Je, kuondoka kwa Mattaka ATCL ni faraja kwa shirika?

Mkora

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
370
55
VYOMBO vingi vya habari leo vimechapisha habari ya kustaafu kwa David Mattaka, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania(ATCL). Kiongozi huyo wa shirika hilo, aliitisha mkutano wa waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam na kusema kuwa ameachia uongozi wa shirika hilo kutokana na kufika umri wa kustaafu, tofauti na kauli za baadhi ya watu wanaodai kuwa hakustaafu, bali amejiuzulu.

Tunampa pole mkurugenzi huyo kutokana na adha aliyoipata mara baada ya kustaafu, kwa kulazimika kuitisha mkutano wa wanahabari kwa lengo la kukanusha uvumi ulioenezwa na watu ambao huenda hawamtakii mema wanaosema kwamba hakuacha kazi hiyo kwa hiari, bali ameshinikizwa kujiuzulu. Tunadhani kuwa adha aliyopata kiongozi huyo ni kubwa pengine kutokana na ukweli kuwa ameliacha shirika la ATCL likiwa limekufa likisubiri kuzikwa rasmi na Serikali wakati wowote.

Tunasema tunampa pole kwa sababu kitendo cha kuitisha mkutano wa waandishi wa habari kutangaza kustaafu siyo kitendo cha kawaida, kwani wajibu wa kutangaza kustaafu kwa mfanyakazi ni wa mwajiri, siyo mwajiriwa. Hatari inayoweza kutokana na hatua hiyo, ni kutokea kwa tafsiri nyingi, ikiwa ni pamoja na kwamba mamlaka iliyomteua imemfukuza kazi au kumuamrisha ajiuzulu.

Ni bahati mbaya kuwa mkurugenzi huyo ameliacha shirika hilo katika hali hiyo ya kusikitisha. Pia ni bahati mbaya kuwa anaacha kuliongoza shirika hilo katika mazingira ya aina hiyo, ambayo yanaweza kutafsiriwa na wengi kuwa ni ya aibu. Tunasema hivyo kwa sababu maelezo aliyoyatoa katika mkutano wake na waandishi wa habari hayaonyeshi kutoka katika kinywa cha mtumishi aliyestaafu akiwa na mafanikio ya kujivunia, bali mstaafu mwenye hasira, lawama, majuto na visingizio lukuki visivyo na msingi wala mashiko.

Tukiangalia hali lililomo shirika hilo la ATCL hivi sasa, tunashindwa kumwelewa mkurugenzi huyo mstaafu alipowaambia wanahabari kuwa, katika utendaji wake katika shirika hilo, anajivunia kubadilisha nembo ya shirika hilo na kuliondoa shirika hilo chini ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini lililokuwa limeingia ubia. Anasema anamshukuru Mwenyezi Mungu kustaafu salama pasipo matatizo yoyote katika shirika hilo, ingawa anasikitika kuliacha shirika hilo likiwa halina ndege hata moja.

Nini lengo la kauli hiyo kama siyo kuamsha na kuchochea hasira za Watanzania? Hivi kweli kubadilisha nembo na kuliondoa shirika katika ubia pekee kunaweza kutafsiriwa kama jambo la kujivunia? Hata kama nembo ingebaki ileile na ATCL ingebaki katika ubia na shirika hilo la ndege la Afrika Kusini, lakini shirika hilo likatoa huduma kwa ufanisi, Watanzania wangeridhika na hali hiyo. Hata hivyo, tukumbuke kuwa alipokabidhiwa uongozi wa shirika hilo zaidi ya miaka minne iliyopita, shirika hilo lilikuwa na matatizo kadhaa, lakini hayakuwa sugu kiasi cha kushindikana iwapo uongozi ungekuwa na dira, weledi na mipango endelevu.

Kichekesho ni pale mkurugenzi huyo anapodai kuwa uongozi wake ulikuwa na nia ya kulifufua shirika hilo tangu alipoteuliwa na Rais Kikwete mwaka 2007, lakini ulishindwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake. Kwa mfano, anadai kuwa, kati ya mwaka 2007/2008, mafuta ya ndege yalipanda kwa asilimia 50, hivyo kuyafanya mashirika yote ya ndege yaliyokuwa hayapati ruzuku kutoka serikalini, kuanguka. Lakini hasemi kwanini mashirika ya ndege, likiwamo la Precisionair la Tanzania, hayakuanguka na sana sana yaliendelea kukua na kushamiri.

Sisi tunadhani kuwa kuondoka kwa mkurugenzi huyo katika shirika hilo, siyo tu ni faraja kwa Watanzania wote, bali pia ni habari njema katika muktadha wa ufanisi katika shirika hilo wakati Serikali ikitafakali namna ya kulijenga upya kutokana na majivu ya shirika hilo marehemu. Ni imani yetu kuwa Serikali imepata fundisho tosha na mara hii itaunda shirika jipya na kuweka uongozi wenye dira, weledi na uadilifu.
 
hando wa clauds alikuwa anamtetea sana asubuhi ya leo- hebu muulizeni atujuze.
 
Sincerely mie naona ni kubadili chupa ya mvinyo bila kubadli KINYWAJI chenyewe!! Huyu naye ni kama waliosema WANAJIVUA MAGAMBA wakati sumu ya mdudu ni ILEILE!!! Kuondoka kwake hakuna msaadas tena kwa shirika LILILOUWAWA TAYARI...MUNGU SAIDIA Tz
 
Moja kati ya watu walioshangaa huyu bwana kuteuliwa kuongoza ATCL, mie ni mmojawapo. Ninadhan alikuwa Mkurugenzi wa NSSF if am not mistaken. Katika kaipindi chake wastaafu walikuwa wakilalamika kuhusiana na mafao yao. Kipindi hicho ndo tulishuhudia uwekezaji usiokuwa na tija yoyote kwa wastaafu. Aliondolewa ndo mana hata katika mkutano huo alionekana kumshutumu Rais mstaafu. Sasa sijui JK alitaka kuonyesha kuwa BM alikosea kumuondoa huko alikokuwa. Naye ameumbuka kwa kuwapa shirika watu wasio na uchungu na mali za nchi hii.

Ni kweli tunahitaji watu makini kwenye kuendesha shirika hilo muhimu. Tunaongelea kuinua utalii hadi kufikia watalii milioni 1, sasa bila shirika imara la ndege tutafikia wapi. Tutakalia siasa tu kwa Rais kusema anataka kulifufua shirika hilo wakati bajeti ya Wizara ya Uchukuzi haitengi fedha kwa ajili ya lengo hilo. TIME WILL TELL
 
alikuwa ppf, kwakweli kwa atcl hsns cha kujivunia, no legacy at all
 
Gerard wa clouds amenishangaza sana leo,amemsifia sana mataka cjui katika basis zipi i geti confused.Nakubaliana na wale wanaosema clouds ni kagenge fulani kanakotumiwa na wenye pesa kuexpress interest zao.Utakuta wanasifia kitu amabcho the rest aof tanzanians know the truth...
 
hivi kampuni hiyo inafanya kazi gani? hawana hata basi achilia mbali ndege? know how hamna, wameshindwa hata videge vya bei ya gari la waziri? vingetoa huduma japo kwa babu, tanzania inachekesha
 
Gerard wa clouds amenishangaza sana leo,amemsifia sana mataka cjui katika basis zipi i geti confused.Nakubaliana na wale wanaosema clouds ni kagenge fulani kanakotumiwa na wenye pesa kuexpress interest zao.Utakuta wanasifia kitu amabcho the rest aof tanzanians know the truth...

Hivi mkuu bado unaendelea kusikiliza redio hiyo tune hata za dini upate neno la Mungu kuliko kuwasikiliza hao unaumiza kichwa bure
 
Mkuu!! Common sense is not common at all!!!! Mwisho ukifika kuondoka ni kuondoka tu!!!!:A S 103:Wapo wengine nao wanafuata!!!!!!

DECREASING RATE AT INCREASING RATE !!!!!!:A S 103:
 
Back
Top Bottom