Je kusambaza nyaraka za serikali katika mitandao ya kijamii ni kosa?

Tareeq

JF-Expert Member
May 3, 2010
831
408
Wadau habari za Magharibi

Bila kufahamu kama ni kosa ama la , nimesambaza document ya serikali katika social media.

Hivi hatia hii ni nini hatima yake? Maana roho inanidunda hapa kama saa mbovu.
 
Jiandae watakurack watakudaka na rafiki ujue Lupango iko njiani!!!
 
Wadau habari za magharibi , bila kufahamu kama ni kosa ama lah , nimesambaza document ya serikali katika sosho midia hivi hatia hii ni nini hatima yake , maana roho inanidunda hapa kama saa mbovu
Raha ya moto ni kuchoma. Nyinyi vijana mkiambiwa kuwa moto unaunguza[hasa mkiwa vijiweni] mnachonga sana hivyo ni bora uungue na huo moto ili iwe funzo tosha
 
Maweeee, umeipata wapi? Umeipost ili iweje? Usingeipost ungekosa nini? pole huwezi kusalimika.
 
kasambaza waraka feki wa kudanganya kuwa walimu hawatoajiriwa huyo itakua.... na ukibainika udakwe tuu maana ulizua tafrani kubwa kwa walimu walio kitaa
 
Haya ndio madhara ya kutenda kwanza kisha unafikiri baadae badala ya kufanya kinyume chake
 
Back
Top Bottom