Je, kuna uwezekano wa Mjamzito kuumwa tumbo mumewe akichepuka?

scientificall

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
453
314
Kwanza nawasalimuni nyote kwa jina la Jamii Forums nanyi itikieni mahusiano mapenzi na urafiki vidumishwe.

Kuna rafiki angu kijana lika langu japo tunazidiana about 2 years yeye ameoa lakini mimi sijaoa. Kwa mara nyingi tunapeana michongo ya pesa na kusaidiana kimawazo na kifedha ili kusogeza life mbele kwani tumekuwa wote na tupo kituo kimoja cha kazi.

Imekuwa utaratibu wetu hata kabla hajaoa kupeana ushauri juu ya mademu wapi wanafaa na wapi ni vichomi na hata kwenda kula bata mademu wetu tulikuwa tunawatoa out pamoja.

Sasa rafiki angu huyu baada ya kuoa akawa anajitoa mdogomdogo kwenye chama maaana nlimwambia ameshakuwa na familia inabidi apunguze kula mademu nae akanielewa na kweli alipunguza takribani mwaka mzima hivi.

Sasa mke wake ana mimba kubwa tu lakini sasa jamaaa kumbe mwaka huu amezama kwenye penzi na mfanyakazi mwenzetu wa kike wa hapa kazini toka mwezi wa kwanza amekuwa akijimegea na alikuja kuniambia hvi karibuni kuwa kashamfanya kama mke wake.

Shida imekuja hivi Juzi mke wa rafiki angu alikuwa anaumwa saaana tumbo usiku kucha kwa maelezo ya jamaa hakulala takribani siku mbili na anakuja kazini amechoka kisa apati usingizi usiku.

Na alijaribu kumpa dawa ya kienyeji lakn bado tatzo ni lile lile. Nilivyomdadisi akasema huwa anagegeda manzi yake na baada ya siku mbili anapiga ya halali kwa mke wake. Hapo mm ndo nimestuka nkahisi tatzo linaweza kuwa linaanzia hapa. Kabla sijamwambia chochote nimeona ni vyema niwashirikishe wadau ili nipate kumshauri vyema.

Je kuna uhusiano kwa mwanamke kuumwa tumbo mimba ikiwa kubwa baada ya mmewe kuchepuka nje ? Na ni ipi dawa na suruhisho la hili. Na ni yapi madhara yake akiendekeza hili jambo.

Nawasilisha
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom