Je, kutanguliza maslahi ya chama badala ya taifa, ni kosa la jinai ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, kutanguliza maslahi ya chama badala ya taifa, ni kosa la jinai ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Feb 26, 2009.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Je kutanguliza maslahi ya chama badala ya taifa ndani ya bunge kunaweza kutafsiriwa kama hujuma dhidi ya umoja wa kitaifa ? Je anayewashawishi wawakilishi wa wananchi ambao wengi wao hawana chama, kutetea maslahi ya chama kuliko ya taifa anatenda kosa la jinai. Je mbunge aliyeapa kuiwajibisha serikali kulinda katiba kwa kuhakikisha utawala wa sheria, haki na usawa, anapoamua kutanguliza na kulinda maslahi ya kikundi katika jamii, anatimiza wajibu ?

  Naomba mchango kutoka kwenu bila jazba na papara kuhusu swala hili. Hawa wana tofauti gani na wanaotumia rasilimali za taifa kujinufaisha wao wenyewe na watu wao. Imebidi niseme hili baada ya serikali kukaa kimya bila kukemea kauli iliyotolewa na gwiji wa siasa ndani ya CCM, Kingunge Ngomable Mwiru akitaka wabunge wa CCM kutanguliza maslahi ya chama kuliko taifa. Je yawezekana mahakama na vyombo vya dola pia vinafanya hivyo ?

  Kutanguliza maslahi ya chama mbele ya taifa ni kuleta vurugu na kuhatarisha amani, utulivu, umoja wa kitaifa na kuchochea utawala usiojali haki na usawa. Ninaamini haya ni mtendo yanayoweza kutafsiriwa kama ya kuvunja amani na hivyo kuwa kosa mbele ya sheria au mnasemaje ?
   
 2. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kutanguliza maslahi ya Chama badala a Taifa ni kosa kubwa, kauli y Kingunge ni ishara kuwa Watawala wetu wamechoka, hawana maono tena, wanachofanya ni kujaribu kuendelea kuwa madarakani na kuwalaghai WaTZ ili waendelee kuishi peponi wakati WaTZ wengi wakiishi Jehanamu. Ndo maana haishangazi kuona hali ya nchi inazidi kuwa tete kila siku, wananchi wamechoka na amani ya Watawala inatoweka na kujiamini hakupo tena.
   
 3. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Sina uhakika lakini kama mzee huyo amesema hivyo atakuwa amepotoka na labda anafikiri nchi hii ni mali ya CCM hivyo mtu kutanguliza maslahi ya chama ni kutanguliza maslahi ya nchi.Pia amesema hivyo kwa sababu hataki kuona CCM ikiondoka madarakani kama ambavyo Rais amesha sema kuwa WAPINZANI hawatakaa waongoze nchi hata wapige kelele vp.
  Mtizamo wangu ni kuwa,kutanguliza maslahi ya chama ni kuangalia kundi fulani katika jamii huku wengine wakipata taabu.Kwa maana nyingine kama wakazi wa eneo fulani hawata chagua chama kinachoongoza nchi basi huduma muhimu na za maendeleo watakuwa wanaona kwa jirani aliyechagua.
  Hii ni mbaya sana na inaleta makundi ktk jamii ambayo kama yakiachwa,yana weza kuasi na kujitangazia uhuru wao.Pia katika hatua za mwanzo machafuko yatatokea katika nchi husika.
  Haifai kutanguliza maslah ya chama kabla ya Nchi.SIJUI SHERIA ZINASEMAJE.
   
 4. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa mtazamo wangu, ni kwamba kutanguliza maslahi yoyote kabla ya maslahi ya nchi ni kosa kubwa, hasa ukiwa kiongozi wa nchi au serikali au taasisi ya umma. Ni kosa kubwa kwasababu unakuwa umetumia dhamana ya nchi kutekeleza maslahi ambayo yanaweza kuwa kinyume na maslahi ya nchi, na pia unakuwa umekiuka kiapo (kwa wale wanaokula kiapo) cha uaminifu na utii wa Katiba. Hakuna sehemu yoyote ndani ya Katiba ya nchi ambayo kwayo, viongozi wote wa siasa na serikali waliopewa dhamana wanapoapa kulinda maslahi ya taasisi zao au vyama vyao kabla ya maslahi ya nchi.

  Ili kujibu swali lako, niseme tu kwamba, naamini kuwa kukiuka kiapo ni kosa la jinai. Kutumia madaraka kinyume na kanuni zilizokupa madaraka hayo ni kosa (sijui kama ni la jinai). Kuteka maslahi ya nchi na kuyafanya kuwa ya chama, taasisi yoyote au ya mtu binafsi (bila kujali maslahi ya taifa) ni matumizi mabaya ya madaraka, uhujumu na kama kiongozi anaefanya hivyo ni wa kitaifa, basi inawezekana akawa amefanya uhaini (kosa kubwa kabisa la jinai).

  Nadhani wanasheria kama wapo humu wanaweza kutusaidia zaidi.
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Kama kuna kitu kimoja watanzania waliweza kujivunia huko nyuma ndani na nje ya mipaka yetu ni umoja wa kitaifa. Huu umoja ulituwezesha kuishi kwa amani kwa kutanguliza utaifa kabla ya mengine yote - na hii ndiyo inavyotakiwa iwe. Huu umoja ulituwezesha kupambana na maadui wetu kwa mshikamano na ujasiri bila kuyumba.

  Tulipoingia kwenye mfumo wa vyama vingi, sheria zilitungwa kuondoa ubaguzi kwa misingi ya itikadi kwenye sehemu za kazi ili kudumisha umoja miongoni mwa wafanyakazi. Lakini kwa makusudi tulishindwa kuondoa huu ubaguzi kwingineko ili kudumisha umoja wa wanawake wa Tanzania, umoja wa wazazi wa Tanzania au umoja wa vijana wa Tanzania ??

  Hebu fikiria kama tungekuwa na umoja wa wakristo wa CCM ama umoja wa waislamu wa CCM !! - nchi ingetawalika ?? Sasa inapotokea kuwa kwenye chombo chetu kikuu cha kutunga sheria, maslahi ya chama yanatangulizwa kuliko ya taifa, huu ni mwanzo wa kulisambaratisha taifa. Anayetoa au mwenye mawazo kama hayo hakika ni adui mkubwa wa taifa.

  Tumeshuhudia vikao vya kichama ndani ya bunge, vinavyozorotesha na kuzima juhudi zozote zile za dhati za kupambana na uovu, kutetea na kukumbatia waovu na kufumbia macho vitendo vinavyohatarisha usalama wa taifa. Tumeshuhudia Spika wa bunge akishiriki kwenye vikao vya kuweka msimamo wa pamoja kulinda maslahi ya chama na si taifa.

  Pamoja na yote hayo, sasa imetamkwa wazi wazi kuwa maslahi ya chama lazima yalindwe hata kama yanapingana na ya taifa. Hii kwa kiongozi aliyekula kiapo kulinda katiba ni zaidi ya kosa la jinai, ni uhaini. Kwamba Kingunge Ngombale alikuwa na jeuri ya kutamka hilo hadharani ni uvunjifu wa sheria na yafaa hatua kali ichukuliwe kwake ili iwe fundisho kwa wote wenye mtazamo kama huo.

  Kwamba hadi leo Kingunge Ngombale Mwiru yuko huru na si lupango, ni jambo linaloashiria hali ya hatari huko mbele ya safari na mapungufu makubwa katika sheria zetu. Siyo ajabu kuwa hivi sasa wahalifu wote wanakimbila uongozi ndani ya CCM kutafuta hifadhi maanake huko nje wanaweza wakachomwa moto kama vibaka na wananchi waliochoshwa na uovu wao.
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Unaweza kutanguliza maslahi ya Chama kisera ,na pia hili huwa linazungumzwa pembeni ya bunge kwenye vyumba vyao vya majadiliano ,kuzilinda sera kuzitangaza na kuzitetea ila panapovurugwa basi hapana kutetea Chama bali kunahitaji kuwajibika kwa maana Chama kitakuwa hakina faida kwa Taifa ikiwa sera zake zinababaishwa au ni za ubabaishaji ,mfano utawala bora ,utawala bora ni nguzo muhimu katika kutekeleza sera ,na utawala bora ni kuwajibika kwa Chama kuweza kuwawajibisha viongozi wake , bila ya kuwaonea huruma au kuwalinda maana utawala bora unaendana na uongozi wa sheria ,pale tunaposema sheria zifuatwe ,zichukue mkondo wake ,hapa Chama kitahesabika kimelinda sera kwa kuchukua hatua ya makusudi kumwadabisha mhusika pengine ambae ni serikali,waziri au mwengine yeyote yule ambae ni mdau katika chama iwapo tatizo litafikishwa bungeni ( kwa maana limefikishwa kwa wananchi) kujadiliwa kwa undani kwa maslahi ya Taifa ,inawezekana Chama kikawa na kamati ya ulindaji au utetezi kupata nafasi ya kutetea hoja zao lakini mengine yanakuwa hayalindiki hivyo ni kosa kwa Chama kuhusisha wabunge katika kutetea na wakifanya hivyo watakuwa wamekula viapo vya uongo ,ila kwa CCM uongo kwao ndio ukweli watatetea kwa kila hali mnazi kuuita Mpapai. Wakidai wamefahamika sivyo.
   
Loading...