Je kuwa na mtoto kabla ya Ndoa imekaaje??

Takwimu simmezisikia nusu ya wanaume ni wagumba ni vizuri ukatest usije ukajuta huko mbele.Kitu mimba biashara nyingine baade.
 
Hakuna bahati mbaya duniani, unapo vua chupi na kukutana na mwenzio tegemea mambo haya mimba/ gonjwa la zinaa ukipata ndo useme bahati mbaya?
kupata mimba kwa bahati mbaya ipo kutokana na uwelewa mdogo wa msichana, rafiki yangu amepata mimba mwanaume alimdanganya kama amemepa dawa za kuzuia mimba na kutokana na uelewa mdogo wa huyo rafiki yangu alikubali na sasa ana mimba, kwa case kama hii utasemaje?
 
Ni u.a.s.h.e.r.a.t.i na Uzinifu hapo unazaa kabla ya ndoa ili iweje? Kama sio umalaya? Shwaini...!!! Alafu unaita Kutest? Unatest nini mzinzi tu we Oa
kutokana na maneno yako idadi ya watoa mimba itaongezeka ili mhusika asionekane kuwa ni mwasherati, mzinifu na malaya.
 
wanaume nanyi mnasababisha haya yote mana mwingine unamkuta kazalia nyumbani mana mwanaume aliyempa mimba amemkataa unategemea afanyaje?
 
kupata mimba kwa bahati mbaya ipo kutokana na uwelewa mdogo wa msichana, rafiki yangu amepata mimba mwanaume alimdanganya kama amemepa dawa za kuzuia mimba na kutokana na uelewa mdogo wa huyo rafiki yangu alikubali na sasa ana mimba, kwa case kama hii utasemaje?

Tutasema walidanganyana kuwa wangeuficha uasherati wao lakini ikashindikana. Naam ni umalaya still
 
Sikujuwa alizaa kabla ya kuolewa lakini Chausiku dada yake hadi anaolewa alikuwa hajawahi kuzaa ila ametoa mimba 4,napo nani malaya,nani muasherati?
 
Husababishwa na tamaa, uhuni na u.m.a.l.a.y.a labda iwe kuwa uliolewa ukaachwa au mumeo kufa...
.

Huu ni wehu sasa! Mtoto siku hizi mwanamke anajipandikiza mwenyewe! ama ndio ule usemi mtoto ni wa mama?


On serious note: watoto nje ya ndoa hata miaka ya zamani walikuwepo ila mara nyingi watoto walitunzwa na mabibi zao ili kutoa nafasi ya mwanamke kuolewa. Lakini, siku hizi taasisi ya familia imebadilika sana - watu wanahofu inamomonyoka. Lakini sio kweli ni inabadilika tu. Watoto wengie wanazaliwa nje ya ndoa.

On interesting note: Hao unaowaita watoto wa nje ya ndoa - yawezekana ndio watoto wa mzazi mmoja na asiye na nia ya kuwa ndani ya ndao ama hajabahatika kuwa na ndoa, na ndivyo hivyo atakuza mtoto/ watoto wake. Labda, ni ulize swali la kizushi tu - je mwanamke ama mwanaume asiruhusiwe kuzaa mpaka awe na ndoa? Tuangalie na takwimu za ndoa pia!
 
Sikujuwa alizaa kabla ya kuolewa lakini Chausiku dada yake hadi anaolewa alikuwa hajawahi kuzaa ila ametoa mimba 4,napo nani malaya,nani muasherati?
hahaaaaaa umeona eeeh. mi kuna rafiki zangu wengi tu nina mifano yao. hawana watoto mpk sasa ila wamezichomoa kama hawana akili nzur nao pia wanatamba kuwa ni mabinti lol......... na kuna wale ndugu zetu wa upande mwingine ye kutwa kucha ni biashara ila hata cku moja hujawahi sikia kuwa ana mtoto ila kuchomoa ni kawaida kama kunywa maji!
 
Mmmmh, mtoto njee ya ndoa is big NO, unless kuna sababu za kulazimu kama ulibakwa. Kwanza si jambo jema kwa jamii, maana inazidisha idadi ya watoto wa kutupwa, ikiwa mama hana uwezo wa kumwangalia huyo kiumbe na baba kaingia mitini. Pili saikolojikali, kuitwa mtoto wa haramu kwenye jamii si jambo la kushangilia. Kuna madhehebu mengine mtoto wa nje ya ndoa hana haki kamili kwenye nyumba za ibada.

Ikiwa tutaona hili jambo ni la kawaida, NDOA itakuwa haina misingi katika familia zetu.
 
Nina swali.. Mtoto wa nje ya ndoa ni wa aina gani??
nimeuliza kwasababu wengine (KE) wako ndani ya hizo ndoa lakini
bado wanapata ujauzito usio kuwa wa waume zao..hii imekaaje?

kwangu mimi Mtoto ni mtoto haijalishi amekujaje, wapi na kwa wakati gani!
umalaya auna nafasi,make wengine wanado once ..kitu!
 
Back
Top Bottom