Je kuwajibika na kutetea maslahi ya kitaifa ni kutaka ubunge au urais 2015?

raffiki

Senior Member
Jun 4, 2011
160
44
Nimekua nikijiuliza hivi Tanzania yetu ya sasa haihitaji tena wawajibikaji au wazalendo bila kutaka kuwa wabunge au marais?????nasema hivi kwakuwa imekuwa desturi sasa Tanzania, hasa kwa wana siasa na wapambe wa wanasiasa, mtu akifanya jambo jema la maendeleo au kutoa maoni yake mazuri ya kizalendo juu ya mstakhabali wa taifa letu anajengewa hoja ya kutaka uongozi 2015. Na pia, wajenga hoja hao ni wanasiasa au wapambe wa wanasiasa ambao wanamakundi yanayolenga kushika dola 2015. SASA TUSEME YUPI ANAYETAKA HUO UBUNGE NA URAIS???? NI HAO WAWAJIBIKAJI NA WATOA MAONI YA KIZALENDO??? AU WANASIASA NA WAPAMBE WAO WATOA HOJA HIYO???



G.Thinkers tujiulize..?
 
Back
Top Bottom