Je kuna vigezo gani mtu kuitisha waandishi wa habari "Press"

monomotapa

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
437
325
Ingawa watu wengine wanapiga kelele kuhusu kuminywa kwa uhuru wa kujieleza, kiukweli nchi hii tupo na uhuru wa kutosha kwa hili, mbali na mambo mengine Mtu yeyote anayo haki ya kuita 'press' na akaongea anachotaka.....Nadhani kila mtu ameshuhudia watu wanaojiita celebrities wa fani mbalimbali wakifanya yao siku za karibuni bila bugudha yoyote. Ingawa bado sijajua kama kuna vigezo vya waandishi wa habari kuitikia mwito.
Hata hivyo bado kuna watu wengi hawaelewi kwamba vyombo vya habari havina uwezo wa kumuondolea makosa mtu kama anayo, vyombo vya habari na vyombo vya sheria ni vitu viwili tofauti ingawa vinasaidiana

Nawasilisha.... Wenye fani yao nijulisheni
 
Ili iwe habari lazima iwe ni public interest, pia waandishi wanaangalia je,habari hii inafaa kuipeleka kwa jamii?? Itauzikaa?. Jina lako ndio litakalouza habari lakini kama huna impact kwa jamii waandishi wanaweza wakaja na wasiandike habari yako. Wanahabari unawaita tuu kwahiyo wenyewe ndio watapima kulingana na taaluma yao. Wewe ukionekana unajisaidia kando ya barabara inaweza isiwe habari lakini tukio kama hilo akilifanya mtu maarufu inakuwa habari.
 
Na hasa ukizingatia Tanzanian journalists
are somehow jobless.
True, waandishi wa habari huku bongo hawawezi kutafuta habari hivyo wana upungufu wa habari muda wote. Hukaa na kusubiri matukio yatokee ili wapate cha kuandika, ikitokea hamna issue yoyote basi wanaandika hata habari za uongo. Wenzetu wa nje waandishi wanazitafuta habari kwa nguvu zote na ndio maana hadi watu maarufu wanakimbia media maana pia maswali yao ni magumu na yanachimbua mambo mengine.
Bongo hadi hamorapa anaitisha press na anawekwa front page,kweli ni maajabu.
 
Kama control haipo katika mambo haya kuna siku mtu ataita media atangaze hali ya hatari....
Hivi nyie ccm mkoje???mwataka kuleta idikteta tena hata kwenye kuita press.????Hivi nyie mnavichwa kweli vyenye ubongo????
 
True, waandishi wa habari huku bongo hawawezi kutafuta habari hivyo wana upungufu wa habari muda wote. Hukaa na kusubiri matukio yatokee ili wapate cha kuandika, ikitokea hamna issue yoyote basi wanaandika hata habari za uongo. Wenzetu wa nje waandishi wanazitafuta habari kwa nguvu zote na ndio maana hadi watu maarufu wanakimbia media maana pia maswali yao ni magumu na yanachimbua mambo mengine.
Bongo hadi hamorapa anaitisha press na anawekwa front page,kweli ni maajabu.
Ni kweli waandish wa bongo hawana puzzed question.....cjui less academic au restricted question au guded question
 
Haaahaahahh... Nacheka kwa uchungu.. bongo tuna kazi sana..
 
Kwa mfa
Ni kweli waandish wa bongo hawana puzzed question.....cjui less academic au restricted question au guded question
mfano kama Jana Steve alipaswa aulizwe kama yale aliyokua akizungumza na bi mkubwa ilikua ni uwongo yani ili tu amridhishe, vp leo anayozungumza hapa? Kwamba na yenyewe pia si itakua ya uwongo anazungumza tu ili kumridhisha mwenye mamlaka?
 
Pia Steve alipaswa aulizwe kama yale aliyokua ya uwongo, mbona mama alipigiwa kweli simu na aliosema amewapa namba? Maana ingekua sio kweli Mama angen'gamua mbona hakuna alie nipigia! Lkn Mama aliitikia kuashiria azungumzacho Steve ni ukweli.
 
Steve anachukulia watanzania kama watoto wadogo, sidhani kama ameweka maslahi ya nchi mbele
 
Hivi nyie ccm mkoje???mwataka kuleta idikteta tena hata kwenye kuita press.????Hivi nyie mnavichwa kweli vyenye ubongo????
Kila kitu huwa kina utaratibu, Utaratibu sio udicteta. Siliongelei kichama bali kijamii na Ki Nchi zaidi
 
Namkumbuka sana Paskal Mayala alimuuliza swali gumu sana Jaji Lewis Makame..marehemu sasa ..alipokuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi mwaka 2000 kuhusu kupoteza kwa gari lililobeba vifaa vya kura siku ya Uchaguzi vya jimbo la Mjini Magharibi....mpaka matangazo ya Press conference hiyo mubashara yalizimwa ghafla kabla ya swali kujibiwa!!!

Waandishi wenye maswali magumu...hard question kwa sasa tz ni kama hatuna au kama wapo basi wamepigwa na ganzi ya mdomo!!
 
Back
Top Bottom