Je, kuna uwezekano wa Papa kuchagua Askofu mwingine Tanzania baada ya Thaddeus Ruwa'ichi kuugua?

Vyema,na kufikiri kwamba Mungu yupo sio tatizo au una tatizo iwapo mtu anafikiri hivyo?Mpumbavu hufikiri moyoni kwake kwamba hakuna Mungu(Zab 53:1 na kuendelea)kasome na uwe na amani moyoni mwako
Wapi nimeandika kufikiri Mungu yupo ni tatizo?

Tatizo mtu kaja na katuambia ukatoliki ndiyo kanisa la pekee ya Mungu wa kweli.

As a statement of fact.

Nikamwambia athibitishe Mungu yupo.

Mpaka sasa hajathibitisha!

Kufikiri Mungu yupo sio tu sina tatizo nako, mimi kama mtu niliyesoma "Universal Declaration of Human Rights" la December 10 1948, natetea haki za uhuru wa kuabudu kama haki za binadamu.

Lakini sitaki mtu aseme Mungu yupo as a statement of fact, because it is not.It is a statement of belief.

Unaelewa tofauti?

Unaelewa kimsingi sijawahi kubishana na mtu anayesema "naamini Mungu yupo" kama kauli ya imani?

Unaelewa nina tatizo na mtu anayesema kama fact kwamba "Mungu yupo kweli na dini yangu ndiyo ya kweli" ?
 
Siyo lazima atoke jimbo Kuu la Dar es Salaam. Angalia hata historia ya Cardinal Laurean Rugambwa.
1943 -Upadirisho
1952 - Vicar General
1953- 1960 Askofu Jimbo la Rutabo
1960- 1968 Askofu Mkuu/ Cardinal wa Jimbo Kuu la Bukoba
1968- 1992 Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam
Kwa hiyo siyo lazima Cardinal atoke Dar es Salaam
Rutabo iliwahi kuwa Jimbo au Bukoba kuwa Jimbo kuu?
 
KANISA lililoachwa na Mungu Haliwezi kuabudu Sanamu.na kuruhusu Mwanadam achukue Nafasi Ya Mungu.. Unamwitaje Mwanadamu mwenzako BABA MTAKATIFU??
Judethadeus Ruwa'ichi sio Kardinali - ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.

Hata hivyo, Kanisa Katoliki lina mifumo thabiti sana ya kiuongozi.

Ndio maana sio Jambo la kushangaza kusikia Jimbo fulani halina Askofu au Askofu Mkuu hata kwa zaidi ya miaka minne, na kila kitu kikaenda sawa sawia.

Hili ndio Kanisa pekee liliochwa na Mungu nafsi ya pili - Kanisa moja, Takatifu, Katoliki na la Mitume.
 
Hapa tupo kwenye dini sio muda wa siasa
MABEBERU ndio wanatuchagulia viongozi?
Mbona mkulu kila siku anatuaminisha mabeberu ndio wametuletea umaskini na hawatupendi alafu na yeye anachaguliwa mtu wa kumwongoza na anamtumikia?

Shikamoo mabeberu,

shikamoo wazungu;
shikamoo beberu
 
KANISA lililoachwa na Mungu Haliwezi kuabudu Sanamu.na kuruhusu Mwanadam achukue Nafasi Ya Mungu.. Unamwitaje Mwanadamu mwenzako BABA MTAKATIFU??
Na ndio maana Kanisa Katoliki linabaki kuwa Kanisa pekee lililo takatifu na ambalo limeachwa na huongozwa na Mwenyezi Mungu, kwasababu hatuabudu sanamu kama Makanisa mengine.

Tatizo unadandia train kwa mbele hauwezi kuelewa kwanini Papa anaitwa Baba Mtakatifu. Anyways, ngoja tukuibie tu maarifa kidogo.

Kuwa Mtakatifu maana yake una uwezo wa kutokutenda makosa yeyote yale. Baba Mtakatifu ni taasisi. Kama taasisi inayoongozwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe, haiwezekani kutenda makosa yoyote.

Ndio maana Papa anakuwa na ataendelea kuwa Baba Mtakatifu.
 
KANISA lililoachwa na Mungu Haliwezi kuabudu Sanamu.na kuruhusu Mwanadam achukue Nafasi Ya Mungu.. Unamwitaje Mwanadamu mwenzako BABA MTAKATIFU??
Mkuu sana.

Hoja zako ni dhaifu sana sana,

1. Unaposema "abudu" maana yake ni kitendo cha kufanyika na mtu, Mfano: Mimi namuabudu Mungu katika Roho na Kweli. Hapo nimeabudu.

2. Wewe unaposema "kuabudu" napata shida kwamba wewe ushawai kushiriki hizi ibada za kuabudu sanamu za kanisa katoliki, kama hujawahi kuabudu au kushiriki izo ibada, umepata wapi mamlaka yakusema wanaabudu!

2a) Niweke wazi pia kuwa Kanisa halijawekeza vyakutosha katika kufundisha wakatekumeni juu ya maswala ya kanisa hususan Ritrujia na Imani Katoliki.

3. Sio kweli kwamba wakatoliki wana abudusanamu, kama imgekua kweli basi tungeskia shuhuda kwa wale wanaohama kanisa katoliki na kwenda makanisa mengine. Mfano: Wachawi wakiacha uchawi huwa wanashuhudia kuwa walikua wanakula nyama za watu nk.

4. Kadili ya Imani ya Kanisa ni kweli Kanisa Lililoachwa na Mitume ni Takatifu Katoliki. Pia, ni wazi kua Kanisa katoliki ndio la kwanza ndio mana haya mengine yanaitwa "Protestants" kwamba walikua wanapinga mambo fulani ya Kanisa.

5. Kumuita "Papa" Baba Mtakatifu sio kitu cha kukuumiza sana, anaitwa hivyo kwa maana ya cheo chake na namna cheo chake kinavyopatikana ndio kwa njia takatifu. Ndio tunasema Baba Mtakatifu.


Hivyo basi nivyema kujipima kabla hujaandika "ujinga" Jifunze kwanza, maarifa hutafutwa.
 
2a) Niweke wazi pia kuwa Kanisa halijawekeza vyakutosha katika kufundisha wakatekumeni juu ya maswala ya kanisa hususan Ritrujia na Imani Katoliki.

Si vyema kuitana wakatekumeni hata km watu wamehamia
 
Si vyema kuitana wakatekumeni hata km watu wamehamia
Mkatekumeni ni yule ambaye ameomba rasmi kupokelewa na Kanisa yaani kubatizwa na ubatizo wa Kanisa Katoliki.

Sasa, Hawa Wakatekumeni ndio wanatakiwa kufundishwa juu ya Dini na Kanisa.

Hapo nimekosea wapi mkuu?
 
Huko ni kuwadhalilisha
Mkatekumeni ni yule ambaye ameomba rasmi kupokelewa na Kanisa yaani kubatizwa na ubatizo wa Kanisa Katoliki.

Sasa, Hawa Wakatekumeni ndio wanatakiwa kufundishwa juu ya Dini na Kanisa.

Hapo nimekosea wapi mkuu?
 
Rutabo iliwahi kuwa Jimbo au Bukoba kuwa Jimbo kuu?
For whatever case, naweza nisiwe thorough kwenye jibu langu lakini nadhani kumekuwa na evolution ya RC administrative structure in the church. So yawezekana hivo. Ila nakumbuka alipofariki Cardinal Rugambwa kwanza alizikwa kwenye Parish Cathedral mahali alipoanzia Uaskofu wake. Then kwenye mwishoni mwa miaka ya 2000 ndipo mabaki yake yakawa exhumed na kuzikwa kwenye kanisa la Bukoba Cathedral pale mjini.
 
Wenye ufahamu wanijulishe huyu Cardinal mpya aliyemrithi Pengo amefanyiwa upasuaji mkubwa sana na itamchukua muda sana kurudi kwenye hali yake kwanini Papa Francis asiteue mwakilishi mwingine kwa kuwa hizi ni kazi za kutumikia watu. Au Pengo arudishwe kwenye hiyo nafasi hadi apatikane mtu mwingine.

Na kumbukumbu zangu zinaniambia kuna Papa aliwahi kuondoka kwenye kiti chake kutokana na Afya haikuwa vizuri

Nimtakie Afya njema apone haraka Mwadhama Ruwa'ichi
Point of koreksheni

Dkt Ruwaichi sio Kadinali
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom