Je, kunahitajika affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuwa Rais wa JMT? | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, kunahitajika affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuwa Rais wa JMT?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Sep 20, 2014.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2014
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,661
  Likes Received: 23,902
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Tanzania ni nchi ya Jamhuri ya Muungano, yenye watu kutoka iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, na kuunda nchi moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao raia wake wa pande zote mbili, wako sawa na wana hadhi sawa na uhuru kamili wa kila kitu ikiwemo kugombea na kushika madaraka ya nafasi juu kabisa ya uongozi kwenye JMT, hii ni nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Baada ya Nyerere kutoka Bara, alifuatiwa na Mwinyi kutoka Zanzibar.
  Wakati wa kipindi cha Mwinyi, makamo wa rais ndiye pia alikuwa Waziri Mkuu wa JMT na Mwinyi alihudumiwa na ma Makamu watatu, Joseph Sinde Warioba, John Samwel Malecela na Cleopa David Msuya, na kipindi hiki cha Mwinyi, 1992, ndipo Tanzania tukaingia kwenye mfumo wa vyama vingi, na CCM kwa kuogopa, wa urais wa Zanzibar kushikwa na mtu wa chama kingine, wakati ndio set up ya muungano kuwa rais akitoka Bara, makamo lazima atoke Zanzibar, iwapo Zanzibar itashikwa na chama kingine, itakuwaje?, ndipo wakaamua kubadili katiba na kumfanya rais wa Zanzibar ni nothing ndani ya set up ya muungano!, na huu ndio ukawa mwisho rasmi wa mtu kutoka Zanzibar kuwa rais wa JMT!.


  Baada ya Mwinyi, akaja Mkapa kutoka Bara, ilibidi Mkapa kufuatiwa na mtu kutoka Zanzibar, lakini yalifanyika mambo ( refer uzi huu JK, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza ..

  Hivi ndivyo zamu ya Zanzibar ilivyopokwa!) hivyo akafuatiwa na Jakaya Kikwete pia kutoka Bara, na sasa tukiwa tunaelekea 2015, sijabahatika kusikia sikia majina yoyote ya possibility ya Mzanzibari yakitajwa tajwa au any possibility ya mgombea yoyote wa nafasi ya urais wa JMT kutoka tena Zanzibar!.


  Naomba kukiri, ninaandika uzi huu kufuatia inspiration niliyoipata toka kwa mwana jf huyu


  Jee inawezekana sababu halali kwa nini Mzanzibari hawezi tena kuwa ni rais wa JMT?.

  Naomba tuanze kwa kuweka facts mezani!.
  1. Eneo lote la Zanzibar lilikuwa ni sehemu ya Tanganyika, hivyo Zanzibar ni sehemu halali ya Tanganyika!.
  2. Kufuatia Zanzibar kuwa ni sehemu ya Tanganyika, wakaazi wake wa asili ni Wamatumbi kutoka Tanganyika!.
  3. Kuna miaka fulani, wavamizi fulani wa Kiarabu kutoka nchi ya Oman, waliivamia Zanzibar, wakajifanya ni nchi yao na kuuhamishia ufalme wao kutoka Oman na kuja Zanzibar, wakazaliana, sasa wanajidhania hapo ni kwao, kiukweli hapo kwao kwa kuzaliwa tuu, lakini kiasili, sio kwao, bali mahali tuu walipozaliwa na kukulia!. Ukizaliwa India, ukakulia India, hakukufanyi uwe Mhindi, wewe utabaki ni Mmatumbi tuu!.
  4. Wavamizi hawa wakaanzisha biashara haramu ya Utumwa, ambapo Watumwa waliokuwa hawana soko, waliachwa Zanzibar. Biashara ya utumwa ulipopigwa marufuku, wengi wa watumwa hawa, walibaki Zanzibar kama watu huru na wao pia kujihesabu ni Wazanzibari!.
  5. December 1963, wavamizi hawa wakapewa uhuru wa bandia na Waingereza!, Wamatumbi wenye nchi yao, hawakukubali, mwezi mmoja baadae, ile Januari 12, 1964, wakiongozwa na Mmatumbi John Okello kutoka Uganda, walifanya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kumfurusha "mvamizi yule!" na kujitwalia Uhuru ambapo mtu mwenye asili ya Malawi, Abedi Amani Karume alitangazwa ndie Rais wa Zanzibar na M/Baraza la Mapinduzi.
  6. Aprili 26, 1964, Rais Nyerere na Karume waliziunganisha nchi hizi mbili, na kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais wa Tanzania siku zote lazima atakuwa ni Mtanzania kutoka upande wowote wa Muungano.
  7. Nyerere alitoka Bara, Mwinyi alitoka Zanzibar, japo alizaliwa bara pale Mkuranga, na ndio maana anaishi Bara! hadi sasa!. Mkapa alitoka Bara japo inasemekana lizaliwa "Nchumbiji!" JK pia ni kutoka Bara, anayefuatia pia atatoka Bara probably "Ule Mwamba wa Kaskazi", na atafuatiwa na Bara, na Bara, na Bara tena!, hakuna wakati mwingine wowote ambao Rais wa JMT, atatoka nje ya Bara!.
  8. Kufuatia Zanzibar kukosa tafsiri rasmi ya Mzanzibari ni nani, Mzanzibari wa asili ni Mmatumbi kutoka Tanganyika, lakini sasa "wale wavamizi!", nao wanajiita Wanzanzibar!, vizalia vya masalia ya Watumwa, nao kwa vile wamezaliwa Zanzibar, nao ni Wazanzibar, hivyo its very risk kukubali mtu kutoka Zanzibar kuwa rais wa JMT, wao mwisho wao ni kututolea Makamo wa Rais tuu.
  9. Be ware, wale ambao sio Wanzanzibari wa asili, na haswa vizalia vya "wavamizi" ndio wenye kelele sana!, tuwe waangalifu sana na kila kelele kwa kumuangalia vuzuri kwa jicho chunguzi, kila anayeupigia kelele zamu ya Uzanzibari kwenye urais wa JMT, kwa kujiuliza kama jee ni Mzanzibari kweli au ni wale "wavamizi!.
  10. Tanzania ni kwa Watanzania asili itatawaliwa na Watanzania asili, na sio "wavamizi", "walowezi", au watu wa kuja!.
  Natanguliza samahani msinione mbaguzi, hizi zinaweza kuwa ndizo sababu halisi zinazosimama kama facts zinazopelekea Mzanzibari, asipate tena nafasi ya kuwa rais wa JMT!, Hamdhani kwamba sasa umefika wakati, kunahitajika some specific measures kama some kind of affirmative action, kuhakikisha, rais wa JMT pia apatikane kutoka upande wa pili wa muungano?, yaani kwa wapenda haki, hatuwezi kuacha ,rais wa JMT , andelee tuu kuchaguliwa by chance, kutoka upande wowote wa JMT wakati kuna kila dalili za kuonyesha kamwe rais wa JMT, hawezi tena kutoka Zanzibar by chance, hivyo marais wote wa Tanzania ya vyama vingi ni kutoka upande mmoja tuu wa Muungano huku bara!. Is this fair kwa wenzetu Wazanzibari ambao ni raia wenye haki sawa ndani ya JMT?!. Hamdhani huu ni wakati muafaka tuwe na affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuwa rais wa JMT?.

  Hii sio mara yangu ya kwanza kuizungungumzia nafasi ya Zanzibar kwenye urais wa JMT, pia niliizungumza hapa!.

  Japo hakuna kupokezana: Kiukweli, kihaki, kihalali na ki Kudumisha Muungano, 2015 Urais wa JMT ni Zamu ya Zanzibar!.

  Wawakilishi wa Zanzibar mlioko Dodoma, lipiganieni hili nalo liingizwe rasmi kwenye Katiba kuwa urais wa JMT, wa kupokezana!.

  Asante.

  Paskali
   
 2. b

  blessings JF-Expert Member

  #41
  Sep 10, 2017
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 5,482
  Likes Received: 3,170
  Trophy Points: 280
  Pasco kama ujuavyo Zenjibar walipigilia msumari wa mwisho kwenyw jeneza lao kuhusu Uraisi wa Muungano kwa Katiba yao ya 2010. Hiyo 2055 tunapiga soga tu lakin ni kama haipo. Bye ZNZ
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #42
  Sep 10, 2017
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 14,362
  Likes Received: 3,304
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo wangesikiliza muda huu ingekua....
   
 4. chabuso

  chabuso JF-Expert Member

  #43
  Sep 10, 2017
  Joined: Feb 18, 2013
  Messages: 3,508
  Likes Received: 2,264
  Trophy Points: 280
  Paskali,Zanzibar ni ya wazanzibari,kuna wazanzibari wenye asili ya Kiafrika,kuna wazanzibari wenye asili ya kihindi,kuna wazanzibari wenye asili ya kichina,kuna wazanzibari wenye asili ya kiarabu,kuna wazanzibari wenye asili ya kishirazi(Iran) na kadhalika

  Kuna Nchi moja inaitwa Marekani(USA),Watu wa mataifa ya Ulaya walitoka wakahamia Marekani miaka mingi iliyopita,uhamiaji huo umefanya raia wa Marekani wachanganye sana,kuna wamarekani wenye asili ya kingereza,kuna wamerikani wenye asili ya kihindi,kuna wenye asili ya kijarumani na kadhalika,machangayiko wa damu umeza utamaduni uitwao umarekani,lakini ukiangalia utakuta hao watu wote ni wahamiaji kutoka ulaya,wengi wao akiwa waingereza na wairish...lakini wahamiaji wa marekali waliwapindua waingereza na kudai uhuru wao..

  Mfano wa nchi ya Marekani hauna tafauti sana na nchi ya Zanzibar,propaganda nyingi za watangayika wanapenda kusema kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanganyika kwasababu watu wengi wa Zanziabar ni makabila kutoka Tanganyika,hiyo ni kweli,baadhi ya wenyeji wa Zanzibar ni watu wa makabila ya Pwani ya Afrika Mashariki,kuna Wadigo,Wasegeju,Wazaramo;wandegereko,Wazigua,wangazija na kadhalika..

  Makabila hao walipochanganyika na makabila ya mashariki ya mbali wahindi,warabu,wachina,wairan ndio hapo Kabila la Kishwahili lilipozaliwa kama vile kabila la Kimarekani lilipozaliwa.

  Kabila hili la kiswahili ndilo lililoamuondoa Sultani wa Zanzibar lakini kumbuka kuwa "plan",ilikuwa sio kuwa wamuondoe kabisa kabisa "Plan" ilikuwa wamuondoe katika siasa yeye sultan aweko Zanzibar kama "symbol" tu,yaani iwe kama Malkia wa Uingereza na United Kingdom,Malkia wa Denmark,Au Malkia wa Holland,huo ndio ilikuwa mpango wa mapinduzi ya zanzibar...

  Kumbuka historia inasema wakati wenyeji wa Zanzibar walipomuomba Sultan wa Oman aje awasaidie wamuondoe Mreno,Zanzibar ilkuwa na watu takriban arubaini elfu (40,000),wakati Nyerere na Karume wanaziunganisha Zanzibar na Tanganyika, Zanzibar ilkuwa na watu laki tatu(300,000) wengi wao wamechanganya Damu.

  CCM na baadhi ya watanganyika wamekuwa wabaguzi wanaleta propaganda kuwa kila Mzanzibari aliechanganya damu ni mwarabu,hapana baba, waliochanganya damu ndio wazanzibari wenyewe kutokana na histoia ya Zanzibar,Hao waliokuweko Dodoma inaweza kuwa ni Wazanzibari lakini ni njaa inayowafanya wawasaliti ndugu zao.huo ndio ukweli wenyewe usioepukia

  Tafakari
   
 5. N

  Ngoshanyi JF-Expert Member

  #44
  Sep 10, 2017
  Joined: Jun 14, 2013
  Messages: 2,417
  Likes Received: 273
  Trophy Points: 180
  Wakati ulipokuwa unampigia debe Lowassa hili swali/wazo lingekuwa zuri sana tu. Lakini sasa hivi ni blabla tu. Tunaitaka Tanganyika. Washauri hao jamaa zako wa Ukawa wamtoe Mzenj agombe halafu uwone watu wasiojulikana watafanya nini. Huko nafasi yakugombea M,kiti na Rais ni hatari kuliko bomu la nuklia
   
 6. b

  blessings JF-Expert Member

  #45
  Sep 13, 2017
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 5,482
  Likes Received: 3,170
  Trophy Points: 280
  Wachaga wenyewe washapigwa pini kwenye zile positions tatu za juu. Itakuwa mvaa kobazi toka Zenjibari? Pole yao, walijiloga wenyewe na katiba yao ya 2010
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...