Je, kuna uwezekano wa Papa kuchagua Askofu mwingine Tanzania baada ya Thaddeus Ruwa'ichi kuugua?

Hakuna haja ya kuchagua Askofu Mkuu mwingine.

Mhashamu Baba Askofu Mkuu Yudathadeus Ruwa'ichi anaendelea vizuri. Mungu ni mwema.

IMG-20190911-WA0002.jpg
 
Nini kimempata Bishop Ruwa'ichi,nimesikia ni mgonjwa,kafanyiwa opasuaji wa kichwa
 
kwani wewe unapoona neno mungu unaamini ni kitu gani....kabla hujataka kupata uthibitisho...
Kwanza kabisa, sitaki kuamini, nataka kujua.

Mungu ni character wa hadithi iliyotungwa na watu, hayupo katika uhalisia nje ya hadithi.

Kama unabishia hili - na inawezekana mimi nikawa nimekosea na wewe uko sawa- thibitisha Mungu yupo.
 
Kwanza kabisa, sitaki kuamini, nataka kujua.

Mungu ni character wa hadithi iliyotungwa na watu, hayupo katika uhalisia nje ya hadithi.

Kama unabishia hili - na inawezekana mimi nikawa nimekosea na wewe uko sawa- thibitisha Mungu yupo.
Wewe ndiye ututhibitishie kuwa hayupo tunaoamini kuwa haya tunayoyaona yameumbwa naye.
 
Wewe ndiye ututhibitishie kuwa hayupo tunaoamini kuwa haya tunayoyaona yameumbwa naye.
Kwanza kabisa, sina tatizo wala mjadala na wanaoamini.

Kama unafikiri nina tatizo au mjadala na wanaoamini naona umekosea mjadala.
 
Kwanza kabisa, sina tatizo wala mjadala na wanaoamini.

Kama unafikiri nina tatizo au mjadala na wanaoamini naona umekosea mjadala.
Unasema hayupo nje ya uhalisia wa hadithi, tuthibitishie na sisi ambao labda tumepotea kiimani.
 
Unasema hayupo nje ya uhalisia wa hadithi, tuthibitishie na sisi ambao labda tumepotea kiimani.

Sipendi tabia ya kuzungumzia imani. Napenda kuzungumzia uchunguzi wa fact.

Lakini pia, sina tabia ya kuacha maswali.

Imani ni kitu cha faragha. Sijaja hapa kujadili imani, nimekuja hapa kwa sababu mtu kasema kanisa Katoliki ndilo kanisa pekee la Mungu wa kweli, as a statemenmt of fact, not faith.

Sasa, kwa kuwa umenuialika, umeniuliza swali, sina njia ya kukataa kukujibu (kwa sababu sitaki kuongelea imani) bila kukimbia swali (kitu ambacho sitaki).

Na kwa kweli, pia sina haja ya kukataa kuongelea imani, wakati umenialika niongelee imani.

Kwanza kabisa.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, ukimfikiria kwa makini, ukamlinganisha na ulimwengu huu tuliomo, kimantiki utaona hayupo, ni wa hadithi tu.

Kwa sababu.

1.Maandiko ya dini mengi yanayomuongelea yana contradiction kwa namna ya kwamba huyo Mungu aliyeandikwa kimantiki hawezi kuwepo (Quran, Bible maandishi yoyote ya Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, amabaye anapata hasira, anapanga na kughairi, ana wivu watu wakiabudu miungu mingine, anaua mpaka vizazi na vizazi kwa makosa ya mababu na mababu zao, anaachia mabaya yawezekane halafu anahukumu watu kwa kufanya mabaya, anaziba mioyo macho na masikio ya watu wasimjue, halafu wasipomjua anawahukumu vikali kwa kutomjua etc)

2. Ukiondoka kwenye maandiko, useme labda maandiko yamechakachuliwa, kidhana tu, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote na utakatifu wote huo anaosemwa kuwa nao, hayupo. Angekuwepo, asingeumba dunia inayowezekana kuwa na mabaya, magonjwa, matetemeko ya ardhi, vimbunga, kuuana, kifo etc.

Ukisema hayo ni matokeo ya shetani, nina maswali mawili kwako.

Unaweza kuthibitisha Shetani yupo?

Kwa nini Mungu aliumba ulimwengu ambao Shetani anaweza kuwepo, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao Shetani hawezi kuwepo?

Ukisema Mungu kaumba ulimwengu huu hivi, lakini kuna mbingu itakuwa haina ubaya, nina maswali mawili kwako.

Huko mbinguni/peponi unaweza kuthibitisha kupo kweli na si hadithi za watu tu? Maana kujibu kitu kimoja ambacho huwezi kuthibitisha kipo (Mungu) kwa kutaja kitu kingine ambacho huwezi kuthibitisha (Roho, Peponi etc) ni ujinga wa kuzunguka katika vitu usivyoweza kuthibitisha vipo.

Pia, nitakuuliza, huyo Mungu alishindwa kufanya dunia hii iwe pepo, wapendanao wasitenganishwe na kifo? Watoto wadogo wasife vifo vibaya? Masikini wasishindwe kupata hata chakula? Watu wasife kwa magonjwa mabaya kabisa? Majambazi wasipore watu? Wanasiasa washenzi wasidanganye watu?

Alishindwa kuumba ulimwengu usio na mabaya? Kama hakushindwa, kwa nini hakuumba hivyo?

Hakuumba hivyo (ulimwengu usio na mabaya) kwa sababu hakutaka tu, lakini angetaka angeweza? Kama hakutaka tu, katubania, ana upendo wote kweli?

Ama alitaka kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya, ila hakuweza tu? Kama hakuweza, je, ni kweli ana uwezo wote?

Huyu Mungu yupo kweli? Au ni hadithi za watu tu?

Kwa nini hbari zake zina contradictions sana?

Kwa nini hamuwezi kumthibitisha kwa wazi kwamba yupo?

Au ni kwa sababu hayupo, ametungwa na watu tu?

Kama unabisha na unasema yupo, thibitisha yupo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom