Je kutahiriwa kusaidia kudhibiti Ukimwi?

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,169
1,576
serikali kupitia kwa Dk Husein Mwinyi' amesema wanaume 287,055 nchini wamepatiwa huduma ya tohara kwa kipindi cha miaka miwili. Amesema ni sehemu ya mkakati wa kupambana na maambukizi ya Ukimwi. Je ni kweli kuwa wanaume ambao hawajatahiriwa ni rahisi kupata maambukizi ya VVU na ukimwi? Naomba wadau wenye utaalam wa masuala ya afya na mahusiano wasaidie kutuelimisha kuhusu tohara na Ukimwi. Mimi ninavyofahamu kuwa unaambukizwa kwa kufanya ngono au uzinzi na usherati. My take: Inaingilianaje na kutahiri au kutotahiriwa?
 

Songoro

JF-Expert Member
May 27, 2009
4,124
1,012
Nenda kwenye darasa la Ngumbaro ujifunze huku ni kwa Great thinkers usiruke Stage! Hiyo elimiu ni ya Ngazi ya Ngumbaru au MEMKWA nyie ndo mnakuja na thread ya kuuliza kwa nini mwanaume akilala mkono lazima atie kwenyew BOXER yake!
 

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,169
1,576
Nenda kwenye darasa la Ngumbaro ujifunze huku ni kwa Great thinkers usiruke Stage! Hiyo elimiu ni ya Ngazi ya Ngumbaru au MEMKWA nyie ndo mnakuja na thread ya kuuliza kwa nini mwanaume akilala mkono lazima atie kwenyew BOXER yake!

mkuu kwetu kuna madara tu, lakini walimu wakufundisha elimu hii ya ukimwi hakuna, ndiyo maana ndugu zetu wamekufa wengi, bilashaka nawewe utakuwa na ndugu ambaye amekufa kwa ukimwi. Yawezeka hata wewe hujui afya yako. Na kama ulimsikiliza vizuri raisi wako JK, juzi alisema maambukizi ya ukimwi yanapungua, na huku upande mwingine' mkuu wa mkoa wa Mbeya anasema maambukizi yamepanda mpaka asilimia 11, hapo uoni kuwa elimu na takwimu zetu siyo sahihi? Kalagabao...
 

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,872
4,528
Veary simpo tohara inasaidia kupunguza uwezo wa kuambikizwa au kuambukiza ukimwi ingawa hakuna ushahidi thabiti. Maana wanaotetea dhana kuwa tohara inasaidia wana-base wanasema kuwa mtu aliyetahiriwa si rahisi kuchubuka ikilinganishwa na ambaye hajatahiriwa. Hata hivyo hawatoi maelezo kuhusiana na maji maji yaani shahawa na utoko wa mwanamke. So jibu ni so-so.
 

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,145
3,187
Jambo hili lina ukweli mkubwa sana kwa kuzingatia statistics za UKIMWI nchini. Kwa mfano ukiangalia katika jamii za watanzania ambao wanatahiri, kasi ya maambukizi ipo chini sana ukilinganisha na jamii za watu wasiotahiri. Mfano wa harakaharaka ni ule wa mikoa ilyowahi kuwa na kiwango cha juu sana cha maambukizi ya UKIMWI kama vile Iringa, Kagera na Mbeya sehemu kubwa ya wakazi wa huko hawana utamaduni wa kutahiri. Kiasi hiki cha maambukizi hakimaanishi kwamba hawa ni wapenda ngono zaidi kuwashinda wale wa mikoa ya Tanga, Dar es salaam, Mtwara, Arusha au Zanzibar.
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,931
287,582
Imetulia hii GT. Hata kule RSA kulikuwa na kampeni maalum kuhusiana na hili (sijui kama bado zinaendelea) baada ya tafiti kuonyesha kwamba tohara inapunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya huu ugonjwa.

Jambo hili lina ukweli mkubwa sana kwa kuzingatia statistics za UKIMWI nchini. Kwa mfano ukiangalia katika jamii za watanzania ambao wanatahiri, kasi ya maambukizi ipo chini sana ukilinganisha na jamii za watu wasiotahiri. Mfano wa harakaharaka ni ule wa mikoa ilyowahi kuwa na kiwango cha juu sana cha maambukizi ya UKIMWI kama vile Iringa, Kagera na Mbeya sehemu kubwa ya wakazi wa huko hawana utamaduni wa kutahiri. Kiasi hiki cha maambukizi hakimaanishi kwamba hawa ni wapenda ngono zaidi kuwashinda wale wa mikoa ya Tanga, Dar es salaam, Mtwara, Arusha au Zanzibar.
 

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,169
1,576
Asante sana wanaJF, walionyesha uwelewa wa suala hili la VVU na ukimwi hasa kwa upande wa elimu ya tohara. Mnajua watanzania wengi hapendi kusikia neno ukimwi.. Na mara nyingi nimekuwa nikuhudhuria misiba tofauti ya watu waliokufa kwa HIV, lakini bado hatuwekiwazi, mara nyingi tunasingizia magonjwa mengine mbali na HIV, watu wengi wanafanya ni siri. Kumbe elimu inatakiwa kutolewa kwa uwigo mpana zaidi kwa tukihusisha maumbile yetu na jinsia zetu: mfano TOHARA, n.k
 

Mzalendo Mkuu

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
735
191
Jambo hili lina ukweli mkubwa sana. Mnaweza kuona nchi za kiarabu zina kiwango cha chini kuliko cha nchi hizi zetu.

Sababu ya msingi ni kuwa ukiwa na govi uume wako unafichwa ndani kama uchi wa kike. Hiyo inafanya hicho kichwa kiwe laini na hivyo iwe rahisi kuchuba kama ilivyo kwa wanawake. Huko kuchubuka NDIKO KUNAFANYA IWE RAHISI KUAMBUKIZWA VVU.

Pili kwa kwa na govi unaweza kuubeba au kukaa na uchafu toka kwa mwanamke kwa muda mrefu. Aliyetahiriwa hutoka hapo akiwa msafi kabisa.

For fun: ukiwa hujatahiriwa unawezaje kuvaa condom? Naona kama inakuwa ngumu. Pia kwa asili huku pwani asiye tahirwa hutangazwa.

Kwa ujumla mikoa iliyoathirika sana na IKIMWI ya Kagera, Mbeya na Iringa haina mila za tohara kabisa hivyo wanakuwa kwenye mazingira hatarishi sana

Habari ndiyo hiyo. Nenda katahiriwe uwe huru.
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,863
30,307
Tohara ni kitendo cha kuondoa ngozi iliyojikunja inayozunguka kichwa cha uume. Ngozi hii huitwa
govi, hufunika kabisa kichwa cha uume lakini inaweza kuvutwa chini ya “mpini” (shafti).

Kufuatana na mila na desturi za waafrika, pamoja na dini fulani fulani kama vile Waislamu na
Wayahudi, watoto wanatahiriwa wakiwa na umri wa siku chache. Katika desturi nyingine za Afrika,

wavulana wanatahiriwa wanapofikia balehe, utaratibu huu unachukuliwa kama utaratibu wa mpito
kutoka utoto kwenda utu uzima.Zipo tamaduni nyingine Afrika ambazo mila haziruhusu kutahiri
kabisa.

Hakuna ubaya wowote wa kutahiri au kutokutahiriwa. Kutahiriwa ni utaratibu wa kidini au
kiutamaduni/kimila. Iwapo katika jamii yenu hawatahiri ni sawa sawa tu.

Je, kutahiri kunaleta tofauti zozote katika hisia ya kujamiiana? Ni vigumu sana kujua jambo
hili kwani kila mwanaume anayo namna yake ya kujisikia. Lililo la uhakika ni kwamba wote,
aliyetahiriwa na asiyetahiriwa wanaweza kufurahia ngono na wanaweza kuwafurahisha wapenzi
wao.

Wakati kutahiri ni utaratibu wa kidini au kimila/ kiutamaduni, watu wengine wanaamini kwamba
kuna faida za kiafya iwapo mwanaume ametahiriwa kwa sababu ni rahisi kusafisha uume wake.

Lakini zipo sababu zingine za kiafya zinazoweza kusababisha watu kutahiriwa. Wapo wavulana na
wanaume wengine ambao govi linakuwa limeshikana sana na kichwa cha uume kiasi cha kwamba

inawia vigumu kuivuta kwa chini. Hii inaweza kusababisha kuvimba kwa uume na maumivu
makali. Namna pekee ya kutatua tatizo hili ni kutahiri.Watu wengine wanafikiri kwamba kutahiri

kunasaidia kuzuia maambukizi ya VVU/UKIMWI na magonjwa mengine ya ngono. Ukweli ni
kwamba, hata kama umetahiriwa unaweza kupata maambukizi ya VVU/UKIMWI na magonjwa ya
ngono. Unashauriwa kufanya mapenzi salama wakati wote.

Mambo yote haya yana maana gani kwako? Kama utamaduni wako hauruhusu wavulana kutahiriwa,
Je, ungependa utahiriwe ili iwe rahisi kuuweka uume wako msafi? Jibu ni hapana unachotakiwa ni
kuwa msafi, kumbuka kusafisha kwa ungalifu chini ya govi. Kwa kawaida haya ndiyo unayotakiwa

kuyafanya. Hata hivyo wavulana ambao hawawezi kuviringisha govi na wale ambao husikia
maumivu uume unapodinda, wanashauriwa kumweleza mfanyakazi wa afya kwa ushauri zaidi.

Sasa hivi watu wengi wanatahiriwa katika vituo vya afya. Lakini sehemu nyingine wanatahiri
wataalamu wa kienyeji (mangariba) kama sehemu ya sherehe. Wakati wowote inapotokea hivyo,

inatakiwa vitumike vyombo visafi, vilivyochemshwa, ili kuua vijidudu kila baada ya kumtahiri
mtu mmoja. Ni hatari sana kutumia kisu kimoja kutahiria wavulana wengi kwa sababu kama

mmojawapo atakuwa na maambuziki ya VVU, kisu kinaweza kueneza maambukizi kwa wavulana
wengine.

Iwapo utatahiriwa kimila, hakikisha utaratibu wa kisasa unatumika ili kuzuia maambukizi ya VVU
na magonjwa mengine yanayotokana na damu. Usikubaliane kabisa na mila/desturi na utamaduni

utakaosababisha maambukizi ya VVU. Taratibu hizo zinaweza kubadilishwa ukawa salama.

Kwa mfano, watu wa Mbale, Uganda walichukua hatua zifuatazo ili kuhakikisha wanatahiri
kiusalama:
• Kila aliyetaka kutahiriwa alilazimishwa kuja na kisu chake.
• Lazima kisu kichemshwa kabla ya kutumika.
• Lazima Mangariba waoshe mikono yao kwa uangalifu kabla na baada ya kumtahiri kila mtu.


UKITAKA USIPATE UKIMWI TUACHE MAMBO YA ZINAA BORA KUWA NA MKE AU MPENZI MMOJA KULIKO KUWA NA WAPENZI WENGI.
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,863
30,307
Tohara (kutoka Kiarabu طهارة tahara - safi, tahiri) ni upasuaji mdogo wa kukata na kuondoa govi, yaani ngozi inayofunika kichwa cha uume.

Wakati mwingine ukeketaji huitwa "tohara ya mwanamke".


Inaweza kufanyika katika umri wowote na kwa sababu za kiutamaduni, za kidini au za kiganga. Mara nyingi desturi za kutahiri

zinachanganya sababu za kidini na kiutamaduni. Kwa mfano, Waislamu wa Misri huamini ya kwamba wanatahiri watoto wao kama amri

ya kidini lakini Wakristo Wakopti wa nchi hiyo hutahiri watoto vilevile. Ukweli ni kwamba tohara inajulikana ilikuwa desturi ya Wamisri tangu kale.


Tohara inafanyika hasa mara baada ya kuzaliwa kwa mtoto au wakati wa kubalehe.


Kufuatana na Shirika la Afya Duniani takriban 30% za wanaume wote duniani wametahiriwa, wengi wao wakiwa Waislamu.


Tohara ya Wanaume.Baada ya upasuaji.

Tohara ya kiutamaduni

Katika makabila mengi ya Afrika mvulana anatahiriwa ili kuingizwa katika kundi la wanaume wanaopaswa kuwajibika katika jamii.
Desturi hiyohiyo inaonekana pia kati ya watu wa Pasifiki k.mf. Wapolinesia wa Samoa, Tonga na Niue, vilevile kati ya Wamelanesia wa Fiji na Vanuatu.
Wakazi asilia wa Australia huwa pia na tohara ya wavulana.

Tohara kama amri ya kidiniUyahudi

Kwa Wayahudi tohara ni ishara ya agano lao na Mungu na inapaswa kufanyika siku ya nane baada ya mtoto wa kiume kuzaliwa ili kumwingiza mapema katika taifa la Mungu.
Kufuatana na habari za Biblia Ibrahimu alikuwa mtu wa kwanza aliyepokea amri ya kutahiriwa kama alama ya agano (Mwanzo 17).

Ukristo


Yesu mwenyewe alitahiriwa siku ya nane kama Wayahudi wote wa kiume. Tohara ya Yesu inakumbukwa kwa sikukuu maalumu katika makanisa mengi duniani hasaWaorthodoksi.
Agano Jipya inaonyesha jinsi gani suala la tohara lilikuwa motomoto mwanzoni mwa Kanisa, wakati Wakristo wengi walitoka katika Uyahudi.
Kufuatana na kitabu cha Matendo ya Mitume (15:23-29) Mtaguso wa Mitume uliofanyika Yerusalemu uliamua Wakristo kutoka mataifa wasilazimishwe kutahiriwa.
Hasa Mtume Paulo alisisitiza kwamba jambo hilo si muhimu tena, cha maana ni kuwa watu wapya kwa imani.
"Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya" (Gal 6:15).
"Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili" (Fil 3:3).
Hata hivyo Wakopti wa Misri na Ethiopia wameendelea kutahiri watoto wao.
[

Uislamu


Katika Uislamu tohara hufundishwa kama wajibu wa kidini kwa kila mwanaume.
Hakuna amri katika Kurani kuhusu tohara lakini inatazamiwa kama sunna ya mtume Muhamad. Kwa imani hiyo ni ishara ya mitume ya kwamba walizaliwa bila govi katika hali ya kutahiriwa tayari.
Utekelezaji wa tohara huwa ni tofauti kati ya nchi na nchi; mara nyingi mtoto mdogo hutahiriwa kwa umri kati ya miaka 5 hadi 10. Katika mazingira ya mjini wazazi wanawahi siku hizi kutahiri mapema.


Tohara kama hatua ya kiafyaMuda mrefu sana na nyembamba govi inaweza kuwa dalili za tohara matibabu​

Siku hizi hata mataifa yasiyokuwa na desturi hiyo yanaanza kuijali kwa sababu za usafi na afya.
Ni kwamba tohara inapunguza hatari ya mtoto kupatwa na fimosis.

Imethibitishwa kuwa inapunguza uwezekano wa kuambukizwa ukimwi pamoja na hatari ya magonjwa mengine kama kansa ya uume.

Katika nchi kadhaa sehemu kubwa ya watoto wa kiume wanatahiriwa mara baada ya kuzaliwa kwa sababu hizi za kiganga. Kwa mfano,

huko Marekani asilimia 56 za wavulana wote waliozaliwa mwaka 2005 walitahiriwa katika hospitali walikozaliwa. Hata hivyo katika nchi

hiyo kuna kampeni dhidi ya tohara kutokana na hoja ya kwamba mara nyingine upasuaji hauendi vizuri na kusababisha madhara ya kudumu kwa viungo vya uzazi.

WASIO KATA MAGOVI YAO TAFADHALI WAKATE MAGOVI YAO MIMI NIMESHAKATA GOVI LANGU TANGU NIZALIWE.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom