Elections 2010 Je kura za oktoba 31 tayari zimeshapigwa?

Kyachakiche

JF-Expert Member
Feb 16, 2009
983
207
Kuna taarifa kutoka chanzo cha kuaminika kuwa vifaa vya kupigia kura vikiwemo shahada na masanduku tayari vimewasili chini siku chache baada ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu. Linalosikitisha ni kuwa, makontena 9 yenye urefu wa futi 40 (9x40ft) na moja la futi 20 (1x20ft) yaliondolewa bandari na kampuni moja iliyo barabara ya Mkwepu karibu na benki ya wanawake(TWB) na kuelekezwa kupeleka vifaa hivyo Bohari kuu ya Taifa.

Magari yaliyobeba hiyo shehena yalipofika Chang'ombe karibu na VETA, yaliamuriwa kusimama na mawili kati ya hayo(1X40' na 1x20') kuambiwa yabadili njia kuelekea kwenye ghala moja lililo maeneo ya Keko ambalo inaaminika linamilikiwa na raia mmoja mwenye asili ya Kiasia. Magari mengine yakaendelea na safari kuelekea Bohari kuu. Madereva wa magari husika walipofika getini(Keko) waliamuriwa kushuka na watu wengine waliokuwa wameandaliwa waliyaingiza ndani kwa ajili kupakua mzigo huku madereva halisi wakiamriwa kuondoka mahali hapo hadi watakapojulishwa muda wa kuyarudia magari yao.

Siku mbili baadaye, kampuni hiyo pia ikatoa makontena mengine mawili 2X40ft kutoka bandarini yakiwa na shehena ya vifaa vya uchaguzi lakini ni kontena moja tu lilifika bohari kuu huku lingine likishia keko. Wakati yote haya yakifanyika macho na masikio ya tulio wengi tumeyaelekeza kwenye kampeni za wagombea bila kujua kuna mbinu chafu zinaendeleea kichini chini za kupenyeza ama masanduku bandia au kura ambazo tayari zimeshapigwa.

Inaelekea Tume ya Uchaguzi na CCM wameshakubaliana namna ya kuhujumu kura za wapinzani hasa maeneo yale ambayo wanakubalika. Haitashangaza kusikia kwa mfano Dr Slaa anakosa kura hata kule Karatu, Moshi, Hai, Kigoma Kaskazini nk. Tunaendelea kufuatilia hujuma hii kwa karibu na ikibidi tutakuja na majina ya kampuni husika. WOTE TUWENI MACHO.
 
Kushinda CCM 2010 ni kwa njia ya wizi tuu.
Cha msingi ni kukomaa vituoni alafu kila kituo majibu mnayaposti wataona haya kuyabadili.
ILA KAMA WANAKOMAA KUTOKA MADARAKANI WAKIWA WAMESHINDWA AM SURE WATATUPELEKA KAMA ILIVYOKUWA KENYA
 
Aisee hayayayayaaaaaaaaaa, wameanza zao. Unajua jana nilikuwa nikiangalia "TV ya taifa" TBC Dr. Mvungi anasema uchaguzi uliopita alipigia kura UDSM lakini wakati wa kuhesabu hata ya kwake haikuonekana. Wizi wa mchana. Safari hii tusikubali slogan ya kwamba ukishapiga kura nenda nyumbani, hakuna kwenda nyumbani kuwapa mwanya wa kufanya exchange kama wanavyofanyaga siku zote. Mkuu tuanikie majina ya makampuni tukachome hayo maghara moto!
 
Back
Top Bottom