Je, kwa hizi 'Siasa' za Tanzania 'ICC Chief Prosecutor' Bi. Fatou Bensouda apite sasa 'Kutusalimia' au aje rasmi 2025?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,466
108,621
Nimeona mahala kuwa huyu Mwanamama ambaye ni Mkuu wa Mashtaka katika Mahakama ya Uhalifu Kimataifa ( ICC ) anaenda zake nchini Sudan huko 'Kumalizana' na aliyekuwa Rais wa muda mrefu wa nchi hiyo na aliyefanya 'Uhalifu' wa kila namna Omar Ali Bashir ambaye yuko 'Kizuizini' huko.

Kwakuwa Tanzania imekuwa ikisifika na bado inasifika kuwa Kisiwa na Amani barani Afrika nilikuwa nataka Watanzania nasi 'tumkaribishe' hata kwa Siku moja tu ili aje 'Kujionea' mwenyewe jinsi Watanzania tulivyo Wakarimu, wenye Amani, hatuuani, hatutekani, hatuchinjani, hatutishani na wala hatuna Wanasiasa ambao wana Kauli / Lugha za Kuhatarisha hii Amani yetu.

Kwa jinsi Tanzania ilivyo 'Salama' na Wanasiasa pamoja na Wananchi wake 'Kiujumla' walivyo na 'Upendo' huenda akija tukapewa 'Tuzo' Kimataifa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom