Je, kupaki gari muda wa miezi 4 bila kuliwasha kuna tatizo?

2699s

Member
Aug 30, 2017
34
18
Naomba kuuliza, nimepaki gari aina ya Carina zaidi ya miezi 4 bila kuitumia. Je, kuna shida kuipaki muda wote huo?
 
Tatizo Lipo, Huo Muda Kwakuwa Hukuwa Unawasha Gari.
Battery Inaweza Kuwa Imeharibika Tayari!

Utaratibu Unataka Iwapo Gari Huitumii Basi Baada Ya Week Unaipasha Moto Hapo Hapo Mpaka Uone Gauge Ya Joto La Gari Inasoma Sawa Sawa
 
Mimi katika safari zangu huwa napaki gari miezi kadhaa nadhani kuna kipindi miezi 4 ilifika.

Ila ninachokifanya ni kutoa terminal ya + (positive) yenye lebel ya red nikiwa na maana battery isiishiwe nguvu na kurahisisha kuiconnect pindi nikirudi. Kiukweli baada ya muda wote huo nawashaga gari na linaitika!
 
Gari gani hiyo usijekuta unazungumzia PASSO?
 
Kupaki gari kwa muda mrefu kuna madhara mengi kama hutozingatia "masharti" yanayotakiwa ili uweze kupaki. Baadhi ya madhara ni:

1. Bodi la gari kushika kutu, wanyama na wadudu waharibifu (mf. Panya) kuingia ndani na kuharibu gari, tenki la mafuta kushika kutu na hata kutoboka

2. Battery kuishiwa nguvu na kushindwa kuwasha gari lako utapolihitaji

3. Mfumo wa breki "kuharibika" hasa brake pads kama ilikua dngaged

4. Tairi za gari kuharibika kwa kuishiwa upepo na kubeba uzito wa gari kwa sehemu moja hivyo kuleta "flat spots"

4. Matatizo kwenye engine kama vile kutu kwenye cyllinder heads na valves, gari kupoteza compression, oil kuharibika na tensions kwenye baadhi ya vifaa kama timing chain/ belt,

Inshort kuna matatizo mengi isipokuwa kuna masharti ukiyafuata gari yako itakuwa salama kabisa. B.T.W kwanini unapaki gari lako??
 
Write your reply...sioni haja ya kupaki gari kwa mda wote huo . automatically lazima kuwe na madhara
Hata hivyo hadi member mwenzetu anauliza hivyo atakuwa na sababu za msingi. These are few tips kama itamlazimu.

A. Ipaki gari yako lakini unashauriwa " kupiga misele" walau mara moja kila wiki mbili, kuanzia walau km 30 tena kwa spidi zaidi ya 50kph ili kuifanya engine iendelee kuwa hai. Kupiga less kila siku haisaidii kwasababu baadhi ya sehemu kama valves, transmission n.k haziwi engaged kikamilifu

B. Kama utakuwa mbali nz hilo haliwezekani fanya yafuatayo
1. Jaza mafuta "full tank" ili ulinde kutu zisiingie kwenye tenk
2. Inyanyue gari kwa " four jacks" kuzuia tairi kuharibika. Zisiguse chini. Usi engage hand brake bali iache gari free ili kulinda breki pads
3. Hifadhi gari lako gereji ya ndani ikiwezekana funika na cover lake ili kuzuia kutu
4. Mwaga oil na tia oil safi, fungua plugs zote kisha tia oil kiasi ili ikae juu ya pistons kuzuia kutu kisha funga hizo plugs, japo hii italeta moshi kiasi baafaye utakapowasha gari lako
5. Fungua + terminal ya battery yako ili kuizuia isipoteze nguvu. Paka grisi kwenye maungio ya battery kuzuia kutu

Kumbuka kuondoa uchafu ndani ya gari unaoweza kuwavutia panya na wadudu wengine

Hata hivyo, fanya haya pale tu unapolazimika kuipaki gari, maana uharibifu mwingine hauzuiliki. Wengine warahazua
 
Hata hivyo hadi member mwenzetu anauliza hivyo atakuwa na sababu za msingi. These are few tips kama itamlazimu

very clear.
 
Mie nasafiri kwa week moja, naacha gari Dar. Halafu sijazingatia yote hayo. Sijui nitaikuta mzima nitakaporudi
 
Back
Top Bottom