Je, kuna uwezekano wa Papa kuchagua Askofu mwingine Tanzania baada ya Thaddeus Ruwa'ichi kuugua?

yitzhak

JF-Expert Member
Jul 3, 2019
616
853
Wenye ufahamu wanijulishe huyu Cardinal mpya aliyemrithi Pengo amefanyiwa upasuaji mkubwa sana na itamchukua muda sana kurudi kwenye hali yake kwanini Papa Francis asiteue mwakilishi mwingine kwa kuwa hizi ni kazi za kutumikia watu. Au Pengo arudishwe kwenye hiyo nafasi hadi apatikane mtu mwingine.

Na kumbukumbu zangu zinaniambia kuna Papa aliwahi kuondoka kwenye kiti chake kutokana na Afya haikuwa vizuri

Nimtakie Afya njema apone haraka Mwadhama Ruwa'ichi
 
Judethadeus Ruwa'ichi sio Kardinali - ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.

Hata hivyo, Kanisa Katoliki lina mifumo thabiti sana ya kiuongozi.

Ndio maana sio Jambo la kushangaza kusikia Jimbo fulani halina Askofu au Askofu Mkuu hata kwa zaidi ya miaka minne, na kila kitu kikaenda sawa sawia.

Hili ndio Kanisa pekee liliochwa na Mungu nafsi ya pili - Kanisa moja, Takatifu, Katoliki na la Mitume.
 
Amefanyiwa upasuaji mkubwa sana itachukua muda kurudi kwenye majukumu
Ndugu Ruwaichi siyo Kadinali ni Askofu mkuu wa jimbo hivyo pia ana wasaidizi wake ikitokea kweli Hajiwezi basi Papa anaweza kufanya hivyo.Asante
 
Mbona Pop Benedict aliwahi tu kujiuzulu bora angepumzishwa huyu
Ndugu Ruwaichi siyo Kadinali ni Askofu mkuu wa jimbo hivyo pia ana wasaidizi wake ikitokea kweli Hajiwezi basi Papa anaweza kufanya hivyo.Asante
 
Sio wivu mkuu tunaangalia uhitaji ile ni nafasi nyeti
Mkuu, mbona mapema sana, mgojwa ata vidonda vya upasuaji havijakauka tayari unataka aondolewe kwenye nafasi yake? embu acheni roho mbaya, yaani mnaona wivu mpaka kwenye kazi za Mungu?
 
Ahsante kwa kuniweka sawa
Judethadeus Ruwa'ichi sio Kardinali - ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.

Hata hivyo, Kanisa Katoliki lina mifumo thabiti sana ya kiuongozi.

Ndio maana sio Jambo la kushangaza kusikia Jimbo fulani halina Askofu au Askofu Mkuu hata kwa zaidi ya miaka minne, na kila kitu kikaenda sawa sawia.

Hili ndio Kanisa pekee liliochwa na Mungu nafsi ya pili - Kanisa moja, Takatifu, Katoliki na la Mitume.
 
Sina uelewa mkubwa ila nafahamu MTU akishindwa kuendelea kutokana na sababu mbalimbali Pop huchagua mwengine
Mtoa mada atakuwa ni Mkatekumeni bila shaka! Haonekani kuwa na uelewa kabisa kuhusu kanisa la Mungu, hivyo anastahili kueleweshwa kistaarabu na kwa kwa kina.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom