Je, kwa maneno haya ya Freeman Mbowe, Tanzania bado ni moja?

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,214
5,940
''Awamu ya tano imetuumiza sana watu wa Kaskazini, mashambulizi mengi yamelenga kaskazini, na sio kwamba ni sisi CHADEMA tu, hata wanachama wa CCM wa Kaskazini wameumizwa sana na serikali hii ya awamu ya tano''

Siamini kama Mbowe Anaweza kusema maneno haya. Mbowe umejidhalilisha sana.

Kaskazini imekosa nini ukilinganisha na Kusini ambapo kuna umaskini mkubwa?

Tuache kumtupia Rais lawama zisizo za kweli.
 
Ungeweka video tuthibitishe

Maana Twitter siku hizi imekuwa ya hovyo kwa kufanya caption zisizo za kweli
 
Kwahiyo kwa mujibu wa Mbowe ni kwamba anataka kusema mikoa yenye umuhimu Tanzania nzima ni hiyo ya Kaskazini pekee na mingine haina umuhimu au nayo haina changamoto zozote zile? Sasa naanza Kuelewa ni kwanini upinzani nchini Tanzania hauwezi Kuing'oa CCM na kushika dola hasa kutokana na kauli zilizo 'very illogical' kama hizi za viongozi wao waandamizi.
 
Kama ni kweli amesema,iwe madai ya Mbowe yana ukweli au hayana, binafsi naona amekosea sana kusema waziwazi haya.

Tunaweza kuligawa taifa kiutani tu.

Analigawa kwa kusema hivyo wazi wazi au limeshagawika yeye anatoa ushuhuda tu? Hakuna kosa kubwa kama kukalia kimya uovu eti kisa ukisema utaligawa taifa. Anayeligawa taifa anafahamika ila anafumbiwa macho.
 
Kwahiyo kwa mujibu wa Mbowe ni kwamba anataka kusema mikoa yenye umuhimu Tanzania nzima ni hiyo ya Kaskazini pekee na mingine haina umuhimu au nayo haina changamoto zozote zile? Sasa naanza Kuelewa ni kwanini upinzani nchini Tanzania hauwezi Kuing'oa CCM na kushika dola hasa kutokana na kauli zilizo 'very illogical' kama hizi za viongozi wao waandamizi.

Hizo lugha zinazungumzwa sana na viongozi walioko madarakani. Kwani kuing'oa ccm madaraka kuna uhusiano gani na ukweli aliousema Mbowe. Kwahiyo watu wafumbie macho ukweli kisa hawataing'oa ccm madarakani?
 
''Awamu ya tano imetuumiza sana watu wa Kaskazini, mashambulizi mengi yamelenga kaskazini, na sio kwamba ni sisi CHADEMA tu, hata wanachama wa CCM wa Kaskazini wameumizwa sana na serikali hii ya awamu ya tano''

Kwani Mbowe ni wa Kaskazini au Mbambabay kule Nyasa kwa akina Sasali?
 
''Awamu ya tano imetuumiza sana watu wa Kaskazini, mashambulizi mengi yamelenga kaskazini, na sio kwamba ni sisi CHADEMA tu, hata wanachama wa CCM wa Kaskazini wameumizwa sana na serikali hii ya awamu ya tano''

Baba Magu kazi zaidi wananyooka.
 
''Awamu ya tano imetuumiza sana watu wa Kaskazini, mashambulizi mengi yamelenga kaskazini, na sio kwamba ni sisi CHADEMA tu, hata wanachama wa CCM wa Kaskazini wameumizwa sana na serikali hii ya awamu ya tano''

Kafika mwisho wa kufikiri,kaishiwa pumzi.....ni kama farasi anayekata roho,hurusha mateke unaweza kufikiri anafufuka kumbe anakata roho.
 
mbuga mpya, teuzi nyingi watu wa uko, viwanja vya ndege, na mengi tu
Mbuga Ya Wanyama Na Uwanja Wa Ndege Chato Ndo Kuenjoy Kwa Watu Wa Kanda Ya Ziwa ?

Hivi Kanda Ya Ziwa Unaijua Hasa Ni Ipi ?

Yaani Kibwengo Kutengeneza Genge Lake Dogo La Watu Wanaomwabudu Wasiozidi 30 Kwaajili Ya Kula Keki Ya Taifa Ndo Useme, Watu Wa Kanda Ya Ziwa Wanaenjoy.

Ally Happy, Spika Ndugai, Tulia Ackson, Angela Kairuki Ni Watu Wa Kanda Ya Ziwa ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom