Je, kunahitajika affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuwa Rais wa JMT? | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, kunahitajika affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuwa Rais wa JMT?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Sep 20, 2014.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2014
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,661
  Likes Received: 23,902
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Tanzania ni nchi ya Jamhuri ya Muungano, yenye watu kutoka iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, na kuunda nchi moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao raia wake wa pande zote mbili, wako sawa na wana hadhi sawa na uhuru kamili wa kila kitu ikiwemo kugombea na kushika madaraka ya nafasi juu kabisa ya uongozi kwenye JMT, hii ni nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Baada ya Nyerere kutoka Bara, alifuatiwa na Mwinyi kutoka Zanzibar.
  Wakati wa kipindi cha Mwinyi, makamo wa rais ndiye pia alikuwa Waziri Mkuu wa JMT na Mwinyi alihudumiwa na ma Makamu watatu, Joseph Sinde Warioba, John Samwel Malecela na Cleopa David Msuya, na kipindi hiki cha Mwinyi, 1992, ndipo Tanzania tukaingia kwenye mfumo wa vyama vingi, na CCM kwa kuogopa, wa urais wa Zanzibar kushikwa na mtu wa chama kingine, wakati ndio set up ya muungano kuwa rais akitoka Bara, makamo lazima atoke Zanzibar, iwapo Zanzibar itashikwa na chama kingine, itakuwaje?, ndipo wakaamua kubadili katiba na kumfanya rais wa Zanzibar ni nothing ndani ya set up ya muungano!, na huu ndio ukawa mwisho rasmi wa mtu kutoka Zanzibar kuwa rais wa JMT!.


  Baada ya Mwinyi, akaja Mkapa kutoka Bara, ilibidi Mkapa kufuatiwa na mtu kutoka Zanzibar, lakini yalifanyika mambo ( refer uzi huu JK, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza ..

  Hivi ndivyo zamu ya Zanzibar ilivyopokwa!) hivyo akafuatiwa na Jakaya Kikwete pia kutoka Bara, na sasa tukiwa tunaelekea 2015, sijabahatika kusikia sikia majina yoyote ya possibility ya Mzanzibari yakitajwa tajwa au any possibility ya mgombea yoyote wa nafasi ya urais wa JMT kutoka tena Zanzibar!.


  Naomba kukiri, ninaandika uzi huu kufuatia inspiration niliyoipata toka kwa mwana jf huyu


  Jee inawezekana sababu halali kwa nini Mzanzibari hawezi tena kuwa ni rais wa JMT?.

  Naomba tuanze kwa kuweka facts mezani!.
  1. Eneo lote la Zanzibar lilikuwa ni sehemu ya Tanganyika, hivyo Zanzibar ni sehemu halali ya Tanganyika!.
  2. Kufuatia Zanzibar kuwa ni sehemu ya Tanganyika, wakaazi wake wa asili ni Wamatumbi kutoka Tanganyika!.
  3. Kuna miaka fulani, wavamizi fulani wa Kiarabu kutoka nchi ya Oman, waliivamia Zanzibar, wakajifanya ni nchi yao na kuuhamishia ufalme wao kutoka Oman na kuja Zanzibar, wakazaliana, sasa wanajidhania hapo ni kwao, kiukweli hapo kwao kwa kuzaliwa tuu, lakini kiasili, sio kwao, bali mahali tuu walipozaliwa na kukulia!. Ukizaliwa India, ukakulia India, hakukufanyi uwe Mhindi, wewe utabaki ni Mmatumbi tuu!.
  4. Wavamizi hawa wakaanzisha biashara haramu ya Utumwa, ambapo Watumwa waliokuwa hawana soko, waliachwa Zanzibar. Biashara ya utumwa ulipopigwa marufuku, wengi wa watumwa hawa, walibaki Zanzibar kama watu huru na wao pia kujihesabu ni Wazanzibari!.
  5. December 1963, wavamizi hawa wakapewa uhuru wa bandia na Waingereza!, Wamatumbi wenye nchi yao, hawakukubali, mwezi mmoja baadae, ile Januari 12, 1964, wakiongozwa na Mmatumbi John Okello kutoka Uganda, walifanya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kumfurusha "mvamizi yule!" na kujitwalia Uhuru ambapo mtu mwenye asili ya Malawi, Abedi Amani Karume alitangazwa ndie Rais wa Zanzibar na M/Baraza la Mapinduzi.
  6. Aprili 26, 1964, Rais Nyerere na Karume waliziunganisha nchi hizi mbili, na kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais wa Tanzania siku zote lazima atakuwa ni Mtanzania kutoka upande wowote wa Muungano.
  7. Nyerere alitoka Bara, Mwinyi alitoka Zanzibar, japo alizaliwa bara pale Mkuranga, na ndio maana anaishi Bara! hadi sasa!. Mkapa alitoka Bara japo inasemekana lizaliwa "Nchumbiji!" JK pia ni kutoka Bara, anayefuatia pia atatoka Bara probably "Ule Mwamba wa Kaskazi", na atafuatiwa na Bara, na Bara, na Bara tena!, hakuna wakati mwingine wowote ambao Rais wa JMT, atatoka nje ya Bara!.
  8. Kufuatia Zanzibar kukosa tafsiri rasmi ya Mzanzibari ni nani, Mzanzibari wa asili ni Mmatumbi kutoka Tanganyika, lakini sasa "wale wavamizi!", nao wanajiita Wanzanzibar!, vizalia vya masalia ya Watumwa, nao kwa vile wamezaliwa Zanzibar, nao ni Wazanzibar, hivyo its very risk kukubali mtu kutoka Zanzibar kuwa rais wa JMT, wao mwisho wao ni kututolea Makamo wa Rais tuu.
  9. Be ware, wale ambao sio Wanzanzibari wa asili, na haswa vizalia vya "wavamizi" ndio wenye kelele sana!, tuwe waangalifu sana na kila kelele kwa kumuangalia vuzuri kwa jicho chunguzi, kila anayeupigia kelele zamu ya Uzanzibari kwenye urais wa JMT, kwa kujiuliza kama jee ni Mzanzibari kweli au ni wale "wavamizi!.
  10. Tanzania ni kwa Watanzania asili itatawaliwa na Watanzania asili, na sio "wavamizi", "walowezi", au watu wa kuja!.
  Natanguliza samahani msinione mbaguzi, hizi zinaweza kuwa ndizo sababu halisi zinazosimama kama facts zinazopelekea Mzanzibari, asipate tena nafasi ya kuwa rais wa JMT!, Hamdhani kwamba sasa umefika wakati, kunahitajika some specific measures kama some kind of affirmative action, kuhakikisha, rais wa JMT pia apatikane kutoka upande wa pili wa muungano?, yaani kwa wapenda haki, hatuwezi kuacha ,rais wa JMT , andelee tuu kuchaguliwa by chance, kutoka upande wowote wa JMT wakati kuna kila dalili za kuonyesha kamwe rais wa JMT, hawezi tena kutoka Zanzibar by chance, hivyo marais wote wa Tanzania ya vyama vingi ni kutoka upande mmoja tuu wa Muungano huku bara!. Is this fair kwa wenzetu Wazanzibari ambao ni raia wenye haki sawa ndani ya JMT?!. Hamdhani huu ni wakati muafaka tuwe na affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuwa rais wa JMT?.

  Hii sio mara yangu ya kwanza kuizungungumzia nafasi ya Zanzibar kwenye urais wa JMT, pia niliizungumza hapa!.

  Japo hakuna kupokezana: Kiukweli, kihaki, kihalali na ki Kudumisha Muungano, 2015 Urais wa JMT ni Zamu ya Zanzibar!.

  Wawakilishi wa Zanzibar mlioko Dodoma, lipiganieni hili nalo liingizwe rasmi kwenye Katiba kuwa urais wa JMT, wa kupokezana!.

  Asante.

  Paskali
   
 2. iparamasa

  iparamasa JF-Expert Member

  #21
  Sep 22, 2014
  Joined: Nov 14, 2013
  Messages: 13,462
  Likes Received: 14,149
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono Pasco, ili mzanzibari awe rais wa tanganyika inahitajika affirmative action,wanasiasa wengi wenye nguvu zanzibar hawako interested na mainland politics, nilimsikia maalim seif wakati anahokiwa na ivona kamuntu alikiri kwamba hayuko interested kuwa rais wa muungano, nafikiri ndio maana hata investment ya CUF bara imekuwa ndogo, pia hata gharib bilal,lengo lake lilikuwa urais wa zanzibar na alikuwa kakaribia kuukamata kama sio zengwe la kumuweka dr shein, pia bilal inaonekana siasa za bara hazimfurahishi wala kumvutia,tunakumbuka kipindi kila alikuwa ameshaanza kutoa kauli mbalimbali kuhusu mwelekeo wake kisiasa lakini sasa yu kimya, na itahitaji nguvu ya ziada kumpitisha mzanzibari katikati ya miale ya moto mkali wa watanganyika walioonyesha nia na pia ccm zanzibar lazima ijipange sana,isitarajie ccm bara itawabeba siku zote
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #22
  Sep 22, 2014
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,161
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0

  Ndoto za mchana kweupeeeeee!!!

  Eti Znz ilikuwa sehemu ya Tanganika ...

  Pole sana
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #23
  Sep 22, 2014
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,661
  Likes Received: 23,902
  Trophy Points: 280
  Kubali, kataa, ukweli ndio huo!, ukiwaondoa "wavamizi" waliotoka walikotoka, wakajifanya pale ni kwao!, then, wale waliowakuta walipoleta uvamizi wao ni Watanganyika, na ndio maana sasa tumewaoa kama wake zetu tuu, tunawalisha, tunawavisha na pesa za matumizi juu, wao kazi yao, kula bure, kulala bure!.

  Rudi kwenye Jiogrofia ya uumbaji, angalia visiwa vya Indian Ocean, tazama visiwa vya Indian Ocean vilitoka wapi?!.

  Pasco
   
 5. s.crony

  s.crony JF-Expert Member

  #24
  Sep 22, 2014
  Joined: Jul 25, 2012
  Messages: 1,288
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mkuu Pasco....Hawa tumesha wajaribu na kuthibitisha hawauwezi Urais....ona mkoa wao tu Zanzibar unawashinda mpaka ulinzi na usalama wao usimamiwe na bara.....na kwa sasa tunapoelekea kurudisha Tanganyika yetu ndo wasahau kabisa kuwa kuna mzenjibara atakuja kuwa rais wa JMT.......N.B;rejea point no:7....huo mwamba wako wa kaskazi hauwezi kuwa Rais wa JMT.....namba 10 nakupa hongera kwa kulitambua hilo....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. chabuso

  chabuso JF-Expert Member

  #25
  Sep 22, 2014
  Joined: Feb 18, 2013
  Messages: 3,508
  Likes Received: 2,264
  Trophy Points: 280
  mmm another porojo,,,,,Mkuu Pasco ukimchukuwa raisi wa mwanzo mwanamapinduzi wa zanzibar sheikh Abeid Aman Karume na kufananisha na Sultan wa mwisho kutawala Zanziba Baraghash bin said utaona kuwa Sultan ana haki ya kuwa mzanzibari kuliko Karume

  Usultan umeanzishwa hapo Zanzibar kuanzia mwaka 19 October 1856 ukifanya hesabu za haraka haraka usltani una kama karne 3 au zaidi,Karume raisi wa mwanzo wa zanziar hakuzaliwa Zanzibar wala hana jamaa Zanzibar sasa nani ana haki ya kuwa mtawala wa zanzibar,Sultan kazaliwa zanzibar,Karume alikuja zanzibar akiwa na miaka 5

  Hao wavamizi historia inasema kuwa,warabu waliitwa na wenyeji wa zanzibar ili waje kuwasaidia kuwadhibiti wareno...Kwa ufupi hayo uliyoandika hapa ni ubaguzi ambao zanzibar umeshaondokana nao tangu 1856.

  Pale wenyeji wa zanzibar walipokubali kuwa Sultan wa Oman ndie awe sultan wao walikuwa wameshaondokana na hisia na dhana za kibaguzi waliona watu wote sawa,kama mtu ana hisia na uzalendo wa zanzbar na kuipenda zanzibar basi mtu huyo anaweza kuwa mtawala wa zanzibar..hali hiyo inapatikana kwa mifano miwili ya Karume na Sultan wote ni wageni lakini waliweza kuwa watawala wa zanzibar

  Ubaguzi unaletwa na watawala wanaotawala Zanzibar tangu walipopindua, wamesahau kuwa Zanzbar ni kisiwa, visiwa vyote duniani vina utamaduni mmoja wa kuwa na watu mchanganyiko,katika kisiwa huwezi kubagua kuwa watu waina fulani wana haki kuliko watu wa aina fulani,hayo ndio yanayoonekana katika utawala wa sasa hivi....waliopindua walipundua kwa njia za kibaguzi na wanasidi kubagua lakini hiyo haitawafikisha wanakotaka kwenda watu wameshachanganyika mpaka hajulikani nani ni nani

  Wazanzibari hawataki uraisi wa JMT wanataka nchi yao,wanataka wajiamulie mambo yao wenyewe
  Pasco,acha kuleta mada za kibaguzi kama hizi,you are more than that :;tafakari
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #26
  Sep 23, 2014
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,661
  Likes Received: 23,902
  Trophy Points: 280
  Mkuu Chabuso, kwanza asante kwa hii, nimeguswa!, najitafakari!, ila pia hii iisue ya ubaguzi wa kuwabagua Wanzanzibari kwenye urais wa muungano, haiwezi kuisha kwa kuikalia kimya!, jee kipi ni afadhali, bora tukae kimya Zanzibar iendelee kubaguliwa au ni afadhali kuufichua ubaguzi, ili uwe adressed affirmatively hata kama ufichuzi wenyewe nao ni ubaguzi?.

  Tulipoungana, makubaliano ya Nyerere na Karume ilikuwa "wewe rais, mimi makamo!", lakini kufuatia uwezekano wa "mvamizi" kuwa rais wa Zanzibar, hivyo kumpelekea kuwa Makamo wa rais wa JMT na if anything happen to rais wa JMT, then automatically, Makamo anakuwa rais, hivyo URT nayo kutawaliwa na "mvamizi", yale mabadiliko ya katiba ya 1992, yalimuengua rais wa Zanzibar kwenye structure ya muungano, he is nobody now!, just to rule out the posibility ya "mvamizi" kuwa rais wa JMT!, huo nao sio ubaguzi?, umepenyezwa mpaka kwenye katiba!, huko hamuusemi!, ila Pasco kausema ndio tunanyoosheana vidole vya ubaguzi?!.

  Wanzanzibari wepi hao unaowazungumzia wanataka nchi yao?, wakati kiukweli wanaojidai kuitaka nchi yao ni "vizalia" vya "wavamizi", Wanzanzibari wenyewe halisi, tuko nao hapa Dodoma, wakihuidhuria BMK ambaolo litaibuka na katiba ya serikali mbili kuelekea serikali moja!.

  Pasco
   
 8. B

  BULOLE BUKOMBE JF-Expert Member

  #27
  Oct 5, 2014
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #28
  Oct 5, 2014
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,661
  Likes Received: 23,902
  Trophy Points: 280
  Mkuu BULOLE BUKOMBE
  Asante, nimekupata.
  P.
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #29
  Apr 11, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,661
  Likes Received: 23,902
  Trophy Points: 280
  2015 ndio hii, bado sijaona dalili zozote za any affirmative action kusaidia rais wa JMT atoke Zanzibar!. Hivyo game la October,panga pangua, ni yule yule!, watu wale wale na chama kile kile!.

  Pasco
   
 11. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #30
  Apr 11, 2015
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,394
  Likes Received: 1,757
  Trophy Points: 280
  Nyerere alitoka Bara, Mwinyi alitoka Zanzibar, japo alizaliwa bara pale Mkuranga, na ndio maana anaishi Bara! hadi sasa!. Mkapa alitoka Bara japo alizaliwa "Nchumbiji!" JK pia ni kutoka Bara, anayefuatia pia atatoka Bara "Ule Mwamba wa Kaskazi", na atafuatiwa na Bara, na Bara, na Bara tena!, hakuna wakati mwingine wowote ambao Rais wa JMT, atatoka nje ya Bara!.
  hapo namba saba ndio sijakubaliana na wewe nani kakwambia kuwa rais anayekuja anatoka kaskazini kuna watu wamekuwa wanaifikiria ccm kiutofauti ukweli mpaka sasa bado hawajapata mgombea kwa sababu wengi waliojitokeza dosari zao zipo waziwazi ndio maana mpaka sasa hujasikia wakitangaza tarehe ya kuchukua fomu kwani bado wanashawishi watu wanaodhani watafaa wamejifunza makosa waliyofanya awamu inayoisha na hawataki kurudia tena
  kuhusu zanzibar unafiki wao ndio uliwaponza kama sio majungu yao leo tungekuwa na rais bora kabisa kiasi cha kwamba hata vyama vya upinzani wasingepata pa kusemea lakini wao waliungana na mitandao kwa kuangalia maslahi yao binafsi matokeo yake watakuwa wakibaki kushangilia wagombea urais kutoka bara na hiki kitu kiliwaudhi sana watu wa bara kiasi cha wao kuhakikisha hawatapata tena nafasi hii adimu,vitendo wanavyofanyiwa bara huko zanzibar,madai yao ya kila siku wanadhulumiwa hayatoi nafasi kwao kupewa nafasi ya kuongoza nchi hii
   
 12. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #31
  Apr 11, 2015
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Siku Rais zkitoka Zannzibar nitatembea uchi kutoka posta hadi kariakoo
   
 13. HNIC

  HNIC JF-Expert Member

  #32
  Jun 5, 2015
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 1,902
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #33
  Jun 17, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,661
  Likes Received: 23,902
  Trophy Points: 280
  Mkuu , huu mstari nauweka kwenye kumbukumbu ili siku ikifika tukumbushane!.

  Pasco
   
 15. l

  logframes JF-Expert Member

  #34
  Jun 17, 2015
  Joined: Jan 30, 2015
  Messages: 812
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Usiape mkuu ...anything may happen, no guarantee in politics
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #35
  Jul 11, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,661
  Likes Received: 23,902
  Trophy Points: 280
  Wanabodi, majina yaliyotoka ni haya,
  Jee kuna uwezekano mgombea wa CCM ni Balozi Amina Salum Ali?!.

  Amepita kwa merits au ndio hii affirmative action ninayoizungumzia hapa?!.

  Pasco
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #36
  Apr 22, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,661
  Likes Received: 23,902
  Trophy Points: 280
  Mkuu
  Mohamed Said
  Karibu
  Pasco
   
 18. Red Giant

  Red Giant JF-Expert Member

  #37
  Apr 22, 2016
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 10,512
  Likes Received: 7,707
  Trophy Points: 280
  hivi mwinyi alikuwa mzanzibari?
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #38
  Apr 26, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,661
  Likes Received: 23,902
  Trophy Points: 280
  Mkuu Maalim
  Mohamed Said
  , jee inawezekana aliyepandisha uzi huu, ni mtu mwenye chuki na Waislamu kiasi cha kutaka rais atoke Zanzibar lakini awe ni Mkristu?!.

  Pasco
   
 20. b

  blessings JF-Expert Member

  #39
  Sep 10, 2017
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 5,482
  Likes Received: 3,170
  Trophy Points: 280
  Bahati aliyopata Mwl. Ally Hassan mwaka 1985 pengine itajirudia 2055 (napo ni kwa kubahatisha).
   
 21. b

  blessings JF-Expert Member

  #40
  Sep 10, 2017
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 5,482
  Likes Received: 3,170
  Trophy Points: 280
  Mwaka 2055 Mola akituweka hai
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...