda ujenzi ukaanza.
hivyo kikubwa sio fedha ila ni nia ya ndani unataka nini na kisha kuondoa uwoga mwisho wa siku tunafanikiwa.
tabu tumezoea fedha yote tunayopata lazima itumie kwa matumizi yanayofuata hatupo tayari yapitie shughuli zingine ndio kisha zitumike.
mfano unaweza kumpa mama mtaji wa biashara kisha biashara ikalisha nyumbani na wewe ni kuahakikisha biashara inasimama.
 
Chunguza kwa makini, kuna wanaolipwa huo mshahara na wanaishi, jua tu maisha ni mchezo. Nilitaja waalimu kwani hawalipwi kulingana na kazi ngumu wanayofanya lakini bado wanamudu maisha. Umeeeeeelewa?
 
Back
Top Bottom