Je, kuna ushahidi kuwa dawa za malaria zinatibu corona?

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542
Anti-malarial drugs

Dawa ilitengenezwa awali kwa ajili ya kutibu malaria

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa ametumia dawa ya malaria ya hydroxychloroquine ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona licha ya kwamba wanasayansi wametoa angalizo dhidi athari ambazo zinaweza kujitokeza.

Utafiti unaendelea kuangalia kama dawa hiyo ya malaria ya hydroxychloroquine ambayo ni sawa na chloroquine zinaweza kukabiliana na virusi vya corona.

Tumeangalia kile ambacho tunakifahamu kuhusu dawa hizi.

Nani ametoa wazo la kutumia dawa hizo
Shirika la afya duniani limesema kuwa linahofia ambao wanajitibu wenyewe kwa dawa hizo kupata madhara makubwa.

US President Donald Trump speaking at the White House

Rais Trump alizungumzia kabla kuhusu matumizi ya dawa hizi kwa ajili ya Covid-19

Hofu ya usalama wao imeibuliwa na ofisa wa zamani wa afya. Dkt. Rick Bright, ambaye aliondolewa katika wadhifa wake mwezi Aprili kutokana na jitihada za serikali za kutengeneza chanjo mpya, alisema nia ya rais Trump katika dawa hizi inavuruga juhudi za wanasayansi wengi.

Je, kuna ushaidi kuwa dawa hizo zinaweza kutibu ugonjwa wa Covid-19?
Awali rais Trump alizungumzia kiufupi kuhusu dawa ya hydroxychloroquine alipokuwa White House. Katika mkutano na waandishi wa habari mwezi Aprili alisema; "Mna kitu gani cha kupoteza? Chukueni."

Na rais wa Brazil Jair Bolsonaro alidai kuwa video inayoonyesha dawa ya malaria ya "hydroxychloroquine inafanya kazi taratibu katika maeneo yote",ingawa video hiyo iliondolewa katika mtandao wa Facebook kwa madai kuwa haikuwa imefuata utaratibu na vigezo vya wa mtandao huo.

Kufuatia maoni ya bwana Trump mwishoni mwa mwezi Machi, nchini Marekani, idadi ya watu ambao wameripotiwa kutumia dawa zote mbili yaani chloroquine na hydroxychloroquine.

Vidonge vya chloroquine vimekuwa vikitumika kwa muda mrefu kutibu malaria au kupunguza homa na to reduce fever sasa zinadhaniwa kuwa zinaweza kupambana na corona pia.

Kumekuwa na majaribio kadhaa ya matumizi ya dawa hii katika mataifa mbalimbali ili kuzuia ugonjwa huu, ikiwa ni sehemu ya utafiti, wahudumu wa afya ambao wako kwenye hatari ya maambukizi zaidi wanakunywa kama tahadhari.

Mpaka sasa hakuna ushaidi wa kutosha kutoka katika majaribio yaliyofanyika kwa ajili ya kuzuia au kutibu ugonjwa wa corona.

Vilevile athari za dawa hizo zimehainishwa kuwa hatari, ikiwemo athari ya kuharibika kwa ini.

Mataifa gani yameruhusu matumizi ya dawa hizi?
Mwishoni mwa mwezi Machi, mamlaka ya chakula na dawa nchini Marekani (FDA) ilihalalisha matumizi ya dharura ya dawa hizo kwa ajili ya kutibu wagonjwa wa corona ambao hali zao si nzuri.

Lakini Aprili, 24 FDA ilitoa angalizo kuhusu hatari ya wagonjwa kuripotiwa kuwa na shida ya kupumua. Mataifa mengine ambayo wanatumia dawa hizi za malaria.

A female scientist in a coronavirus testing lab

Wanasayansi nchini Marekani wamenza jaribio kuangalia ikiwa chloroquine itasaidia kutibu virusi vya corona
Ufaransa, imeruhusu madaktari wake kuwapa wagonjwa wa Covid-19, licha ya angalizo la madhara yake kutolewa.

Wizara ya afya nchini India imeshauri watu kutumia dawa ya hydroxychloroquine kama dawa ya kuzuia wahudumu wa afya kupata maambukizi na kama dawa ya kutibu endapo daktari atakuandika.

Hata hivyo taasisi za utafiti nchini humo zimeonya matumizi ya dawa hizo na kutaka zitumike katika dharura tu.
Aidha mataifa mengine ya mashariki ya kazi yameanza kutumia dawa hizo za malaria.

Je, kuna chloroquine za kutosha?
Ikiwa uhitaji wa dawa hizi unakuwa kwa ajili ya kutibu Covid-19, mataifa mengi yamekumbana na uhitaji mkubwa na uhaba wa dawa kuingezeka.

Chloroquine zimekuwa zinapatikana katika maduka ya madawa haswa katika mataifa yanayoendelea kwa ajili ya kutibu malaria.

Baadhi ya nchi zimeweka zuio la mauzo ya dawa hizo za chloroquine na kupatikana katika hospitalini tu.
India - ambaye ni mtengenezaji mkubwa wa dawa za malaria imesitisha kuuza nje ya nchi.L akini imeondoa zuio hilo kwa Marekani baada ya rais Trump kutuma maombi yake kwa waziri mkuu wa India, Narendra Modi.

Nigeria bado wanatumia dawa hizo kutibu malaria ingawa kuna angalizo la kuzuia kutumia dawa hizo kwa ajili ya kutibu corona.

Chanzo: BBC
 
Back
Top Bottom