mimiks
JF-Expert Member
- Mar 17, 2013
- 1,416
- 2,789
Hebu weka mchanganuo wa gharama za usafiri na chakula kwa siku.Maisha yako ndio yataamua.
Mimi kipato changu kwa mwezi hakizidi laki 3 kwasasa ila mahitaji yangu yote nafanya ikiwemo kumsaidia mama, kulipa kodi, kula, maji, nauli, SACCOS, kuwekeza, kuhonga, kuwapa wapiga mizinga.
Na hii ni kwasababu binafsi,
- Sinywi pombe
- Sivuti sigara wala chochote
- siyo mtu wa mambo mengi sijui parties, birthday
- Huwa natoka mara moja moja sana nikiwa stressed.
- Mara nyingi mimi ni mtu wa kukaa ndani tu, na sio kwamba najitesa au najinyima hapana. I just enjoy being alone
Kwahiyo lifestyle yako ndio ita determine kama kipato hicho kinatosha amma la.
Hivi vipato vya watu vingi mtu hutoboi bila kujiongeza. Hata hao walinzi na wafanya usafi maofisini wana namna nyingine ya kupata hela. Mfano wafanya usafi wanakubali kutumwa huku na kule. Ukimtuma unamlipa elfu 1. Kwahiyo ana uhakika wa kuongeza kipato na kupunguza makali ya maisha kwa kutumwa tumwa. Yani kila mmoja ana namna yake ya kuongeza kipato. Sasa watu huwa wanasahau kupigia mahesabu hizi hela wanazopata kila siku hata kama ni elfu 2 ndio maana watu wanasema kwamba mimi kipato changu 150,000 na nimejenga.
Mkiwaambia watu muwaambie na zile namna nyingine mmejiongeza kupunguza ukali wa maisha.