- Thread starter
- #41
Mtiririko wa kauli zake mara tu alipoapishwa na za baada ya siku 100 utawalani, zimeshatuonyesha aina ya raisi wetu mpendwa alivyo. Mahojiano yake na BBC juzi yameonyesha pia umahiri wake katika upitiaji wake wa masuala ya sheria na katiba aliyoapa kuilinda na kuitekeleza, ahukumiwe kwa hayo.
Alisema pia, Mbowe alipoona katenda jinai, alikimbilia NBI lakini alipoona mambo yamekuwa moto, katafta sababu ili yatakapompata hayo yanayompata, apate visingzio na huruma...nk. Kuna wengne wameanza kuwahusisha Lema na Lissu ktk jinai hiyo pia.
Ukimsikliza IGP akizngmza na kuwaonya watu wasizungmzie suala lililopo mahakamani ndo utapoelewa kuwa sheria inamhusu nani na nani haimhusu. Kwamba yeye anaposisitiza kuwa wanao ushahidi, yeye hainglii chochote. Na anapoonya wengne, yeye ni mahakama tayari anayo hiyo haki. Anawaonya wengine kama vile yeye ndo sheria yenyewe.
Ikiwa hayo yameanza kuonekana mapema hivi, Rais kaonyesha anachokitegmea, kwamba Mbowe alishakimblia nchi jirani na IGP tayari anao ushahidi...nk ni suala la kuomba Mungu jambo hilo lishughulikiwe na mahakimu wacha Mungu. Je, wako wangapi?
Na ikiwa tu kuhudhuria mahakamani kuisikiliza kuna mashrti kiasi hicho, je kuionyesha mubashara...? Nakwambia, pamoja ingependeza, si rahisi. Ngoja uone
Haipo siri ndani ya nchi kuwa baada ya siku 100 za mwanzo alibadilika:
Baada ya siku 100: Tunapoachana kwenye Mataa na Rais Samia
Ndani ya siku 100 sifa alivuna ndani na nje ya nchi.
Alipo sasa anataka kuendelea kuvuna za nje akiita rebranding akiamini ndani hakuhitaji tena.
Tuweke rekodi sahihi kwa kuzipima kauli zake kwa vitendo mbele ya macho ya dunia. Hata dhahabu hupimwa kwa moto.
Kwa kauli yake: "umesikia kuna vyombo vya habari vinalalamika kuhusu uhuru?"
Samia: Vyombo vya habari vipo huru, hakuna kilicholalamika
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari na hadi sasa hakuna hata kimoja kilichowahi kulalamika.
www.mwananchi.co.tz
Ijumaa tuko live kutokea Kisutu.