Je kuna uwezekano wa Mtu kufanya wizi kwa Account ya mtu, kwa kupitia Account namba tu?

Ulisikia Wapi

JF-Expert Member
Sep 6, 2019
1,797
2,000
Wakuu kuna hili swali nimekua nikijiuliza, ika nikaona ni bora nipate na mawazo ya wadau kutoka humu kwa katika jukwaa hili la Great Thinker.

Hivi inawezekana mtu kufanya uhalifu(wizi) kwa kupata Account/Akaunti namba ya mteja wa Benki fulani?

Sijui nimeeleweka wakuu.
 
Hazchem plate

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
10,427
2,000
sema unaweza pigwa kwa VISA/Master card.
kama mtu anajua ile namba yako ya Visa na vile vinamba kule nyuma anakuibia vizuri tuu kama account yako ipo active kununua huko duniani
 
MoseKing

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
1,678
2,000
Wakuu kuna hili swali nimekua nikijiuliza, ika nikaona ni bora nipate na mawazo ya wadau kutoka humu kwa katika jukwaa hili la Great Thinker.

Hivi inawezekana mtu kufanya uhalifu(wizi) kwa kupata Account/Akaunti namba ya mteja wa Benki fulani?

Sijui nimeeleweka wakuu.
Mtu akiwa na account number, CVV na exp date.

Anahamisha tu pesa awezavyo.
 
maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
9,361
2,000
Kama ni just account number hakuna anaeweza kukuibia unless apate kingine cha ziada. Ndio maana account namba za shule zinaandikwa tu kwenye mafomu na hata kwa mawakala wa benki wanazibandika tu ukutan
 
MoneyHeist4

JF-Expert Member
Jul 10, 2017
1,558
2,000
Kupitia Account Number haiwezekani kabda awe na CVV pamoja na Exp date, hapo mtandaoni ataagiza mziko kwa kutosha tu, ikiwezekana hadi kuhamisha mzigo wote kabsa
 
covid 19

JF-Expert Member
May 9, 2014
1,695
2,000
Wakuu kuna hili swali nimekua nikijiuliza, ika nikaona ni bora nipate na mawazo ya wadau kutoka humu kwa katika jukwaa hili la Great Thinker.

Hivi inawezekana mtu kufanya uhalifu(wizi) kwa kupata Account/Akaunti namba ya mteja wa Benki fulani?

Sijui nimeeleweka wakuu.
inawezekana km mtu huyo atapata kadi ya account husika iwe mastermastercard au visacard basi nirahisi sana within 1 min ele inaamishwa tu online..
 
nerilan

JF-Expert Member
Dec 11, 2013
296
500
Kupitia Account Number haiwezekani kabda awe na CVV pamoja na Exp date, hapo mtandaoni ataagiza mziko kwa kutosha tu, ikiwezekana hadi kuhamisha mzigo wote kabsa
Kuna kitu watu wanachanganya kidogo linapokuja swala la malipo/ utoaji wa fedha kwa njia ya mtandao.

Unapozungumzia fedha kutoka kwenye akaunti ya mteja endapo mdukuaji/mwizi amepata CVV na Expiry date ya kadi ya benki, kitu kingine kinachohitajika ni kadi namba na sio akaunti namba.

Kwa kusema hili, kama nitatoa akaunti namba tu, bila taarifa zangu za kadi kujulikana na mtu mwingine na kama kadi yangu imewezeshwa kufanya manunuzi ya mtandao, basi hapatakuwa na hatari ya mtu kutoa fedha kwa njia ya mtandao.

Kinyume chake ni kwamba tunapswa hifadhi kadi zetu za benki katika hali ya usalama ili kuficha taarifa za kadi ikiwa ni pamoja na kadi namba, expire date na CVV. Pia haishauriwi kumpigia mtu picha ya kadi yako na kumtumia kwa njia ya mitandao, maana unatoa taarifa muhimu za kadi yako. Hata tunapotuma taarifa za kadi zetu mfano namba za kadi basi kuna utaratibu wa kuficha zile namba kwa kutoziandika zote, bali kureplace baadhi ya namba kwa ***.

Utaratibu ni kuandika namba sita za mwanzo, kisha unaficha sita zinazofuata na kuandika nne za mwisho. Na hii hufanyika kama unashare kwenye mitandao au email na mtu.

Ila endapo utapaswa fanya manunuzi basi zinapohitajika hizi namba basi utalazimika kuzituma kama zilivyo pamoja na taarifa nyingine zitakazo hitajika.

Jambo la kujifunza ni kuwa usitumie kadi yako kufanya manunuzi ya kimtandao yanayo hitaji utoaji wa taarifa za kadi yako kwenye mitandao isiyokuwa secured. Pia inashauriwa kutumia njia zingine kama Paypal ambao hawa kimsingi utawapa taarifa ya kadi yako, na pindi utakapofanya malipo basi itahitajika wewe ukubali kwanza kabla fedha haijakata kwenye akaunti. Wao wanafanya kazi kama mtu kati baina ya mnunuzi na muuzaji.

Mwisho kabisa, unaweza fanya manunuzi kwa njia ya kadi kwa kadi ambazo hazina hata akaunti namba zaidi ya namba ya kadi na taarifa zingine kama CVV na expiry date.
 
nerilan

JF-Expert Member
Dec 11, 2013
296
500
"CVV na expiry date" naomba fafanua mkuu..cjaelewa.
CCV kirefu chake ni Card Verification Value au watu wengine huiita Card Security Code. Hizi ni namba zilizo nyuma ya kadi zianziazo tatu hadi tano kulingana na kadi husika. Ni "namba ya siri" ya kadi husika. Hii haina maana CVV ni namba ya siri inayoweza tumika kutolea fedha kwenye ATM au wakala hata pindi ukiipata kadi ya mtu husika. Hii huhusika zaidi yanapofanyika manunuzi ya kimtando.

Expiry date ni muda wa kuisha matumizi ya kadi husika. Kadi zote zenye nembo za VISA, Mastercard, Maestro, Union Pay n.k zimepewa ukomo wa muda wa matumizi tangu siku zilipotengenezwa. Muda huu waweza kuwa miaka 3, 4, 5 n.k

Endapo mwezi na mwaka wa matumizi utafikia ukomo basi kadi hii haitaweza kufanya miamala kwenye mashine za ATM pamoja na manunhzi ya kimitandao.

Mwisho kabisa, kadi moja huweza kufanya kazi kwenye mitandao ya benki nyingine au kufanya manunuzi ya kwenye mitandao kwa hisani ya makampuni tajwa hapo juu (VISA, Mastercard, Maestro n.k)
 
  • Thanks
Reactions: Eco

kitonger

JF-Expert Member
Jan 31, 2020
494

blessed mkuu..nmekuelewa.
 
JAKUGOTE

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
546
1,000
Wakuu kuna hili swali nimekua nikijiuliza, ika nikaona ni bora nipate na mawazo ya wadau kutoka humu kwa katika jukwaa hili la Great Thinker.

Hivi inawezekana mtu kufanya uhalifu(wizi) kwa kupata Account/Akaunti namba ya mteja wa Benki fulani?

Sijui nimeeleweka wakuu.
Unataka umwibie nani kwani?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom