Je, kunahitajika affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuwa Rais wa JMT? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, kunahitajika affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuwa Rais wa JMT?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Sep 20, 2014.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2014
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,759
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Tanzania ni nchi ya Jamhuri ya Muungano, yenye watu kutoka iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, na kuunda nchi moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao raia wake wa pande zote mbili, wako sawa na wana hadhi sawa na uhuru kamili wa kila kitu ikiwemo kugombea na kushika madaraka ya nafasi juu kabisa ya uongozi kwenye JMT, hii ni nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Baada ya Nyerere kutoka Bara, alifuatiwa na Mwinyi kutoka Zanzibar.
  Wakati wa kipindi cha Mwinyi, makamo wa rais ndiye pia alikuwa Waziri Mkuu wa JMT na Mwinyi alihudumiwa na ma Makamu watatu, Joseph Sinde Warioba, John Samwel Malecela na Cleopa David Msuya, na kipindi hiki cha Mwinyi, 1992, ndipo Tanzania tukaingia kwenye mfumo wa vyama vingi, na CCM kwa kuogopa, wa urais wa Zanzibar kushikwa na mtu wa chama kingine, wakati ndio set up ya muungano kuwa rais akitoka Bara, makamo lazima atoke Zanzibar, iwapo Zanzibar itashikwa na chama kingine, itakuwaje?, ndipo wakaamua kubadili katiba na kumfanya rais wa Zanzibar ni nothing ndani ya set up ya muungano!, na huu ndio ukawa mwisho rasmi wa mtu kutoka Zanzibar kuwa rais wa JMT!.


  Baada ya Mwinyi, akaja Mkapa kutoka Bara, ilibidi Mkapa kufuatiwa na mtu kutoka Zanzibar, lakini yalifanyika mambo ( refer uzi huu JK, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza ..

  Hivi ndivyo zamu ya Zanzibar ilivyopokwa!) hivyo akafuatiwa na Jakaya Kikwete pia kutoka Bara, na sasa tukiwa tunaelekea 2015, sijabahatika kusikia sikia majina yoyote ya possibility ya Mzanzibari yakitajwa tajwa au any possibility ya mgombea yoyote wa nafasi ya urais wa JMT kutoka tena Zanzibar!.


  Naomba kukiri, ninaandika uzi huu kufuatia inspiration niliyoipata toka kwa mwana jf huyu


  Jee inawezekana sababu halali kwa nini Mzanzibari hawezi tena kuwa ni rais wa JMT?.

  Naomba tuanze kwa kuweka facts mezani!.
  1. Eneo lote la Zanzibar lilikuwa ni sehemu ya Tanganyika, hivyo Zanzibar ni sehemu halali ya Tanganyika!.
  2. Kufuatia Zanzibar kuwa ni sehemu ya Tanganyika, wakaazi wake wa asili ni Wamatumbi kutoka Tanganyika!.
  3. Kuna miaka fulani, wavamizi fulani wa Kiarabu kutoka nchi ya Oman, waliivamia Zanzibar, wakajifanya ni nchi yao na kuuhamishia ufalme wao kutoka Oman na kuja Zanzibar, wakazaliana, sasa wanajidhania hapo ni kwao, kiukweli hapo kwao kwa kuzaliwa tuu, lakini kiasili, sio kwao, bali mahali tuu walipozaliwa na kukulia!. Ukizaliwa India, ukakulia India, hakukufanyi uwe Mhindi, wewe utabaki ni Mmatumbi tuu!.
  4. Wavamizi hawa wakaanzisha biashara haramu ya Utumwa, ambapo Watumwa waliokuwa hawana soko, waliachwa Zanzibar. Biashara ya utumwa ulipopigwa marufuku, wengi wa watumwa hawa, walibaki Zanzibar kama watu huru na wao pia kujihesabu ni Wazanzibari!.
  5. December 1963, wavamizi hawa wakapewa uhuru wa bandia na Waingereza!, Wamatumbi wenye nchi yao, hawakukubali, mwezi mmoja baadae, ile Januari 12, 1964, wakiongozwa na Mmatumbi John Okello kutoka Uganda, walifanya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kumfurusha "mvamizi yule!" na kujitwalia Uhuru ambapo mtu mwenye asili ya Malawi, Abedi Amani Karume alitangazwa ndie Rais wa Zanzibar na M/Baraza la Mapinduzi.
  6. Aprili 26, 1964, Rais Nyerere na Karume waliziunganisha nchi hizi mbili, na kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais wa Tanzania siku zote lazima atakuwa ni Mtanzania kutoka upande wowote wa Muungano.
  7. Nyerere alitoka Bara, Mwinyi alitoka Zanzibar, japo alizaliwa bara pale Mkuranga, na ndio maana anaishi Bara! hadi sasa!. Mkapa alitoka Bara japo inasemekana lizaliwa "Nchumbiji!" JK pia ni kutoka Bara, anayefuatia pia atatoka Bara probably "Ule Mwamba wa Kaskazi", na atafuatiwa na Bara, na Bara, na Bara tena!, hakuna wakati mwingine wowote ambao Rais wa JMT, atatoka nje ya Bara!.
  8. Kufuatia Zanzibar kukosa tafsiri rasmi ya Mzanzibari ni nani, Mzanzibari wa asili ni Mmatumbi kutoka Tanganyika, lakini sasa "wale wavamizi!", nao wanajiita Wanzanzibar!, vizalia vya masalia ya Watumwa, nao kwa vile wamezaliwa Zanzibar, nao ni Wazanzibar, hivyo its very risk kukubali mtu kutoka Zanzibar kuwa rais wa JMT, wao mwisho wao ni kututolea Makamo wa Rais tuu.
  9. Be ware, wale ambao sio Wanzanzibari wa asili, na haswa vizalia vya "wavamizi" ndio wenye kelele sana!, tuwe waangalifu sana na kila kelele kwa kumuangalia vuzuri kwa jicho chunguzi, kila anayeupigia kelele zamu ya Uzanzibari kwenye urais wa JMT, kwa kujiuliza kama jee ni Mzanzibari kweli au ni wale "wavamizi!.
  10. Tanzania ni kwa Watanzania asili itatawaliwa na Watanzania asili, na sio "wavamizi", "walowezi", au watu wa kuja!.
  Natanguliza samahani msinione mbaguzi, hizi zinaweza kuwa ndizo sababu halisi zinazosimama kama facts zinazopelekea Mzanzibari, asipate tena nafasi ya kuwa rais wa JMT!, Hamdhani kwamba sasa umefika wakati, kunahitajika some specific measures kama some kind of affirmative action, kuhakikisha, rais wa JMT pia apatikane kutoka upande wa pili wa muungano?, yaani kwa wapenda haki, hatuwezi kuacha ,rais wa JMT , andelee tuu kuchaguliwa by chance, kutoka upande wowote wa JMT wakati kuna kila dalili za kuonyesha kamwe rais wa JMT, hawezi tena kutoka Zanzibar by chance, hivyo marais wote wa Tanzania ya vyama vingi ni kutoka upande mmoja tuu wa Muungano huku bara!. Is this fair kwa wenzetu Wazanzibari ambao ni raia wenye haki sawa ndani ya JMT?!. Hamdhani huu ni wakati muafaka tuwe na affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuwa rais wa JMT?.

  Hii sio mara yangu ya kwanza kuizungungumzia nafasi ya Zanzibar kwenye urais wa JMT, pia niliizungumza hapa!.

  Japo hakuna kupokezana: Kiukweli, kihaki, kihalali na ki Kudumisha Muungano, 2015 Urais wa JMT ni Zamu ya Zanzibar!.

  Wawakilishi wa Zanzibar mlioko Dodoma, lipiganieni hili nalo liingizwe rasmi kwenye Katiba kuwa urais wa JMT, wa kupokezana!.

  Asante.

  Paskali
   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2014
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,740
  Trophy Points: 280
  Pasco mada yako ni nzuri na inafikirisha. Ulichokosea ni kuandika ukiwa hauko huru. Kichwani kwako unawaza ni CCM tu ndio ina nafasi ya kutoa rais hivyo kwakuwa miongoni mwa wana ccm na ccm yenyewe Mzanzibari hatajwi basi hakuna uwezekano wa Mzanzibar kuwa Rais.

  Ukawa hawajasema watamweka nani. And I tell you, siku UKAWA watakapomtaja mgombea wao hata kama anatoka Pemba au Mwanakwerekwe huenda ikawa imemtangaza Rais wa JMT.

  Ushauri wangu kwako, unapoleta posts fikirishi kama hizi ondoa UCCM wako.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2014
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,936
  Likes Received: 190
  Trophy Points: 160
  Pasco either umeamua kupotosha kwa makusudi au huijui historia sahihi ya Zanzibar.

  Unaposema Uingereza wakatoa 'uhuru bandia' unataka kumaanisha nini?
   
 4. J Mbungi

  J Mbungi Senior Member

  #4
  Sep 20, 2014
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ndugu Pasco, Na wana JF Wengi, Tambueni kuwa kwa mfumo uliopo wa Tanganyika kumezwa Na Tanzania.. Haiwezi kuwa sawa Mzanzibari kuwa rais wa Jamuhuri Ya Muungano..(Hapo Mwanzo Nyerere alifanya tu kwa utashiwake na kuwaridhisha wazanzibari, Siyo Kimantiki..Nasema hivyo kwasababu Rais Wa Muungano anapotoka Zanzibar.. Ina Maana Zanzibar Ina marais wawili..( Wa Muungano na wa Wa Zanzibari kwao,Kwasababu wao wana rais na Tanganyika haina rais....

  Kwa bahati mabay Zaidi,katika mfumo wa Kiungozi Raisi ndiyo mwenye mamlaka na mkuu wa Serikali( siyo Kama Uingereza ambako Waziri Mkuu ana mamlaka( Hiyo ingetufanya walau tuseme Waziri Mkuu ndiye atakaye simamia Tanganyika kama kiongozi wa Serikali).. Ya kwangu ni hayo tu!!
   
 5. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2014
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 15,402
  Likes Received: 2,037
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2014
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,759
  Trophy Points: 280
  Mkuu Remote, hao jamaa tangu nilipowaita ni vijana wa "muuza utumbo fulani", wakitokea tuu, haupita muda thread inavamiwa na kozongwa na ma inzi, kibao, siku hizi, wanacheza mbali!.

  Pasco
   
 7. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2014
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Wewe ni mfano wa graet thinker wachache waliyopo humu ndani....kula like kubwaaaa....hofu yangu kuna watu watakuja kuchafua huu uzi hasa uliposema ukweli usiopingika kuhusu mwamba wa kaskazini....nafkiri tunawajua waleeee WAMA project wakiongozwa na Lizaboni...
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2014
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,759
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mzito K, kwanza asante kunikumbusha tena ule UCCM wangu!.

  Swali kama hili niliishamjibu mtu!, UKAWA so far, as it is now, it's jus "a marriage of convenience", unless otherwise!.

   
 9. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2014
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 26,400
  Likes Received: 17,583
  Trophy Points: 280
  Pasco wakipigania hilo, wapiganie pia kubadili KATIBA yao pia? Kama la Katiba ya Zanzibar basi hata hili wasithubutu kulipigania.Waswahili wanasema Mtaka yote hukisa yote.
   
 10. i

  isotope JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2014
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 2,404
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Pasco huoni kuwa Zanzibar pamoja na udogo wake inayo nafasi ya kuwa na marais wanne kwa mpigo? yaani mkamu wa rais wa JMT, rais wa SUK, makamu wawili wa SUK. Mi nafikiri hao marais ni wengi mno kutoka kwenye nchi ya watu milioni moja ikilinganishwa na rais mmoja wa JMT anayetokana na watu milioni 44. Raha iliyoyoje kwa wanasiasa wa Zanzibar!?
   
 11. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2014
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 26,589
  Likes Received: 4,723
  Trophy Points: 280
  Time to take Affirmative Action son
  They just don't understand, youknowImean?
  Niggaz comin sideways thinkin stuff is sweet man
  Yknahmean?
  Niggaz don't understand the four devils:
  Lust.. Envy.. Hate.. Jealousy
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2014
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,759
  Trophy Points: 280
  Mkuu Isotope, hawatakuwa wanne, watabaki watatu hivyo hivyo, rais wa Zanzibar ndie atakuwa makamo wa Kwanza wa Rais huku bara, position ambayo ni just ceremonial, na makamo wa pili wa rais ndiye PM ambaye ndiye mkuu wa serikali. Wale makamo wawili wa SUK wataendelea hivyo hivyo, ila huyo makamo wa kwa ni boya tuu, lolote likimtokea rais wa JMT, nafasi inashikwa na makamo wa pili kama vile Seif Sharof alivyo boya, ila kwa viongozi wengine, kingora tuu, roho zimewatulia!.

  Rais akitoka Zanzibar, Makamo wa kwanza sasa ndie atakuwa PM na makamo wa pili ndie rais wa Zanzibar.

  Pasco
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2014
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,759
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ocampo4, asante kwa kunidhania mimi ni miongoni mwa ma GT wa jf, kwa taarifa kwenye ma GT wa humu mimi sipo, kwa sababu mimi ni mropokaji na masema hovyo, na tatizo langu kubwa ni kuropoka ukweli mtupu!. Kuhusu yule "jamaa yetu", siku hizi mimi kimya maana kwa sasa ni kwa mwendo wa promo za kila uchao!.

  Thanks.

  Pasco
   
 14. B

  BULOLE BUKOMBE JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2014
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Pasco naona unamatatizo ya uelewa ningekuona wa maana sana kama ungesema pia urais wa zbar nao uwe wa kupokezana lakini nasikitika sana tena unanifanya nilie kwa kutowathamini watanganyika wanaoibeba zbar ili tu balance inabidi m-bara naye awe rais wa zbar kwani huo ndiyo muungano toka uhuru sijasikia M-bara kawa hata Mkuu wa mkoa mmojawapo wa zabar wao ya zbar ni yao na bara pia yao mbona sisi hatusemi? Hakuna mzanzibar kuwa rais wa JMT mpaka tu-equalize na shibuda awe rais wa Zanzibar hapo tutakuwa tume balance.
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2014
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145

  Mbona SCOTLAND hawagombei UNITED KINGDOM PREMIERSHIP na wameuthibitisha Muungano? sasa ZANZIBAR vingapi wanafaidi tokana na huu Muungano??
   
 16. i

  ibangu Member

  #16
  Sep 21, 2014
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tume ya Jaji Warioba iliona hili. Ndio maana ikapendekeza Serikali Tatu. Kwa mfumo wa sasa wa Muungano, ambamo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mdiye pia Rais wa Tanganyika au Tanzania Bara haiwezekani Mzanzibari awe rais wa JMT. Haiwezekani
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2014
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,759
  Trophy Points: 280
  Mkuu Bulole Bukombe, kwanza asante kwa hili, kiukweli kuna tatizo ambalo wengi hamlijui kutokana na seriksli ya muungano kulivaa koti la Tanganyika!. Kwa muungano wetu ulivyo, Mzanzibari kwanza ni Mzanzibari, na ana kitambulisho cha ukaazi, ndio kisha ni Mtanzania. Mambo yote ya Zanzibar ambayo sio ya muungano, hayo ni mambo ya Zanzibar na yanawahusu Wanzaibari tuu, na hayatuhusu Watanzania!, hivyo kwa mantiki hiyo, ukiondoa mambo ya muungano, Zanzibar ni nchi nyingine, haiwezekani Mtanzania ambaye sio Mzanzibari akashika madaraka nchi nyingine!.

  Kwa Tanzania nako ilipaswa kuweko mambo ya Tanganyika ambayo sio ya muungano, yawahusu Watanganyika pekee, yaan ilibidi ukiondoa vizara ambazo sio za muungano, Wanzanzibari walipaswa kukomea huko ili Watanganyika nao kuwa na haki zao nje ya muungano, Tume ya Jaji Warioba ililiona hili, ikalisawazisha kwa kupendekeza serikali tatu, ili kwa yale yasiyo ya muungano, kila serikali iyashughulikie!. Mijitu mijinga fulani Dodoma ikamuona Warioba ndio mjinga, ikabadilisha na kubaki vile vile kama tulivyo, serikali mbili.

  Kufuati serikali ya Muungano kuwa moja inashugulikia mambo ya muungano na yale yasiyo ya muungano, the dividing line is almost invisible kati ya mambo ya Tanganyika na mambo ya Tanzania, as a result, Mzanzibari kwanza ni Mzanzibari, ana haki zote za Uzanzibari, kisha ni Mtanzania, ana haki zote za Utanzania ikiwemo ajira, uongozi, na kila kitu ambacho sisi tunacho zikiwemo haki za Utanganyika zilizofichika ndani ya Utanzania!, hivyo ni haki kwa Mzanzibari kuja kumiliki ardhi huku, kuajiri huku na kuwa rais huku, kwa kutumia kofia yake ya Utanzania sawa na mimi na wewe, kwa sababu Utanganyika wetu, tuliufuta na kuvaa koti la Utanzania jumla, wakati wao Uzanzibari hawakuufuta.

  Kila Mzanzibari ni Mtanzania, na kila Mtanzania ni Mtanzania, ila sio Kila Mtanzania ni Mzanzibari, hii inaitwa Chako changu, chako chetu, ila changu changu!. Kila kitu cha Mtanzania pia ni Mzanzibari (Chako changu), halafu kama taifa sisi Watanhanyika tulio Tanzani, na Wanzanibari walio Tanzania, wote ni wamoja hivyo vitu vyetu ni vitu vyao (chako chetu),
  lakini likija suala la Zanzibar, mambo ya Zanzibar na kila kitu chao kule ni chao pekee (changu changu).

  Hili nililisemea mahali kuwa huu muungano nimkama ndoa, mke akiisha olewa anakuwa ni ndugu wa kwa mumewe, anakuja kwenu, anapokelewa anahudumia ndugu zako, anamiliki mali zako ni sehemu yenu, ila nyie wa kiumeni sii sehemu ya ukweni!. Ndugu za mkeo ni ndugu zako, ila vya mkeo ni vyake!, Hata sheria yetu ya ndoa ya mwaka 1971, inalitambua hili, mume akifunga ndoa, mali za mume zinakuwa ni mali za ndoa, nyumba ya mume inakuwa ndio nyumba ya ndoa, kama mke amekuja na mali zake, zile ni mali za mke na sii mali za ndoa!, ubless mke mwenyewe kwa ridhaa yake asiingize kuwa mali za ndoa, vinginevyo ndoa ikivunjika, mali zinazogawanywa ni mali za mume tuu, hata kama mke alikuwa golikipa!.

  Nadhani nimeeleweka!.

  Tofauti na ndoa, kisiasa hapa nazungumzia zamu ya mke kuwa mkuu wa nyumba, nyumba yenye uswa, haiwezekani siku zote baba tuu kuwa ndie kichwa cha nyumba, mara moja moja mama nae apewe madaraka kama baba!, uongozi wa nyumba uwe ni kwa zamu zamu, japo zamu hizo ni kwenye uongozi tuu, ila majukumu yanabaki pale pale, baba kazi yake kutafuta, ikiwemu kumuhudumia mama na mama kazi yake kutumia, na kuihudumia nyumba zikiwemo kutoa "zile huduma"!.

  Pasco.
   
 18. B

  Bijou JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2014
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,180
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145

  Acha KUJIPENDEKEZA Rais, visiwani SI wanae? Wacha TANGANYIKA iongozwe NA watanganyika
   
 19. Bome-e

  Bome-e JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2014
  Joined: Jan 3, 2014
  Messages: 8,602
  Likes Received: 5,442
  Trophy Points: 280
  Huyu pasco anabadilika kama kinyonga,ni bendera fata upepo!
   
 20. i

  isotope JF-Expert Member

  #20
  Sep 22, 2014
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 2,404
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kumbe unaongelea Katiba ya chama! Mbona chama kina utaratibu wa zidumu fikra za mwenyekiti ambapo anaweza kuamua kuwa mhula ufuatao mgombea urais atoke zanzibar au awe mwanamke na ikawa hiyo?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...